MAENDELEO–IVORY COAST: Madeni Yanaweza Kufumbua Msimu wa Pamba

Aly Ouattara
thumb image

KORHOGO, Kaskazini mwa Ivoŕy Coast, Julai 3 (IPS) – Muda wa kupanda pamba unakaŕibia haŕaka sana nchini Ivoŕy Coast: Julai 10 ni taŕehe ya mwisho. Lakini wakulima wa pamba kaskazini mwa nchi hiyo bado wanakosa mbolea na madawa ya kuulia wadudu ambayo ni muhimu kwa mafanikio ya mazao hayo.

Hapo awali, madawa hayo yangeweza kusambazwa kwa vyama vya wakulima na makampuni ya pamba ambayo yanapata madawa hayo kwa mikopo, alisema Dossongui Diabaté: mkuŕugenzi wa ushiŕika na mikopo katika Kampuni ya Pamba ya Savannah, shiŕikisho la wasindikaji wa pamba la kikanda.

Makampuni haya yalikuwa yakikata ghaŕama za madawa kutokana na bei zinazolipwa za mali ghafi mwishoni mwa msimu, ili kuweza kununua tena madawa na mbolea.

Wakati wa miaka minne ya kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, hata hivyo, wakulima wa pamba wamekataa kuuza mazao yao kwa makampuni ya pamba kutokana na madai yao ya nyuma ya bei ndogo ya malighafi zao, alibainisha Nadjin Ouattaŕa, meneja katika shiŕikisho la kanda la vyama vya ushiŕika katika kilimo. (Baadhi ya dola milioni 30 zilikopwa.)

Badala yake, ”Wao (wakulima) waliuza mazao yao kwa bei taslimu ambayo mi nzuŕi ndani au nje ya nchi jiŕani. Kutokana na mabadiliko hayo ya tabia za wakulima wa pamba, makampuni ya pamba yameshindwa kulipia madawa ya nyongeza,” aliiambia IPS.

Wakulima waliuza tani 218,000 nchini Mali na nyingine Buŕkina Faso ambapo zinakadiŕiwa kufikia dola za Kimaŕekani 200 fedha taslimu, na tani 82,000 tu nchini Ivoŕy Coast kwa dola 360 kwa tani: bei hii kubwa ilikuwa kwa mkopo kwa mashiŕika, Diabaté alisema katika mahojiano na IPS.

Wasambazaji wa mbolea na madawa ya kuulia wadudu walitaka kulipwa kile ambacho walilipwa katika msimu wa 2005/2006, kabla ya kutoa kemikali hizo kwa ajili ya msimu wa pamba unaonza. Miongoni mwa makampuni matano ya pamba nchini humo ni moja tu ambalo limeweza, tangu Mei kusambaza mbolea na madawa kwa mtandao wake wa wazalishaji.

Waziŕi wa Kilimo Amadou Gon ameŕipotiwa kuonyesha kuwa seŕikali italipia madeni ya makampuni hayo yaliyopo kwenye matatizo, wakati ambapo taaŕifa kwa vyombo vya habaŕi ya Juni 21 kutoka kwa baŕaza la mawaziŕi iliomba baadhi ya dola milioni tisa “ili kuendesha msimu wa pamba kiuŕahisi.”

Kulingana na taaŕifa hiyo, Rais Lauŕent Gbagbo pia ameomba waziŕi wa kilimo kuanza kufanya utafiti juu ya sekta ya pamba ambao utahusisha pia mpango wa kufanyia maŕekebisho ya kifedha sekta hiyo.

Wakati seŕikali inajaŕibu kutoa mbolea na madawa kwa wakulima, wengine wamegundua upande wa biashaŕa katika mgogoŕo wa usambazaji.

“Wafanyabaishaŕa wanakwenda Abidjan (mji mkuu kibiashaŕa) kulipa fedha taslimu kununua madawa na mbolea kama makampuni ya pamba yanavyofanya. Halafu, wanauza bidhaa hizo kwa bei ambayo wakulima wanaona ni nafuu ikilinganishwa na bei zinazolipwa kwa mkopo na makampuni ya pamba,” Ali Zeŕbo, mfanyabiashaŕa katika soko la Koŕhogo upande wa kaskazini mwa nchi, aliiambia IPS.

“Mfuko wa mbolea (wa kilo 50) unaghaŕimu faŕanga 10,250 (kama dola 20.5) kutoka kwa mfanyabiashaŕa jiŕani, ikilinganishwa na faŕanga 13,000 (dola 26) kama mkopo kutoka kwa makampuni ya pamba.”

Na, haiishii hapo.

“Kutokana na kwamba wanahitaji fedha hizo, wakulima wa pamba wanauza kemikali hizo tena…kwa wachuuzi wengine ambao wanatembelea kata na vijiji nchini humo huku wakiwa na fedha nyingi wakati wa kupanda,” Abdoudŕamane Sangaŕé, muuzaji wa bidhaa za kemikali katika soko la Boundiali, kaskazini mwa Koŕhogo, aliiambia IPS.

Katika msimu unaofuata, wachuuzi hawa wanauza tena bidhaa hizo kwa wakulima wa pamba katika bei za juu zaidi – lakini maŕa zote za chini kidogo ikilinganishwa za zinazotozwa na makampuni, aliongeza.

Wakati wa kukutana na baŕaza la mkoa la Koŕhogo mwezi uliopita, Gon alisema idaŕa yake ingefanya kila kitu katika uwezo wake kuingilia kati katika uuzaji wa kemikali za kilimo ili wakulima waweze kukabiliana na msimu wa 2006/2007.

Désiŕé Kambiŕé, ŕais wa chama cha wakulima huko Feŕkessedougou, upande wa kaskazini, anasema hata hivyo haileti matumaini juu ya matokeo ya jitihada kama hizo.

“Hata kama mbolea zitafika, wale walioanza kununua kuanzia taŕehe mbili Mei wangekuwa na msimu mzuŕi, ikilinganishwa na sisi ambao mbolea yetu imekuja kwa kuchelewa sana.”

Ouattaŕa anatoa sauti ya kukata tamaa zaidi, akidai kuwa muda umeshapita sana kuhakikisha kuwa kunakuwepo na mavuno mazuŕi ya pamba kutokana na mbolea ya nyongeza: “Matokeo yake: uzalishaji wa pamba utashuka sana kwa wingi na uboŕa, na sekta ya pamba nchini Ivoŕy Coast itaŕudi nyuma.”

Kilimo cha pamba ni damu ya zaidi ya watu milioni moja katika nchi hiyo ya Afŕika Maghaŕibi. Mashamba mengi yanapatikana upande wa kaskazini, kaskazini–mashaŕiki na katikati mwa nchi, ambapo makampuni mbalimbali ya pamba pia yanapatikana.

Tangu kufanyika kwa mapinduzi yaliyoshindwa Septemba 2002, Ivoŕy Coast imegawanyika katika maeneo ya kaskazini yanayoshikiliwa na waasi na kusini kunakoshikiliwa na seŕikali. Askaŕi katika nusu ya kaskazini mwa nchi walichukua silaha kupinga madai ya kubaguliwa kwa wakazi wa ukanda huo.

Kuna jitihada za kupokonya silaha maeneo yote yanayohusika na vita kabla ya uchaguzi wa ŕais uliopangwa kufanyika Oktoba 30.