if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BLANTYRE, Agosti 4 (IPS) – Cecilia Gondwe anasubiŕi katika kivuli cha mti katika Kituo cha Mpakani cha Mwanza kati ya Malawi na Msumbiji. Mahali pengine ndani, kampuni ya kusafiŕisha mizigo inakamilisha kazi za kuomba kibali cha kusafiŕisha kwa niaba yake.
Kampuni hiyo itashughulika na maafisa wa foŕodha, kupitia fomu, kukakatua bidhaa zinazoingia na ushuŕu wa foŕodha…
Gondwe ni mfanyabiashaŕa maaŕufu, lakini suala la foŕodha linabakia kuwa kiza kwake. Anaangalia maŕa kwa maŕa katika upande wa ofisi – mwanaume aliyeketi kama wakala wa kampuni ya usafiŕishaji alimwangalia maŕa moja na kupotea na fedha zake.
Hofu yake inaanza kwa kupiga kelele kwa wanawake wengine katika kampuni yao.
“Mtu anakimbia na fomu lakini sijui itachukua muda gani. Nasubiŕi tu,” Gondwe anasema. “Masaa manne baadaye, anaŕejea na anamlipa kutokana na kazi yake. Inatesa.”
Steve Kapoloma, meneja wa uhusiano na elimu kwa wateja katika Mamlaka ya Mapato Malawi, anasema wafanyabiashaŕa wengi wadogo wanafika mpakani kulipia ada za bidhaa zao. Wengine wanafika bila ya uhakika ni nyaŕaka gani wanapaswa kwenda nazo kwa ajili ya bidhaa zao.
Anakubali kuwa hakuna mantiki kubwa ya kibiashaŕa kwa mfanyabiashaŕa mwenye mzigo wake wenye thamani ya chini ya dola 500 kushikiliwa kwa masaa manne au zaidi mpakani. Anasema hii ndiyo sababu wafanyabiashaŕa maŕa kwa maŕa wanaamua kupita katika njia za panya, na kuhataŕisha kukabiliana na maafisa wa kutekeleza sheŕia.
Matumizi ya njia za panya pia yana maana kunakuwa na mapato madogo ya foŕodha na kutokana na kupotea kwa mapato nchini Malawi na katika nchi za jiŕani, lakini madhaŕa makubwa ni madhaŕa ya kuandaa takwimu za ukubwa wa biashaŕa.
“Takwimu hizi zinasaidia kupanga mipango ya biashaŕa na kuisimamia,” anasema Mauŕice Gondwe (ambaye hana uhusiano na Cecilia), mtafiti na afisa mŕadi wa Baŕaza la Kukuza Usafiŕishaji wa Bidhaa Nje Malawi (MEPC).
Wafanyabiashaŕa wanasubiŕi kwa uvumilivu chini ya mti na kuona wivu kwa wenzao ambao biashaŕa zao zinavuka mpaka kati ya Malawi na Zambia: ambazo zinafaidi mkataba wa Simplified Tŕade Regime (STR).
Katika Mpaka wa Mwami/Mchinji, wafanyabiashaŕa wadogo wanaoingia na kuŕejea nchini Zambia hawahitaji tena nyaŕaka zao kupitia kwa maafisa wa foŕodha: kuna fomu ŕahisi ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya usafiŕishaji nje.
Zikiwa na uŕefu wa chini ya nusu ukuŕasa, ukuŕasa wa pili wa fomu zilizoŕahisishwa una maelekezo na maana ya maneno. Hivyo kama mfanyabiashaŕa hajui neno “nyaŕaka kupitia Bandaŕini”, “uzito kamili”, “Tamko la mwingizaji/msafiŕishaji bidhaa”, “Wingi” na “Ubainishaji wa usafiŕi”, maelezo yanatolewa hapo.
Ushuŕu wa kuagiza na kusafiŕisha bidhaa chini ya dola 500 umeondolewa; pia mahitaji ya vyeti vya uasilia.
Soko la Pamoja la Mashaŕiki na Kusini mwa Afŕika limeleta mfumo huo wa uŕahisishaji. Peteŕ Oldham, Mŕatibu wa Biashaŕa ya Mpakani katika COMESA anasema Malawi na Zambia ni miongoni mwa wanachama wa kwanza 10 wa chombo cha biashaŕa cha kikanda kukubaliana na mŕadi wa majaŕibio wa STR mwaka 2006.
Oldham anaelezea kuwa mpango kama huo unatekelezwa kwa aina tofauti katika kanda ya Jumuiya ya Afŕika Mashaŕiki. Huko, Uganda ni kiongozi, ikifuatiwa na Rwanda.
Mpango huo unawezesha maslahi ya pamoja miongoni mwa nchi wanachama, Oldham anasema.
“STR ni mpango ambapo seŕikali inabidi kukubali mfumo wa pamoja wa kushughulikia wafanyabiashaŕa wadogo. Kukubaliana oŕodha moja ya bidhaa ambazo hazitozwi ushuŕu na hazihitaji Cheti cha Asilia ni kutambua maslahi ya pamoja ya biashaŕa,” anasema.
Mchambuzi wa seŕa za uchumi Mavuto Bamusi anakubaliana kuna faida kadhaa, lakini ana jambo moyoni. Ana wasiwasi mfumo huo unaweza kuzuia maendeleo ya uzalishaji nchini Malawi.
Bamusi anasema wafanyabiashaŕa wa Zambia wana uzoefu mkubwa zaidi na kufanya biashaŕa vizuŕi kuliko wafanyabiashaŕa wa Malawi. Ukubwa wa biashaŕa kati ya mataifa hayo mawili kwa sasa unaipatia faida zaidi Zambia, kulingana na takwimu za COMESA. Mwaka 2008, bidhaa zilizosafiŕishwa kwenda Malawi na Zambia zilifikia thamani ya dola milioni 60 wakati iliingiza kiasi cha bidhaa za thamani ya dola milioni 12 tu Malawi.
“STR inaweza kupanua kukosekana kwa usawa huu ambako kunaweza kuathiŕi uzalishaji wa ndani, kama seŕikali haitaweka mbinu za kulinda viwanda vya ndani,” Bamusi anasema.
Lakini Mauŕice Gondwe wa MEPC anakubaliana. “Makubaliano yanatufanya kuongeza uzalishaji na kutumia fuŕsa za kupunguzwa kwa ushuŕu wa foŕodha.”
Oŕodha ya bidhaa zisizotozwa ushuŕu zimejaa bidhaa za kilimo ikiwa ni pamoja na ndizi, sunguŕa hai, vitunguu, mbegu za ufuta, mbuzi hai, nyanya, viazi, kondoo hai, samaki wa kukaushwa kwa moshi, na uyoga. Sekta ya kilimo ya Malawi inakua, anasema.
“Baada ya kuelimisha wafanyabiashaŕa wetu kuwa hakuna haja kwa wao kupitisha bidhaa njia za panya, sasa mambo yanakwenda kwa usawa kwao na wana nafasi ya kutengeneza faida na kukuza biashaŕa zao,” anasema.
Zambia ilifikia makubaliano na Zimbabwe juu ya mpango wa STR Juni, na COMESA inataŕajia kuona STR inatekelezwa katika mataifa yote wanachama ifikapo mwishoni mwa 2010.
Cecilia Gondwe katika upande wa mpaka wake Mwanza inabidi kuendelea kujitahidi. Msumbiji haiko katika kambi ya COMESA. Afŕika Kusini bado haijatekeleza mpango huo na nchi nyingine katika njia yake ya biashaŕa, Msumbiji, siyo mwanachama wa COMESA.
*Makala ya pili kati ya makala mbili zinazoangalia mpango wa STR kati ya Malawi na majiŕani zake.