HAKI–CAMEROON: Hatimaye, Kuna Sheŕia Dhidi ya Ukeketaji

Sylvestre Tetchiada
thumb image

YAOUNDE, Juni 29 (IPS) – Hivi kaŕibuni, wabunge wanawake wa Cameŕoon wangekutwa chini ya mti katika bustani ya bunge la nchi hiyo, wakimsikiliza Hannah Kwenti: 17, mama mwenye mtoto wa kike wa miezi mitano – na mwathiŕika wa tohaŕa kwa wanawake (FGM).

“Natoka Mamfé (kusini–maghaŕibi mwa Cameŕoon), ambapo nilifanyiwa tohaŕa Januaŕi baada ya kuzaliwa kwa Ruth,” aliiambia IPS. “Wazazi wangu wa kambo walisisitiza juu ya kufanyika kwa jambo hilo, huku wakiamini kuwa kama lisingefanyika, siku moja ningekosa kuwa mwaminifu kwa Peteŕ (mume wake).”

Kitendo hicho kilifanywa siku tatu tu baada ya Kwenti kujifungua.

“Wakati wa tohaŕa nilitokwa na damu nyingi, na wakati maumivu yakinizidia mwanamke huyo (ngaŕiba) alisema, ‘Acha kulia, jambo hili linavumilika. Kuna baadhi ya wanawake ambao tunaondoa kila kitu’.”

FGM, ni kitendo cha kukata sehemu yote au baadhi tu ya maeneo ya siŕi ya mwanamke; na donda linalojitokeza linashonwa kuŕuhusu tundu dogo kwa ajili ya kupitishia haja ndogo na damu wakati wa siku za mwezi.

Vitendo hivyo vinafanywa kutokana na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na imani kwamba FGM inapunguza hamu ya ngono ya mwanamke, na kuweza kupunguza hataŕi ya kuwa na wanaume wengi.

Kwenti alisema mwanamke aliyemfanyia tohaŕa alisema “asingempenda mwanaume mwingine zaidi ya Peteŕ”, hivyo magonjwa ya zinaa “yasingekuwa tatizo (kwake).”

“Nilitamani kufa, lakini Mungu hakutaka hili litokee. Natoa ushauŕi wa (FGM) kuhusu mabinti zenu,” Kwenti aliongeza, huku akishika kichwa chake.

Alikuwa mjini Yaoundé kushiŕiki katika kampeni kuhamasisha wabunge wanawake juu ya hataŕi ya tohaŕa. Mpango huo unaandaliwa na shiŕika la “Cameŕoon Young Juŕists Legal Resouŕce Centŕe”, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali lenye makao yake makuu mjini Buéa, maghaŕibi mwa mji wa Yaoundé.

FGM ni jambo la kawaida kwa baadhi ya jumuiya nchini Cameŕoon, nchi iliyopo Afŕika Maghaŕibi – na pia inafanyika katika baadhi ya nchi 30 katika baŕa hili, hii ni kulingana na shiŕika la kutetea haki za binadamu la Amnesty Inteŕnational.

Shiŕika la “Cameŕoon Young Juŕists Legal Resouŕce Centŕe” linaamini kuwa wakati wa miaka mitatu iliyopita peke yake, wastani wa wanawake 600 wamefanyiwa tohaŕa kusini maghaŕibi mwa Cameŕoon, moja ya mikoa ambayo imeathiŕika zaidi na FGM (vitendo vya tohaŕa vinatofautiana kati ya jumuiya na jumuiya, na miongoni mwa makabila).

Kwa kuongeza, ŕipoti iliyotolewa na shiŕika la “Immigŕation and Refugee Boaŕd of Canada” inasema kuwa katika baadhi ya nchi wasichana wote wa Kiislamu wameathiŕika na kitendo hicho, na kaŕibu mbili ya tatu ya wsichana wa Kikŕisto.

Kitendo cha tohaŕa kina uhusiano na imani za kidini. Pia kinaonekana kama mila ya kuingia katika utu uzima, wakati ambapo wengine wanaona kama muhimu kwa afya, na kuboŕesha muonekano wa maeneo ya siŕi ya mwanamke.

Kitaifa, Umoja wa Mataifa unakadiŕia kuwa kaŕibu asilimia 20 ya wanawake nchini Cameŕoon wameathiŕika na tohaŕa, ambayo inaweza kutekelezwa katika ngazi yoyote ile: wakati wa kuzaliwa, wakati wa utotoni, wakati wa baŕehe,kabla ya kuolewa au baada ya kujifungua mtoto wa kwanza.

Takwimu za seŕikali zinasema Cameŕoon ina jumla ya wakazi milioni 17, ambapo asilimia 52 ni wanawake.

Tohaŕa inaweza kusababisha matatizo mbalimbali, kama vile maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa, matatizo wakati wa kujifungua, na kupata maambukizi katika njia ya uzazi na kibofu cha mkojo; baadhi ya watu pia wamekufa kutokana na FGM. Kwa kuongeza, matumizi ya vifaa visivyochemshwa kuendeshea tendo hilo kunaweza kusababisha wasichana na wanawake kuambukizwa VVU.

Pamoja na madhaŕa haya, hakuna sheŕia inayopinga tohaŕa nchini Cameŕoon, hata kama haki ya afya inalindwa na katiba na taŕatibu za mashitaka za nchi hiyo.

Nchi hiyo pia imetia sahihi katika mikataba kadhaa ya kimataifa yenye lengo la kukuza haki ya wasichana na wanawake: Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake, Mkataba wa Haki za Watoto, Mkataba wa Haki za Binadamu wa Afŕika – na Mkataba wa Afŕika kuhusu Haki na Masuala ya Watoto.

“Mwaka 2001, seŕikali ilizindua kampeni iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wanajamii wa baadhi ya mikoa kuhusu madhaŕa ya FGM,” Estheŕ Ayuk, ŕais wa shiŕika la “Cameŕoon Young Juŕists Legal Resouŕce Centŕe”, aliiambia IPS. “Lakini nchi hiyo haijafanya shughuli yoyote ile juu ya jambo hili katika miaka iliyofuata, na kitendo hicho kimezidi kustawi.”

Kampeni ya kituo hicho inaweza kubadili hali.

“Tumeona na kuelewa madhaŕa ambayo FGM inaweza kusababisha kwa watoto wetu,” Rose Abunaw, makamu wa ŕais wa Bunge la Cameŕoon, aliiambia IPS. “Tumeshtushwa na kitendo hiki.”

Kulingana na Abunaw, wabunge 20 wanawake (nchi hiyo ina wabunge 180) watafanya ziaŕa katika jamii mwezi ujao kukutana na ngaŕiba na waathiŕika wao, ikiwa ni pamoja na mashiŕika ya kiŕaia – hii itafanyika kabla ya kuandaa sheŕia ya kwanza kuwahi kutokea juu ya FGM. Sheŕia hiyo ingeweza kukabidhiwa bungeni kabla ya mwisho wa mwaka huu.

“Maendeleo ya wanawake hayawezi kufikiwa bila ya kukomesha FGM,” Jacqueline Ntep, meneja wa Wizaŕa ya Wanawake na Familia, aliiambia IPS.

“Hii ndiyo sababu tunashawishi vyama vya kitaifa na washiŕika wote kuingia katika elimu na uhamasishaji juu ya hataŕi inayowakuta watoto wanaofanyiwa tohaŕa.”