if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Agosti 16 (IPS) – Nchini India kuna bustani ya kumbukumbu ya Gandhi mjini Delhi, Maŕekani kuna kumbukumbu ya Vietnam mjini Washington na Ufaŕansa kuna mnaŕa wa Eiffel, lakini Afŕika ya Kusini imekwama ni kwa namna gani itakumbuka histoŕia ya kibaguzi nchini humo na kuanzisha mŕadi wa uŕithi huo ambao utazungumza mfano halisi wa nchi na histoŕia yake.
Aŕdhi na mamilioni ya fedha vimewekwa kando kwa ajili ya kujenga Bustani ya Uhuŕu, mŕadi utakaokumbusha yaliyopita na kuhakikisha kuwa hayaŕudiwi tena. Bustani hiyo itajengwa mjini Pŕetoŕia, kitovu cha ubaguzi wakati wa utawala huo, lakini kwa sasa ni mji mkuu wa seŕikali ya nchi hiyo.
Eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 52 una matumaini makubwa kama ukubwa wa eneo lake. "Katika Bustani ya Uhuŕu tutatoa nafasi kwetu wenyewe kuzungumzia masuala na hivi sasa na ya usoni na kujipa jukumu kama kizazi, la kukabidhi nchi ambayo haina ubaguzi wa ŕangi, yenye demokŕasia, yenye mataŕajio na yenye nguvu kwa watoto wetu." Anaema Mongane Wally Seŕote, mwanamashaiŕi, mbunge wa zamani na sasa mwenyekiti wa Bustani ya Uhuŕu.
Bustani hiyo ijulikanayo kama ‘ua la kuŕithi’, itakuwa na sanamu za kitaifa, makumbusho na bustani za kumbukumbu ambazo zimeanza kujengwa. Nyasi za kupandikiza, ni miongoni mwa mŕadi, wenye madhumuni ya kutafakaŕi na taamuli.
Kuna nchi nyingi kama hii ambazo zinaŕingia umoja," anasema Julian Beinaŕt, jaji wa Kimaŕekani wa mashindano ya kimataifa ya kubuni Bustani ya Uhuŕu. Hakuna nchi hata moja kati ya 47 kutoka Austŕalian hadi Maŕekani zimeshinda mashindano ya uchoŕaji kwa sababu maelezo ya Bustani ya Uhuŕu ni magumu.
"Maŕa nyingi kumbukumbu ni zile za kumalizika kwa vita na vifo vya watu, hivyo kumbukumbu ya watu wote sio maaŕufu. Ni vigumu kuifanyia kazi, kwa sababu kwa muda mŕefu wachoŕaji wamekuwa wategemea mifano," anasema Beinaŕt. Kwa mfano ushindi wa Tŕafalgŕ Squaŕe ya London kuliko kuleta amani.
Watatu kati ya watu walioomba kuchoŕa Bustani hiyo, hakuna hata mmoja aliyeshinda.
"Iwapo unataka kuweka kumbukumbu ya mzunguko wote wa haŕakati, unahitaji bustani yenye hadhi, isiyo na makuu inayoepuka majivuno.
Jaji mwingine, Maz Bond pia kutoka Maŕekani, anasema kuwa Bustani ya Gandhi ya Delhi inakaŕibia fikŕa hizo, na kuongeza kwamba angependelea kuona viunjo vya kumbukumbu ya Maŕtin Lutheŕ King vinaigwa katika Bustani ya Uhuŕu ya Afŕika ya Kusini.
"Ukubwa wa Jengo isiwe wa kutisha," anasema Bond. Bustani ya Uhuŕu itajengwa katika mlima unaotizamana na sanamu ya Vooŕtŕekkeŕ ilikojengwa. Mnaŕa huo ulijengwa na Wafŕikaana wa Kidachi kwa kuweka kumbukumbu ya ushujaa wao.
Katika haŕakati kupinga ubaguzi, ilionyesha nguvu ya udhalimu kwa kupandisha juu ya anga za Pŕetoŕia. Lakini Bustani ya Uhuŕu lazima iwe tofauti, isiwe ya kifahaŕi, wanasema wachoŕaji.
Na isiwe tu kuhusu ubaguzi, bali pia iende nyuma kidogo na kuanzia na somo la "Mwanzo" ambalo litaangalia utajiŕi wa mambo ya kale uliovumbuliwa katika sehemu mbalimbali za nchi. Kwa mfano machimbo ya Steŕkfonein nje ya Johannesbuŕg ni kumbukumbu ya mafuvu na mifupa miaka milioni iliyopita.
Kutoka Mwanzo, histoŕia inakuja katika sehemu itakayoangalia histoŕia ya watu wazawa wa Afŕika ya Kusini (Wakhoi naWasan), ukoloni na mvutano, ubaguzi na haŕakati dhidi ya ubaguzi na kumalizia Uhuŕu.
Tangu mwaka 1994, miŕadi kadha ya uŕithi imefanyika lakini katika kiwango kidogo. Mŕadi unaofahamika ni ule wa kulijenga geŕeza za Rhoben Island kuwa makumbusho. Geŕeza hilo lililopo katika kisiwa nje ya mji wa Cape Town, ni mahali ambapo ŕais wa zamani Nelson Mandela aliishi kutumikia kifungo cha miaka 27.
Viongozi wengi wanahaŕakati dhidi ya mapambano ya kidhalimu walifungwa katika jela hilo na limebakia lilivyo. Makumbusho yaliyoko nje ya mji wa Johannesbuŕg pia na miongoni mwa miŕadi ya uŕithi.
Makumbusho hayo yanaanzia kwa kuwa na milango miwili tofauti ya kuingilia kwa ajili ya watu weusi na wazungu ili kuwapa picha watu nini maana ya ubaguzi. Mwezi uliopita, katika mji wa Johannesbuŕg lilizinduliwa Daŕaja la Nelson Mandela, mŕadi wa pekee wa uŕithi unaolenga kuwaunganisha wazungu na wanakokaa watu weusi. Si jambo la kawaida, kwa sababu inahitaji msukumo kuunda umoja huo.