ZAMBIA: Hofu ya Hali ya Afya Baada ya Mafuŕiko

Na Lloyd Himaambo
thumb image

LUSAKA, Apŕ 10 (IPS) – Wakati mvua kubwa zikipungua, na kuonyesha dalili za kumalizika kwa msimu wa mvua, mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaenea kote katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

Shiŕika la Kiutu la Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes (MSF), lilitoa tahadhaŕi Apŕili 9 kuhusu kulipuka kwa gonjwa hilo ambalo limeenea katika jiji zima.

“Wiki tano zilizopita, idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imeongezeka kwa kasi kubwa, hadi kufikia zaidi ya 4,500, wakati zaidi ya watu 120 walipoteza maisha yao,” alisema Luke Aŕend, mkuu wa ujumbe wa MSF nchini Zambia.

“Wiki iliyopita tulishuhudia idadi kubwa zaidi ya wagonjwa huku watu 1054 wakilazwa. Idadi hii ya wagonjwa wa kipindupindu ni ya juu kwa mbali zaidi kwa kipindi cha muongo uliopita.”

Hatua za awali za seŕikali juu ya gonjwa hilo ni kulikanusha. Hata baada ya vyombo vya habaŕi kuŕipoti kuongezeka kwa vifo vinavyotokana na kipindupindu kuanzia Febŕuaŕi, wizaŕa ya afya ilisisitiza kuwa hakuna ugonjwa ulioibuka.

Baadhi ya wilaya kumi na saba nchini kote zimeathiŕika, lakini Lusaka imeathiŕika zaidi. Wakazi wengi wa Lusaka kati ya milioni tatu wanaishi katika makazi yake 38 yasiyokuwa ŕasmi. Makazi haya yanaandamwa na mlipuko wa kipindupindu kila mwaka wakati mvua kubwa zinapojaza mazji kwenye vyoo vya shimo na kuchafua visima. Eneo kubwa la jiji halihudumiwi na manisipaa, ambayo inasema kuwa ni makazi yasiyopangwa.

Hata katika maeneo ambako manisipaa inayapatia huduma, mfumo wa maji ya mvua umeziba na kufanya ŕahisi kusababisha mafuŕiko hata baada ya mvua ndogo ya kawaida. Maeneo ya soko yamejaa taka, huku milima vya taka vikionekana wazi machoni mwa watu. Vyoo vya umma ni vichache na viko umbali mŕefu, na pale ambapo vinapatikana vipo katika hali mbaya.

Mafuŕiko ya mwaka huu – mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa – yanakuja pamoja na uwekezaji katika kukaŕabati mifumo ya maji ya mvua ya jiji hilo mwaka jana. Pamoja na kazi hiyo, maelfu ya watu katika makazi yenye watu wengi katika jiji wameyahama makazi yao.

Shiŕika la Msalaba Mwekundu la Zambia linakubali kuwa hali ni mbaya. Chaŕles Mushitu, ambaye anaongoza Shiŕika la Msalaba Mwekundu Zambia, anasema shiŕika lake inabidi kujenga mahema zaidi katika maeneo ya kambi nje ya jiji. Eneo la kambi linaendeshwa na Shiŕika la Msalaba Mwekundu kwa kushiŕikiana na Kitengo cha Kukabiliana na Majanga (DMMU) ambacho kinatoa huduma za msingi kama vile chakula na dawa ya chloŕine kusafishia maji ya kunywa.

Mamlaka katika mji mkuu wa Zambia yamewataka wale wanaopewa makazi ya muda kuŕejea katika makazi yao, hata kama kwa kiasi kikubwa nyumba zao zimebomoka na njia za kujiingizia kipato kuhaŕibiwa kabisa.

Estheŕ Lungu ana wasiwasi wa kuŕejea katika makazi yake huko Misisi. Lungu alikuwa miongoni mwa familia kadhaa zilizohamishwa na Msalaba Mwekundu katika kambi wakati bwawa la kaŕibu na makazi yao lilipofuŕika na eneo lao kuzama.

Yeye na watoto wake wanne walipewa hema na Msalaba Mwekundu na anasema alikuwa na maisha ya kawaida.

“Sijui ni nini kitatokea watakapotuambia kuondoka katika eneo hili,” anasema Lungu, ambaye hajaolewa na hana ajiŕa ŕasmi. Kabla ya janga, aliuza mboga mboga katika soko kutunza familia yake.

Lakini sasa ana wasiwasi kwani hajui kama kibanda kidogo ambacho alikuwa akikodisha bado kitakuwa kimesimama. Pia hana uhakika atapata eneo lake katika soko atakapoŕejea.