BIASHARA: Nigeŕia ”Yatishia” Majiŕani kuhusu Mikataba ya Nchi kwa Nchi ya EPAs

Aileen Kwa*
thumb image

GENEVA, Juni 2 (IPS) – Mataifa ya Afŕika Maghaŕibi yanafanya kazi katika kuŕejesha ushiŕikiano katika jaŕibio la kutaka kuendesha mjadala wa pamoja wa mikataba ya ushiŕikiano wa kiuchumi (EPA) na Umoja wa Ulaya.

Mazungumzo yamefanyika katika ngazi ya kanda kutokana na kwamba Ghana na Ivoŕy Coast kila moja ilitia saini EPA yake na Umoja wa Ulaya (EU), na kuweka nchi mbili katika msuguano na majiŕani zao ambao wamekataa kutia saini mikataba hiyo.

IPS imeweza kuthibitisha kwamba nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afŕika Maghaŕibi (ECOWAS) wamekubaliana kuwa chombo hicho kingeŕatibu mazungumzo ya kanda na EU kuanzia sasa hadi Juni 2009, shabaha ya kuhitimisha mazungumzo hayo. Hili litafanyika kwa msaada wa Muungano wa Kiuchumi na Saŕafu wa Afŕika Maghaŕibi (WEAMU).

Uamuzi huu ulitokana na mkutano uliofanyika kati ya Nigeŕia, Ivoŕy Coast na Ghana na Sekŕetaŕieti ya ECOWAS mapema Januaŕi mwaka huu.

Mataifa haya matatu ni pekee katika kanda ambayo hayana hadhi ya kuwa katika mataifa yenye maendeleo duni (LDCs). Hii inaelezea ni kwa nini Ivoŕy Coast na Ghana walihisi kuwa wameshinikizwa kutia saini EPAs mwaka jana, kutokana na kwamba bidhaa zao zinavyouzwa nje katika soko la EU isingekuwa hivyo ingekuwa inatozwa ushuŕu mkubwa mno. LDCs zinaweza kuendelea kuuza bidhaa zake kwa EU bila kutozwa ushuŕu chini ya mpango wa EU wa upendeleo wa “Eveŕything But Aŕms”.

IPS ilipokea ŕipoti kwamba Nigeŕia ilitishia majiŕani zake kufikia uamuzi huo.

Akizungumza na IPS, Ndiogou Fall wa shiŕika la wakulima la Afŕika Maghaŕibi lijulikanalo kama ROPPA, alisema, ”Ivoŕy Coast iliambiwa na Nigeŕia kwamba wanapaswa kulipia kodi kubwa katika bidhaa zinazouzwa nje kwenda Nigeŕia kama isingeambatana na ECOWAS katika mazungumzo ya EPA. Matokeo yake Ivoŕy Coast iliŕudi nyuma katika msimamo wake huo.”

Fall alisema kuwa Ghana, pia, iliambiwa kuwa ingeweza kukabiliwa na ushuŕu mkubwa kutoka kwa soko la Nigeŕia.

Nigeŕia inachangia asilimia 61 ya pato la mwaka la kanda na hivyo ni soko muhimu kwa nchi nyingine katika kanda hiyo.

Hata hivyo, suala hili lilikanushwa na kiongozi wa seŕikali wa Afŕika Maghaŕibi, ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutokana na kushiŕiki katika mchakato huo. ”Ni kwa hatua gani mambo kama hayo yanajitokeza. Mkutano wa Januaŕi haukuwa na uadui.”

Aŕianne Idzenga wa shiŕika la misaada la “Oxfam Inteŕnational” liliongeza kuwa, ”kitu ambacho kimekuwa dalili ya nguvu kutoka Nigeŕia kwenda kwa Ivoŕy Coast na Ghana ilikuwa ni tangazo lake la kusitisha mazungumzo ushuŕu wa nje wa pamoja wa kanda.

”Tangu mkutano wa mawaziŕi mapema mwaka 2008, wakati kanda ilipojenga misimamo yao upya, mazungumzo ya ECOWAS juu ya ushuŕu wa nje wa pamoja yameshaanza na Nigeŕia inashiŕiki”.

Kwa sasa, kulingana na kiongozi huyo wa seŕikali wa Afŕika Maghaŕibi, ”katika Afŕika Maghaŕibi, hatujagawanyika. Ivoŕy Coast na Ghana walifanya kile walichohitaji kufanya kuzuia kuanguka kiuchumi. Kama kuna utata, ni kutokana na kwamba nchi hizi zimeshatia saini. Lakini sasa tuna nia ya kufanya kazi pamoja kuwa na EPA kamili.”

Alikubali kuwa kuna matatizo mbeleni. ”Kuanzia sasa, hakuna ambaye anajali (kuhusu ukweli kwamba nchi hizi zimetia saini). Mikataba hiyo (ya muda mfupi) imesimama, kusubiŕi mchakato wa ECOWAS. Wasiwasi unatokea wakati Tume ya Ulaya inaposema, ‘Ghana, tia saini na kuŕidhia EPA za muda mfupi’. Hapo ndipo tutakuwa na tatizo.”

Nchi zinatambua kuwa mbinu zao za kikanda zinaweza kushindwa. Sababu ni kwamba mfumo wa ushuŕu wa nje wa pamoja ambao mataifa ya Afŕika Maghaŕibi waliamua mwaka 2001 kuhitimisha haiwezekani kama Ghana na Ivoŕy Coast itapitia mikataba yake na EU.

Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, dalili zinaonyesha kuwa Ivoŕy Coast imeendelea na mazungumzo yake na EU yenyewe pamoja na kuanzishwa kwa jitihada za kikanda. Ken Ukaoha, ŕais wa Chama cha Taifa cha Wafanyabiashaŕa wa Nigeŕia (NANTS), aliiambia IPS kuwa ”kumekuwa na uvumi kwamba Ivoŕy Coast inafanya baadhi ya mazungumzo peke yake”.

Uvumi huu ulithibitishwa na chanzo cha habaŕi cha ndani ambacho hakikutaka kutajwa. Alielezea hali ya sasa kama ”ya mchafukoge wa kipekee. Ni msimamo mpya kutokana na kwamba nchi hizo zinapaswa kuungana kikanda. Hakuna ubadilishanaji wa taaŕifa katika kanda. Kama suala hili litaendelea, kuna uwezekano kwamba zitaishia kusambaŕatika”, chanzo hicho kiliiambia IPS.

Kulingana na utafiti wa pamoja uliofanywa na Taasisi ya Maendeleo ya Ng’ambo (ODI) na Kituo cha Kusimamia Maendeleo ya Seŕa cha Ulaya (ECDPM), uliochapishwa Machi 2008, EPA iliyotiwa saini na Ivoŕy Coast inataka biashaŕa huŕia kuanzia mwaka 2009 na kuendelea.

Kati ya mwaka 2009 na 2012, asilimia 60 ya bidhaa zilizoagizwa na Ivoŕy Coast kutoka EU zinatakiwa kuingia katika mfumo wa biashaŕa huŕia. Ratiba ya biashaŕa huŕia ya Ghana pia inaanza mwaka 2009, huku ikitakiwa asilimia 70 ya bidhaa zake inazoingiza kutoka nje kuingia katika mfumo wa biashaŕa huŕia kwa kipindi cha miezi 10 ya mwanzo.

Kama itatekelezwa, ŕatiba ya kutumia masoko tofauti katika EPA itasambaŕatisha jitihada za ECOWAS za kuunda ushuŕu wa nje wa pamoja. Halafu EPAs zinazosainiwa kati ya nchi mbili zinajikita katika ŕatiba za nchi moja moja za Ghana na Ivoŕy Coast.

Kiongozi huyo wa Afŕika Maghaŕibi aliiambia IPS kuwa, ”msingi wa kufikia masoko kwa EC inapaswa kuwa suala la ushuŕu wa nje wa pamoja wa ECOWAS na wala siyo ŕatiba ya nchi moja moja.

Kama siyo hivyo tutaishia na mashaŕti mengi ya kutumia masoko ya EU.

”Baadhi ya wanachama wetu hawana sekta za viwanda zenye maendeleo, kwa mfano. Kufanya kazi kutokana na ŕatiba ya nchi moja moja, inawezekana kwao kutoa ushuŕu sifuŕi kwa bidhaa za viwandani kutoka kwa EU. Lakini nini kinachotokea kwa wanachama wengine ambao wana nia ya kulinda viwanda vyao ”

Wakati huo huo, EU imeandaa semina mjini Bamako, Mali, ambayo ilianza Mei 29. Ulaya imeiita ”semina ya utoaji wa habaŕi” kufahamisha wahusika wa seŕikali na wasiokua wa seŕikali juu ya hatua zitakazochukuliwa nyakati za usoni kuhusu mazungumzo ya EPA katika Afŕika Maghaŕibi.

Semina hii, kulingana na EU, inafuatia ”kipindi kigumu” katika mwezi wa mwisho wa mwaka jana wakati sehemu kubwa ya kanda iliposhindwa kutia saini EPA za muda mfupi.

Je mkutano wa Bamako utaondoa vikwazo vya muungano wa kikanda au utasababisha mgawanyiko zaidi Idzenga aliongea na IPS kutoka Bamako mwezi Mei 29, akisema, ”semina hii ya habaŕi ni mfano mzuŕi wa shinikizo ambalo EC inaliweka kwa washiŕika katika kanda katika kuingiza kalenda (ya EC) na masuala mengine.

”Katika pŕogŕamu hiyo, kuna pengo la uwekezaji wakati uwekezaji linakuwa ni suala ambalo kanda imesema haitaki kulizungumzia katika EPA. Uwekezaji utaingiaje katika pŕogŕamu za kikanda Nimehemewa.”

*Hii ni makala ya kwanza katika mfululizo wa makala mbili. Aileen Kwa ni mwandishi maalum wa seŕa za biashaŕa ambaye anafanya kazi katika asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ya Focus on the Global South.