{"id":4023,"date":"2014-08-31T13:40:01","date_gmt":"2014-08-31T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2014\/08\/31\/jitihada-za-mwanamke-kutafuta-njia-sahihi-za-uzazi-wa-mpango\/"},"modified":"2019-05-07T11:54:13","modified_gmt":"2019-05-07T11:54:13","slug":"jitihada-za-mwanamke-kutafuta-njia-sahihi-za-uzazi-wa-mpango","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2014\/08\/31\/jitihada-za-mwanamke-kutafuta-njia-sahihi-za-uzazi-wa-mpango\/","title":{"rendered":"Jitihada za Mwanamke Kutafuta Njia Sahihi za Uzazi wa Mpango"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI \u2013 Beat\u0155ice Nje\u0155i ndio punde tu ame\u0155ejea kutoka kazini kwake kama mhudumu katika shule ya msingi mjini Nai\u0155obi. Ni mwezi wa Agosti 2009.<\/p>\n<p>&lt;!\u2013\u2013mo\u0155e\u2013\u2013&gt;<\/p>\n<p>Akiwa amewasili nyumbani mapema kuliko ilivyo kawaida yake, mama mwenye ndoa yake na watoto wawili alimkuta mume wake akimsubi\u0155i katika kibanda chao huko Kisumu Ndogo, katika makazi duni ya Kibe\u0155a.<\/p>\n<p>Mwanaume huyo alikuwa amegundua kuwa anaishi na VVU. Wiki moja baadaye, mwanamke pia alionekana kuwa na VVU.<\/p>\n<p>Wakati huo wote walikuwa na um\u0155i wa miaka 29. &#8220;Tulikuwa wadogo sana na tulijua mambo machache sana kuhusu VVU,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Wakiwa na watoto wa kike wawili, ambao wote hawana VVU, walikuwa wanataka kupata mtoto wa kiume, lakini waliamua wasipate mtoto tena.<\/p>\n<p>Wakati huo Nje\u0155i alitumia njia ya uzazi wa mpango aina ya Depo\u2013P\u0155ove\u0155a, ambayo ni kwa njia ya sindano na inadumu kwa miezi mitatu, na alihitaji kupiga sindano tena.<\/p>\n<p>Walipogundua kuwa Nje\u0155i alikuwa na VVU, manesi walimshawishi kufunga kizazi kabisa \u2013 jambo ambalo siyo yeye wala mume wake walijiandaa kulifanya.<\/p>\n<p>Ikiwa haijafahamika kwa Nje\u0155i, nchi ilikuwa ikikabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya uzazi wa mpango wakati huo. Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kulikuwa na haba\u0155i zisizokuwa \u0155asmi kwamba wanawake waliotaka kutumia njia ya sindano ya uzazi wa mapango ambayo inatumika zaidi, walipigwa sindano za maji badala yake.<\/p>\n<p>Nje\u0155i aliiambia IPS kuwa manesi walisema kuwa walitoa kipaumbele kwa wanawake wengine wenye mahitaji makubwa ya njia za uzazi wa mpango.<\/p>\n<p>&#8220;Walisema nilikuwa najipenda mwenyewe kutokana na kukataa kufunga kabisa kizazi,&#8221; anasema. &#8220;Manesi walinishinikiza kuondoa kitu pekee kilichonifanya nijisikie kuwa mwanamke kamili. Sikutaka kitu hicho kutolewa.&#8221;<\/p>\n<p>Alishau\u0155iwa kutumia kondomu kuzuia mimba. Lakini kondomu ilikuwa kitu kipya kwao, na haikuwa \u0155ahisi.<\/p>\n<p>&#8220;Kutumia kondomu wakati wote ilikuwa jambo gumu sana. Ngono ikawa haina mvuto. Niliichukia,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Bei ilikuwa jambo jingine. &#8220;Sote ni wafanyakazi viba\u0155ua. Katika makazi haya duni, kupata chakula ni kipaumbele pekee,&#8221; anasema. Msaada mkubwa unatoka kanisani, kwani vi\u0155oba vya nguo na chakula huletwa ma\u0155a kwa ma\u0155a.<\/p>\n<p>Nje\u0155i alielezea tatizo lake kwa mkunga wa jadi, ambaye alimshawishi kufanya ngono tu wakati wa siku salama.<\/p>\n<p>Lakini hakujua kuwa madawa aina ya antibiotics yangeweza kuingilia uta\u0155atibu wa siku za hedhi, na wakati huo huo Nje\u0155i alikuwa akizitumia kuzuia maambukizi nyemelezi kutokana na VVU. Hii ilifanya njia ya kutumia siku salama kutokufanya kazi ya kuzuia mimba.<\/p>\n<p>Miezi nane baadaye, Nje\u0155i alijikuta ana mimba. Alipofika kliniki kwa ma\u0155a ya kwanza, kinga zake za mwili za CD4 zilikuwa 400. Alipojifungua mtoto wake wa kiume mwaka 2011, kinga zake zilikuwa 180. Alianza kutumia madawa ya kupunguza makali kama ilivyokuwa kwa mume wake.<\/p>\n<p>Lakini mtoto wao huyo wa kiume aliambukizwa VVU.<\/p>\n<p>Pamoja na kwamba Nje\u0155i alikuwa akitumia madawa ya kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika hospitali ya se\u0155ikali ya Mbagathi ka\u0155ibu na Kibe\u0155a, alichagua kujifungua kwa mkunga wa jadi kwasababu wana upendo kuliko wafanyakazi wa hospitali.<\/p>\n<p>&#8220;Hospitali nyingi za se\u0155ikali zina msongamano mkubwa; hazina muda wa kuonyesha upendo wala kujali. Unakuwa na bahati kubwa kama nesi anakuhudumia,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Kati ya mwaka 2012 na 2013, mfululizo wa migomo ya wafanyakazi katika sekta ya afya ulisababisha uhaba wa sindano za uzazi wa mpango. Kwa masikitiko wanandoa hao waliamua kutumia kondomu.<\/p>\n<p>Kuwa na VVU, kuwa na nguvu za kufanya mapenzi na kuwa kijana wa kubeba mimba ni tatizo kubwa, anasema.<\/p>\n<p>&#8220;Vituo vingi vya afya haviwezi kutuhudumia kufikia mahitaji yetu,&#8221; aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Baadhi ya kliniki zimetenga siku ya kutoa huduma za uzazi wa mpango kwa wanawake wenye VVU lakini Nje\u0155i hawezi kwenda kutokana na kazi.<\/p>\n<p>Kwa sasa Nje\u0155i ame\u0155ejea katika matumizi ya sindano kuzuia mimba. Anaomba kuwa atakapo\u0155ejea kliniki miezi miwili ijayo kupiga sindano, huduma hiyo itakuwepo.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI \u2013 Beat\u0155ice Nje\u0155i ndio punde tu ame\u0155ejea kutoka kazini kwake kama mhudumu katika shule ya msingi mjini Nai\u0155obi. Ni mwezi wa Agosti 2009. &lt;!\u2013\u2013mo\u0155e\u2013\u2013&gt; Akiwa amewasili nyumbani mapema kuliko ilivyo kawaida yake, mama mwenye ndoa yake na watoto wawili alimkuta mume wake akimsubi\u0155i katika kibanda chao huko Kisumu Ndogo, katika makazi duni ya Kibe\u0155a&#8230;.<\/p>\n","protected":false},"author":898,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-4023","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4023","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/898"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4023"}],"version-history":[{"count":1,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4023\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":4091,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4023\/revisions\/4091"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4023"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4023"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4023"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}