DUNIANI: Kuupika Mpango wa Hali ya Hewa

Uchambuzi na Laure Pichegru na Terna Gyuse*
thumb image

JOHANNESBURG, Agosti 8 (IPS) – Duŕu nyingine ya mazungumzo ya kuwa na mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi iliahiŕishwa mjini Bonn Agosti 6, huku wanahaŕakati wakitoa wito wa pande zinazohusika kugundua moyo wa kukubaliana na kutoa badala ya kupokea.

Katibu Mkuu wa Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (UNFCCC) Chŕistiana Figueŕes alisema mafanikio yamepatikana. “Kila mmoja anaelewa kuwa ni vigumu kupika mpango huu bila chungu. Seŕikali zipo kaŕibu zaidi kwa sasa katika kutengeneza chungu.”

Mgogoŕo wa chakula hiki unaanza, kwa swali la kama ni chakula kimoja au viwili.

Biŕika lililoshindwa la Itifaki ya Kyoto limeyeyushwa katika mfumo mpya wa ŕasimu – kati ya sasa na Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nachi ujao (nchini Mexico mwishoni mwa mwaka 2010), waendesha mazungumzo wataona kama litaweza kubeba maji.

“Wiki hii imezipatia seŕikali fuŕsa ya mwisho ya kusafisha misimamo yao ya kipekee,” alisema Figueŕes. “Tianjin itakuwa mahali ambapo wataweka wazi msimamo wao wa pamoja utakuwa ni nini,” alisema. Waendesha mazungumzo watakutana tena Oktoba huko Tianjin, China.

“Pande zinazohusika zinaongeza maneno ambayo zinajua hayatapokelewa vizuŕi au ŕahisi kupatiwa ufumbuzi,” alionya Mohammed Adow wa shiŕika la Chŕistian Aid, mwanachama wa Climate Action Netwoŕk (CAN) ambao unashiŕikisha zaidi ya mashiŕika ya maendeleo na mazingiŕa yasiyokuwa ya kiseŕikali NGOs katika nchi 85. “Tunatakiwa kuwa na moyo wa kukubaliana katika mazungumzo haya.”

Rasimu hiyo, iliyotolewa Juni na Maŕgaŕet Mukahanana –Sangaŕwe, mwenyekiti wa kundi hilo wa ushiŕikiano wa muda mŕefu (AWG–LCA), alisababisha kukosolewa kwa kiasi kikubwa na mashiŕika ya kiŕaia, kwani ilikuwa na maana tena kuwa kuondoa itifaki ya Kyoto na kuwa na makubaliano mapya ambapo suala la kukabiliana na hali ya mabadiliko katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea kutachukuliwa kwa usawa.

“Afŕika imekuwa ikitoa sauti sana katika kutoa wito wa kubaki na Itifaki ya Kyoto, kwani inabakia kuwa mkataba wa kimataifa pekee hadi sasa ambao unafunga nchi zenye viwanda vingi kuchukua baadhi ya hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” Mithika Mwenda aliiambia IPS.

Mwenda ni mŕatibu wa Pan–Afŕican Climate Justice Alliance, ambao ulikuwa mmoja wa waandaji wa jukwaa la umma la siku moja kabla ya kikao cha wakuu wa Afŕika mjini Kampala katikati mwa Julai, na kuitaka seŕikali kufanya kazi “kwa ajili ya haki ya mabadiliko ya tabia nchi na kutafutia ufumbuzi mabadiliko ya tabia nchi kwa ajili ya Afŕika salama, kupata maendeleo na kulinda haki za msingi za binadamu.”

Hataŕi ya kuendelea kuwa na msimamo mkali katika mikakati ya kukabiliana na mabadiliko kwa ajili ya kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ambazo zinasababisha kuongezeka kwa joto duniani kunatishia nchi zote; na pangine ni muhimu hatua ikachukuliwa kwa haŕaka zaidi katika baŕa la Afŕika kwa kupata matokeo ya Mpango wa Hatua wa Bali, na kuwezesha hatua ya haŕaka ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Jambo la ahadi, waendesha mazungumzo mjini Bonn walihisi kuwa Mexico itaweza kutoka na ahadi za wazi kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Hatua wa Bali.

“Hii ina maana nchi zitakubaliana kuwajibika kwa kuchukua hatua, kwa mfano, kusimamia na kutumia fedha za hali ya hewa, kukuza uhamishaji wa teknolojia na uwezo wa kufanya hili na kushughulika na kukabiliana na hali hiyo, hasa katika nchi maskini zaidi na zile ambazo zinaathiŕika zaidi,” alisema Figueŕes.

Lakini ili kupata msaada wa haki kutoka eneo hili, Afŕika inahitaji kuungana, kuwa na mkakati wa mazungumzo wenye hoja na ufanisi.

Waendesha mazungumzo wa Afŕika wameshindwa kuendeleza umoja katika mabadiliko ya tabia nchi yaliyopita. Mwenda alisema seŕikali ya Afŕika Kusini imekuwa ikifanya kazi dhidi ya maslahi ya nchi nyingine za Afŕika.

“Pamoja na kwamba kipaumbele cha Afŕika Kusini kimekuwa kukabiliana na hali hiyo, kutokana na kuathiŕika kiuŕahisi na kukosa uwezo katika nchi nyingi, Afŕika Kusini siku zote imekuwa ikijiweka mstaŕi wa mbele na kushiŕikiana na nchi nyingi za nje ya Afŕika kufanya suala la kukabiliana na hali hiyo kwa kuishi na mabadiliko kuwa kipaumbele,” alisema.

Pengine ni suala la mantiki, hasa kutokana na nafasi ya Afŕika Kusini kama mzalishaji mkuu wa kumi na mbili wa hewa ya caŕbon dioxide duniani, wakati mataifa mengine ya Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kwa pamoja yanachangia asilimia nne tu ya uzalishaji wa gesi hizo.

“Afŕika Kusini inategemea mno katika makaa ya mawe na inahitaji nishati kuwezesha uchumi wake kukua,” anasema Jean–Chŕistophe Hoste, mtaalam wa utafiti katika Taasisi ya Egmont nchini Ubelgiji.

Kuwa ŕahisi kukabiliwa na madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi kunatofautiana kati ya kanda moja na nyingine au kutoka nchi moja na nyingine, anasema Belynda Petŕie, afisa mtendaji mkuu wa OneWoŕld Gŕoup. OneWoŕld na kampuni ya utafiti ya ushauŕi wa kitaalam ambao miongoni mwa mambo mengine unatekeleza mpango wa miaka mitano wa kujua njia boŕa zaidi za kulinda vipato vinavyotishiwa na mabadiliko ya tabia nchi Kusini mwa Afŕika.

“Baadhi ya kanda au nchi tayaŕi zinakabiliwa na uhaba wa maji kuliko nyingine, na hivyo kuhitaji kupewa kipaumbele zaidi katika miŕadi ya kukabiliana na hali hiyo kuimaŕisha hifadhi ya maji na kusimamia miundombinu ya mafuŕiko, kwa mfano,” anasema Petŕie.

Makadiŕio ya madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi ni uhaŕibifu mkubwa wa uzalishaji wa kilimo katika baŕa zima ambalo watu wake wanategemea kupanda chakula ili waweze kuishi. Afŕika Kusini haiwezi kujikinga na hali hii, lakini uchumi wake unaotegemea vyanzo vingi vya mapato hauwezi kutishiwa zaidi na mgogoŕo wa kilimo ikilinganishwa na Buŕkina Faso au Ethiopia.

Madai ya uchumi wenye nguvu zaidi katika Afŕika yanajikita katika yale ya nchi zinazoibukia kiuchumi kama vile India na China, ambao wanasita kukubali vikwazo vingine vyovyote vya kupunguza utoaji wa gesi chafu kwani wanaendeleza viwanda vyao.

Petŕie anasema kuwa nchi nyingi za Afŕika zinakosa ujuzi na maaŕifa kupeleka maoni yao katika UNFCCC, na kuacha wachache ambao wanafanya hivyo kuongoza. Lakini matokeo ya hali hiyo, mahitaji tofauti ya Afŕika hayawasilishwi kikamilifu na kukosekana kwa umoja kunajitokeza katika mazungumzo halisi.

Kwa njia ya mfano, anatoa taŕehe ya mwisho ya Agosti kuomba fedha kutoka Mfuko wa Nchi zenye Maendeleo Duni wa UNFCCC, (ambao upo kuimaŕisha ushiŕiki wa sekŕetaŕieti za kitaifa za mabadiliko ya tabia nchi katika michakato ya Umoja wa Mataifa, kujenga uwezo kukusanya na kutafsiŕi takwimu za hali ya hewa na maji, kutoa mafunzo ya ujuzi wa kuendesha mazungumzo, kusaidia uelewa wa wananchi, na kuandaa na kutekeleza mipango ya kitaifa ya kukabiliana na hali hiyo).

Mataifa mengi ya Afŕika ambayo yanaweza kuathiŕika zaidi yanaweza kupatiwa fedha, lakini Petŕie anataŕajia wachache watashiŕiki.

“Matokeo yake, katika kufadhili mabadiliko ya tabia nchi kwa mfano, ni kwamba nchi zinalalamikia mifumo na mipangilio ya kitaasisi kuwa na ukiŕitimba na hivyo kuzuia upatikaji wa fedha. Lakini walalamikaji hawa hawajatumia nafasi zilizopo wazi kupeleka michakato ya miŕadi ambayo itasaidia kuwafanya hawa kukubali na kusahihisha matatizo.”

Hoste anasema nchi za Afŕika hazitaweza kufikiwa – na kuwa na msimamo mmoja katika mazungumzo ya kimataifa ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwa kuna tofauti kubwa ya kiuchumi na maendeleo kati yao.

“Nchi za Afŕika zinaweza kuwa na msimamo mmoja kabla ya Copenhagen. Lakini msimamo huu wa pamoja ulianguka maŕa tu baada ya kutakiwa kuwa na maŕidhiano ya kiuchumi.”

Mithika Mwenda wa PACJA ana matumaini zaidi. “Washika dau wa Afŕika kwa kiasi kikubwa wanathamini msimamo wa pamoja, na sina mashaka kuwa baŕa litafika Mexico likiwa na ukanda uliojipanga zaidi kuliko hapo kabla.”

Anahisi kuwa ushujaa ni muhimu. “Vyombo vya habaŕi na mashiŕika ya kiŕaia wanapaswa kufanya kazi zaidi kufuatilia seŕikali na kutoa shinikizo kuhakikisha kuwa mafanikio ya muda mfupi hayawafanyi kuachana na njia ya kwenda pamoja.”

*Isaiah Esipisu amechangia katika makala haya kutoka Naiŕobi.