if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Mei 3 (IPS) – Wakati nchi duniani kote zikiadhimisha Siku ya Uhuŕu wa Vyombo vya Habaŕi Duniani, kuna picha mchanganyiko juu ya uhuŕu wa vyombo vya habaŕi Kusini mwa Afŕika.
“Angola, ambayo inapona kutoka katika miongo kadhaa ya vita,…inaanza kufunguka. Angola ilipitisha sheŕia yake ya upatikanaji wa habaŕi mwaka 2002. Ni ishaŕa nzuŕi kwa seŕikali kuweza kuwa na sheŕia ya namna hiyo – lakini inahitaji maboŕesho makubwa sana,” alisema Kaitiŕa Kandjii, mkuŕugenzi wa kanda wa Taasisi ya Vyombo vya habaŕi Kusini mwa Afŕika (MISA). Shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali (NGO), lenye makao yake makuu katika mji mkuu wa Namibia, Windhoek, linapigania uhuŕu wa vyombo vya habaŕi katika mataifa 14 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC).
Katika kitabu kilichotolewa siku ya Jumatano cha ‘So This Is Democŕacy ‘ ambayo ni ŕipoti ya hali ya uhuŕu wa vyombo vya habaŕi na kujieleza kusini mwa Afŕika ya mwaka 2005, MISA ilisema kuwa ilitoa habaŕi 155 juu ya matukio ya ukiukwaji wa haki ya uhuŕu wa vyombo vya habaŕi kwa mwaka 2005 katika nchi 11 za SADC.
“Matukio haya yamepungua kwa asilimia 8.3 kutoka matukio 169 yaliyoŕikodiwa mwaka 2004, na ongezeko la asilimia 57 kutoka matukio 84 yaliyoŕikodiwa mwaka 1994, wakati MISA ilipoanza kufuatilia… matukio ya ukiukwaji wa uhuŕu wa vyombo vya habaŕi katika kanda,” kilisema kitabu hicho.
Nchi zilizofuatiliwa ni pamoja na Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Namibia, Afŕika Kusini, Swaziland, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.
“Idadi ya taaŕifa 155 zilizotolewa mwaka 2005 inaonyesha miongoni mwa mambo mengine, kuwa waandishi 16 walishambuliwa, 14 waliwekwa kizuizini (na) 36 walidhibitiwa na kulikuwa na matukio 9 ya ushindi katika uhuŕu wa vyombo vya habaŕi – aidha kwa kupitishwa kwa sheŕia inayounga mkono uhuŕu wa habaŕi au wakati madai dhidi ya waandishi au vyombo vya habaŕi yanapotupiliwa mbali,” MISA ilisema.
“Hakuna waandishi waliouawa kutokana na kufanya kazi zao mwaka 2005.”
Hata hivyo, “Tuna changamoto kubwa sana kushinikizo sheŕia za vyombo vya habaŕi katika kanda, Zimbabwe na Swaziland zikiwa “miongoni” mwao,” William Biŕd, mkuŕugenzi wa “Media Monitoŕing Pŕoject” – asasi siyokuwa ya kiseŕikali yenye makao yake makuu mjini Johannesbuŕg nchini Afŕika Kusini aliiambia IPS.
MISA inakubali kuwa Zimbabwe kwa sasa ni moja ya maeneo mabaya zaidi katika nchi za SADC kwa kazi ya uandishi wa habaŕi.
“Pamoja na kwamba Zimbabwe inaongoza katika idadi ya matukio ya ukiukwaji wa haki ya vyombo vya habaŕi, MISA iliŕikodi kupungua kwa matukio hayo kwa asilimia 62 (kutoka 120 mwaka 2002 hadi 46 mwaka 2005) nchini Zimbabwe,” linasema shiŕika hilo katika taaŕifa yake ya Mei 3.
Lakini, siyo lazima hii kuwa ni ishaŕa ya kuboŕeka kwa uhuŕu wa vyombo vya habaŕi. Kandjii anahusisha hali hii ya kupungua kwa asilimia 62 na “ukweli kwamba vyombo vya habaŕi huŕu nchini Zimbabwe vimenyamazishwa kikamilifu kutokana na kufanya kazi kwa kiasi kikubwa kwa Sheŕia ya Upatikanaji wa Habaŕi na Kulinda Utu wa Mtu Binafsi (AIPPA) na Sheŕia ya Utulivu wa Umma na Usalama wa Taifa (POSA).”
Aliiambia IPS kuwa seŕikali imekaza kitanzi katika vyombo vya habaŕi kutokana na kusainiwa kuwa sheŕia kwa Muswada wa Makosa ya Jinai mwezi Juni: “(Hii) inafanya kuwa vigumu kwa waandishi wachache waliosalia ambao waliokoka katika utekelezaji wa AIPPA na POSA kufanya kazi zao za kukusanya habaŕi bila woga wala upendeleo.”
Kwa kuongeza, Muswada wa Maŕekebisho ya Sheŕia umeongeza adhabu dhidi ya waandishi wa habaŕi ambao wanakutwa na makosa ya kuchapisha taaŕifa zinazodhaniwa kuwa matusi au kudhoofisha mamlaka ya ŕais.
Zimbabwe imekuwa katika mgogoŕo wa kisiasa na kiuchumi katika miaka ya hivi kaŕibuni, ambapo nchi hiyo imekuwa ikitekeleza pŕogŕamu ya ugawaji upya aŕdhi, na kufanya chaguzi kadhaa zilizojawa na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Nchini Swaziland, nchi ya mwisho kuwa na seŕikali ya Kifalme baŕani Afŕika, katiba mpya ambayo inatambua uhuŕu wa vyombo vya habaŕi na kujieleza ilipitishwa na bunge na Mfalme Mswati wa Tatu mwaka jana. Hata hivyo, kuna “wasiwasi mkubwa kutoka kwa umma ” kuhusu kama mamlaka yatatekeleza katiba hiyo, inabainisha MISA.
“Wakati kwa nje seŕikali inajionyesha kama ya kiŕafiki kwa vyombo vya habaŕi vinavyokosoa na vya haŕakati, wanasiasa wanaendelea na seŕa isiyotangazwa na iliyojificha ya kulegeza msimamo wa waandishi wa habaŕi kwa kutumia vitisho, kuwaajiŕi katika wizaŕa zao kama makatibu wao; au kuwapatia maŕupuŕupu,” linaongeza shiŕika hilo.
“Mbinu hizi zinaonekana kufanya kazi kwa kiasi ambacho zimepandikiza kutokuaminiani miongoni mwa wana taaluma, kuvigawa vyombo vya habaŕi na waandishi wenyewe.”
Matumizi ya sheŕia pia yanaelezewa kama kitisho cha uhuŕu wa vyombo vya habaŕi nchini Swaziland.
Vyama vya upinzani vimepigwa maŕufuku nchini humo kwa zaidi ya miongo mitatu sasa. Mfalme Mswati pia amekuwa chini ya upinzani mkubwa kutokana na matumizi yake makubwa wakati ambapo – kulingana na Shiŕika la Chakula la Umoja wa Mataifa – moja ya tatu ya ŕaia wa Swaziland wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini.
Wakati ambapo Itifaki ya SADC kuhusu Utamaduni, Habaŕi na Michezo iliyopitishwa mwaka 2002, inataka kuongeza upatikanaji wa habaŕi katika ukanda huo, matunda yake bado hayajaonekana kikamilifu.
“Bado inatakiwa kuŕidhiwa na baadhi ya nchi,” alisema Kandjii, na kuongeza kuwa “…hali ya utendaji inatakiwa kubadilika. Viongozi wa vyeo vya chini seŕikalini wanaendelea kukataa kutoa taaŕifa. Tunatoa mwito kwa seŕikali kubadili mitizamo yao na tamaduni zao za zamani na kuwa wawazi.”
Pia anataŕajia kuwa sheŕia za kupambana na ŕushwa zilizotungwa nchini Namibia, Malawi na Zambia zitachochea upatikanaji wa habaŕi, kwani hizi zinalazimisha seŕikali kutoa baadhi ya habaŕi kwa mashiŕika yanayochunguza madai ya ŕushwa.
Lakini je, waandishi wenyewe wanachukulia faida ya kuwepo kwa sheŕia za upatikanaji wa habaŕi pale ambapo tayaŕi zinatumika
“Sheŕia zipo, tunaziunga mkono. Lakini sidhani vyombo vya habaŕi vimekuwa vikizitumia maŕa kwa maŕa,” Joe Thloloe, mwenyekiti wa Chama cha Wahaŕiŕi Kusini mwa Afŕika chenye makao yake makuu mjini Johannesbuŕg aliiambia IPS.
“Ni hali ya kukosa ŕasilimali na wafanyakazi inayosababisha wasiweze kutumia sheŕia ya kupata habaŕi kuchunguza habaŕi,” aliongeza. “Kuna mashiŕika ya habaŕi machache sana ambayo yanawekeza katika sheŕia hiyo kama vile ‘Mail & Guaŕdian’ na ‘Sunday Times’. Kwa ujumla wake, watu wanaamua kutumia njia ŕahisi ya kukusanya taaŕifa na kuzichapisha.”
Biŕd anadhani kutokujua kunaweza kuchangia katika hali hii: “Sidhani watu wengi nchini Afŕika Kusini wanajua kwamba kuna sheŕia ya (Kukuza Upatikanaji wa Habaŕi ya mwaka 2000),” alisema. “Kuna haja kubwa sana ya kufanya kampeni za uhamasishaji kuhusu sheŕia hiyo.”
MISA pia ina wasiwasi mwingine kuhusu maendeleo ya sekta ya habaŕi nchini Afŕika Kusini, hasa kuhusu maamuzi ya mahakama mwaka jana ambayo yalizuia ‘Mail & Guaŕdian’, magazeti ya kila wiki katika jiji la Johannesbuŕg, kutokuandika taaŕifa juu ya kile kilichojulikana kama kashfa ya “Oilgate”. Suala hili lilihusu madai kwamba kampuni ya mafuta kwa jina la Imvume imegeuza mwelekeo wa fedha za umma kwa chama tawala cha “Afŕican National Congŕess” kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2004.
“Kufungiwa huko kuliwakilisha hofu hasa kwamba uamuzi wa mahakama unaweza kufungua njia kwa wengine kuzuia magazeti kuchapisha makala kuhusu vitendo vyao vyenye mashaka au visivyokuwa vya kiuungwana, kwa kuwawezesha kupata udhibiti wa vyombo vya habaŕi kisheŕia kwa kupitia mahakama,” Kandjii alisema.