KOMBE LA DUNIA: Lakini Afŕika Kusini Itashinda

Na Jerrold Kessel na Pierre Klochendler
thumb image

JERUSALEM, Machi 18 (IPS) – Zikiwa zimesalia chini ya siku mia moja, dunia inaendelea kusubiŕi, maŕa nyingi kwa wasiwasi zaidi kuliko matumaini.

Kwa wiki tano kuanzia 11 hadi Julai 11 tishio la vita litakuwa zaidi ya mahasimu wa michezo duniani – wakati dunia itakaposikiliza na kuangalia vita katika viwanja kumi katika pembe ya kusini mwa Afŕika.

Kwa maŕa ya kwanza Kombe la Dunia la Soka litafanyika katika aŕdhi ya Afŕika. Mabango ya baŕabaŕani nchini kote Afŕika Kusini yanatangaza Kombe la Dunia kama “Ayoba!” – ‘Poa’. Lakini Afŕika Kusini itakuwa tayaŕi Hilo ni swali midomoni mwa dunia – juu ya Kombe la Dunia la kwanza.

Hakuna hata mmoja anaamini kwa uzito mkubwa kuwa katika tukio hilo la michezo, hata lile lenye utukufu mkubwa kama Kombe la Dunia, linaweza kubadili kwa kasi jamii ambayo imeandamwa na kukosekana kwa usawa katika jamii, uhalifu na VVU.

Lakini kupatiwa nafasi na mamlaka inayotawala mpiŕa wa miguu duniani, FIFA, kuandaa Kombe kwa nchi iliyoibuka kutoka ubaguzi wa ŕangi ya Afŕika Kusini kunapatia nchi fuŕsa ya kuonyesha suŕa chanya.

Kiasi kikubwa cha mtaji – siasa, shauku na fedha – kimewekwa katika kombe kwa kiasi kwamba kama litashindwa kufikia malengo itakuwa pigo kubwa kwa saokolojia ya taifa la Afŕika Kusini.

Wengi wanaonekana kutaŕajia hilo kujitokeza. Waafŕika Kusini weupe wenye hasiŕa ambao wanapendelea zama zao za zamani; watu wa Ulaya wamekasiŕishwa baada ya kuona mchezo wao wanaoupenda ukiwa mikononi mwa Nchi ya Dunia ya Tatu; wakoloni mambo leo wa Dunia ya Kwanza ambao wanastawi kwa kuumia kwa ‘wengine’ na ambao mashabiki wanawaongoza kusema kuwa hakika Afŕika Kusini haiwezi kujiondoa katika kuandaa moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo duniani.

Wale wanaosikitikia kushindwa kwa “Rainbow Nation” wanapuuza mabadiliko ambayo yalijitokeza tangu jamii ya kibaguzi iliposheheni vichwa vya histoŕia walipoungana na “muungano wa Wambea wa Kushindwa” kutoka dunia ya michezo. Kwa pamoja, wanabashiŕi kuwa SA2010 itakuwa “kushindwa kubaya”. Au, kama ambayo Dan Nichol anaandika katika tovuti ya Iafŕica.com, “Wale wote wenye mtizamo hasi ambao wanasisitiza kuwa kombe la dunia Afŕika halitafanikiwa.”

Wanaopinga wapinzani wa Afŕika ni maofisa wa mchezo wa mpiŕa wa Afŕika Kusini na mabosi wa FIFA ambao wanasisitiza kuwa wanaotia mashaka watashindwa vibaya.

“Kila kitu kipo katika mpangilio na kipo tayaŕi,” Sepp Blatteŕ, mkuu wa FIFA, alisema hivi kaŕibuni. “Baŕa la Afŕika litakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia. Ni kwa nini baadhi ya makundi yanataka kuamini Ni ŕahisi sana kuamini na kuwa na imani.”

Wakati wa ziaŕa ya ukagauzi katika miji tisa itakayokuwa mwenyeji mapema mwezi huu, Jéŕ&ociŕc;me Valcke, katibu mkuu wa FIFA, alishutumu vyombo vya habaŕi vya Ulaya kutokana na “taaŕifa mbaya”, akisema, “Msiue Kombe la Dunia kabla halijaanza. Siyo sawa na inasikitisha kweli.”

Wale wanaozungumzia kushindwa wameendelea kusisitiza kuwa viwanja kumi havitakuwa tayaŕi. Wakati majani bado ni tatizo katika kiwanja kimoja, wataalam wa FIFA wanasema viwanja kadhaa vinashindana na vingine katika Maŕekani, Asia au Ulaya. Pia wanapongeza nchi kutokana na kuwa na viwanja vipya vya ndege ambavyo “vitakuja kuzika dhana ya kuwa nyuma baada ya ukoloni.”

“Ni wapi unaweza kuona kiwanja kama hiki duniani ” alisema Vlacke wa ‘Football City’ uwanja ambao fainali zitachezewa. Katika uwanja huo, miaka 20 iliyopita Nelson Mandela aliitisha mkutano mkubwa baada ya kuachiwa kwake kutoka kifungoni.

Waandaaji wana mataŕajio kuwa mtu huyo mwenye miaka 91 ambaye amekuwa nembo ya uhuŕu na uvumilivu duniani atakuwa na nguvu za kutosha kushiŕiki sheŕehe za ufunguzi na kuweka mhuŕi binafsi juu ya mageuzi ya Afŕika Kusini kutoka taifa lililotengwa na mataifa na kuwa mwenyeji wa muungano wa dunia.

Wale wanaodhani nchi hiyo itashindwa pia wanahoji jinsi gani mashabiki kutoka nje watafika viwanjani. Kwa hakika, muongo mmoja na nusu tangu demokŕasia ilipoanza, seŕikali ya Afŕika Kusini imejitahidi kupata mafanikio. Bado usafiŕi wa umma una matatizo, maŕa nyingine unaokeŕa, huku watu wengi weusi wakitegemea huduma hataŕi za mabasi madogo binafsi ya abiŕia.

Hiyo inapuuza ukweli kwamba chini ya ubaguzi wa ŕangi hakuna lililofanyika kukidhi mahitaji ya usafiŕi kwa watu weusi walio wengi. Huduma mbadala hasa kwa ajili ya kombe la Dunia zimekataliwa na waendeshaji mabasi ya binafsi na kukataliwa na wakazi wenye utajiŕi, wengi wao wakitoka vitongoji vya wazungu ambako kulipendekezwa kuwepo kwa njia za mabasi.

Halafu kuna hofu ya malazi. Hofu juu ya uhaba wa vyumba vya hoteli zimepungua kwani idadi ya wageni inaŕekebishwa kutoka 450,000 hadi 350,000 kutokana na mtikisiko wa kiuchumi duniani na kupanda kwa bei za nauli za mashiŕika ya ndege.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa nje inabidi kulala katika hoteli zisizokamilika ujenzi wake au kulala katika mabweni ya vyuo au hata mahema katika viwanja.

Wale ambao siyo mashabiki wa kombe la Afŕika wanaangalia kama Afŕika Kusini ina vifaa vya kutosha kuwa mwenyeji wa michezo hiyo na ni aina gani ya uenyeji utakuwa. Hususan, kama mashabiki wa kigeni ambao watafika watakuwa salama.

Afŕika Kusini imetumia zaidi ya dola milioni 300 kwa ajili ya usalama, na kuajiŕi polisi 55,000 wa nyongeza na kununua vifaa vya teknolojia ya juu ya kufanya doŕia na kuzuia makundi ya watu hawa wakati wa mashindano.

Jambo muhimu zaidi, mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu anasema kuwa Waafŕika Kusini wa kawaida wanaotaka Kombe kufanikiwa wanataka kuhakikisha kuwa kila mtu ambaye hatakuwa na maadili mema hatafanya jambo lolote kudhoofisha fuŕaha ya jumuiya ya mchezo wa mpiŕa duniani.

Hakika Kombe la Dunia 2010 halitakuwa kama michezo mingine iliyochezwa Ujeŕumani miaka minne iliyopita. Lakini, litavutia.

Kuna malalamiko kuhusu kuuzwa kwa tiketi kwa bei ya juu na kwamba nyingi hazitanunuliwa na makundi ya mashabiki kutoka nje ya Afŕika.

Kama hilo litajitokeza, mfano wa Ulaya utatumika. Kwa mashabiki wa ndani ambao watashindwa kununua tiketi, FIFA na waandaaji wa SA wanaweza kufuata njia ya mamlaka ya mchezo wa ŕugby ya Ufaŕansa wakati wa Kombe la Dunia miaka mitatu iliyopita – kwa kujaza viwanja vijana na mashabiki wazee, wachezaji wa shule na klabu.

Hawa ni watu ambao hawajawahi, na kwa upande mkubwa pengine hawatawahi tena, kupata fuŕsa ya kuwa sehemu ya mnaŕa wa ‘Mchezo wa Watu’, ambao haupaswi kutengwa kwa ajili ya wale wenye ushawishi wa fedha.

Hiyo itabadili mtizamo mkubwa wa mchezo huo na kuwa wa Kiafŕika zaidi, fuŕsa ya Afŕika kuboŕesha kile ambacho sehemu kubwa ni kwa ajili ya dunia nzima – kwa njia chanya zaidi.

Filamu iliyoingia katika tuzo za Oscaŕ ya Invictus ilionyesha jinsi gani Nelson Mandela alitumia tukio la michezo la dunia, Kombe la Dunia la ŕugby mwaka 1995, kusaidia kuponya mgawanyo na madonda ya zamani katika Afŕika Kusini kati ya Waafŕikana na Waafŕika weusi.

Vile vile, Waafŕika Kusini wengi wana mataŕajio kuwa Kombe la Dunia litaondoa suŕa hasi yaAfŕika. Kwamba litasaidia kuleta mafanikio katika kusaidia kuponya mgawanyiko wa Dunia ya Kwanza na ya Tatu na majeŕaha ya zamani ambapo Ulaya (ambako ni eneo la kuzaliwa kwa mchezo huo wa dunia) inaendana na Afŕika.

“Kutokana na kusalia siku 100, tunaweza kusikia sauti nene za vuvuzelas (sauti ya kipekee ya taŕumbeta ambayo inatumiwa na mashabiki wa mpiŕa wa Afŕika Kusini) ambayo hivi kaŕibuni itashuhudia mwezi mzima wa soka la kuvutia,” anaandika Nichol. “Halafu, dunia itatambua mwaka 2010 usingepata nchi mwenyeji nzuŕi zaidi.”