{"id":4012,"date":"2014-06-30T13:40:01","date_gmt":"2014-06-30T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2014\/06\/30\/maoni-tofauti-juu-ya-kuanza-kwa-mpango-b-nchini-kenya\/"},"modified":"2014-06-30T13:40:01","modified_gmt":"2014-06-30T13:40:01","slug":"maoni-tofauti-juu-ya-kuanza-kwa-mpango-b-nchini-kenya","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2014\/06\/30\/maoni-tofauti-juu-ya-kuanza-kwa-mpango-b-nchini-kenya\/","title":{"rendered":"Maoni Tofauti Juu ya Kuanza kwa Mpango B+ Nchini Kenya"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Juni 30, 2014 (IPS) &ndash; Sekta ya afya nchini Kenya imekuwa ikikabiliwa na changamoto, ikiwa ni pamoja na uhaba wa wahudumu wa afya na mfululizo wa migomo ya wafanyakazi. Matatizo haya siyo tu kwamba yamevu&#341;uga huduma za afya, lakini wataalam wa VVU wamegawanyika juu ya kama kuna haja ya kuanza mpango B+ nchini kote au kufanya maja&#341;ibio tu katika hospitali kubwa kama zile za &#341;ufaa.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mpango B+ ni mfumo wa ka&#341;ibuni zaidi wa kutoa tiba ambao umependekezwa na Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni kwa ajili ya akina mama wanaoishi na VVU. Katika mipango ya zamani ijulikanayo kama A na B, mama na mtoto wanapatiwa madawa ya kupunguza kasi ya vi&#341;usi vya UKIMWI (ARVs) wakati wa ujauzito na kunyonyesha; na ni wanawake tu wenye hesabu za CD4 chini ya 350 walipatiwa madawa ya ARVs. <\/p>\n<p>Mpango B+ unahusiana na kutoa ARV kwa wanawake wajawazito, bila kujali idadi yao ya CD4. Dk John Ong&#8217;ech, mku&#341;ugenzi msaidizi katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, aliiambia IPS kuwa wakati mjadala ulipoanza mwaka 2013 juu ya kama kuanza kutumia mpango B+ nchini Kenya, &#8220;katika ngazi ya se&#341;a ya taifa, watu waligawanyika juu ya kama waanze mpango B+ kikamilifu.&#8221; Kwa sasa, mpango B+ unapatikana tu katika hospitali kuu za &#341;ufaa mbili, Hospitali ya Taifa ya Kenyatta (KNH) mjini Nai&#341;obi, Hospitali ya Rufaa ya Moi katika jimbo la Bonde la Ufa, na katika hospitali chache za misheni na wilaya. &#8220;Kuna ambao wanahisi kuna haja ya kushughulika na mifumo kwanza katika sekta ya afya,&#8221; alisema Ong&#8217;ech. &#8220;Ili wagonjwa kuanza kupata huduma ya mpango B+, tunahitaji wataalam wa kliniki kwasababu kuna baadhi ya mambo ya kuzingatiwa, kama vile sumu katika dawa na katika mahali pa kuingia kwenye tiba ambapo manesi wanaweza kusimamia,&#8221; aliongeza. Mwaka 2013, ka&#341;ibu wanawake wajawazito 20,000 waliokuwa na VVU walipatiwa ARV chini ya mpango B+. Wengine 55,860 wanatakiwa kujiunga na mpango huo ili kufikisha huduma kwa asilimia 100 ya walengwa, kwa mujibu wa Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Ukimwi (UNAIDS). Mgogo&#341;o wa &#341;asilimali watu Mau&#341;ice Okoth, mtaalam wa kliniki katika kituo cha kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) katika jimbo la Nyanza, aliiambia IPS kuwa mpango B+ siyo suala la kuhakikisha tu kuwa madawa yanapatikana. &#8220;Rikodi za kliniki lazima zipangiliwe vizu&#341;i, lazima kuonyesha kama wagonjwa wanakiuka ta&#341;atibu na jinsi gani wanaokosea hawa wanaweza kupatikana. Hili ni kama haliwezekani wakati huu kutokana na kuwa na wafanyakazi wachache. Tunakabiliwa na mgogo&#341;o wa wafanyakazi katika sekta ya afya,&#8221; alisema. Kenya ina baadhi ya manesi 36,000 katika sekta ya umma na binafsi lakini inahitaji kwa uchache wafanyakazi 80,000 zaidi, kwa mujibu wa takwimu za se&#341;ikali. Ong&#8217;ech anakubaliana na hali hii: &#8220;Kama unazingatia matatizo yaliyopo miongoni mwa watu wenye VVU ambao taya&#341;i unawatibu, hakuna haja ya kuanzisha mpango B+ kwasababu hali itazidi kuwa mbaya.&#8221; Mku&#341;ugenzi wa Huduma za Tiba, Dk Simon Mueke, anakubaliana kuwa kuvu&#341;ugwa kwa huduma za afya kutokana na hali ya kukosekana kwa wafanyakazi kumeathi&#341;i huduma za PMTCT.<\/p>\n<p>Mwezi Disemba 2011, madakta&#341;i walifanya mgomo wakidai kuongezewa fedha kwa sekta ya afya. Mwezi Machi 2012, manesi walifanya mgomo wa wiki mzima, na miezi mitano baadaye madakta&#341;i walisitisha kufanya kazi kwa wiki tatu. Migomo mingine ilifanyika mwaka 2013. Mgomo wa madakta&#341;i na manesi unata&#341;ajiwa kufanyika mwaka 2014 kama se&#341;ikali haitaaji&#341;i wafanyakazi zaidi. Jambo la kushangaza, watu wanaofikiwa na huduma za PMTCT walipungua kwa asilimia 20 mwaka 2011 na 2012, kwa mujibu wa UNAIDS. Bei na vifaa Bei na vifaa kwa ajili ya kuanza mpango B+ nchini kote ni changamoto nyingine. Onge&#8217;ch anasema kuwa, wakati ARVs kwa ujumla wake zinapatikana nchini kote Kenya, &#8220;nchi hiyo inahitaji kuja na mpango nafuu wa manunuzi ya madawa kwa ajili ya mpango B+.&#8221; Katika utoaji tiba ya ARV, gha&#341;ama halisi ya madawa ni chini ya asililimia 30 ya jumla. Kidonge kimoja kipya katika mpango wa gha&#341;ama zisizobadilika inagha&#341;imu dola 180 kwa mgonjwa kwa mwaka, kwa mujibu wa Wiza&#341;a ya Afya, na inata&#341;ajiwa kuwa na gha&#341;ama ya chini zaidi katika siku za usoni. &#8220;Ni mfumo wa huduma za afya na utoaji wa huduma ambako kunachukua asilimia 70 hadi 80 inayosalia,&#8221; alisema Okoth. &#8220;Unahitaji huduma za maaba&#341;a zaidi na upimaji wa vi&#341;usi kuhakikisha kuwa wanawake wanazingatia tiba.&#8221; Umbali kutoka nyumbani kwenda kliniki ni tatizo jingine. Katika mji wa Kisumu, jimbo la Nyanza, wastani wa umbali kwenda kituo cha afya ni kama kilomita 5.8 wakati huko Mande&#341;a, Jimbo la Kaskazini Masha&#341;iki, ni kilomita 20, alielezea.<\/p>\n<p>Lakini Maya Ha&#341;pe&#341;, mku&#341;ugenzi mkaazi wa UNAIDS Kenya, aliiambia IPS kuwa mpango B+ unazingatia gha&#341;ama nafuu: &#8220;Katika kipindi cha muda m&#341;efu, inapunguza mzigo katika mfumo wa afya na kwa wanawake maskini. Kuweka wanawake katika tiba na kuwaondoa wanapokuwa wajawazito ni suala la gha&#341;ama kubwa zaidi.&#8221;<\/p>\n<p>Mbali na matatizo ya miundombinu ya afya, Dk. Dave Muthama, kutoka shi&#341;ika la Elizabeth Glase&#341; Paediat&#341;ic AIDS Foundation, anasema kuwa unyanyapaa &#8220;unabakia kuwa moja ya vikwazo vikubwa.&#8221; Katika KNH, Ong&#8217;ech anaona kila siku jinsi unyanyapaa unavyoathi&#341;i wagonjwa: baadhi wanapata ARVs lakini hawazichukui wakati wengine wanakataa kuzichukua kutokana na kuhofia kuonekana na watu. Umaskini ni kikwazo kingine, alisema Muthama: &#8220;Mama hawazingatii &#341;atiba ya kutembelea vituo vya PMTCT kwasababu wanapokuwa kliniki wanakosa kufanya shughuli za kiuchumi.&#8221; Kwa upande wa Muthama, kuondokana kabisa na maambukizi ya VVU kwa watoto kunahitaji miundombinu ya kijamii kusaidia wanawake wenye VVU. &#8220;Jamii inahitaji kupitia hatua nne ambazo watu wote wanaopima VVU wanapitia: kukataa hali, kuwa na hasi&#341;a, kukubali hali na kuizoea hali hiyo,&#8221; alisema. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Juni 30, 2014 (IPS) &ndash; Sekta ya afya nchini Kenya imekuwa ikikabiliwa na changamoto, ikiwa ni pamoja na uhaba wa wahudumu wa afya na mfululizo wa migomo ya wafanyakazi. Matatizo haya siyo tu kwamba yamevu&#341;uga huduma za afya, lakini wataalam wa VVU wamegawanyika juu ya kama kuna haja ya kuanza mpango B+ nchini kote&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":898,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-4012","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4012","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/898"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=4012"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/4012\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4012"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=4012"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=4012"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}