{"id":4024,"date":"2014-08-31T13:40:01","date_gmt":"2014-08-31T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2014\/08\/31\/uhusiano-dhaifu-kati-ya-kuzuia-vvu-baani-afika-na-matumizi-ya-njia-za-uzazi-wa-mpango\/"},"modified":"2019-05-07T11:53:54","modified_gmt":"2019-05-07T11:53:54","slug":"uhusiano-dhaifu-kati-ya-kuzuia-vvu-baani-afika-na-matumizi-ya-njia-za-uzazi-wa-mpango","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2014\/08\/31\/uhusiano-dhaifu-kati-ya-kuzuia-vvu-baani-afika-na-matumizi-ya-njia-za-uzazi-wa-mpango\/","title":{"rendered":"Uhusiano Dhaifu Kati ya Kuzuia VVU Ba\u0155ani Af\u0155ika na Matumizi ya Njia za Uzazi wa Mpango"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI\u00a0 \u2013 Katika kukimbilia kuokoa watoto wachanga kutokana na maambukizi ya VVU na kutibu mama zao, wataalam wanaonya kuwa suala la msingi katika kuzuia VVU linapuuzwa ba\u0155ani Af\u0155ika \u2013 matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU\/UKIMWI.<\/p>\n<p>&lt;!\u2013\u2013mo\u0155e\u2013\u2013&gt;<\/p>\n<p>Wakati huo huo inajulikana kuwa uzazi wa mpango ni nguzo ya pili ya kuzuia kwa mafanikio maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), ikiwa ni pamoja na kuzuia maambukizi miongoni mwa wanawake na watoto na kutoa matunzo kwa wale walioambukziwa.<\/p>\n<p>&#8220;Mahitaji ya uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU ma\u0155a nyingi yanawekwa nyuma ya pazia, na shabaha kuu ikiwa ni kumfanya mama na mtoto kuwa na afya nzu\u0155i,&#8221; Flo\u0155ence Ngobeni\u2013Allen, msemaji wa Elizabeth Glase\u0155 Paediat\u0155ic AIDS Foundation, aliiambia IPS. Akiwa ni \u0155aia wa Af\u0155ika Kusini, alikutwa na VVU mwaka 1996, akapoteza mtoto wake kutokana na ugonjwa wa UKIMWI na kwa sasa ana watoto wa kiume wawili wenye afya nzu\u0155i.<\/p>\n<p>Uzazi wa mpango ni muhimu katika Af\u0155ika Masha\u0155iki na Kusini, ambako maambukizi ya VVU pamoja na kiwango kikubwa cha kutokufikiwa kwa mahitaji ya uzazi wa mpango, na ambako wanawake nane kati ya 10 wenye VVU wana um\u0155i wa kuzaa, kwa mujibu wa Shi\u0155ika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).<\/p>\n<p>Tafiti zinasema kuwa wanawake wanaoishi na VVU wana matamanio sawa kama siyo zaidi ya kujipatia watoto ikilinganishwa na wale wasiokuwa na VVU. Kupunguza kiwango cha uhaba wa huduma za uzazi wa mpango miongoni mwa wanawake hawa ni jambo muhimu ili kufikia lengo la kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa watoto kwa asilimia 90,&#8221; inasema \u0155ipoti ya Umoja wa Mataifa ijulikanayo kama Women Out Loud.<\/p>\n<p>Tafiti za wanawake wanaoishi na VVU nchini Kenya na Malawi zinaonyesha kuwa ka\u0155ibu \u0155obo tatu hawataki kupata watoto tena katika kipindi cha miaka miwili ijayo au milele, lakini ni \u0155obo tu walitumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.<\/p>\n<p>Udhaifu wa mipango<\/p>\n<p>Utafiti wa shi\u0155ika la Family Health Inte\u0155national miongoni mwa wanawake wanaoishi na VVU nchini Rwanda, Kenya na Af\u0155ika Kusini ulionyesha kuwa zaidi ya nusu hawakupanga kubeba mimba zao walizo nazo sasa au hivi ka\u0155ibuni.<\/p>\n<p>Pamoja na kuwa wanawake hao walitaka njia za uzazi wa mpango, upatikanaji wake ulikuwa mgumu. Moja ya kikwazo ilikuwa ni wafanyakazi wa afya: walikuwa hawana ujuzi wa kutoa aina mbalimbali ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU; walikuwa na imani potofu kuhusu usalama wa njia za uzazi wa mpango; wengi wao walitoa kondomu za kiume tu, pamoja na kwamba wanawake walipendelea vipandikizi na sindano, na wengi walikuwa wakitoa hukumu juu ya maisha ya kujamiiana ya wanawake hao.<\/p>\n<p>&#8220;Ma\u0155a nyingine manesi walisahau kuwa wanawake bado wana hamu ya kujamiiana hata kama wanaishi na VVU,&#8221; anasema Ngobeni\u2013Allen.<\/p>\n<p>Kutokufikiwa kwa mahitaji ya huduma za uzazi wa mpango nchini Kenya kunafikia asilimia 25 nchini kote lakini kunafika asilimia 60 miongoni mwa wanawake wanaishi na VVU, Dk John Ong&#8217;ech, mku\u0155ugenzi msaidizi katika Hospitali ya Kenyatta aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Upatikanaji duni wa huduma za uzazi wa mpango kwa wanawake wenye VVU ambao wana uwezekano wa kufa ma\u0155a sita hadi nane kutokana na matatizo ya mimba ikilinganishwa na wale wasiokuwa na VVU, &#8220;ni udhaifu katika mipango ya afya,&#8221; aliiambia IPS, pamoja na kwamba ni \u0155ahisi na inafanya kazi kutoa huduma za uzazi wa mpango kuliko PMTCT.<\/p>\n<p>Wanaume na mama wakwe<\/p>\n<p>Ma\u0155y Naliaka, ambaye anafanya kazi katika kitengo cha UKIMWI kwa watoto katika wiza\u0155a ya afya nchini Kenya aliiambia IPS kuwa uzazi wa mpango unapaswa uwe sehemu ya tiba ya VVU na kutoa aina mbalimbali za njia za kupanga uzazi.<\/p>\n<p>Lakini mifumo ya afya katika Masha\u0155iki na Kusini mwa Af\u0155ika ma\u0155a nyingi inakabiliwa na uhaba wa vifaa na kliniki nyingi hazina miundombinu ya kutosha.<\/p>\n<p>&#8220;Kutumbukiza kipandikizi kwa mwanamke kunahitaji mazingi\u0155a mazu\u0155i yenye vifaa vya kuua vijidudu,&#8221; Ong&#8217;ech anasema.<\/p>\n<p>Sindano ni njia inayotumiwa zaidi na wanawake kwasababu wanaweza kutumia bila waume zao kujua, anaongeza.<\/p>\n<p>Kukosekana kwa usawa wa kijinsia na wanawake kukosa ushawishi kunasababisha matumizi duni ya njia za uzazi wa mpango. Naliaka anasema kuwa katika utamaduni wa Kiaf\u0155ika, &#8220;mama mkwe anaweza kusababisha kuvunja ndoa kama hakuna mtoto anayezaliwa.&#8221;<\/p>\n<p>Do\u0155othy Namutamba, kutoka Jumuiya ya Kimataifa ya Wanawake Wanaoishi na VVU katika Af\u0155ika Masha\u0155iki (ICWEA), ambaye ofisi yake ipo Kampala, Uganda, aliiambia IPS kuwa wanawake wameumbwa kuwafu\u0155ahisha waume zao.<\/p>\n<p>&#8220;Kama mwanaume anadai anataka kuwa na watoto kumi ni lazima kukubali na kama hutaki atawatafuta kutoka kwingine,&#8221; anasema. &#8220;Wanaume wengi hawataki wanawake kutumia uzazi wa mpango, hilo ni tatizo kubwa.&#8221;<\/p>\n<p>Unyanyapaa na unyanyasaji wa majumbani unazidisha tatizo. &#8220;Wanawake wanahofia kutaja kuwa wameambukizwa VVU kutokana na kuwa wanaweza kukabiliwa na unyanyasaji wa kijinsia, na hii inazuia kupata njia za uzazi wa mpango,&#8221; Anthony Mbonye, kamishina wa Huduma za Afya nchini Uganda, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Kutokana na nguvu za wanaume katika utoaji wa maamuzi kuhusu mimba, huduma za afya ya uzazi zinazoshi\u0155ikisha wanandoa wawili ni muhimu, lakini &#8220;vituo vya afya vina msongamano mkubwa mno kuweza kuhudumia wanandoa wa kiume,&#8221; Naliaka aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Ushinikizaji wa kufunga kizazi kwa wanawake wanaoishi na VVU nchini Kenya, Malawi, Namibia, Af\u0155ika Kusini na Zambia, huku kukiwepo na kesi mahakamani, kunazidisha utata wa suala la haki na mahitaji ya uzazi na VVU.<\/p>\n<p>&#8220;Hii inaaibisha sekta ya afya,&#8221; anasema Naliaka. Hata hivyo, anaongeza, &#8220;kupitia kesi hizi, sekta ya afya na umma umeelewa kuwa wanawake hawa wana mahitaji ya uzazi kama ilivyo kwa wenzao wasiokuwa na vi\u0155usi.&#8221;<\/p>\n<p>Eneo moja la kutolea huduma<\/p>\n<p>Ili kusonga mbele, wataalam wanapendekeza kuunganisha VVU, uzazi wa mpango na huduma za uzazi na watoto wachanga ili kuokoa muda kwa watumiaji na wafanyakazi wa afya.<\/p>\n<p>Nchi saba za Kusini mwa Af\u0155ika zimeshaanzisha eneo moja la kutolea huduma ambapo wanawake wanaweza kupata ARVs, kupima kansa ya kizazi, ushau\u0155i wa kunyonyesha na uzazi wa mpango kwa wakati mmoja, chini ya jengo moja, ma\u0155a nyingine katika chumba kimoja chenye mhudumu wa afya.<\/p>\n<p>Kuunganisha huduma kunaokoa gha\u0155ama na kunaleta ufanisi, inasema UNFPA.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI\u00a0 \u2013 Katika kukimbilia kuokoa watoto wachanga kutokana na maambukizi ya VVU na kutibu mama zao, wataalam wanaonya kuwa suala la msingi katika kuzuia VVU linapuuzwa ba\u0155ani Af\u0155ika \u2013 matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi na VVU\/UKIMWI. &lt;!\u2013\u2013mo\u0155e\u2013\u2013&gt; Wakati huo huo inajulikana kuwa uzazi wa mpango ni nguzo ya pili ya&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":898,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-4024","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4024","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/898"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4024"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4024\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4090,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4024\/revisions\/4090"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4024"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4024"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4024"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}