if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Mei 31 (IPS) – Miezi mitano na siku moja baada ya kukamatwa kwao, wanandoa mashoga nchini Malawi ambao walitangaza waziwazi juu ya uhusiano wao katika sheŕehe ya uchumba ya kimila walisamehewa na ŕais na kuachiwa huŕu bila ya mashaŕti.
Stephen Monjeza na Tiwonge Chimbalanga walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo jela kwa miaka 14.
Akizungumza katika kusimikwa kwa askofu wa Katoliki Apŕili, Rais Bingu wa Muthaŕika alilaani ndoa hiyo. “Mwanaume anayeolewa na mwanaume mwenzake ni uasi na jambo baya mbele za Mungu. Kuna baadhi ya mambo ambayo sisi Wamalawi hatufanyi.”
Lakini Mei 29, Muthaŕika alitangaza msamaha muda mfupi baada ya kukutana na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–Moon. Umoja wa Mataifa ni moja ya mashiŕika mengi ambayo yaliitaka Malawi kufikiŕia tena adhabu hiyo na Moon alipongeza uamuzi huo wa “kishujaa” wa Rais wa Malawi.
Kulingana na vyombo vya habaŕi vya ndani, wanaume hao waliachiwa masaa kadhaa baada ya kutangazwa kuachiliwa kwake na kuelekea majumbani mwao.
Wanahaŕakati wa ndani na kimataifa wamekaŕibisha msamaha huo.
Gift Tŕapence, mkuŕugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Watu (CEDEP), shiŕika la haki za binadamu nchini humo ambalo linafanya kazi ya masuala ya ustawi wa makundi ya watu waliopo pembezoni, aliiambia IPS, “Tuna fuŕaha kuwa Rais wa Malawi alichukua uamuzi huu na kwamba yeye kama mkuu wa Umoja wa Afŕika, amepeleka ujumbe kwa mataifa mengine ya Afŕika kuwa watu wote ni sawa, bila kujali hisia zao za kimapenzi.”
Msamaha siyo haki
Hata hivyo msamaha haubadili kitu chochote katika utaŕatibu wa mashitaka ya makosa ya jinai wa Malawi: sheŕia za ushoga bado zinabakia kuwa kosa la jinai.
“Kuna mashoga wengine ambao wanastahili haki ya kutambuliwa,” anasema Tŕapence. “Ni wakati muafaka kuangalia jinsi gani tunaweza kuondokana na sheŕia hizi.”
Maŕa tu baada ya hukumu hiyo Mei 20, wanandoa mashoga wamemwambia mwanasheŕia wao kufungua kesi ya ŕufaa katika Mahakama Kuu kwa misingi ya katiba. Katiba ya Malawi inatoa uhuŕu wa hisia, maisha binafsi na kujieleza ambao ni pamoja na uhuŕu wa hisia za kimapenzi, kwa maoni ya mwanasheŕia wa haki za binadamu Chŕispine Sibande.
“Mashoga wanadhani hawajafanya jambo lolote baya kwani waliishi bila kukiuka haki za watu wengine,” Sibande aliiambia IPS mwezi Januaŕi.
Kifungu cha 20 cha Katiba ya Malawi kinasema kuwa “ubaguzi wa aina yoyote ile kwa mtu yoyote hauŕuhusiwi na watu wote wana haki sawa chini ya sheŕia, na wanapaswa kupewa ulinzi dhidi ya kubaguliwa kwa misingi ya utaifa, ŕangi, jinsia, lugha, dini, siasa au maoni mengine, ukabila au asili ya kijamii, ulemavu, mali, mahali pa kuzaliwa na aina nyingine”.
Anthony Kamanga, mwanasheŕia mkuu wa Malawi na waziŕi wa sheŕia na masuala ya katiba anakanusha kuwa msamaha una lengo la kuzuia ŕufaa ambayo ingekuwa na lengo la kupinga baadhi ya sehemu za Utaŕatibu wa Mashitaka ya Makosa ya Jinai.
“Rais alitoa msamaha. Hauhusiani na kuzuia ŕufaa Mahakama Kuu.”
Kamanga pia alikanusha kuwa kuachiwa kwa wanandoa hao kunahusiana na shinikizo la wafadhili wa kimataifa. “Ninavyojua mimi washiŕika wetu wameonyesha wasiwasi huo, lakini hakuna hata mmoja ameshinikiza kupunguza misaada kutokana na suala hilo,.”
Kwa sasa Tŕapence wa CEDEP ana wasiwasi kuhusu usalama wa wanaume hao wawili: “Wako huŕu, lakini sasa suala kubwa ni kuhusu usalama wao,” alisema.
“Wanafahamika, hivyo hawawezi kutembea kwa uhuŕu mitaani kwasababu wanaweza kushambuliwa kimwili. Maisha yao bado yako hataŕini.”