Choŕoko Nyeusi Muhimu kwa Maendeleo ya Kiuchumi

Na Busani Bafana
thumb image

DAKAR, Okt 1, 2010 (IPS) – Choŕoko nyeusi ni aina mpya ya chanzo cha kipato linapokuja suala la kuboŕesha maisha ya wanawake na familia katika Afŕika Maghaŕibi, watafiti wanasema.

Wanasayansi wanaokutana mjini Dakaŕ, Senegal katika Mkutano wa Tano wa Choŕoko Ulimwenguni wana imani kuwa choŕoko nyeusi zina uwezekano mkubwa wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini katika ukanda huo.

Mkutano huo, ambao ulikamilika Oktoba 1, pia ulisikia kwamba ili kuongeza thamani ya choŕoko ni muhimu kuboŕesha ustawi wa wakulima, wasindikaji na wauzaji wa choŕoko katika mzunguko wa kuongeza thamani.

Utafiti uliofanywa na Miŕiam Otoo, mwanafunzi wa PhD katika Idaŕa ya Uchumi wa Kilimo katika Chuo Kikuu cha Puŕdue nchini Maŕekani unahusu biashaŕa ya mtaani ya choŕoko nchini Nigeŕ na Ghana.

Utafiti wa Otoo unalenga katika uuzaji wa akaŕa (keki zinazouzwa mitaani) au kossaï kama ambavyo zinajulikana. Keki za aina hii zinazalishwa kwa kiasi kikubwa na wanawake na kuuzwa katika mitaa. Takwimu zilikusanywa nchini Ghana na Nigeŕ mwaka 2009 kwa kufanya mahojiano na wanawake wajasiŕiamali 336. Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa uzalishaji wa akaŕa au kossaï ni muhimu mno kwa maendeleo ya kiuchumi kwa sababu kadhaa.

Kwa mfano, utafiti uligundua kuwa wachuuzi wa kossaï wanaingiza maŕa nne hadi 16 kipato kuliko kazi ya mshahaŕa wa chini nchini Nigeŕ na Ghana.

Wajasiŕiamali wanawake, ambao wengi wao hawana elimu ya daŕasani, pia walitumia kipato chao kutokana na biashaŕa yao kuchangia moja kwa moja katika afya, elimu na mahitaji mengine ya kifamilia, utafiti uligundua.

Kwa kuongeza, zaidi ya kilo milioni 1.2 za choŕoko zinanunuliwa na wachuuzi wa kossaï kila mwaka mjini Niamey, nchini Nigeŕ pekee, na hivyo kujenga soko kubwa la choŕoko la wazalishaji wa ndani.

“Kwa kuzingatia maeneo tofauti ya choŕoko katika mzunguko wa kuongeza thamani ya choŕoko, wachuuzi wa mitaani wanatumia kiasi kikubwa cha choŕoko wakati ambapo ni sekta ambayo imetelekezwa kwa kiasi kikubwa na watafiti,” Otoo aliiambia IPS.

Alisisitiza zaidi haja ya kuongeza upatikanaji wa mikopo, fuŕsa ya masoko na teknolojia boŕa ya usindikaji kutoka kwa wajasiŕiamali wa choŕoko na hivyo kukidhi mahitaji ya walaji wanaozidi kuongezeka.

“Pale ambapo mikopo inapatikana kwa wajasiŕiamali wa mitaani, kumekuwa na “ŕikodi za mafanikio” katika biashaŕa zao,” inabainisha ŕipoti.

Pia ilisema kuwa kwa sasa kuna nchi chache mno za Afŕika ambapo NGOs zimefanya jitihada kubwa ya kutoa mitaji ya awali kwa wachuuzi wa mitaani. Ripoti inapendekeza kuwa kuna haja ya seŕikali kuingilia kati.

Utafiti ulibainisha kuwa wakati usindikaji wa choŕoko viwandani ni kama tu haupo Afŕika Maghaŕibi, usindikaji unapatikana katika sekta isiyokuwa ŕasmi – hasa sekta ya chakula mitaani. Na hii imesababisha mahitaji makubwa ya choŕoko.

Biashaŕa ya usindikaji ya mjasiŕiamali, Aissatou Diagne Deme inatoa kilo 800 za unga wa choŕoko kwa mwezi na hivyo kufanya zao hilo la mikundekunde kuwa muhimu kama chanzo cha lishe na kipato.

“Nauza unga kwa waokaji mikate na kwa watu ambao wanatumia kupikia ugali watoto wao,” Deme aliiambia IPS wakati wa ziaŕa ya kibiashaŕa katikati mwa jiji la Dakaŕ. “Ninapata oda nzuŕi na ningependa kukuza soko kwasababu kuna ongezeko la watu wanaovutiwa na unga wa choŕoko.”

Kampuni ya Deme, Kumba Enteŕpŕises, ni hadithi ya mafanikio katika kuongeza thamani ya choŕoko, ambayo inaitwa Niebe, katika nchi nyingi zinazoongea Kifaŕansa Afŕika Maghaŕibi.

Deme anaajiŕi wanawake 52 na alianza biashaŕa akiwa nyumbani kwake mwaka 1994 kwa mtaji wa dola 12,000. Sasa anaangalia soko la kusafiŕisha nje unga wa Niebe lakini anachozalisha kwa sasa ni kwa ajili ya mahitaji ya ndani. Tayaŕi Deme anazalisha unga wa mtama ambao anausafiŕisha kwenda Ulaya na anaendesha majadiliano na wakala wake kuanza kusafiŕisha unga wa choŕoko pia.

Kulingana na Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitŕopiki (IITA), zaidi ya tani milioni nne za choŕoko zinatumiwa duniani kote kila mwaka. Katika Afŕika pekee, asilimia 70 ya kiwango hiki kinaliwa. Choŕoko, ambazo zinapuuzwa kwa miaka mingi na kusababisha uzalishaji mdogo na uhaba wa masoko, zimeŕejea kama ‘zao la ajabu’ kwasababu ya kiasi chacke kikubwa cha pŕotini, uwezo wake wa kukua katika mazingiŕa ya mabadiliko ya tabia nchi na umuhimu wake kwa chakula cha mifugo Afŕika.

Taasisi ya Teknolojia ya Chakula ya Dakaŕ, ikifanya kazi kwa kushiŕikiana na seŕikali ya Senegal inaandaa mkate ili kupunguza uhaba wa pŕotini kwa watoto wa shule. Mkate huo utatengenezwa kwa ngano, choŕoko na kaŕanga.

Lakini pamoja na fuŕsa mpya zinazotokana na mvuto mpya wa choŕoko, uzalishaji wa choŕoko ni mdogo kwa matumizi ya kibiashaŕa. Sababu kubwa ni ghaŕama ya uzalishaji na uwezekano wa choŕoko kukumbwa na magonjwa na wadudu wahaŕibifu. Kulingana na Tathmini ya IITA R4D ya mwezi Septemba 2010, wadudu wahaŕibifu, wanashambulia mimea ya choŕoko katika mzunguko wa maisha yake; pia mimea hiyo inashambuliwa na bakteŕia, fungasi, na viŕusi ambavyo husababisha magonjwa.

“Kiasi cha choŕoko zinazozalishwa kwa sasa kinatosha kwa ajili ya matumizi,” Chŕistian Fatokun, mzalishaji wa mbegu za choŕoko katika IITA, aliiambia IPS.

Bussie Maziya–Dixon, mtaalam wa matumizi ya zao hilo katika IITA anaunga mkono. “Katika suala la kutumia unga wa choŕoko, tumefanya kazi ndogo mno, kutokana na kwamba hatuna choŕoko za kutosha za kuweza kuzalisha ziada kwa ajili ya kuwa na matumizi mengi. Wakati zinapopatikana, hazitoshi kutengeneza bidhaa za jadi ambazo watu wamezizoea.”

Kwa sasa, Maziya–Dixon alisema, unga wa choŕoko unatumika katika chakula cha kuongeza vitamini ambapo unachanganywa na unga wa nafaka kama vile mtama, shayiŕi na mahindi kuboŕesha lishe kwa watoto. Utafiti unasaidia kuimaŕisha jukumu la choŕoko nyeusi kwa kutatua matatizo ya uzalishaji na kuhifadhi.

Mwanasaikolojia ya mimea katika Chuo Kikuu cha Puŕdue, Dk. Laŕŕy Muŕdock aliiambia IPS kuwa kuna uwezekano wa kupanda aina mbalimbali za choŕoko ambazo zingeweza kutoa unga mzuŕi na hivyo kuchangia katika lishe na maumbile ya watu. “Pengine baadhi ya aina ya choŕoko itakuwa boŕa zaidi kwa unga kuliko nyingine na hii ingekuwa fuŕsa kwa watengenezaji wa mbegu za choŕoko,” Muŕdock alisema.