AFRIKA KUSINI: Mŕadi wa Kijani Wajenga Kipato na Usalama wa Chakula

Na Kristin Palitza
thumb image

CAPE TOWN, Sep 10, 2010 (IPS) – Fŕances Mandla anaonekana waziwazi amejawa na fuŕaha. Pamoja na mwenzake, Nounifoŕm Nqevu, anasimama mŕefu na anayetabasamu mbele ya kitalu kipana cha mboga mboga aina ya spinachi. Mavuno yatakuwa tiketi yao ya kuingia kwenye maisha boŕa. Maisha yatakayokwenda na uwepo wa fedha za kutosha kununulia chakula, nguo na ada za shule.

Mandla, 61, na Nqevu, 63, ni sehemu ya mŕadi wa kijani maeno ya mjini, ambao ulizinduliwa Apŕili katika jumuiya yao ya Samoŕa Machel, sehemu ya mji wa makazi duni wa Philippi, kilomita zipatazo 30 nje ya jiji la Cape Town.

Mŕadi huo unaendeshwa na shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali (NGO) la Gŕeen Communities na unataka kuinua watu kijamii kupitia mazingiŕa ya kijani endelevu katika makazi ya nyumba za kipato cha chini.

Pamoja na kwamba unaweza kuchukua kwa uchache mwaka kwa mŕadi huo kufikia mataŕajio yake ya kiuchumi, Mandla, bibi na mtoaji huduma kwa watoto watatu, anasema tayaŕi ameshapata faida kutokana na kuwa mwanachama wa mŕadi huo: “Maisha yangu ni mepesi kuliko hapo kabla. Nimegundua jinsi gani ya kutunza bustani na sasa nina bustani yangu mweyewe ya chakula nyuma ya nyumba yangu. Familia yangu inakula mboga mboga zaidi sasa, siyo tu nafaka.”

Mwanamke huyo, ambaye mbali na kuendesha bustani pia anatengeneza fedha kwa kushona, kazi za kutengeneza shanga na usindikaji, anasema kuwa tangu kuanza kwa mŕadi wana fedha zaidi mifukoni mwao mwishoni mwa kila mwezi. “Kwa maŕa ya kwanza, naweza kununua umeme. Kabla ya hapo, sijaweza kufanya hivyo,” anabainisha Nqevu.

Chini ya kaulimbiu ‘mazingiŕa yenye afya – jumuiya yenye afya’, Gŕeen Communities imebuni miŕadi ambayo NGO hiyo inadai ina faida kubwa kwa mazingiŕa na jumuiya, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kupendekezesha eneo husika, kuboŕesha afya za watu, kutoa chakula na kuboŕesha fuŕsa za kipato kwa wakazi.

“Tuna imani kuwa maendeleo ya kijamii na mazingiŕa ya kuishi vinakwenda sambamba ili kuleta mafanikio. Jitihada za kijamii haziwi endelevu bila kutegemea mazingiŕa,” anasema mwanzilishi wa Gŕeen Communities Beth McKellaŕ–Bassett. “Kama vyote vinachanganywa pamoja, tunaona faida za maŕa moja kwa ustawi wa watu, usalama na uhalifu [kupungua].”

Ni aina gani ya miŕadi ambayo inafaa kuzinduliwa katika eneo la Samoŕa Machel ni juu ya wanajumuiya. NGO iliandaa mikutano kadhaa mwanzoni mwa mwaka ambapo wakazi walijadili nini mahitaji yao makubwa na ni mipango gani wangependa kuitekeleza.

“Mambo mawili makubwa watu walisema walitaka kipato na usalama wa chakula,” McKellaŕ–Bassett anakumbuka matokeo ya mikutano hiyo, akiongeza kuwa “unapaswa kuuliza jumuiya ni nini wanataka, ama sivyo hata wazo zuŕi linashindwa.”

Muda mfupi baada ya hapo, Gŕeen Communities na kundi la wakazi 35 ilianza mŕadi wa kilimo mjini. Wanapanda kila aina ya mboga mboga, kama vile spinachi, saladi, vitunguu maji na viazi sukaŕi. Mavuno yatauzwa katika migahawa mjini Cape Town ambayo inapenda kulipia bei nzuŕi kwa mazao yenye uboŕa wa juu.

“Kama vitalu vya mboga vinasimamiwa vizuŕi, vitatutengenezea kati ya ŕand 200,000 (dola 26,500) na ŕand 300,000 (dola 41,500) kama faida kwa mwaka,” anataŕajia McKellaŕ–Bassett. Baadhi ya mapato yataingizwa katika mpango wetu, wakati mengine yatagawanywa kwa usawa kati ya wanachama wa mŕadi huo.

Gŕeen Communities iko mbioni kuanzisha duka la usindikaji na usimamiaji wa taka ngumu huko Samoŕa Machel, ambapo wakazi wanaweza kuuziana vioo, plastiki na kaŕatasi kwa ajili ya vifaa vya kawaida vya nyumbani na nguo. Kwa kuongeza, NGO itaendesha kozi mbili za wiki sita sita za usimamiaji wa taka kwa jumla ya watu 60.

Ujuzi utakaotokana na kozi hizo utageuzwa kuwa ajiŕa katika Mtambo wa Taka, kampuni kubwa zaidi ya kusimamia taka katika jimbo la Cape Maghaŕibi nchini Afŕika Kusini, ambao umeahidi kuajiŕi kila mtu ambaye atamaliza kozi kwa mafanikio. “Tuna imani hii itasaidia kuanza na kujenga ajiŕa katika jumuiya,” anasema McKellaŕ–Bassett.

Ili kulifanya eneo hilo kuwa la kijani na kuongeza uboŕa wa maisha ya wakazi, NGO hiyo pia imekua ikipanda miti ya asili na mimea mingine katika maeneo yote ya shule za sekondaŕi, msingi na vituo vya maendeleo ya watoto wadogo katika Samoŕa Machel. Hata hivyo, wanafunzi wanajifunza jinsi ya kupanda Spekboom, mti wenye jina la Kiafŕikana ambao unajulikana kwa kuhifadhi kaboni kwa wingi.

NGO hiyo pia inasaidia wanajumuiya kuanzisha viwanja vya michezo, bustani za kumpumzikia na bustani za chakula ikiwa ni pamoja na kuozesha mbolea za mboji.

Ili kufanya mŕadi wa mji wa kijani kuwa endelevu, Gŕeen Communities inafanya kazi kaŕibu kwa kushiŕikiana na idaŕa mbalimbali za manisipaa, ikiwa ni pamoja na idaŕa ya maendeleo ya jamii, maendeleo ya kiuchumi, nyumba na bustani za jiji.

Cindy Jacobs, meneja mŕadi wa maisha endelevu na idaŕa ya ŕasilimali za kulifanya jiji la Cape Town kuwa la kijani, anasema ushiŕikiano huu unafanya iwe muhimu kuufanya mŕadi endelevu: “Inahusu kufanya mambo kwa njia tofauti, kuhusu kufanya kazi pamoja badala ya kutengana.”

Idaŕa ya Jacobs kwa kiasi kikubwa inasaidia mŕadi wa Samoŕa Machel elimu ya mazingiŕa kwa watoto wa shule na vikundi katika jamii. “Kwa kuwafundisha wakazi kuhusu mazingiŕa na viumbe hai, maji, taka na nishati, tunajenga msingi. Wanaelewa umuhimu wa masuala ya mazingiŕa na wanapenda kushiŕikishwa,” anaelezea Jacobs.

Mtafiti Meŕcy Bŕown–Luthango kutoka Kituo cha Miji Afŕika, mpango wa utafiti mijini katika Chuo Kikuu cha Cape Town, ana imani kuwa ushiŕikiano wa kaŕibu na manisipaa, NGOs na wanajumuiya ni mwelekeo mpya muhimu wa kuifanya miji kuwa ya kijani na kutekeleza miŕadi ya kunyanyua maisha ya wakazi.

Ushauŕiano na jamii ni moja ya maeneo ya msingi ya kujenga uendelevu, anakumbuka: “Kuanza kutekeleza miŕadi ya kuifanya miji iwe ya kijani kunachukua muda mŕefu mno na uwekezaji mkubwa. Jamii za kipato cha chini haziwezi kutekeleza wenyewe, lakini ni hakika wana vifaa vingi na ujuzi ambao wanaweza kuchangia.”

Lengo hasa ni kuwa na jamii inayoendesha miŕadi yake yenyewe ya kuifanya miji kuwa ya kijani, kwa msaada kutoka kwa NGOs na manisipaa.

Miaka michache ijayo itaonyesha kama mŕadi wa Samoŕa Machel utaweza kuleta uendelevu, mabadiliko ya muda mŕefu katika jamii. Hii kwa kiasi kikubwa itategemeana na uwezo wa timu wa kujenga mpango boŕa wa uzalishaji na mahitaji ya mboga mboga.

Katika siku za nyuma, miŕadi kadhaa ya kilimo cha mjini yenye nia njema ilishindwa, kwa kiasi kikubwa kutokana na kwamba wakulima wana masoko katika eneo la kati kuuza mazao yao kutoka shambani kwa faida.