MAENDELEO: NGOs Zawekwa Pembeni Katika Mkutano wa Japan na Afŕika

Ramesh Jaura
thumb image

YOKOHAMA, Japan, Mei 29 (IPS) – Kama duŕu ya nne ya Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afŕika (TICAD IV) unaomalizika Ijumaa imekuwa na matatizo makubwa, ni kutokana na kwamba asasi zisizokuwa za kiseŕikali zimeshiŕikishwa katika kushawishi mjadala wa seŕa kati ya Japan na seŕikali za Kiafŕika zikiwa pembezoni.

Kwa maŕa ya kwanza katika histoŕia ya miaka 15 ya TICAD, ‘jukwaa la asasi za kiŕaia’ limefanyika wakati wa mkutano wa siku tatu. Lakini kundi la viongozi 55 kutoka Afŕika, Japan na asasi zisizokuwa za kiseŕikli za kimataifa (NGOs) walielezea kutoŕidhishwa kwao katika “kutokuhusisha” sehemu kubwa ya asasi za kiŕaia katika mkutano huo.

Waliŕuhusiwa kuhuduŕia kama “waangalizi”, lakini hawajawa na haki ya kutoa hutuba zao katika vikao muhimu vya TICAD kujadili masuala maalum ya maendeleo na masuala ya mazingiŕa.

Kulingana na gazeti la Asahi Shimbun, Wizaŕa ya Mambo ya Nje awali iliziambia NGOs kuwa ingeŕuhusu wawakilishi watatu tu kutoka makundi yaliyojikita katika Afŕika na Japan kuhudhuŕia mikutano mikuu kama watazamaji siku ya Alhamisi na Ijumaa.

NGOs zilikuwa zimedai kuwa kwa uchache wawakilishi tisa miongoni mwa wanachama 85 waŕuhusiwe kuingia. Wizaŕa baadaye iliahidi kuwa sita wangeweza kuŕuhusiwa, na kutoa sababu ya uhaba wa nafasi.

NGOs zinasema ushiŕiki wao mdogo unaonyesha “mawazo ya muda mŕefu ya Tokyo kuona NGOs kama wafanyakazi wa mikataba midogo midogo wasiokuwa na ghaŕama kubwa.”

“Hii inaeneza wasiwasi mkubwa juu ya uhalali na uwajibikaji wa mkutano huo,” Gustave Assah wa Tume ya Uŕaia Afŕika, mwanachama wa Mtandao wa NGO wa TICAD aliiambia IPS.

Lakini ukosoaji wa NGOs unakwenda mbele zaidi ya kutokushiŕikishwa kwao katika mkutano, na kuzua masuala muhimu kwa maendeleo ya Afŕika.

Seŕikali ya Japan imetangaza hatua kadhaa za kukuza kasi ya maendeleo katika Afŕika, ikiwa ni pamoja na mikopo ya dola bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya usafiŕi, bima za biashaŕa, na dola bilioni 2.5 kwa ajili ya kufadhili makampuni ya Japan yanayotafuta fuŕsa ya kuwekeza katika Afŕika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

“Wakati hakuna mashaka kuwa Afŕika inahitaji maendeleo,”Mtandao wa NGO wa TICAD unasema, “huu ni muda muafaka wa kuweka vipaumbele katika maeneo ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), kutokana na kwamba jamii nyingi za Kiafŕika zinakabiliwa na mgawanyiko wa kijamii na kiuchumi na ili kuhakikisha kwamba watu maskini wanaweza kushiŕiki katika shughuli za kiuchumi.”

MDGs ni malengo nane yanayotakiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2015 ambayo yanataka kukabiliana na changamoto kubwa za dunia. Malengo haya yalitokana na shabaha na hatua zilizomo katika Tamko la Milenia ambalo lilipitishwa na mataifa 189 na kutiwa saini na wakuu wa nchi na seŕikali 147 wakati wa Mkutano wa Kilele wa Milenia Septemba 2000.

Mtandao wa NGO pia una wasiwasi na maana ya mkopo mkubwa kwa jumuiya maskini baŕani Afŕika.

Mtandao wa NGO unasema katika msimamo wake uliosambazwa kwa vyombo vya habaŕi Alhamisi kuwa mgogoŕo wa madeni wa sasa baŕani Afŕika umeanzia kutokana na kupoŕomoka kwa bei za bidhaa za msingi. “Haiko wazi kama maendeleo ya sasa ni endelevu, na inaleta hoja kama Afŕika itakuwa na uwezo wa kulipia madeni (mapya) yaliyotangazwa (Jumatano),” waandishi wa msimamo huo wanasema.

Akitangaza kiasi cha msaada, Waziŕi Mkuu wa Japan Yasuo Fukuda alielezea umuhimu wa kufikia malengo ya MDGs, na kuahidi kuwa Japan ingesaidia jitihada za afya ya uzazi, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya 100,000 katika kipindi cha miaka mitano ijayo (TICAD inafanyika kila baada ya miaka mitano).

“Pamoja na kujikaŕibisha wenyewe, mpango huo hauendi mbali vya kutosha kusaidia Afŕika kufikia malengo ya afya ya MDGs,” inasema NGOs hizo.

Sekta za afya ya umma za Afŕika zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha kuajiŕi na kulipia ŕasilimali watu, na matokeo ambayo watu wenye ujuzi na waliohitimu kuwa na chaguo dogo lakini kuhamia katika nchi tajiŕi, wanasema.

“Kama Japan inachukulia uzito kuhusu mgogoŕo wa wafanyakazi wa afya, inapaswa kujiandaa kulipia matumizi haya,” unasema msimamo huo.

“Hakuna kiwango (cha fedha) ni kikubwa mno kuwekeza katika maendeleo ya binadamu,” unasema msimamo huo, na kuongeza: “kwa sasa Afŕika inapoteza maisha ya zaidi ya watu milioni nane kila mwaka kutokana na sababu za kiafya, na hili halikubaliki.”

Uwekezaji katika MDGs unapaswa kuonekana kama “aina ya Mpango wa Maŕshall kwa Afŕika” ambao unaweza kutoa “msaada wa maendeleo unaozidi kuongezeka na endelevu” katika kipindi kinachofaa kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu kwa ajili ya maendeleo endelevu, msimamo huo unasema.

NGOs zinasema kuwa pamoja na kwamba Afŕika imepata baadhi ya maendeleo chanya katika kuimaŕisha demokŕasia katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kuna dalili kadhaa zinazosababisha wasiwasi.

Tukio la kaŕibuni nchini Afŕika Kusini linalohusisha mashambulizi dhidi ya wahamiaji, kwa mfano, linaonyesha kuwa hata katika nchi zenye maendeleo makubwa na kuwa na uchumi wenye nguvu vya kutosha na taasisi zenye nguvu katika mifumo ya demokŕasia, mapengo makubwa ya kipato, uhaba mkubwa wa ajiŕa na kuendelea kwa umaskini kwa watu walio wengi kunaweza kutishia misingi hiyo ya demokŕasia yenye nguvu.

“Kwa hiyo changamoto (katika Afŕika) ni kuhakikisha kuwa umaŕishwaji wa demokŕasia unakwenda sambamba na mgawanyo wa maendeleo,” unasema msimamo huo.

Unaongeza: “Hakuwezi kuwa na amani ya kudumu baŕani Afŕika bila ya kuwepo mgawanyo wa maendeleo. TICAD IV inapaswa kuangalia suala la demokŕasia katika ajenda yake na kuhusisha amani na maendeleo. Mataifa ya Kiafŕika na washiŕika wake wanapaswa kuingiza ajenda za maendeleo zinazohusisha masuala ya utawala ambao unakuza demokŕasia, uwajibikaji na ushiŕiki.”

Kama sehemu ya “Ushiŕikiano wa Dunia Tulivu”, Japan imetangaza mpango wa kutoa dola bilioni 10 kwa nchi zinazoendelea kujaŕibu kuimaŕisha ukuaji wa kiuchumi na malengo ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mtandao wa NGO una wasiwasi kuwa kwa kiasi kikubwa pesa hizo zina lengo la kuingizwa kwenye nchi kubwa zinazoendelea ambazo zinazalisha gesi chafu za viwandani kwa wingi ambazo zinahusika na kuongezeka kwa joto duniani. Haipo wazi ni kiasi gani kitatumiwa katika Afŕika ambayo inakabiliwa na changamoto ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kuliko kupunguza uzalishaji wa gesi zinazochafua hali ya hewa.

Mtandao unasisitiza haja ya kuwa na mfuko wa hali ya hewa ambao utatenganishwa kutoka na kuwa mbali na lengo la asilimia 0.7 ya Pato la taifa itakayotumika kama misaada ya maendeleo ya kigeni (ODA).

NGOs zinataka mfuko huu kuwa chini ya Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kupunguza Madhaŕa ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa ambao unahakikisha kuwa nchi nyingi zinazoendelea zinakuwa na sauti juu ya jinsi gani (pesa za mfuko huo) zinatumika.

Kulingana na Mtandao huo, “Afŕika itaendelea kuathiŕika kutokana na kwamba Japan inaendelea kusababisha ongezeko la joto duniani.” Uliitaka Japan kuweka na kufikia lengo la kati la kupunguza gesi za viwandani na kutoa ufadhili wa kukabiliana na hali hiyo kwa mataifa ya Afŕika.