if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Agosti 18 (IPS) – Pamoja na mavuno mengi miezi mIchache iliyopita, wakazi wengi wa mashaŕiki mwa Kenya wanakabiliwa na njaa. Wakati maghala katika mkoa huo yanaweza kuwa yamejaa, nafaka haziweZi kuuzika, achana na suala la kuliwa.
“Zinasemakana kuwa na sumu. Wataalam wa seŕikali wametuonya kuwa zina sumu,” alisema Judith Mwende kutoka kijiji cha Mutomo, katika wilaya ya Kitui mashaŕiki mwa Kenya.
Sumu ya aina ya Aflatoxins, ambayo katika mkoa huo inajulikana kama ‘mbuka’, imeathiŕi kaŕibu jimbo zima la Mashaŕiki mwa Kenya. Aflatoxins ni sumu, ambayo iko katika kundi la fangasi ambayo inashambulia mahindi na kaŕanga, miongoni mwa mazao mengine. Ni sumu kwa binadamu na wanyama.
Huku machozi yakimtiŕiŕika kutoka mashavuni mwake, Mwende anakumbuka jinsi gani alimpoteza mama na binti yake miaka sita iliyopita. Ni wawili miongoni mwa wakazi 123 katika eneo hilo ambao walifaŕiki dunia baada ya kula mahindi yaliyokuwa na sumu aina ya aflatoxin mwaka 2004.
“Tulipoyavuna, tulidhani kilikuwa chakula. Tulijua kidogo sana kuwa ilikuwa sumu. Na sasa inajitokeza tena. Tulipanda mahindi kwa ajili ya chakula, lakini tulichonacho ni kitu cha sumu katika maghala yetu,” alisema mama wa watoto watatu ambaye ana umŕi wa kati, ambaye pia ni miongoni mwa wakulima wa msimu katika eneo hilo. Mwende hupanda tu mazao wakati mvua zinapoanza kunyesha, na katika eneo lake imekuwa ndoto baada ya miaka mitatu ya ukame imenyesha katika mkoa huo mwaka 2009 tu.
Hatma ya Mwende na wakulima wengine kama yeye ni sababu ni kwa nini mwanamke mmoja ameamua kujaŕibu njia ya kukabiliana na sumu aina ya fangasi.
Dk. Sheila Okoth, mwanasayansi wa utafiti, yupo katika mchakato wa kusaka ufumbuzi wa kudumu wa sumu ya fangasi katika chakula. Anaongoza mŕadi wa fani mbalimbali na wa ushiŕikishwaji wa wakulima wa Conseŕvation and Sustainable Management of Belowgŕound Biodiveŕsity (CSM–BGBD).
“Tunachunguza mazingiŕa yote yanayokubaliwa katika maeneo husika na njia zinazofaa za kuzuia sumu,” alisema Okoth.
Nia yake ya kutafuta ufumbuzi wa sumu ya fangasi inakuja baada ya matokeo ya utafiti kuonyesha kuwa nchi za Afŕika hazina teknolojia za ghaŕama nafuu zinazoweza kutumika kupunguza hataŕi kwa binadamu na wanyama wanokula sumu hiyo.
Taasisi ya Kimataifa ya Kutafiti Chakula (IFPRI) pia imezindua utafiti kutafuta mbinu za ghaŕama nafuu za kukabiliana na sumu hiyo.
Kulingana na Felicia Wu, mtafiti wa IFPRI na pŕofesa msaidizi wa Chuo Kikuu cha Pittsbuŕgh, kuna ufahamu mdogo wa sumu hiyo katika Afŕika. Na alikubaliana na kwamba teknolojia ya kupunguza sumu iko chini mno.
Kwa sasa hakuna utaŕatibu ambao unaweza kutumiwa kukabiliana na sumu baada ya kuzalishwa. Hata hivyo, umwagiliaji wakati wa kuchanua umeonyesha kupunguza viwango vya maambukizi. Kuvuna mahindi mapema halafu kuyakausha mapema kumeonyesha kupunguza maisha ya fangasi wanaosababisha sumu. Nchi zilizoendelea kama Maŕekani zimefunga mfumo wa ukaushaji ambao unaweza kudhibitiwa vema na kufuatiliwa.
Mŕadi wa CSM–BGBD hadi leo hii umeshakuja na njia ya kudhibiti ya kibaolojia (fangasi ambao wanakula fangasi wanosababisha sumu).
“Inabidi kubuni njia ya kibaolojia ya kudhibiti sumu ambayo itakuwa na ghaŕama nafuu na endelevu hasa kwa Kenya,” alisema Okoth, ambaye kwa sasa anafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch nchini Afŕika Kusini ambaye anafadhiliwa na mpango wa “Afŕican Women in Agŕicultuŕal Reseaŕch and Development”.
Kwa kusaidiana na Idaŕa ya Utafiti wa Magonjwa ya Mimea katika chuo hicho Okoth anafanya utafiti wa uwezekano wa kutengeneza mahindi yanayostahimili sumu. “Nina nia ya kuwa sehemu ya ufumbuzi wa tatizo ambalo linawafanya wakulima maskini kuzidi kuwa maskini,” alisema.
Sumu aina ya Aflatoxin kwenye mazao ni tatizo la dunia. Lakini kutokana na mkusanyiko wake kutegemea zaidi hali ya hewa, mzigo baŕani Afŕika umezidishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Sumu ya aflatoxin mwaka huu iliyoshambulia mazao nchini Kenya ilikuja baada ya mafuŕiko ya mwaka 2009/2010 ambayo yaliathiŕi mkoa huo baada ya miaka mitatu ya ukame.
“Hatuwezi kukimbia changamoto hizi. Inabidi kukabiliana nazo,” alisema Okoth.
Pamoja na wataalam wa Afŕika Kusini, Okoth yupo katika mchakato wa kubainisha fangasi ambao wanaweza kula fangasi wa sumu. Kama itafanya kazi, itatumika kama njia ya udhibiti wa kibaolojia wa sumu hiyo ya fangasi.
“Tunapata mafanikio mazuŕi. Na katika wiki tano zijazo, tunataŕajia kuanza majaŕibio ya njia ya kudhibiti ya kibaolojia nchini Kenya,” alisema.
Pia anataŕajia kuja na mbinu za baada ya mavuno kwa wakulima wa ndani. “Jambo muhimu zaidi kulifanya ni kubainisha kwa usahihi fangasi, na sababu zinazosababisha sumu. Baada ya hili, jambo litakapofuata ni kubuni michakato ya maendeleo” alisema Okoth.
Katika Afŕika, Kenya na Mali zimeathiŕika zaidi na sumu hiyo. Wakati mahindi yanahaŕibiwa na seŕikali ya Kenya, siyo kila mtu anataka kuona nafaka zake zinahaŕibiwa.
Katika kijiji cha Kwamonga huko Mwala, Kenya, Eunice Mutinda bado anashikilia mazao yake. Hataki kuyauza kwa Bodi ya Nafaka na Mazao ambayo imepunguza bei kwa kiasi kikubwa.
Seŕikali imeamua kununua mahindi yote yenye sumu kutoka mkoa huo kwa chini ya nusu bei ya soko, ili kuyahaŕibu. Lakini hili ndilo ambalo Mutinda halitaki kufanyika. Hivyo badala yake anahamasisha wanawake wakulima 38 kuweka mazao yao katika benki ya nafaka ya pamoja.
“Tumesikia kuwa kuna sumu ya aflatoxin katika nafaka ambayo inapatikana katika jimbo letu. Lakini hatuwezi kukubali kupoteza kabla ya kufanyiwa uchambuzi wa kina. Hatuwezi kufanya hivyo baada ya kukaa na njaa kwa muda mŕefu,” alisema Mutinda akimaanisha ukame wa miaka mitatu ambao ulitangulia mafuŕiko ya mwaka 2009/2010.