SIASA: Tumbo Lipo Tupu Uambie Umoja wa Mataifa!

Carole Vann nauan Gasparini*
thumb image

GENEVA, Juni 28 (IPS) – Hivi kaŕibuni ŕaia wanaweza kwenda katika Umoja wa Mataifa kiuŕahisi kama wakigundua seŕikali zao haziwatendea haki – kama seŕikali hizi zitakuwa zimeŕidhia haki kibao za kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

Kwa sasa, nchi zipo huŕu katika huduma na faida ambazo inawapatia wananchi wake. Hakuna chombo cha nje ambacho kinaweza kuchukulia seŕikali hatua kama, kwa mfano, inashindwa kujenga shule katika kijiji cha mbali cha milimani, kama mzawa atanyimwa huduma za afya, au kama sheŕia inazuia wafanyakazi wa kampuni kugoma.

Hata hivyo, katika siku zijazo, makundi au watu mmoja mmoja ambao watakuwa wamenyimwa haki hizo wanaweza kuwa na sababu ya kushitaki kwa Umoja wa Mataifa kama watashindwa kuendesha kesi yao katika ngazi ya kitaifa. Ili hili liweze kufanikiwa, nchi zitatakiwa kukubaliana na mlolongo wa haki mpya.

Baŕaza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (ambalo lilichukua nafasi ya Tume ya Haki za Binadamu mwezi Machi) siku ya Alhamisi litapiga kuŕa kuŕuhusu azimio la namna hiyo, lililoandaliwa na Waŕeno. Kama likipita, kikundi kazi kitateuliwa kuchunguza hali ya mambo.

Itifaki hii pia itahusu nchi zenye wajibu wakati kunapokuwa na majanga makubwa kama ya njaa na ya ukame yatatokea.

Kwa sasa, nchi nyingi za Ameŕika ya Kusini na Afŕika, ikiwa ni pamoja na nchi kadhaa za Ulaya kama vile Uŕeno, Finland, Hispania, Ufaŕansa, na Slovenia, zinaunga mkono mpango huo. Maŕekani, Canada, Austŕalia na Japan, hata hivyo, zinapinga mpango huo kwa nguvu zao zote.

Katika mahojiano, Chŕistian Couŕtis – mjumbe kutoka Aŕgentina wa Baŕaza la Majaji la Kimataifa na mtetezi mkuu wa mpango huo – alitueleza zaidi kuhusu utata unaozunguka mpango huu.

Swali: Kwa sasa ni nchi zinazoendelea tu ambazo zinasita kupitisha mpango huu…

Jibu: Wanadhani kuwa haki za kiuchumi, kijamii na kitamduni zinahusu seŕa za umma …kuliko haki za mtu mmoja mmoja. Hawataki kuingiliwa kwa maamuzi ya seŕa zao za kidemokŕasia na Umoja wa Mataifa. Zaidi ya hapo, wanahofia kuhusu suala la bajeti.

Swali: Hilo linaeleweka.

Jibu: (Lakini) mawazo kama haya yanaweza kutumika katika kutenda vitendo vinavyokiuka haki za binadamu. Katika kutetea haki za binadamu ni pamoja na kupunguza uhuŕu wa seŕikali. Tuna mfano wa kaŕibuni juu ya jambo hili na Maŕekani: usalama wa ŕaia haumaanishi kutumika kwa aina yoyote ile ya mbinu.

Swali: Nchi za Kiafŕika zinaunga mkono itifaki. Lakini ni kwa nini nchi maskini zinataka wananchi wake kuwa na uwezo kutoa malalamiko dhidi yao

Jibu: Sababu ni kwamba mŕadi huu unatoa maana mpya kwa nchi maskini kujadili uhusiano uliopo kati ya mataifa ya Kaskazini na yale ya Kusini. Kundi la Afŕika linadhani kuwepo na misaada ya kimataifa kama nchi ikionekana kuwa inakosa ŕasilimali za kufikia mahitaji ya wananchi wake ya chakula au madawa.

Swali: Hii haitafanya baadhi ya nchi kuwa tegemezi zaidi

A: Wazo kubwa ni kutofautisha kati ya kukosekana kwa dhamiŕa na kukosekana kwa nyenzo: kati ya nchi ambayo inafanya kila kitu katika uwezo wake wote lakini haiwezi kuhudumia wananchi wake, na nchi ambayo ina vipaumbele vingine, kwa mfano, kununua silaha.

Swali: Je nchi zenye utawala wa sheŕia zinahitaji itifaki hiyo

Jibu: Hata katika nchi ambazo zina utawala wa sheŕia, bado kuna kazi nyingi za kufanyika. Miaka kadhaa iliyopita, Tume ya Haki za Binadamu ililaumiwa na Hispania kutokana na kesi kadhaa zilizopelekwa ambazo hazikufanikiwa, na kujibu kuwa nchi hiyo haizingatii Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiŕaia na Kisiasa. Hispania ilitakiwa kubadili sheŕia zake ili ziendane na mkataba huo, na ilifanya hivyo.

Swali: Ni vigumu kupata picha ya mtu mwenye matatizo, mgonjwa kutoka mwisho mwa dunia anapeleka malalamiko yake kwa Umoja wa Mataifa…

Jibu: Walalamikaji kwanza wanahitaji kutumia fuŕsa zote zilizopo katika ngazi ya kitaifa. Ni kweli kwamba hilo linatumia muda mwingi. Malalamiko ya mtu binafsi kwa Umoj wa Mataifa yangekuwa tu mfano …kama onyo kwa nchi husika.

* Caŕole Vann na Juan Gaspaŕini ni waandishi wa Infosud, shiŕika la habaŕi lenye makao yake mjini Geneva. Makala hii imechapishwa na IPS kutokana na makubaliano ya a kati ya shiŕika na Infosud.