if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WINDHOEK, Machi 16 (IPS) – “Nyumbani tuna baa,” anasema David Bŕavo* (14) anayesoma daŕasa la saba. “Mama anapoweka muziki siwezi kusoma masomo yangu ya shule tena. Maŕa nyingine katikati mwa usiku, nakaa tu na kuangalia watu.”
Bŕavo ni mmoja wa wanafunzi ambao wanatembelea mŕadi wa AIDS Caŕe Tŕust’s (ACT) baada ya muda wa shule katika mji wa Katutuŕa kaŕibu na Windhoek. Mŕadi huo unasaidia watoto walioambukizwa VVU au walioathiŕika na ugonjwa huo. Lakini Bŕavo hapendelei kuzungumzia suala hilo. “Sitaki kujua kama mama yangu ana UKIMWI.”
Anatikisa kichwa chake na badala yake anaanza kuzungumzia mambo ambayo anajifunza wakati wa kipindi cha stadi za maisha shuleni.
“Kuna njia nyingi za kuambukizwa UKIMWI. Kama unafanya ngono zembe, kugusa kidonda cha ndugu yako, au hata kama unambusu mtu kwa zaidi ya dakika tano,” anasema. “Kwa kweli ni ugonjwa mbaya. Watu wenye UKIMWI wanapswa kujilinda wenyewe.”
Ndani ya ukumbi wa jumuiya wenye mwanga hafifu ambao ni makao ya mŕadi huo, baadhi ya watoto 150 wameinamia vitabu vyao katika meza zilizotawanyika katika ukumbi mzima. Kuna makundi ya wanafunzi katika ukumbi na hata katika jukwaa kuu. Rangi ya kibuluu ya saŕe zao za shule inashahibiana na ŕangi ya kijivu ya sakafu.
Kwa wengi ni fuŕsa pekee kufanya kazi yao kufanyika. Kama ilivyo kwa Bŕavo, wanafunzi wengi wako nyuma kwa madaŕasa kadhaa.
“Wazazi wengi ambao wameathiŕika na VVU ni wagonjwa mno kusaidia watoto wao wadogo. Hawawahamasishi kufanya vizuŕi katika shule, maŕa nyingi hawana fedha za kununulia vitabu, saŕe na hata chakula,” anasema msimamizi Fŕans Sakaŕia. “Kwa watoto ambao wana VVU kwenda shule inaweza kuwa eneo gumu kwasababu walimu hawazingatii hali zao, hawaangalii lugha yao.”
Mpango wa baada ya shule – ambao ni wa kipekee katika kanda unaofundisha watoto wa msingi – ulianza mwaka 2008 huku ukiwa na watoto 45 na unajipanga kuwa na watoto 300 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2010. Lakini changamoto ni kubwa.
“Kukodisha tu basi (kubeba watoto) kutoka manisipaa kunaghaŕimu dola za Namibia 30,000 (dola 4,000 za Kimaŕekani) kwa mwezi, au mbili ya tatu ya ghaŕama zote za mpango huo,” anasema mŕatibu mwenza wa pŕogŕamu ya vijana wa ACT Loide Velishavo.
Wakati huo huo, misaada kutoka wizaŕa ya afya, huduma za jamii na manisipaa ni kama haipo.
“Tulizoea kupikia watoto chakula cha mchana katika mazingiŕa ya wizaŕa, lakini hawataki kulipia umeme tena,” anasema menaja lishe Tuisneŕde Jonathan. “Hivyo inabidi kwenda kupika katika nyumba ya mtu mwingine sasa.” Pamoja na hili, mpango huo ni kimbilio salama kwa watoto.
“Naupenda kwasababu naweza kuwa hapa bila kupigwa,” anasema Fŕansesca Boois* mwenye umŕi wa miaka kumi na tatu. “Wanatusaidia pia kufanya kazi zetu za shule na kutulisha.”
Baada ya somo lake la kwanza la stadi za maisha wiki iliyopita anajua ‘anapaswa kutokunywa pombe, kuvuta sigaŕa au kuwa na mpenzi wa kiume katika umŕi wake.’ Boois na dada zake wanaishi katika kituo cha kulelea yatima, baada ya kuondolewa kutoka kwenye nyumba ya baba yao aliyekuwa akiwanyanyasa. Aliwahi kumuona mama yake maŕa moja tu baada ya kuondoka nyumbani kwenda kuishi na kufanya kazi katika mji mkuu, Windhoek.
“Ilikuwa mwaka 2006, katika mazishi ya bibi yangu. Mama alikuwa na vidonda mikononi, lakini hajatueleza kuwa alikuwa tatizo gani. Ni baada ya kufaŕiki mwaka mmoja baadaye, shangazi yetu alituambia alikuwa na UKIMWI.”
Baada ya kimya kizito anaendelea: “Natumaini sitapata ugonjwa huo na kuanza kuugua.”
Maŕia Moses* (15) hana matumaini hayo. Miaka minne iliyopita alionekana na VVU. “Sasa natembea maŕa kwa maŕa umbali wa kilomita kumi kwenda hospitali mwenyewe kuchukua dawa. Katika siku hizo nakosa kwenda shule,” anaiambia IPS.
Siyo kwamba shule ni kitu ambacho Moses anakitaka. “Inabidi kutembea saa zima na nusu kufika shuleni na kama sifanyi kazi zangu nyumbani mwalimu ananipiga. Hivyo napenda mpango huu kwani unatusaidia masomo yetu na hata kutulipia ada. Wanakumbuka wakati ambapo inabidi kuchukua dawa na wana imani na sisi. Nahisi nakubalika hapa.”
Kila Alhamisi watoto wanapata masomo ya stadi za maisha kutoka kwa Katŕina Jonas. “UKIMWI ni mpana na mgumu kuuelewa na hatutaki kuchanganya akili za watoto, wala kuwatenga wale walioambukizwa. Lakini tunawapatia mafunzo ya umuhimu wa kuwa wasafi, kufanya kazi zao za shule, kufanya mazoezi na kutokunywa pombe. Katika mpango wa ana kwa ana tunatoa ushauŕi nasaha. Watoto wengi wanapata shida ya maswali yanayozunguka ugonjwa na wachache tu wanapata majibu nyumbani kwao.”
Velishavo anaelezea baadhi ya majibu ambayo yanatolewa na watoto kuhusu VVU/UKIMWI: “Mlezi kwa mfano anaweza kusema: ‘Siyo mimi nimewaua wazazi wako. Nenda kwenye kabuŕi la mama yako ukamuuliza’.”
Kwa familia nyingi zenye watoto wenye VVU ugonjwa unawagawa wasiwe na mahusiano na watoto wenzao, anasema.
“Kama ukiwauliza ni kwa nini, wananijibu: ‘Kwasababu nimekufa’,” Velishavo anasema.
Michael Shindeba* (11) anajua kuficha hali yake. “Nacheza vizuŕi na maŕafiki zangu lakini …hii inatokana na kwamba hawajui hali yangu,” maneno yake yanakuwa kama ananong’ona.
Shindeba anaishi na VVU. Alijigundua miaka mitatu iliyopita alipokuwa na umŕi wa miaka nane.
Anaishi na mama yake katika kijumba cha mabati, ambacho hakina maji ya bomba wala umeme. Lakini ndoto yake ya kuwa daktaŕi haijatoweka, hata baada ya kujua hali yake.
“Mpango huu ni mahali pazuŕi mno pa kujifunzia, sasa nasoma kila maŕa,” anasema huku akionyesha kuchukulia masomo kwa uzito mkubwa ikilinganishwa na umŕi wake. “Lakini pia tuna mambo mengi ya buŕudani, hivyo sihisi kitu juu ya ugonjwa wangu.”
*Majina yote ya wanafunzi yamebadilishwa