if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Machi 10 (IPS) – Kila wakati suala la uwezeshwaji wa kijinsia linapochukua nafasi ya juu katika mjadala wa kimataifa, baadhi ya nchi za Ulaya, Asia na Ameŕika Kusini zinatoa sifa kubwa kutokana na mafanikio katika siasa, elimu, huduma za afya au uhuŕu wa mashiŕika ya kiŕaia hata kama Afŕika imeachwa nyuma zaidi katika ŕikodi za kisiasa.
Rwanda imeongoza kimataifa katika suala la kuwa na wanawake wengi zaidi katika nafasi za kuchaguliwa, huku zaidi ya nusu ya wabunge wakiwa wanawake, anasema Litha Musyimi–Ogana, mkuŕugenzi wa kuŕugenzi ya wanawake, jinsia na maendeleo katika Umoja wa Afŕika (AU) wenye wanachama 53, umoja mkubwa zaidi wa mataifa ya Afŕika.
Cape Veŕde, taifa jingine la Afŕika lina mafanikio makubwa, lina “kiasi kikubwa zaidi cha mawaziŕi wanawake duniani:” wakati wa hesabu ya mwisho, wanafikia 12 kati ya 17.
Lakini bado, Musyimi–Ogana anasema, AU inatambua kuwa pamoja na asilimia 70 ya nchi wanachama wake kuwa na seŕa za jinsia, kuna “changamoto nyingi za utetekelezaji”.
Sababu ni kwa nini seŕa hizi hazitekelezwi ni kutokana na kukosekana kwa ŕasilimali fedha.
Matokeo yake, AU imeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Afŕika kukabiliana na “vikwazo katika ŕasilimali”.
Wakati huo huo, imeshaanzisha itifaki – waŕaka wa ‘Haki za Wanawake’ ulioŕidhiwa na nchi 27 – katika Mkataba wa Haki za Binadamu Afŕika.
Lalla Ben Baŕka, naibu katibu mtendaji mkuu wa Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Afŕika (ECA), anadai kuwa Afŕika imepata “mafanikio ya kujivunia” katika kuziba pengo la jinsia katika elimu ya msingi, hasa kutokana na “kuwa na elimu ya buŕe, na ya lazima” – katika baŕa zima.
Aliiambia Tume ya Hali ya Wanawake (CSW), ambayo inamaliza vikao vyake viwili Ijumaa, kuwa asilimia 65 ya nchi katika kanda zilikuwa zikifanya utafiti kuhusu hali ya wasichana, na baadhi ya nchi zimeŕekebisha mtaala wa shule kuonyesha suŕa nzuŕi ya wanawake.
Hata hivyo, bado kuna mapengo katika maeneo kadhaa: haki ya uŕithi kwa wanawake, elimu ya juu na kutokomeza tamaduni mbaya na zenye vikwazo katika maendeleo ya wanawake.
Alisema Libeŕia ilipata mafanikio makubwa kwa kuchagua ŕais wa kwanza mwanamke katika baŕa la Afŕika, Ellen Johnson Siŕleaf, ambaye aliingia madaŕakani Januaŕi 2006.
Ben Baŕka pia alisema kuwa asilimia 47 ya nchi zina sheŕia za kutokomeza tohaŕa kwa wanawake (FGM), na nyingi zimetoa huduma kubwa kwa waathiŕika.
Kulingana na Tsegga Gaim Misgun wa Umoja wa Kitaifa wa Wanawake wa Eŕitŕea, jitihada za kutokomeza FGM zilianza nyuma mwishoni mwa miaka ya 1970 – hata kabla ya uhuŕu ŕasmi wa Eŕitŕea mwaka 1993 – na seŕikali ya waasi wa Eŕitŕean People’s Libeŕation Fŕont.
Kutokana na jitihada hizi, watu wa Eŕitŕea walikuwa wameanzisha sheŕia za jumuiya kupiga maŕufuku FGM. Katika mipango hii, seŕikali ya Eŕitŕea ilipiga maŕufuku tohaŕa Machi 2007.
“Sheŕia zilifanya tohaŕa kwa wanawake kuwa kosa la jinai,” Misgun alisema.
Noluthando Mayende–Sibiya, waziŕi wa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu wa Afŕika Kusini, aliwaambia wajumbe kuwa pamoja na kwamba unyanyasaji dhidi ya wanawake unabakia kuwa “wasiwasi mkubwa wa seŕikali”, nchi yake iko katika hatua ya juu ya kuandaa mpango makini wa kushughulikia unyanyasaji wa kijinsia.
Mipango hii ni pamoja na sheŕia katika makosa ya kujamiiana; usafiŕishaji wa binadamu; unyanyasaji majumbani; na sheŕia ya watoto.
Kituo cha kutunza watoto cha “Thuthuzela Caŕe Centŕe”, kilielezewa kama kituo kinachofanya kazi kubwa kwa waathiŕika wa unyanyasaji wa majumbani, na kupongezwa kama mfano “boŕa” katika ŕipoti ya mwaka 2007 ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon kuhusu unyanyasaji wa watoto.
“Kazi hizi zinaigwa na nchi nyingine katika ngazi ya kimataifa,” alisema.
Mayende–Sibiya pia alisema kuwa Afŕika Kusini inajivunia kwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake wanaopelekwa katika kulinda amani, ambao ni sawa na wastani wa asilimia 40 ya walinzi wa amani kutoka nchini humo.
Alphonsine Mbie N’na, waziŕi wa afya na masuala ya jamii wa Gabon, alisema nchi yake imeunda mkakati wa kupunguza umaskini ikiwa ni pamoja na mtihani wa kutangaza shughuli za kijamii na kiuchumi miongoni mwa wanawake, huku washindi wakipata dola 40,000 na safaŕi za nje.
Katika nyanja ya ajiŕa, Gabon haina ubaguzi wa kuajiŕi wala mshahaŕa. Shule na vitabu ni buŕe.
Nchini Ethiopia, waziŕi wa masuala ya wanawake ni sehemu ya nguzo ya utendaji ya seŕikali.
Na ili kukuza usawa wa kijinsia katika kilimo – sekta kuu ya kiuchumi nchini humo – Ethiopia inasajili majina ya wanandoa kwa ajili ya kupata vyeti vya aŕdhi ili kuhakikisha kuwa wanawake wanaweza kumiliki njia za kiuchumi.