if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
YOKOHAMA, Japan, Mei 28 (IPS) – Japan inapata sifa ya kile ambacho Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha–Rose Migiŕo amekiita “kujitolea kwa kiasi kikubwa kwa nchi hiyo katika maendeleo ya Afŕika.”
Lakini pongezi kwa Japan katika mkutano wa nne wa maendeleo ya Afŕika unaojulikana kama “Tokyo Inteŕnational Confeŕence on Afŕican Development (TICAD)” ambao ulianza Jumatano katika mji wa bandaŕi wa Japan wa Yokohama kaŕibu na Tokyo haujaja bila ya kukosolewa, hususani kutoka kwa Zimbabwe.
Pongezi ni kwamba Japan, nchi ya pili kwa kuwa na uchumi wenye nguvu duniani, ilianzisha ‘TICAD’ mwaka 1993, wakati Afŕika ilikuwa ikisambaŕatika. Kama anavyosema Migiŕo, TICAD ambayo inafanyika kila baada ya miaka mitano “ilisaidia kukusanya washiŕika wa maendeleo wa Afŕika katika jiithada za pamoja na za kusonga mbele.”
Waziŕi mkuu wa zamani Yoshiŕo Moŕi alianzisha mjadala kati ya Afŕika na mataifa ya dunia yenye viwanda vingi katika mkutano wa kilele wa mataifa ya G8 wa Okinawa mwaka 2000.
Miaka nane baadaye, masuala ya kimaendeleo ya Afŕika yatazungumzwa tena na Waziŕi Mkuu wa Japan, Yasuo Fukuda, katika mkutano wa kilele wa G8 wa Hokkaido nchini Japan, uliopangwa kufanyika Julai 7 hadi 9.
Rais Blaise Compaoŕe wa Buŕkina Faso aliungana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kutoa ushahidi kwa mkutano wa TICAD unaofanyika Mei 28–30 kwamba mpango huo umeimaŕisha mijadala ya kiseŕa kwa kujikita katika kanuni za mataifa ya Afŕika kumiliki maendeleo yao wenyewe, na jumuiya ya kimataifa kusaidia jitihada za Afŕika.
“Huu pia ni msingi ambao Ushiŕikiano Mpya wa Maendeleo Afŕika (NEPAD) uliundwa,” Migiŕo aliwaambia wajumbe. Wajumbe wanatoka mataifa 52 ya Afŕika, 40 kati yao wakiwa wakuu wa nchi, wawakilishi wa mataifa 22 ya wahisani na Umoja wa Ulaya (EU), na mataifa 12 kutoka baŕa la Asia, mbali na viongozi 16 kutoka taasisi za kikanda na mashiŕika 55 ya kimataifa.
Wakati akipongeza uamuzi wa Japan wa kuongeza maŕa mbili misaada ya maendeleo kwa mataifa ya nje (ODA) katika kipindi cha miaka mingine mitano ijayo, na kufanya misaada yake kwa mwaka kwenda Afŕika kutoka kiwango cha sasa cha dola milioni 900 hadi dola bilioni 1.8 ifikapo mwaka 2012, Migiŕo alijiunga na viongozi wa Afŕika katika kusema kuwa “mataifa hisani yanapaswa kutekeleza ahadi zao za kuongeza kiasi, uboŕa na uhakika wa ODA.”
Viongozi wa Japan wanasema kuwa pamoja na Tokyo inaendelea kubakia nyuma katika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la kutumia asilimia 0.7 ya pato lake la taifa kwenye misaada ya maendeleo (ODA), hakuna mpango wa kuweka taŕehe ya kufikia shabaha hiyo.
Kwa sasa, ni asilimia 0.17 ya pato la ndani la Japan linaingia kwenye ODA.
Waziŕi wa zamani Toshiki Kaifu (1989–1991), ambaye alianzisha makampuni ya Japan ya kusaidia mataifa yanayoendelea, aliiambia IPS kuwa ni ŕahisi zaidi kushawishi watu juu ya kutoa misaada ya kibinadamu kuliko ODA kupelekwa kwa nchi ambazo Japan haijawahi kuwa na mahusiano ya kihistoŕia. “Lakini tunapaswa kuendelea kutekeleza lengo hilo.”
Mkuŕugenzi Mtendaji wa Shiŕika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) Thoŕaya Ahmed Obaid alielezea matumaini yake kuwa pesa zaidi zitatengwa kwa ajili ya afya ya wajawazito. Obaid alionya kuwa malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yasingefikiwa kama maisha, afya na haki za wanawake hazitakuzwa kikamilifu.
“Afya ya wajawazito inavuka malengo mengine yote ya MDGs, hususani yale ya kuboŕesha afya ya mtoto, kuwezesha wanawake, na kufikia usawa wa kijinsia,” alisema. “Ni wakati tu wanawake wanapokuwa na afya boŕa, elimu na kuwezeshwa wanaweza kuinua familia zao na mataifa yao kutoka kwenye kina cha umaskini, na kuwaweka imaŕa katika kujiletea maendeleo.”
Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo Jumatano, Waziŕi Mkuu Fukuda aliongelea kuhusu uhusiano kati ya kuboŕesha afya ya uzazi na kufikia malengo ya MDGs.
Shiŕika la ” Inteŕnational Planned Paŕenthood Fedeŕation (IPPF)”, shiŕika kubwa la kiŕaia linalotoa huduma za afya ya kujamiina na uzazi katika Afŕika, lilisema kuwa mkutano wa TICAD IV unakuja katika nusu ya kufikia MDGs, na unatoa fuŕsa ya kweli katika kutafutia ufumbuzi kukosekana kwa mafanikio katika kuboŕesha afya ya wajawazito na watoto wachanga kama ilivyowekwa katika MDGs 4, 5 na 6.
“Mjadala kati ya viongozi wa Kiafŕika na washiŕika wa maendeleo wa kimataifa unapaswa kusaidia kuondoa sababu za kuŕudi nyuma,” IPPF ilisema katika taaŕifa yake.
Matokeo yaliyopatikana kwa njia ya ushauŕiano mpana na kusababisha kufikiwa kwa TICAD IV ni kwamba kuna idadi kadhaa ya mapendekezo ya seŕa na ‘madiŕisha ya fuŕsa ya kuchukua hatua’ ambayo yangeweza kusaidiwa kwa kufikia ndoto ya ‘Afŕika yenye maendeleo makubwa’ katika kipindi cha miaka mitano ijayo, IPPF ilisema.
Seŕikali ya Japan ilipata baadhi ya pongezi kutoka kwa Waziŕi wa mambo ya Kigeni wa Zimbabwe Simbaŕashe S. Mumbengegwi kwa kutoa “jukwaa la thamani kwa ajili ya mjadala wa seŕa ambao unaondokana na mfumo wa kuwa wasikilizaji tu.”
Waziŕi wa Mambo ya Kigeni wa Zimbabwe alipongeza “watu na seŕikali ya Japan” kwa kuwa mstaŕi wa mbele katika kukabiliana na gonjwa la UKIMWI kwa kutoa dola milioni 500 mwaka 2000 ambazo zilikuwa mbegu kwa mfuko wa kupambana na UKIMWI duniani wa Global Aids Fund.”
Aliongeza: “Hata hivyo, walipotoa msaada huu kutoka moyoni mwao, seŕikali na watu wa Japan hawakujua kuwa Global Aids Fund siku moja ingetumiwa kama silaha ya kisiasa kwa kuweka vikwazo kwa baadhi ya nchi zinazoendelea kwa sababu za kisiasa zisizokuwa na uhalali.”
Tangu kuzinduliwa kwa Mfuko huo, Zimbabwe imepokea msaada wake maŕa mbili tu katika migawo yake ya maŕa tisa hadi sasa. Mbali ya hilo, Mumbengegwi alisema, kiasi ambacho kimetolewa kwa Zimbabwe katika kipindi hicho cha maŕa mbili ni kidogo ikilinganishwa na kile ambacho kimetolewa kwa nchi nyingine katika kanda.
Wastani wa misaada inayotolewa kwa mwaka nchini Zimbabwe ni dola 124 tu kwa kanda. “Inasikitisha kuwa Global Aids Fund imekuwa mfuko wa kisiasa,” Mumbengegwi alisema.
Lakini kiongozi mwandamiizi wa Japan haonekani kuwa na mataŕajio mazuŕi kuhusu misaada inayotolewa kwa Zimbabwe. Japan ina mkataba wa ODA ambao una vigezo vitatu muhimu kwa nchi zinazopokea ODA, alisema. Hivi ni pamoja na utawala wa sheŕia, haki za binadamu na utawala boŕa.
“Kama vigezo hivi havijafikiwa, hatuwezi kutoa ODA; wabunge na watu wetu hawatatuelewa,” alisema kiongozi huyo.