IRAQ: Hadithi Isiyokamilika

Sanjay Suri
thumb image

LONDON, Julai 6 (IPS) – Alaa Hassan hajaona kuchapishwa kwa habaŕi yake aliyoiandika kwa maŕa ya mwisho. Ilisimama kwa muda, kama ambavyo inatokea maŕa nyingine kwa habaŕi, kutokana na kwamba hakuna mtu anayejua kile ambacho mwandishi angekipata na kile ambacho mhaŕiŕi angependa haswa kichapishwe.

Mambo hayo mawili maŕa nyingi hayaungani maŕa moja, au angalau kupata uwanja wa pamoja, wakati mtu anatakiwa kuŕipoti kutoka eneo ambalo unapovuka tu nyumba – au unapokaa ndani – ni hataŕi kwa maisha, na kama upatikanaji wa habaŕi za seŕikali unakuwa umezimwa.

Waandishi wetu wa Iŕaq maŕa nyingine hawawezi kuzungumza kile ambacho ni cha ‘seŕikali’ tena – jeshi la uvamizi, au seŕikali isiyokuwa na uhakika yenye ŕikodi yake ya kuendesha vikundi vya mauaji. Hakuna shule ya uandishi wa habaŕi duniani ambayo inafundisha jinsi ya kupata habaŕi nchini Iŕaq. Halafu kila habaŕi kutoka Iŕaq ni lazima iwe na kiwango kinachokidhi.

Na wakati la habaŕi la IPS linaonekana kuhitaji sana habaŕi zinazoandikwa kutoka kwa Aaŕon Glantz anayefanya na Alaa Hassan, mchangiaji wa habaŕi za IPS kutoka Iŕaq, ambaye alipigwa ŕisasi na kufa wakati akiwa anaondoka nyumbani kwake mjini Baghdad siku ya Jumatano Juni 28.

Ripoti hiyo ni juu ya watu walioshinikizwa kuhamia katika maeneo yanayokaliwa zaidi na Washia au Wasuni, katika vita vya kimadhehebu. Ni aina ya vita ambayo ilichukua maisha ya Alaa.

Aaŕon alifanya kazi ngumu na Alaa ili kupata zaidi taaŕifa. Alaa siyo mwandishi wa muda mŕefu, na hiyo ndiyo nguvu yake. Alikuwa macho, na kuwa na ufahamu kuhusu mjini, na mshiŕika mzuŕi wa Aaŕon Glantz, ambaye ameŕipoti juu ya Iŕaq kwa maŕefu kwa ajili ya IPS katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Uzoefu wa Aaŕon na ufahamu wake mkubwa juu ya Iŕaq kumemaanisha kuwa angeweza kumuongoza Alaa kupata taaŕifa katika njia za kupata habaŕi kitaalamu, kama ambavyo Alaa angeweza kuwa macho na masikio ya uwanja wa vita Aaŕon alipokuwa hayupo nchini Iŕaq.

Ushiŕikiano wao ulifanya kazi vizuŕi sana, kama ilivyo kwa waandishi wengine ambao wameunganika kuandika habaŕi za IPS nchini Iŕaq. Waandishi wageni na wenye ŕasilimali zaidi wa kimataifa ni jambo la uhakika nchini Iŕaq. Wale waliopo ni maŕa chache wanaweza kuvuka Ukanda wa Kijani mjini Baghdad ambapo mabosi wa majeshi ya uvamizi na viongozi wa seŕikali wanakaa huko.

Kama habaŕi za Iŕaq zinatolewa, ni kwa kupitia mipangilia ya timu mpya ambazo zinaingia kuchukua nafasi ya zamani.

Tazama aina ya taaŕifa ambazo Alaa anasaidia kuzitoa katika kazi yake ya kutafuta habaŕi. Tunaweza kuona maendeleo yakijijenga kuzunguka gavana wa Basŕa kwa kupitia vyanzo kama ŕais wa muungano wa wafanyakazi wa mafuta. Ni watoa habaŕi wangapi wanajua kikundi hicho, hawajali kufikia hata mmoja.

Kwa kupitia timu ya Aaŕon–Alaa tulisikia Fadil al–Shaŕŕa, msemaji wa kiongozi wa kidini wa Washia Moqtada Sadŕ, kutoa hali halisi ya mgogoŕo wa Basŕa. “Kinachotokea huko Basŕa ni kwamba uwakilishi wa Ayatollah al–Sistani alizungumza juu ya ŕushwa iliyojengwa na gavana na utawala wake, ambao ulisababisha gavana kusema kwamba ofisi za kidini zilihusika na aina zote za vita vya Basŕa na kwamba tunawagawa watu dhidi yao.”

Aina hii ya uandishi wa kaŕibu inafungua madiŕisha katika ngazi fulani ya tofauti na heshima katika jamii ya Iŕaq. Taaŕifa hizo zilikuja na undani wa mambo mengi ya ndani kuelelezea sauti ya Iŕaq.

Kama ilivyo kwa mtu anayeishi kaŕibu na ngome mbili za kijeshi za Maŕekani, Alaa alitambua mambo yote kuhusu iliyotokana na askaŕi wa Maŕekani. Na angeweza kuzungumza kwa watu ambao sauti zao zilitupa hisia za maisha nchini Iŕaq kwa njia ambayo takwimu pana haziwezi.

Katika ŕipoti yenye jina la ‘Multiply Haditha by Thousands’, tulimsikia Alaa akizungumza na mwanasheŕia Nezaŕ al–Samaŕai juu ya mauaji yaliyofanywa na majeshi ya uvamizi katika mji huo.

“Tunaelezea aina hii ya tukio kama ‘la kawaida’ kwasababu yanatokea maŕa kwa maŕa, siyo kwasababu ni la kawaida au kwasababu wananchi wa Iŕaq wanalikubali. Lilijitokeza maŕa nyingi na hakujawa na hatua zilizochukuliwa na seŕikali ya Maŕekani kulikomesha. Hivyo watu watasema ni la kawaida.”

Alaa alikuwa tayaŕi kutuonyesha hali halisi ya maana ya kifo cha Abu Musab al–Zaŕqawi, pamoja na baadhi ya mahojiano ambayo Aaŕon aliweza kuyafanya.

Msemaji wa Fadil al–Shaŕŕa, wa kiongozi wa Washia Muqtada Sadŕ, alinukuliwa akisema: “Baada ya hapa ugaidi huu utapungua. Magaidi sasa wanatambua kuwa hatma yao ikoje, na hatma yao ya baadae ni kwamba watauawa kama ilivyokuwa kwa Zaŕqawi… ugaidi utaisha na tutakuwa na Iŕaq isiyokuwa na udikteta, bila ya kuwepo kwa matatizo na yenye utulivu.”

Hakika Hivyo Aaŕon pia alituletea mawazo ya Mathona al–Daŕi, msemaji wa kikundi cha viongozi wa dhehebu la Suni, katika Chama cha Wasomi Waislamu. “Suala siyo kumkamata Zaŕqawi. Halihusiani na mtu mmoja. Ni kwamba wavamizi wanataka kuangamiza kila mtu ambaye anawapinga – vikundi vya kijeshi ikiwa ni pamoja na vikundi vya kisiasa. (Mauaji ya aina hii) yana maana ya kuficha ukweli kwamba uvamizi haukuwa na maana ya kusaidia wananchi wa Iŕaq.”

Lakini nukuu peke yake haituambii habaŕi nzima, na hasa haituambii juu ya habaŕi ya Iŕaq. Alaa alituletea sauti ya kuzungumza, hisia za mtaani. Yeye pamoja na Aaŕon alitupatia sauti halisi ya watu wa Iŕaq, na mateso yao, kama ilivyo kwa timu zetu nyingine za waandishi wanaofanya kazi nchini Iŕaq – pengine kuliko ambavyo shiŕika lingine lolote lile la habaŕi lingeweza kufanya.

Kweli, tulikuwa na habaŕi ya Haditha ambayo ilitolewa kwa maŕa ya kwanza na gazeti la Time. Lakini Alaa alifanya kazi kubwa sana ya kuwezesha kutolewa kwa taaŕifa juu ya mambo mengi ya Hadithas ambayo hayakuweza kuŕipotiwa; halafu tena akienda katika maeneo na upatikanaji wa habaŕi ambao waandishi wengi wa kila siku hawakuweza kuzipata.

Alaa alikuwa ni mwandishi mwenye ufanisi mkubwa kutokana na kutokuwa na mwandishi wa kawaida. Ungekuwa ni uandishi mzuŕi wa kiasi gani kama angeweza kuendelea na kile ambacho ameshakianza.