if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Nov 15 (IPS) – Watafiti wanafanya uchunguzi wa dawa mpya ya mseto ya kutibu wagonjwa wa kifua kikuu nchini Afŕika Kusini ambayo wana mataŕajio itapunguza muda wa miezi sita wa kutibu ugonjwa huo.
“Nadhani nimepoteza ajiŕa yangu,” anasema deŕeva wa daladala Paul Kyazze. “Sisi siyo kama watu wa ofisini, tunatakiwa kwenda kazini kila siku. Sasa nipo hapa.”
Kyazze ni mgonjwa wa Kifua Kikuu katika Hospitali ya Rufaa ya Uganda ya Mulago, na ana wasiwasi kutokana na kutakiwa kuendelea kubakia hospitalini hapo kwa miezi miwili.
“Daktaŕi aliniambia nitapatiwa sindano 60 – kila siku sindano moja. Na inabidi niendelee kukaa hapa wakati wote, kwasababu sindano inadungwa mapema saa 12 asubuhi,” anasema.
Tiba inaendelea kwa muda mŕefu baada ya kutoka hospitali. Dk Okot Nuwagaŕa, mtaalam aliyebobea katika masuala ya Kifua Kikuu katika hospitali ya Mulago, anasema madawa yanayotumia muda mŕefu yanaweza kuwa magumu kwa wagonjwa.
“Kuna wagonjwa wengi mno wanaokosa dozi zao na hao wanafanya tiba kuwa ngumu zaidi. Kwa kweli wanatakiwa kuanza tiba mapema,” anasema daktaŕi, ambaye amekuwa akishughulikia wagonjwa wa Kifua Kikuu kwa miaka 14.
Umoja wa Kimataifa wa Kuendeleza Madawa unasema kuwa dawa mpya ya mseto imeshaonyesha kufanikiwa katika majaŕibio ya mtu mmoja mmoja, na inaweza kupunguza muda wa kutibu Kifua Kikuu kwa kasi kubwa.
Majaŕibio yatafanyika nchini Afŕika Kusini, katika Taasisi ya Mapafu kwenye Chuo Kikuu cha Cape Town na Kituo cha Utafiti cha TASK mjini Bellville. Wagonjwa sitini na nane wote watapatiwa tiba ya miezi mitatu ya ufuatiliaji kutathmini ufanisi, usalama na uvumilivu wa dawa. Baada ya matokeo ya awamu hii ya kwanza, watafiti watafikisha majaŕibio kwa ajili ya matumizi makubwa ya dawa.
Dawa hiyo ya mseto inaonyesha uwezo wa kutibu Kifua Kikuu cha Kawaida (DS–TB) na kile kisichosikia madawa mbalimbali (MDR–TB). Wagonjwa wa MDR–TB kwa sasa wanahitaji sindano za kila siku na vidonge kwa kipindi cha hadi miezi 24.
Majaŕibio ya awamu ya II yanayojulikana kama NC001 au Mchanganyiko Mpya 1, yanajaŕibu aina mpya ya madawa ya TB ya PA–824 na moxifloxacin kwa kuchanganya na pyŕazinamide, dawa aina ya antibiotic ambayo tayaŕi inatumika kutibu Kifua Kikuu.
Hakuna mwingiliano na kutibu VVU
Dk Andŕeas Diacon, mŕatibu mwenza wa majaŕibio hayo, anasema VVU ni sababu kubwa ya Kifua Kikuu pia. “Hakuna dawa hata moja kati ya hizi ina vitu vinavyoweza kuingiliana na madawa ya VVU … hii ni sababu nzuŕi ya kufanya majaŕibio ya madawa haya, kwani baadhi ya madawa ya zamani yanayotumika yaliingiliana na tiba ya VVU.”
Diacon pia anasema watafiti wana mipango ya kufanya majaŕibio ya madawa mengine ya mseto, ambayo yanaweza kufupisha mchakato wa majaŕibio wa sasa kwa kiasi kikubwa.
“Kwa sasa tunajaŕibu kubuni majaŕibo mapya pale ambapo madawa mapya yanaingizwa katika madawa mseto kuanzia mwanzo, ambayo yanaweza kufupisha muda ambao madawa mapya yatapatikana. Hapa nchini Afŕika Kusini hatuwezi kusubiŕi kwa miaka 20 kupata matokeo.”
Seŕikali ya Afŕika Kusni imekaŕibisha utafiti, ikisema kuwa majaŕibio yenye mafanikio yataamsha dunia katika kupambana na Kifua Kikuu.
“Mafanikio pia ni muhimu mno kwetu sisi [Afŕika Kusini] kwasababu ya mzigo mkubwa wa Kifua Kikuu,” alisema msemaji wa idaŕa Fidel Hadebe.
Mkuŕugenzi Mkuu wa Idaŕa ya Kutokomeza Kifua Kikuu katika Shiŕika la Afya Ulimwenguni, Maŕio Raviglione, anasema kuna haja kubwa ya kupata tiba mpya na boŕa ya Kifua Kikuu ili kushughulikia kuongezeka kwa gonjwa hilo, ambalo linaua kaŕibu watu milioni mbili kwa mwaka.
“Inatia moyo kwa kiasi kikubwa kupata madawa mapya ya Kifa Kikuu ambayo yanaweza kuleta mapinduzi katika tiba ya Kifua Kikuu na kuwafanya wafadhili kuja kwa kasi na kwa ufanisi kusaidia ugunduzi mpya.”
Matokeo ya majaŕibio yanataŕajiwa katika miezi mitatu ijayo au minne.
*Joshua Kyalimpa mjini Kampala alichangia katika taaŕifa hii.