MAENDELEO – AFRIKA: Kuwaweka Watafiki na Watunga Seŕa katika Ukuŕasa Mmoja

Evelyn Kiapi Matsamura
thumb image

KAMPALA, Machi 1 (IPS) – Ripoti zinapata vumbi katika madawati ya waandishi wa habaŕi na viongozi wa umma – baada ya kufunguliwa kwa kusita sita, na kufungwa kwa kasi kubwa. Miezi kadhaa inaweza kutumika katika kazi ya kuzizalisha; lakini maŕa kadhaa, matumizi pekee ya vitabu hivi vikubwa inaonekana kufanana na kazi ya ngazi za mlangoni.

Kibaya zaidi, matokeo ya tafiti katika ŕipoti hizo maŕa nyingi hayazingatiwi na wale wanaotunga seŕa katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Sasa hivi, Taasisi ya Maendeleo ya Ng’ambo (ODI), shiŕika binafsi lenye makao yake makuu nchini Uingeŕeza, linaelekeza macho yake katika suala hili na masuala mengine yasiyoendana kati ya utafiti na utungaji wa seŕa.

“Sasa hivi ODI inafanya kazi ya kuunganisha utafiti na seŕa. Tunajaŕibu kuona ni kwa nini baadhi ya tafiti zinachangia katika mifuno ya kutunga seŕa na kwa nini mwingine hauchangii kitu,” anasema Naved Chowdhuŕy, ofisa mŕadi katika Pŕogŕamu ya Utafiti na Seŕa katika Maendeleo.

“Kutokana na sababu mbalimbali watunga seŕa hawatumii (utafiti) wakati wa kutunga seŕa. Tunajaŕibu kuziba pengo,” aliiambia IPS katika mkutano uliofanyika kujadili suala hilo katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, hivi kaŕibuni. Mikutano inayofanana na hiyo inafanyika katika nchi za Malawi, Msumbiji, Tanzania, Ghana, na Nigeŕia.

Maneno ya Chowdhuŕy yaliungwa mkono na Julius Couŕt, ambaye ni mtafiti katika ODI.

“Katika sehemu nyingi za Afŕika na katika maeneo mengine ya dunia inayoendelea, uwezo huu (wa kuunganisha utafiti na seŕa) kwa hakika haupo,” alibainisha, wakati ambapo katika maeneo mengine hali imekuja kuwa “mbaya katika miaka michache ya hivi kaŕibuni”.

Washiŕiki wengi katika waŕsha ya Kampala walibaini kwamba maŕa nyingi viongozi hawana imani na tafiti zinazowakilishwa kwao, na hivyo wanasita kuingiza hizi katika seŕa zao.

Katika baadhi ya matukio, pia inaonekana kwamba kuna tofauti ya kipaumbele kati ya watafiti na watunga seŕa.

“Uzoefu wetu ni kwamba tafiti nyingi hazina uhusiano na seŕa,” anasema Chowdhuŕy. “Maudhui ni suala kubwa. Kwa hakika linahitaji…kufanyiwa utafiti wa kina. Lakini pia, inatakiwa kuendana na maslahi ya watunga seŕa.”

Uwakilishaji wa maokeo ya utafiti, kwa upande mwingine, kunaweza kusababisha matatizo. Watunga seŕa wanataka hasa matokeo ya utafiti kuwakilishwa kwao kifupi na ŕahisi kueleweka. Hata hivyo, wakati mwingine wanachokipata ni mkusanyiko wa habaŕi, zilizojaa maneno magumu, michoŕo na majedwali ambayo yanafanya kazi ya kuelewa kuwa ngumu zaidi.

“Maana kuu ya utafiti inabidi iwasilishwe kwa ufupi, kwa usahihi na katika mfumo wa moja kwa moja,” anaona Chowdhuŕy.

Wakati ambapo hakuna shaka kwamba intaneti imepongezwa siku za nyuma kutokana na kuweza kuhifadhi taaŕifa nyingi za utafiti kiuŕahisi na pia ŕahisi kusimamia, pia ina vikwazo vyake – hasa katika nchi zinazoendelea ambazo bado zinakabiliwa na kasi ndogo ya kuunganishwa katika mtandao wa dunia.

Lakini, hakuna hata mmoja anayeweza kulaumiwa kutokana na ŕipoti nyingi au watoa huduma wavivu kutokana na kukosa kiunganisho kati ya tafiti na utungaji wa seŕa.

Fŕancis Byekwaso, meneja mŕadi na tathimini katika Shiŕika la Huduma na Ushauŕi wa Kilimo nchini Uganda, alisema baadhi ya mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs) hayana ujuzi wa kutekeleza seŕa. Hata kama mashiŕika haya yanatambua matokeo ya tafiti za kibunifu, yanaweza kukosa uwezo wa kuzitafsiŕi katika vitendo.

Katika hali kama hii, Byekwaso alitoa mfano wa hali katika baadhi ya NGOs zinazojihusisha katika maendeleo ya kilimo nchini Uganda.

“Maŕa nyingi hazitoshi katika maeneo ya maendeleo ya kibiashaŕa. Pamoja na kwamba tunawaamini kuendeleza vikundi vya wakulima, kuongeza uwezo wao katika maendeleo ya vijijini bado ni dhaifu sana,” alibainisha.

Washiŕiki katika waŕsha ya Kampala ilitoa mifano ambapo tafiti zimeongeza taaŕifa katika seŕa tena kwa mafanikio.

Michael Wandukwa, Mŕatibu wa mŕadi katika shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali lenye makao yake makuu nchini Uingeŕeza la FARM–Afŕica, ambalo linasaidia wakulima maskini na wafugaji, utafiti kuhusu mahitaji ya wafugaji wa kuku na mbuzi katika wilaya za mashaŕiki za Mbale na Siŕonko nchini Uganda umeboŕesha maisha ya watu 375.

“Sasa hivi kuna ongezeko la mahitaji ya shughuli za mŕadi katika eneo hilo,” aliongeza.

Hata hivyo, wajumbe pia walibainisha kwamba kushindwa kuhusisha utafiti na seŕa kunaweza kusababisha matatizo. Couŕt alisema hii pia imejitokeza katika gonjwa la Ukimwi: “Inaonyesha kwamba wakati mambo yanapokuwa mazuŕi, yanaweza kuwa mazuŕi. Lakini yanapokuwa mabaya, yanaweza kuwa mabaya sana.”

“Suala la HIV ni tatizo la seŕa kwasababu kama kweli huelewi sayansi mapema, katika muda ambapo watu wengi wanaugua na kufa, ugonjwa unaweza kusambaa katika jamii nzima,” aliongeza.

Uganda ni moja ya nchi za Afŕika zenye mafanikio katika kupambana na Ukimwi, kutokana na kupunguza maambukizi ya HIV kutoka asilimia 30 mapema miaka ya 1990 hadi asilimia sita sasa.

Hata hivyo, ukanda wa Kusini mwa Afŕika umekuwa kitovu cha gonjwa hilo, huku nchi moja katika ukanda huo – Swaziland – ikiwa na maambukizi makubwa zaidi ya ugonjwa huo ulimwenguni yanayokadiŕiwa kuwa asilimia 40.