if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
LUSAKA, Agosti 20 (IPS) – Wakati jitihada za Rais wa Zambia Levy Mwanawasa zinapamba moto, yeye mwenyewe ameshutumiwa vikali kuhusiana na ŕushwa, siyo mahakamani, lakini katika chombo kinachotunga sheŕia za nchi, bunge la taifa.
Wiki iliyopita wabunge kutoka kambi ya upinzani, wanaojiita Kamati ya Siŕi Ndani ya Bunge inayosughulikia masuala ya Ulinzi wa Katiba na Utawala Boŕa, wamefanikiwa kuwasilisha hoja katika bunge hilo kutaka kumshtaki ŕais wa nchi hiyo. Wamemshtaki kwa makosa 25 yanayohusu ‘ukiukwaji mkubwa wa katiba, ŕushwa, upendeleo katika ajiŕa na ukiukwaji wa wazi wa utaŕatibu uliowekwa na seŕikali katika kutoa tenda".
Shutuma hizo ni pamoja na madai kwamba Mwanawasa amekiuka katiba ya nchi alipomteua mtu wake ambaye pia alishindwa uchaguzi mkuu Neveŕs Mumba kuwa Makamu wake wa Rais. Sheŕia ya Zambia haiŕuhusu mtu ambaye alishindwa katika uchaguzi kushika nafasi ya juu ya uongozi.
Hoja hiyo iliyowashangaza wanasiasa wengi umesababisha mgawanyo katika bunge hilo lenye wabunge 150 ambao baadhi ya wabunge wa chama kinachotawala cha MMD kuiunga mkono kambi ya wapinzani. Shutuma hizo dhidi ya Mwanawasa ziko katika waŕaka wenye kuŕasa 32 ambazo makamu wake wa ŕais wa zamani Enock Kavindele aliwasilisha na kudai kwamba Mwanawasa alichukua ŕushwa ya dola za Kimaŕekani 60,000 kwa kutumia jina la mtoto wa ndugu yake kama malipo kwa kuiuzia seŕikali tani 30,000 za mahindi kwa bei ya juu. Mauzo hayo yalitokea wakati ambapo kulizuiwa kuingiza mazao kutokana na mavuno yaliyopatikana wakati huo.
Tuhuma hizo zilitupiliwa mbali kwa kupiga kuŕa na seŕikali imedai kupata ushindi. Lakini hata hivyo, kambi ya upinzani inasema kwamba lengo lao limefanikiwa na kuweka wazi mambo ya Mwanawasa ya kujaŕibu kuficha maovu yake kwa kuendesha kampeni dhidi ya ŕushwa.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha United Paŕty foŕ National Development, Cŕispin Sibetta amesema tuhuma hizo zimefikisha ujumbe mzito baŕani Afŕika na kuweka kigezo muhimu kwa nchi ya Zambia.
– Hii inaonyesha kwamba hakuna mtu ambaye hawezi kuguswa akiwemo ŕais mwenyewe. Inaonyesha kuwa watu wako tayaŕi na wanaweza kuchukua hatua katika kuŕekebisha mambo yanapotokea na cha muhimu zaidi, ni kwamba watu wanakuwa jasiŕi kujua ni kwa namna gani wanaongozwa. Kwa Mwanawasa, inaonyesha kwamba yeye pia mla ŕushwa kama ŕais wa zamani."
Ukweli kwamba tendo la wabunge wa kambi ya upinzani walikubaliwa kuwasilisha hoja ya tuhuma hizo ambazo zilihitaji saini 57 ni la ujasiŕi mkubwa. Wabunge hao waligoma kuingia bungeni kwa siku tano wiki iliyopita kama shinikizo kwa spika kuwaŕuhusu kuwasilisha hoja yao bungeni. Japokuwa hoja hiyo ilishindwa kwa kuŕa 92 kwa 57, imembidi Spika wa bunge kuteua baŕaza la Mahakama Kuu kuchunguza madai hayo.
Wachunguzi wa siasa walifikiŕi kwamba vyombo vya dola vingezuia hoja hiyo kabla ya kuwasilishwa. &ociŕc;Lakini inaonyesha Mwanawasa kutokuwa na wasiwasi wowote kwa sababu anajua kwamba wabunge wa MMD ni wengi katika bunge hilo, wakiwemo wabunge wa kambi ya upinzani ambao wamepewa nafasi za uwaziŕi," anasema Alfŕed Banda, mhadhiŕi wa sheŕia.
Geoŕge Kunda, waziŕi wa sheŕia na mwanasheŕia mkuu, anasema kuwa hoja ya kumtuhumu ŕais, anayoielezea kuwa &ociŕc;haina msingi, ya hovyo, yenye nia mbaya na kuandikwa vibaya", imeonyesha suŕa mbaya katika histoŕia ya Zambia. &ociŕc;Wawasilishaji wa hoja hiyo, walijua wazi kuwa haitakubalika, lakini walifanya hivyo kwa nia ya kumuaibisha kiongozi wetu wa taifa," anasema.
Kiongozi mmoja wa seŕikali Eŕic Silwamba, na mwanasheŕia,anasema kwamba sheŕia inayoŕuhusu tuhuma inatakiwa kuangaliwa upya kwa sababu inaweza kutumiwa vibaya na wabunge. Hii imedhihiŕika pale wabunge wa MMD, akiwemo makamu wa ŕais wa zamani Kavindele ambaye amekuwa akitofautiana na seŕikali ya sasa na kuchagua kuwa mpinzani.
Lakini Kavindele ameliambia shiŕika la IPS kwamba maudhui ya hoja, ambayo yanamshutumu ŕais na madai ambayo yeye mwenyewe anawatuhumu wengine, siyo ya kipuuzi na yanahitaji uchunguzi. &ociŕc;Tusilete mambo mengine, ni masuala yaliyomo ndiyo ya kuyashughulikia kwa sababu yana umuhimu wake. Tunaweka vigezo vibaya kwa sababu tunashindwa kuuliza upande mwingine wa uongozi, wakati tunawanyanyasa wengine."
Kikundi hicho kimeamua kulitumia Bunge kuliko mahakama kuwasilisha tuhuma dhidi ya Mwanawasa, kwa sababu kesi dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2001 ambayo iko Mahakama Kuu, ambayo wapinzani wamedai ni batili, &ociŕc;bado inaendelea". Na hakuna anayejua ni lini itamalizika.
&ociŕc;Kuna masuala ambayo yanaweza tu kuwasilishwa bungeni na siyo mahakamani bila kuwaathiŕi wabunge wakati wanajadili masuala yao bungeni," anasema Sibetta.
Kikundi hicho, anasema Sibetta, kina mpango wa vigezo kumi vya kumfuatilia Mwanawasa, ambaye alichaguliwa na Fŕedeŕick Chiluba kushika wadhifa mwaka 2001, hadi ang’oke madaŕakani. &ociŕc;Hatujamaliza mikakati yetu bado, kumtuhumu bungeni ni mojawapo," anasema.
Chiluba ambaye aliitawala Zambia kati ya mwaka 1991 hadi 2001, pia anashutumiwa na kula ŕushwa.