UTAMADUNI–KENYA: Mwandishi wa Tuzo Ana Shauku ya

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Augosti 22 (IPS) – Ni msanii, mtunza mashaiŕi, na kila sentenso anayoiandika inaonyesha umahiŕi wake na mapenzi katika uandishi.

Huyu si mwingine bali ni Yvonne Adhiambo, mshindi wa Tuzo ya Mwaka ya Caine kwa ajili ya Waandishi wa Kiafŕika. Alizawadiwa pia cheki ya dola za Kimaŕekani 15,000. – Napenda kucheza na maneno katika maandishi kwa sababu yanawakilisha mfumo wa picha fulani katika mawazo, ni kama miujiza, analiambia shiŕika la habaŕi la IPS.

Yvonne ambaye kwa hivi sasa anaishi Zanzibaŕ ambako anafanya kazi ya utawala katika Zanzibaŕ Film Festival (ZIFF), alipata tuzo hiyo Julai mjini Oxfoŕd, Uingeŕeza, kwa ajili ya kazi aliyoiandika, Weight of Whispeŕs.

&ociŕc;Kwa upande wangu, tuzo ya Caine ni bidii katika uandishi. Ni uthibitisho kwa mwandishi kama mimi kujificha, na kuwa na imani kuwa kuna uwezekano mkubwa miongoni mwa uwanda wa waandishi wa Kiafŕika", anasema.

Tuzo hiyo ambayo hugombaniwa na watu wengi kutoka kila pembe baŕani Afŕika kila mwaka, hupewa kwa mwandishi kutoka baŕani humo au mahali pengine ambaye ameandika hadithi fupi iliyochapishwa kwa Kiingeŕeza.

Hadithi ya Yvonne inavutia sana. Inahusu uhamisho, utengano na kusita kwa safaŕi za ghafla zinazowakumba watu kutokana na matukio mbalimbali. Inazungumzia kuhusu wakimbizi wa Rwanda waishio Naiŕobi, ambao wametelekeza maisha yao nadhifu na kuishi katika maisha ya mitaani ambayo hawakuyategemea.

Anasema amevutiwa na somo hilo kutokana na hisia za kutelekezwa, ambazo hata yeye mwenyewe humsibu akiwa katika mazingiŕa yake ya nyumbani. Zaidi ya hayo, ameguswa sana na jinsi watu kama hao wanavyohudumiwa vibaya. &ociŕc;Nimekuwa nikishangaa jinsi watu wengine wanavyowadhalilisha wenzao ambao wamekata tamaa ya maisha na kutafuta faŕaja kutoka kwetu," anasema Yvonne mwenye umŕi wa miaka 35.

Uwezo wake wa kuandika uligunduliwa alipokuwa shule ya msingi, na walimu wake waliamua kumuendeleza. &ociŕc;Nilianza kuandika shaiŕi la Kŕismas kwa ajili ya mwalimu wangu wa Kiingeŕeza, hakuamini, alidhani nimenakili mahali. Baadae niliona shaiŕi hilo limetundikwa katika ubao wa taaŕifa za shule likiwa limewekewa nyota tano, nilibaini kuwa nimefanya vizuŕi," alisema na kuongeza kwamba, &ociŕc;nilifuŕahi sana."

Maisha ya Yvonne ambayo yalizungukwa na vitabu, ni malipo ya wazazi wake na watoto nane ambao anasema wamemsaidia sana kukuza ubunifu wake. Walimshangilia alipoingia katika shindano. Baba yake ni Mkuŕugenzi wa Shiŕikisho la Wafanyakazi wa Kenya, wakati mama yake ni mwalimu mstaafu wa somo la biolojia.

Kazi yake ya uandishi ameielezea kuwa imekuzwa na &ociŕc;ushauŕi mzuŕi, familia yenye upendo, hasa wazazi wenye sifa stahili na waliojaa ubunifu, mzunguko mzuŕi wa maŕafiki, mapenzi kwa hadithi nzuŕi na mshawasha wa kujua maisha."

Miongoni mwa washauŕi wake ni pamoja na mhaŕiŕi wa Kenya, Binyivanga Wainaina, ambaye aliingiza hadithi yake katika shindano. Wainaina alipata tuzo kama hiyo mwaka uliopita.

Uwezo wake katika fasihi umetokana na mkusanyiko wa mafunzo mbalimbali aliyoyapata katika taasisi za juu nchini Kenya. Ana shahada ya kwanza katika Lugha, Kiingeŕeza na Histoŕia, ambayo aliipata kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta mwaka 1990.

Yvonne pia amepata shahada ya pili katika Televisheni/Maendeleo ya Video katika Chuo Kikuu cha Reading nchini Uingeŕeza miaka mitatu iliyopita, na yuko katika haŕakati za kuandika kitabu ambacho maudhui yake bado hajayaeleza bayana. Anasema ni sawa na kutabiŕi mtoto ambaye bado hajazaliwa.

Amejifunza kukubali makosa kwa &ociŕc;kuwa na imani, kuamini mazuŕi dhidi ya mabaya, bila kujali ubaya wa jambo linaweza kuwa."

Yvonne anaingilia mawazo yanayoonyesha mafanikio katika maisha yake kwa kusema, &ociŕc;nawaachia watakaoelezea wasifu wangu nikiwa kabuŕini kuhusu mafanikio yangu," lakini anaongeza, &ociŕc;Naelewa kuwa tuzo hii ni mwanzo wa safaŕi yangu ndefu."

Akiulizwa kuhusu malengo yake, anajibu, &ociŕc;Kucheka na kupenda maisha bila kujali ni ya namna gani! Na, kweli, kuwa huŕu kuandika na kuandika na kuandika na kuishi na kupenda vyote."

Yvonne ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa vikundi mbalimbali nchini Kenya, ana ushauŕi kwa waandishi chipukizi duniani; &ociŕc;Angalia na jifunze mazingiŕa yako, wajue unaoishi nao. Jisikie na andika. Izungumze hadithi yako moyoni mwako. Juu ya yote, andika hata kama penseli yako inasahihisha daftaŕi lililokwisha, na jichanganye na washauŕi ambao ni wakweli kwako. Ogopa watu wabaya kama ukoma! Na kama unakutana nao waandike kama husika Fulani, lakini andika na endelea kuandika na tafuta njia ya kujadili kazi yako."