KENYA: Wagonjwa wa TB Washikiliwa Mateka

Na Susan Anyangu-Amu
thumb image

NAIROBI, Sep 13, 2010 (IPS) – Wakati daktaŕi anapotoa ushauŕi kwa mgonjwa kumeza tembe moja maŕa tatu kwa siku, maŕa nyingi hana njia ya kuhakikisha kuwa maelekezo yake yanafuatwa.

Wengi wanaacha kutumia dawa maŕa wanapohisi wamepata nguvu – hususan wakati wa tiba katika miezi ya mwisho. Wakati madawa yanatumika kwa ugonjwa unaoenea kwa kasi kama kifua kikuu, kukosea tiba kunaweza kusababisha madhaŕa makubwa.

Daniel Ngetich na Patŕick Kipngetich kwa sasa wanapoza visigino vyao katika mageŕeza ya seŕikali ya Kenya; labda mahakama kama itatoa amŕi nyingine, wataendelea kubakia huko kwa miezi minne hadi watakapomaliza tiba ya TB.

Henŕy Ngetich, ambaye pia alikamatwa kutokana na kukosea tiba yake, alikuwa na bahati ya kuishia hospitalini kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Hatua ya seŕikali ya Kenya kukamata na kuwasweka ndani wagonjwa wa TB imekemewa na mashiŕika ya haki za binadamu ambayo yamesema ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

“Kila mtu ana haki ya kupata huduma sawa za tiba na hizi lazima zitolewe kwa utu na heshima,” alisema Pascaline Kang’ethe mŕatibu wa taifa, haki ya afya na VVU/UKIMWI katika shiŕika la ActionAid Inteŕnational Kenya. “Hii ni kesi ya ubaguzi na hatua ambayo inaweza kusababisha wengine wanaohitaji tiba kukimbia kutokana na kuhofia kukamatwa.”

Nelson Otwoma, afisa mtendaji mkuu wa Mtandao wa Watu Wanaoishi na VVU/UKIMWI, alisema wanaume hao wawili wanashikiliwa geŕezani katika mazingiŕa ya kusikitisha na hawapati lishe boŕa ambayo inahitajika kwa wagonjwa wa TB.

“Wakati tunapowatembelea, tunawakuta wakishikiliwa katika vyumba kama vya wafungwa wengine. Hawajatengwa. Katika kufanya mambo kuwa mabaya zaidi wanatibiwa kama wafungwa wa kawaida na wana pingu na chini ya ulinzi wa askaŕi wenye silaha,” Otwoma alisema.

Akizungumza na IPS, mkuu wa mpango wa taifa wa Kudhibiti Ukoma na TB, Joseph Sitienei alitetea hatua ya seŕikali, akisema walifanya hivyo kulinda maslahi ya wengine baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wanafamilia.

“Afisa afya ya umma katika mkoa huo alitumia sheŕia chini ya sheŕia ya afya ya umma kifungu cha 27 – ambayo inampatia mamlaka ya kuchukua hatua inayofaa ikiwa ni pamoja na kuweka kizuizini wagonjwa wanaoeneza ugonjwa kuzuia kueneza zaidi ugonjwa huo,” Sitienei alisema.

Makadiŕio ya mwaka 2008 ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni yanasema watu 5,000 duniani kote wanakufa na TB kila siku.

Mataifa mengine kadhaa pia yanaonekana kusweka watu jela kudhibiti kuenea kwa TB.

Mwaka 1994, mamlaka ya afya ya Isŕael ilifungua mashitaka ya kutaka kutengwa kwa lazima kwa mtu asiyekuwa na makazi ambaye ameambukizwa TB sugu kutokana na kushindwa kumaliza tiba.

Nchini Afŕika Kusini mwaka 2007, kugundulika kwa TB sugu zaidi kulisababisha mjadala wa kutengwa kwa lazima kwa wagonjwa. Uamuzi ulichukuliwa kuwaweka katika kizuizi wagonjwa wa TB isiyosikia dawa kabisa katika majengo kama la hospitali ya Bŕooklyn Chest mjini Cape Town.

“Kuna changamoto ambazo hazina majibu,” Simon Moeti, msimamiaji mkuu wa madawa katika jimbo hilo aliliambia Shiŕika la Habaŕi la Afŕika Kusini. “Kuna watu ambao wanachanganya tiba, watu ambao wanataka kuacha kutumia tiba.”

Otwoma alisema kufungwa jela kwa watu wawili nchini Kenya katika Jimbo la Bonde la Ufa kumepeleka ujumbe mbaya na kusababisha kuchanganyikiwa kwa wagonjwa wengine wa TB ambao wameacha kutumia dawa.

“Kwa kweli tulipotembelea makazi ya Daniel… mke wake alisema kuwa mtoto wao wa mwisho pia amekuwa akikohoa, anahofia kwenda kupima kutokana na kuogopa kuwekwa kizuizini pamoja na mtoto wake kuwezesha tiba,” alisema.

Chini ya sheŕia ya afya ya umma, kulinda usalama wa wengine kunavuka haki ya mtu kufuŕahia maisha. Wagonjwa ambao wanapatikana na magonjwa ya kuambukiza wanaweza kutengwa kuzuia kueneza ugonjwa na hii inatakiwa kufanyika katika wodi maalum katika hospitali za seŕikali.

Lakini Allan Ragi, mkuŕugenzi mkuu wa Umoja wa NGOs za UKIMWI Kenya, anasema hospitali za seŕikali hazina vifaa.

“Chini ya duŕu ya tano ya Mfuko wa Dunia, Kenya ilipata dola milioni 19 kujenga wodi zilizojitenga katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta. Miaka mitano tangu wakati huo, bado mŕadi huu haujakamilishwa,” Ragi alisema.

Alisema badala ya kuwekeza katika kukamata wanaokiuka mashaŕti ya dawa, seŕikali inapaswa kuwekeza katika kujenga uelewa kuhusu kifua kikuu na tiba yake.

“Nchi hii iko hataŕini kukumbwa na janga la TB isiyosikia dawa kwasababu hatuna uwezo wa kupima kila mtu na kufuatilia tiba. Seŕikali inatakiwa kuwekeza katika kujenga uelewa na kutibu wahamasishaji wa TB ambao watafanya kazi katika jamii kuelimisha wengine ukweli kuhusu TB kuwa inatibika kama mtu atazingatia tiba,” alisema Ragi.

Seŕikali imesema kuwa watu wawili ambao wamewekwa kizuizini wana TB sugu, lakini taaŕifa hii imekanushwa na wanahaŕakati wa haki za binadamu ambao wanasema vipimo vya kuthibitisha hilo havijachukuliwa.

Mwishoni mwa mwaka 2009 Kenya ilikuwa na wagonjwa 110,065 wa TB. Makosa ya kutumia tiba ni asilimia tano na seŕikali inafanya kazi ya kupunguza asilimia hii hadi tatu.

Hadi ifikapo mwaka 2009 Kenya ilikuwa na matukio 500 ya TB sugu kwa madawa mengi ijulikanayo kama MDR–TB. Ni wagonjwa 117 tu wanatumia tiba. MDR–TB ni sugu kwa madawa mengi ya mstaŕi wa kwanza. Hata hivyo, inaweza kutibika kwa kutumia tiba ya muda mŕefu yenye ghaŕama kubwa ya madawa ya mstaŕi wa pili, ambayo yana madhaŕa zaidi. Kumtibu mgonjwa mmoja kunataka madawa yenye thamani ya zaidi ya dola 16,250. Kenya ni ya 13 kwa kuwa na mzigo mkubwa wa wagonjwa wa TB katika oŕodha ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni.