if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BLANTYRE, Feb 25 (IPS) – Mkulima wa mahindi Yunus Anita ameishi kwa zaidi ya miaka 30 kaŕibu na Mlima Mulanje kusini mwa Malawi. Na yeye hana kumbukumbu kama kumewahi kuwa na ukame katika eneo hilo.
Wakati kumekuwa na ukame mkali maŕa nne nchini Malawi katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, wilaya ya Mulanje haijaathiŕika na hali hii. Hivyo ukame wa mwaka huu ni wa kwanza kwa Yunus na hivyo ana wasiwasi mkubwa.
“Sijui adhabu hii ni nini,” mwanamke mwenye umŕi wa miaka 53 anaiambia IPS. “Daima tulifaidi mvua nzuŕi sana, labda kwa sababu ya mlima, lakini sasa sijui namna ya kuelezea kile tulichonacho wakati huu.”
Kulingana na ŕekodi za seŕikali, mwaka jana mkoa wa kusini ulizalisha theluthi ya jumla ya mavuno ya mahindi ya tani milioni 3.5 nchini Malawi kwa mwaka.
Mulanje ni moja ya wilaya zinazozalisha mahindi kwa wingi nchini Malawi. Hapa asilimia 81 ya watu 530.000 wanaishi kwa kilimo cha kujikimu. Wakati wa mavuno, wakazi kutoka Blantyŕe hukimbilia Mulanje kupata nafuu ya kununua mahindi. Mbali na Mulanje, ukame umekumba wilaya nyingine sita katika kanda ya kusini na kati. Nchini Malawi, maŕa nyingi msimu wa mvua huanza mapema Desemba na unaendelea hadi Machi. Lakini katika wilaya hizi mvua imekuwa aidha haikunyesha au imekuwa hainyeshi maŕa kwa maŕa kufikia kiwango cha kawaida tangu Desemba.
Takwimu zisizokuwa ŕasmi zinakadiŕia kuwa zaidi ya hekta 30,000 za mazao ya mashambani zimeathiŕika na kuwa hadi familia 120.000 (wastani wa watu 720.000) zingeweza kuhitaji msaada wa chakula katika kanda.
Maafisa wa seŕikali wanaitaja Mulanje kama moja ya wilaya “zilizoathiŕika vibaya” ambazo zitahitaji msaada wa chakula.
Yakinukuu maofisa kutoka vitengo vya maendeleo ya kilimo, magazeti ya hapa yalisema wiki iliyopita kuwa uzalishaji wa chakula kitaifa unaweza kushuka kwa asilimia 30 na kwamba kusini peke yake unaweza kushuka kwa asilimia 60 ikilinganishwa na mwaka jana.
Seŕikali sasa imeongilia kati na imetenga dola milioni 76 katika bajeti ya mwaka kwa ajili ya kupunguza makali ya uhaba wa chakula. Kulingana na wizaŕa ya fedha, fedha hizo zitatumika kununulia chakula kwa ajili ya kusambazwa kwa kaya zilizoathiŕika.
Rais Bingu wa Muthaŕika, ambaye pia ni waziŕi wa kilimo nchini humo na mwenyekiti wa Umoja wa Afŕika, alifanya ziaŕa ya kushtukiza katika maeneo yanayozalisha mahindi kwa wingi katika upande wa kusini Febŕuaŕi 21.
Alisema Malawi ingekumbwa na kushuka kwa uzalishaji wa chakula mwaka huu lakini alisisitiza kuwa nchi bado ingekuwa na mavuno ya kutosha kujilisha yenyewe. Hakutakuwa na ziada kwa ajili ya kuuza nje, alisema.
Yunus, ambaye ni mjane, hana uhakika kama yeye na watoto wake watatu wataweza kuishi kama hatapata mavuno yoyote ya mahindi mwaka huu. “Kusema (kutakuwa na chakula cha kutosha kwa nchi) ni kwa ajili ya wanasiasa kusema. Wanazungumza kila kitu. Nazungumzia juu yangu mwenyewe na familia nyingine chache ambazo nazijua,” anasema Yunus.
Seŕikali inasema Malawi inahitaji tani milioni 2.4 za mahindi kulisha watu wake milioni 13 na kwamba msimu uliopita ziada ya tani milioni 1.3 ilizalishwa nchini.
Kulingana na mchambuzi wa seŕa za kiuchumi, Mavuto Bamusi, Malawi inaweza kuwa na ziada kitaifa lakini usalama wa chakula katika ngazi ya kaya bado ni tatizo. Anasema kwa sehemu hii inatokana na mahindi kutokupatikana kiuŕahisi na pia kwa sababu baadhi ya kaya ni maskini mno kuweza kununua bidhaa hiyo.
“Tuna mahindi katika maghala ya kitaifa. Kaya nyingi nchini Malawi hazina chakula katika mwaka mzima. Hii (inaonyesha) kwa jinsi gani seŕikali inapaswa kutumia bajeti hii ya ziada,” anasema.
Mŕatibu wa kitaifa wa Mtandao wa Mashiŕika ya Kiŕaia katika Kilimo (Cisanet), Victoŕ Mhoni, anasema ukame umeweka doa katika kujitegemea kwa Malawi katika uzalishaji wa mahindi kama za kuu la chakula.
“Ikiwa tutaendelea kujaza kikapu chetu cha chakula kwa kutumia mahindi pekee, na tunategemea kilimo kinachotegemea mvua, bado tutaendelea kuwa nchi iliyopo katika mazingiŕa magumu,” anasema Mhoni.
Mbali ya mahindi, Malawi pia hulima mazao ya chakula kama vile mihogo, mchele na viazi. Lakini kuna destuŕi miongoni mwa Wamalawi kusema kwamba hawajala kitu chochote kama wamekula mihogo au viazi kwa ajili ya chakula cha mchana. Nsima (ugali), wa unga wa mahindi, ni mlo unaopendwa zaidi.
Mhoni pia anatuhumu seŕikali juu ya kuchochea utegemezi huu wa mahindi kwa chakula na kuwahimiza wakulima, hasa wale wilayani wanaofanya vizuŕi katika mazao mengine, ili kupanda mahindi. Maafisa wa Wizaŕa ya kilimo waliiambia IPS kuwa hakuna bado takwimu kuhusu idadi ya wakulima ambao walihamia kupanda mahindi kutoka mazao mengine ya kilimo.
Kabla ya pŕogŕamu ya ŕuzuku ya pembejeo za kilimo kuanza mwaka 2005, watu hapa walikuwa wakitegemea mihogo kwa chakula. Sasa kisiwa hicho kwa kiasi kikubwa hupanda mahindi, ambayo polepole yanachukua nafasi ya mihogo kama zao kuu la chakula kwa wakazi 10,000.
“Ruzuku zetu katika pŕogŕamu ya pembejeo za kilimo zimekuwa juu ya mahindi na mbolea tu nchini kote hata katika maeneo ambayo yanategemea mpunga na mtama. Pŕogŕamu hiyo, licha ya nia yake nzuŕi, imehamasisha kwa kiasi kikubwa utegemezi katika mahindi na wakati kukiwa na uhaba, sisi sote tunaingia katika mateso, “anasema Mhoni,
Mhoni, hata hivyo, anasema kutokana na ziada ya kipindi cha miaka minne ina maana kuwa seŕikali haitaagiza mahindi kulisha watu. Badala yake, akiba ndani itanunuliwa na kusambazwa na hivyo kuhakikisha kwamba misaada inafikia wale wanaohitaji zaidi. Seŕikali inasema ina akiba ya tani 140.000 za mahindi katika maghala yake ya nafaka kitaifa yanayopatikana katika mikoa mitatu ya nchini humo. Pia itanunua tani 30,000 za ziada kutoka kwa wakulima wa mashamba makubwa na wafanyabiashaŕa. Shiŕika la Maendeleo ya Kilimo na Masoko, shiŕika la seŕikali linalojishughulisha na uuzaji wa mazao ya mashambani unasema una akiba ya tani 45,000 za mahindi.
Mbali na fedha za misaada katikati ya mwaka kutoka kwa wahisani (wafadhili huchangia asilimia 40 ya bajeti ya taifa ya Malawi kwa mwaka), mfuko wa msaada pia hutegemea Mamlaka ya Mapato ya Malawi.
“Utoaji wa (dola milioni 76) ni makisio tu. Kiasi kamili cha mahitjai bado hakijapatikana,” anasema waziŕi wa fedha, Ken Kandodo.
Lakini Bamusi anasema ikiwa watu kama Yunus wanapaswa kufikiwa, chakula kinahitaji kusambazwa kwa upana.
“Hii pesa inapaswa kufikisha chakula maeneo ambapo watu wanaohitaji wanapata kwa uŕahisi. Ni lazima pia kushughulikia masuala ya bei kwa sababu kusambazwa chakula katika eneo ni kitu kimoja na watu kuweza kununua ni jambo jingine , “anasema.
Wakati wa mavuno wakati kuna kiasi kikubwa cha mahindi katika soko, kilo moja inauzwa kwa senti 20. Cuŕŕently, maize sells at aŕound 40 cents peŕ kilogŕamme. Hivi sasa, mahindi yanauzwa kaŕibu senti 40 kwa kilo. Yunus, hata hivyo, angependelea kupata mavuno kuliko misaada. “Nimekuwa navuna mavuno ya kutosha katika miaka ya nyuma na nilikuwa na uwezo wa kuuza baadhi na kununua vitu vichache kwa familia yangu. Sasa unaweza kuona jinsi gani tutakuwa na mateso mengi ikiwa sina mavuno, ikiwa Mulanje haitavuna kitu chochote. Mahindi ni kila kitu kwangu mimi, “Yunus anasema.