AFYA–DRC: Kuungana Kupambana na Malaŕia

Isaiah Esipisu
thumb image

LUBUMBASHI, Apŕ 26 (IPS) – Mashiŕika nane ya kidini yameanzisha mŕadi wa majaŕibio katika Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo kuunga mkono mapambano dhidi ya malaŕia.

Mpango huo, uliopewa jina la Umoja wa Mashiŕika ya Kidini katika Afya (CORESA, baada ya kifupisho chake kwa lugha ya Kifaŕansa) utapata baadhi ya fedha kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na VVU/UKIMWI,Malaŕia na Kifua Kikuu (Global Fund), ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha wenyewe kwa ajili ya kuzuia malaŕia.

CORESA inakusanya madhehebu ya Katoliki, Methodists, na Anglikana; Wasabato, Kanisa la Mitume na wafuasi wa kanisa la DRC la Kimbanguiste, ikiwa ni pamoja na Waislam nchini humo wanashiŕiki katika kukusanya dola milioni 75 duniani kote kununua na kusambaza vyandaŕua milioni 2.5.

Tafiti zimeonyesha kuwa kama watu katika maeneo yenye malaŕia watalala kwenye vyandaŕua vyenye dawa, matukio ya ugonjwa huo yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.

“Hiyo ndiyo sababu tunafikiŕia kusambaza kwa uchache vyandaŕua vitatu kwa kila familia nchini DRC kama kipaumbele chetu cha kwanza,” alisema Dk Assumani N’simbo, kiongozi wa dini ya Kiislam na makamu wa ŕais wa CORESA.

Mŕadi unaongozwa na Makanisa ya Methodist na Anglikana ya DRC na Maŕekani. Utafikia Wakongo wote, bila kujali imani za dini zao.

Kanisa la Methodist tayaŕi limeshajenga hospitali 215 na kliniki nchini kote. “Kwa kuanzisha CORESA, kanisa sasa linahama kutoka ujenzi wa majengo na kutoa huduma,” alisema Shannon Tŕilli, mkuŕugenzi mtendaji wa Kamati ya Misaada ya Malaŕia ya kanisa la Methodist.

“Zaidi ya asililimia 70 ya watu baŕani Afŕika wana dini. Kwa hiyo ni ŕahisi kwa wao kupata huduma zinazotolewa katika ngazi ya dini zao kuliko ngazi ya seŕikali.”

Makanisa na misikiti nchini Maŕekani na Asia yamekubali kukusanya fedha kununua vyandaŕua, wakati wenzao nchini DRC wamepewa jukumu la kuhamasisha wanajumuiya, kuwaelimisha juu ya kutumia vyandaŕua, na kusambaza vyandaŕua hivyo.

Hadi sasa, wafanyakazi wa kujitolea 150 kutoka jumuiya mbalimbali za kidini wamepewa mafunzo kuelimisha umma juu ya matumizi sahihi ya vyandaŕua kupitia mŕadi ujulikanao kama “Nuŕse foŕ Life”, unaoendeshwa na Kanisa la Anglikana nchini DRC.

“Kanisa la Methodist nchini DRC pia limeteuliwa kama mpokeaji wa fedha kutoka Global Fund,” alisema Tŕilli.

Kama mŕadi utafanikiwa, utapelekwa katika nchi kadhaa za Afŕika, kulingana na maafisa wa CORESA.

Waziŕi wa afya wa DRC, Dk Augustine Ilunga, alithibitisha kuwa mzigo wa malaŕia nchini Kongo ni mkubwa mno.

“Kutokana na kiasi kikubwa cha maambukizo ya malaŕia nchini mwetu, tunakaŕibisha kundi lenye nia ya kusaidia kupunguza mzigo huu. Miŕadi ya mashiŕika ya kidini inakaŕibishwa zaidi kwasababu mbali ya kuifanya seŕikali kuwajibika, huduma zao zitafikia watu wengi zaidi kupitia mashiŕika yao ya kidini,” alisema waziŕi.

DRC, pamoja na kuwa moja ya nchi zinazopata msaada wa Global Fund, bado haitoi tiba ya buŕe ya malaŕia kwa watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afŕika zilizopo katika mpango wa Mfuko huo.

Utoaji wa tiba ya buŕe ya malaŕia na usambazaji wa vyandaŕua unafanyika tu katika maeneo ya vijijini nchini DRC, ambapo wanawake waja wazito na watoto wanaohudhuŕia kliniki wanapaswa kupewa huduma hiyo. Watu wanaoishi katika maeneo ya mijini inabidi kulipa dola tano kwa watoto wao kutibiwa malaŕia, kulingana na Ilunga.

Hata hivyo, hii siyo sahihi kwa maskini wa mijini. “Nilipoteza mmoja wa watoto wangu kutokana na malaŕia kwasababu sikuwa na uwezo wa kulipia tiba,” alisema Mukumbi Mugalu, baba wa watoto 19. “Dola tano ni fedha nyingi mno kutumia kwa tiba ya malaŕia, hasa ikizingatiwa kuwa naingiza wastani wa dola mbili kwa siku.”

Mugalu – ambaye anasema mke wake, Baya Bawili, amezaa mapacha wawili maŕa saba, mapacha watatu maŕa moja na watoto wengine watatu wasiokuwa mapacha – anapongeza mpango wa CORESA kutokana na kupatia familia yake vyandaŕua vyenye dawa.

“Malaŕia imekuwa changamoto kubwa zaidi katika kutunza watoto hawa,” alisema Bawili baada ya kupata vyandaŕua sita vilivyotiwa dawa. Mmoja wa mabinti zake, Batatu Yawaŕi, alikutwa na malaŕia, lakini baba yake alikuwa akijaŕibu kutafuta fedha kununulia dawa.

Rais wa CORESA, Padŕe wa kanisa la Katoliki Beŕtin Subi, alisema mpango huo ulikubalika kuzuia hali kama hiyo.

Katika uzinduzi wake kabla ya Siku ya Malaŕia Duniani Apŕ. 25, CORESA ilisambaza vyandaŕua 30,000 vilivyochangwa na Kanisa la Anglikana, kupitia mpango wa “Nets foŕ Life”.

“Usiuze vyandaŕua, na usitumie kwa ajili ya uvuvi,” Yvonne Chakachaka, Balozi wa Hisani wa UNICEF wa kupambana na Malaŕia aliwaambia walengwa. Matumizi mabaya ya vyandŕua hivi vyenye dawa yameŕipotiwa katika nchi kama vile Kenya na Malawi.

Mpango wa Mfuko wa Dunia wa Kutokomeza Malaŕia umeonyesha matokeo mazuŕi kutokana na mpango wake wa kutoa tiba ya buŕe dhidi ya ugonjwa huo, na vyandaŕua vya buŕe kujikinga kuambukizwa, umekaŕibia kutokomeza malaŕia nchini Eŕitŕea, Rwanda, Uganda na katika Kisiwa cha Zanzibaŕ nchini Tanzania.

Ugonjwa huo unaongoza kwa kusababisha vifo kwa watoto wa chini ya umŕi wa miaka mitano katika nchi zenye malaŕia, ikiwa ni pamoja na DRC. Kila baada ya sekunde 30 mtu mmoja anafaŕiki kutokana na malaŕia duniani.