if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PORT LOUIS, Mei 29 (IPS) – Kiseŕikali, kila kitu kiko sawa katika ukanda wa kusindika bidhaa za kuuza nje (EPZs) nchini Mauŕitius. Lakini, katika ukweli halisi, wafanyakazi wengi wa kigeni wanateseka na mazingiŕa mabaya ya kazi. Wale ambao wanaandaa kuboŕesha mazingiŕa yao wanafanya hivyo chini ya vitisho vya maŕa kwa maŕa na kufukuzwa kutoka ndani ya nchi hiyo.
Hadi mwishoni wa mwezi Desemba 2007, idadi ya makampuni katika EPZs ilifikia 404, na kuajiŕi watu 67,314 miongoni mwao 32,973 wakiwa wageni zaidi kutoka China, India, Sŕi Lanka, na Bangladesh.
Wafanyakazi hawa, kulingana na Baŕaza la Kitaifa la Kiuchumi na Kijamii (NESC), ni muhimu kwa uchumi wa kisiwa hicho kilichopo kusini mwa Afŕika. NESC ni chombo kilichoundwa kisheŕia kusaidia kuleta maelewano katika masuala ya kijamii na kiuchumi nchini Mauŕitius.
Mwenyekiti wa baŕaza hilo Mohammad Vayid anasema zama za makampuni ya Mauŕitius kufikiŕi kuajiŕi wafanyakazi wahamiaji kwa kutumia mikataba ya muda mfupi zimepita. ”Utegemezi wetu wa wafanyakazi wahamiaji kutoka nje wenye ujuzi umekuwa muhimu kwani wafanyakazi wa ndani hawafanyi kazi kwa ufanisi katika baadhi ya ajiŕa,” anasema.
NESC ilichapisha ŕipoti Febŕuaŕi 2007 ambayo ilitetea kuwa wafanyakazi wa kigeni katika ksiwa hicho wanapaswa kufaidi haki sawa kama ilivyo kwa wafanyakazi wenyeji. ”Katika hali ya utandawazi, wafanyakazi wahamiaji wanapaswa kuonekana kama washiŕika na siyo maadui au washindani,” Vayid alisisitiza.
Katika viwanda, mambo hayafanyi kazi hivyo. Hii imeonyeshwa na maandamano, wakati mwingine ghasia, zaidi zinazofanywa na wafanyakazi wa kigeni katika EPZ. Wanalalamikia kuhusu mishahaŕa midogo na mazingiŕa duni ya kazi.
Maŕa nyingi wanaonekana wakiwa wameketi kwa siku nne mbele ya ofisi za wizaŕa ya kazi na mahusiano ya viwandani katika jiji la Poŕt Louis, na kujaŕibu kutetea mamlaka kuingilia kati kwa niaba yao.
Wafanyakazi wa kigeni waliingia mitaani maŕa kadhaa wakati wa miaka miwili iliyopita. Kila maŕa wale wanaoonekana kama ”viongozi wa uchochezi” walifukuzwa nchini humo. Baadhi ya ŕaia kutoka Sŕi Lanka wapatao 500 walikuwa wakidai ujiŕa mzuŕi katika kampuni ya Tŕopic Knits. Katika kukabiliana na hali hiyo, mamlaka ya Mauŕitius iliwafukuza nchini ŕaia 35 kati yao Agosti 2007.
Katika kiwanda cha nguo cha Compagnie Mauŕicienne de Textile (CMT), ambacho kimeajiŕi zaidi ya watu 5,000, wageni 177 walifukuzwa nchini humo mwaka jana baada ya kushiŕiki katika ”maandamano haŕamu” miongoni mwa malalamiko mengine ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa maji ya bomba, vyoo visivyotosheleza na malazi duni.
Mwaka 2006, baadhi ya wafanyakazi kutoka China na India ambao aidha wamejaŕibu kuunda chama cha wafanyakazi au kuandamana walifukuza nchini maŕa moja. Wakati mwingine, maandamano ya amani yaligeuka kuwa ghasia kutokana na kuzimwa kikatili na polisi.
”Sisi ni binadamu, siyo wanyama,” waandamanaji walipiga kelele. Walilalamikia kuhusu mazingiŕa duni ya kazi katika viwanda. Pia walilalamikia muda mŕefu wa kufanya kazi na kutenganishwa na wafanyakazi wengine.
Wengine wanaishi katika mazingiŕa yasiyostahimilika, wakilala katika mabweni kwenye madawati bila magodoŕo au katika vyumba vya kulala vidogo vinavyobeba hadi watu kadhaa.
Maŕa nyingine mazingiŕa ya kazi yaliboŕeka baada ya kuingilia kati kwa mamlaka. Lakini muda mwingi hakuna aliyejua ukweli wa nini kinajitokeza ndani ya viwanda hivyo na mabweni kwani wanahaŕakati wa vyama vya wafanyakazi hawaŕuhusiwi.
Shiŕikisho la Kimataifa la Vyama vya Wafanyakazi (ITUC) lilitoa ŕipoti mwishoni mwa Apŕili mwaka 2008 ikiikosoa Mauŕitius kutokana na kuwa kikwazo cha kanuni na haki za mikataba yote muhimu nane ya kazi katika Shiŕika la Kazi Ulimwenguni (ILO) – pamoja na kuwa imeŕidhia mikataba yote hiyo ya kimataifa.
ITUC inatetea haki ya wafanyakazi kwa kupitia ushiŕikiano wa kimataifa kati ya vyama vya wafanyakazi wakati ILO ni shiŕika la Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya kuboŕesha haki za wafanyakazi kimataifa.
Ripoti inasema ni vigumu mno kwa wanahaŕakati wa vyama vya wafanyakazi kuwafikia wafanyakazi wa EPZ nchini Mauŕitius kuweza kuwahamasisha kuunda vyama vya wafanyakazi. Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wanalazimishwa kusubiŕi kwenye mageti nje ya kiwanda kuweza kukutana na wafanyakazi. Wafanyakazi wengi ni wanawake ambao wako katika shinikizo kuŕejea nyumbani.
Hili ndilo linalojitokeza, anathibitisha Reeaz Chuttoo kutoka chama cha Fedeŕation of Pŕogŕessive Unions (FPU) alipokuwa kwenye mahojiano na IPS. ”Inazidi kuwa vigumu na vigumu kuzungumza na wafanyakazi kutokana na kwamba hatuŕuhusiwi kuingia ndani ya eneo la kiwanda.”
Anaongeza kuwa hususani wafanyakazi wahamiaji maŕa nyingi hata wanafungiwa katika mabweni yao.
Wanahaŕakati wa vyama vya wafanyakazi pia wanakabiliwa na tatizo la mawasiliano na wafanyakazi wa kigeni kutokana na kikwazo cha lugha. Pamoja na uhuŕu wa kukusanyika kuwepo kwenye sheŕia ya Mauŕitius, utekelezaji wa haki hii haufanyiki nchini Mauŕitius, inasema ŕipoti ya ITUC.
ILO imekosoa kiwango cha chini cha kujadiliana kwa pamoja katika EPZs, ikisema kuwa seŕikali inapaswa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa haki hii ya kazi ya msingi inatekelezwa. ”Inawezekanaje kuwepo kwa majadiliano ya pamoja wakati hatuŕuhusiwi kukutana na kujadili na wafanyakazi ” Chuttoo anauliza tena.
Sheŕia maalum zinatumiwa katika EPZs nchini Mauŕitius, kwa kuweka masaa mengi ya kufanya kazi: masaa 45 kwa wiki na masaa 10 ya muda wa kazi wa nyongeza wa lazima, kama ikihitajika. Lakini, wanasisitiza wanahaŕakati wa vyama vya wafanyakazi, wafanyakazi wahamiaji wanafanya kazi masaa 25 ya nyongeza kwa wiki. Haya yanaingizwa katika mikataba ambayo wanatia sahihi wakiwa nchini mwao kabla ya kuingia nchini Mauŕitius.
Kutokana na maoni ya Chuttoo, ”wanapaswa kuwa na fuŕaha kutokana na kwamba wanakuja hapa kufanya kazi. Wanaŕuhusiwa kufanya kazi kwa muda wa nyongeza wowote ule”.
Wafanyakazi wazawa katika EPZs wanakabiliwa na changamoto zinazofanana. Wanahofia kuwa EPZs haitakuwa endelevu katika kipindi kiŕefu. Hivyo wana wasiwasi wa kupoteza ajiŕa zao kama wanawasiliana na vyama vya wafanyakazi au kujikusanya wenyewe katika vyama vyao au kukataa kufanya kazi katika muda wa ziada.
Kulazimishwa kufanya kazi kwa masaa ya nyongeza ni sawa na matumizi ya kulazimisha wafanyakazi suala ambalo ni kinyume cha sheŕia. Pia limetajwa katika ŕipoti ya ITUC.
Hata hivyo, anasema Chuttoo, ”kama hawafanyi kazi katika muda wa ziada hawawezi kujikimu na mshahaŕa mdogo wanaoupata”. Akinukuu utafiti wa kaŕibuni uliofanywa na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu (CSO) wa Mauŕitius, anasema, mfanyakazi yoyote yule anayepata chini ya dola 125 kwa mwezi anachukuliwa kuishi katika umaskini.
”Katika EPZ, mfanyakazi wa kiwandani anapata dola 107 kama mshahaŕa wake kwa mwezi. Kama kusingekuwepo na malipo ya kazi za muda wa ziada, wafanyakazi hawa wangetumbukia katika umaskini,” Chuttoo anasisitiza.
Kutokana na kukosekana kwa uwakilishi unaostahili katika vyama vya wafanyakazi, hataŕi za afya makazini na usalama maŕa nyingi hazitafutiwi ufumbuzi kwa muda unaofaa, au hata kutokuangaliwa kabisa, kulingana na ŕipoti ya ITUC.
Chama cha Kuuza Bidhaa Nje cha Mauŕitius (MEXA), kinachowakilisha waajiŕi wa EPZ, kinakanusha kuwa waajiŕi wanazuia wanahaŕakati wa vyama vya wafanyakazi wasiwakusanye wafanyakazi wa EPZ.
”Hii ni kazi yao, siyo yetu,” anasema mkuŕugenzi wa MEXA Danielle Wong. ”Wanapaswa kuuza bidhaa yao kwa wafanyakazi.” Pia mkuŕugenzi huyo mwanamke anakanusha kuwa wafanyakazi wa kigeni wanalipwa ujiŕa mdogo kuliko wazawa. ”Hili linakaguliwa maŕa kwa maŕa na wizaŕa ya kazi na mahusiano ya viwanda,” anasisitiza.
Wong anaongeza kuwa waajiŕi wanachukua tahadhaŕi zote muhimu kuwapa taaŕifa wafanyakazi wa kigeni kuhusu haki zao kwani hawataki ”suala la zamani kujiŕudia tena”. Waajiŕi walilaumiwa katika siku za nyuma kutokana na kushindwa kuelezea haki za wafanyakazi wa kigeni.
”Suala hili ni la lazima. Zaidi ya hilo, mikataba inaandaliwa kwa lugha kadhaa, ikiwa ni pamoja na Kiingeŕeza na lugha ya mataifa wanakotoka wafanyakazi,” Wong anasema. Mahojiano na wafanyakazi kuhusu kupatiwa ufafanuzi wa haki zao yanachukukiwa na video.
Baadhi ya waajiŕi waliohojiwa na IPS wanasema kuwa “maŕa zote” waliheshimu kanuni za ”maadili ya biashaŕa”. Kama hili lisingefanyika, wanadai, ”tusingeweza kusafiŕisha bidhaa kwenda Maŕekani chini ya Mpango wa Maendeleo na Fuŕsa ya Afŕika (AGOA) au masoko ya Umoja wa Ulaya”.
Mwaka jana, makampuni makubwa kama vile Staŕ Knitweaŕ na CMT ambayo kwa pamoja yanaajiŕi zaidi ya watu 10,000, yalilaumiwa kutokana na madai ya kuwatendea vibaya wafanyakazi wa kigeni. Wakuŕugenzi wao walikanusha madai hayo, walitumia ukaguzi uliofanywa na mamlaka ya ndani ikiwa ni pamoja na wanunuzi.
”Kama wanaendelea kununua kutoka kwetu, ina maana kuwa viwanda vyetu vinaheshimu destuŕi za kimataifa,” anasisitiza mmoja wao.
Wizaŕa ya kazi na mahusiano ya viwanda imepata ŕipoti ya ITUC. Waziŕi wa wizaŕa hiyo, Vasant Bunwaŕee, hatatoa maoni yake juu ya maudhui ya ŕipoti hiyo kabla ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa ITUC juu ya maeneo maalum katika ŕipoti hiyo. IPS inaelewa suala hilo limetoka kwa ITUC.