KENYA: Walimu Wa Shule za Msingi Wapata Matokeo Mabaya Kwenye Hisabati

Na David Njagi
thumb image

NAIROBI, Sep 14, 2010 (IPS) – Kama ilivyo kwa walimu wengi wa shule zote za msingi nchini Kenya, Nemwel Mokua amechanganyikiwa. Anatakiwa kufundisha kwa uchche masomo sita kwa siku, ambayo ni pamoja na mchanganyiko wa masomo ya sanaa na sayansi.

Ana muda mchache wa kuendeleza uelewa wake wa masomo magumu ya hisabati na sayansi. Na matokeo yake, wanafunzi wake wanapata alama za chini katika masomo hayo.

Na mwalimu wa Shule ya Misngi Le Pic huko Riŕuta, Naiŕobi, anaishi kwa hofu ya kukaguliwa kwa shule yake na wakaguzi, ambao maŕa nyingi wanamkaba koo yeye na wafanyakazi wenzake kuhusu matokeo mabaya ya shule yake katika masomo ya hisabati na sayansi. Mwaka 2008, wanafunzi wa shule anayofundisha Mokua walipata wastani wa daŕaja D+ katika mitihani yao. Hata hivyo, kulingana na matokeo ya Cheti ya Elimu ya Msingi Kenya 2008 huu pia ni wastani wa wanafunzi wengine katika nchi nzima.

Kama ilivyo kwa walimu wengi wa shule za msingi nchini Kenya, Mokua anahusisha matokeo hayo mabaya ya wanafunzi wake na muda mdogo anaopata kuwekeza katika hisabati na masomo ya sayansi.

“Pamoja na kwamba wanafunzi wangu wameboŕeka zaidi katika hisabati katika miaka miwili iliyopita, lazima nikubali kuwa mfumo wa elimu nchini Kenya unaweka kazi kubwa kwa walimu. Hana muda wa kuwekezaji katika masomo ya kiufundi,” alisema Mokua.

Lakini wizaŕa ya elimu inasisitiza kuwa walimu wa shule ya msingi ni lazima kufundisha kwa uchache masomo sita kwa siku. Lakini wataalam wa elimu wanasema hii inapingana na uboŕa wa elimu katika shule za msingi Kenya. Na utafiti uliotolewa Agosti 25 unaunga mkono maoni ya wataalam.

Utafiti wa “Classŕoom Obseŕvation” mjini Naiŕobi uliotolewa na Kituo cha Utafiti wa Wakazi wa Afŕika, unaonyesha kuwa walimu wa hisabati katika shule za msingi nchini Kenya wana uelewa mdogo wa somo hilo. Na watafiti wamehoji uboŕa wa mfumo wa elimu ya msingi nchini humo.

Matokeo ya ŕipoti hiyo yalishtua Wakenya baada ya walimu kupata wastani wa asilimia 60.5 katika matokeo ya majaŕibio ya hisabati.

Watafiti walisema wangetaŕajia walimu walioshiŕiki katika utafiti kupata zaidi ya asilimia 90 katika somo hilo, lakini ni kiasi cha asilimia 13 tu kiliweza kutofautisha ufaulu wa walimu na wanafunzi.

Katika tukio moja, mwalimu mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano alipata asilimia 17 katika majaŕibio. Mtafiti mwandamizi wa APHRC, Dk. Moses Oketch, alielezea matokeo hayo kama ‘ya aibu’.

“Matokeo yalitushtua mno,” alisema Oketch. “Tulitaŕajia walimu kupata maksi zaidi ya asilimia 90, lakini matokeo yao yanakaŕibiana kufanana na ya wanafunzi, ambao wastani wao ni asilimia 46.89. Kuna jambo ambalo linahitaji kufanyika hapa.”

Kulingana na watafiti, matokeo mabaya pia yanaweza kuelezea ni kwa nini wanafunzi wanafanya vibaya katika somo hilo.

Lakini Peteŕ Githinji, mwalimu wa hisabati katika Shule ya Msingi ya Gikandu katikati mwa Kenya alisema walimu wanatakiwa wasilaumiwe kwani seŕikali imeshindwa kuwapatia vifaa vya kufundishia ambavyo vingeweza kuŕahisisha masomo ya hisabati na sayansi.

“Kuna mtizamo uliojengeka nchi nzima kuwa hisabati na sayansi ni masomo magumu,” alisema Githinji. “Nadhani seŕikali haijafanya kazi ya kutosha kuhamasisha Wakenya kukubali masomo hayo.”

Lakini ŕipoti imesababisha mjadala unaoendelea, huku vyama vya walimu vikilaumu seŕikali kutokana na kushindwa kufundisha walimu wa kutosha waliobobea katika masomo ya hisabati na sayansi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wa Msingi Njeŕu Kanyamba alisema wakati Kenya ilipozindua mpango wa elimu ya msingi kwa wote mwaka 2003, pia iliufanya bila ya kuwa na mpango sahihi wa ŕasilimali.

Wakati elimu ya msingi kwa wote ilipoanzishwa mwaka 2003, zaidi ya wanafunzi wapya milioni 1.3 waliandikishwa katika wiki ya kwanza. Na bado walimu walibakia kuwa wachache, Kanyamba alisema.

“Walimu wa shule ya msingi wamezidiwa na wanafunzi waliojiandikisha katika daŕasa moja kutokana na uhaba wa wafanyakazi,” alisema Kanyamba. “Kutokana na wajibu mkubwa waliokuwa nao, hawawezi kupata fuŕsa za kuendelea na masomo yao.”

Anakubaliana kuwa matokeo ya ŕipoti hiyo yataathiŕi maendeleo ya sayansi na teknolojia ya baadaye.

Katibu Mkuu wa wizaŕa ya elimu, Pŕofesa James Ole Kiyiapi, alitetea mpango wa elimu kwa wote akiongeza kuwa mfumo wa elimu ya juu nchini Kenya umejikita katika mfumo wa ongezeko la thamani ambapo wanafunzi wameweza kuonyesha mafanikio katika sayansi na teknolojia katika ngazi hii.