{"id":3993,"date":"2013-05-28T13:40:01","date_gmt":"2013-05-28T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/05\/28\/tanzania-saccos-zasaidia-kuinua-kilimo-bagamoyo\/"},"modified":"2013-05-28T13:40:01","modified_gmt":"2013-05-28T13:40:01","slug":"tanzania-saccos-zasaidia-kuinua-kilimo-bagamoyo","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/05\/28\/tanzania-saccos-zasaidia-kuinua-kilimo-bagamoyo\/","title":{"rendered":"TANZANIA: SACCOS Zasaidia Kuinua Kilimo Bagamoyo"},"content":{"rendered":"<p>BAGAMOYO, Mei 28 (IPS) &ndash; &#8220;Kilimo Kwanza&#8221; ni mkakati mzu&#341;i kama utatekelezwa kwa ufanisi&#8221;, alisema Salum Shamte, Mwenyekiti wa Bodi ya Ba&#341;aza la Kilimo Tanzania wakati wa mahojiano maalum kwa njia ya simu na mwandishi wa makala haya.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Akifafanua kuhusu mkakati huo, alisema unalenga katika kuwafanya wananchi kuendesha kilimo chenye faida na tija. Alisema Kutokana na se&#341;ikali kujitoa kuendesha kilimo, itapata fu&#341;sa kuwezesha kilimo kupitia kwa wananchi. <\/p>\n<p>&#8220;Hivyo, kama mkakati utatekelezwa wakulima watafaidika kwa kupata mbolea kutoka se&#341;ikalini, kupata mikopo ya kifedha kutoka Benki ya Kilimo itakayoanzishwa na pia kuweza kukopa pembejeo kama vile mat&#341;ekta. Pia masoko yatapatikana, kwani mkakati huo pia utahamasisha sekta binafsi kufungua viwanda vitakavyotumia malighafi kutoka mashambani&#8221;. Alisema Shamte. <\/p>\n<p>Alisema jambo zu&#341;i la mkakati huo ni kwamba Ba&#341;aza lake limeshi&#341;ikisha wananchi tangu dhana yenyewe ilipoanza mwaka 2006 hadi &#341;ipoti ilipowasilishwa se&#341;ikalini Juni 2009. <\/p>\n<p>&#8220;Tulifanya kazi ya kukusanya maoni ya wakulima nchini kote. Tulifanya wa&#341;sha kuanzia Kigoma hadi Mtwa&#341;a kuchukua maoni ya wananchi,&#8221; alisema akiongeza kuwa Ba&#341;aza lilikuwa sehemu ya kikundi kazi ambacho kiliundwa kwa pamoja kati ya se&#341;ikali na sekta binafsi kufanikisha dhana na hatimaye mkakati huo. <\/p>\n<p>&#8220;Kushi&#341;ikishwa kwa wananchi kunasaidia kwasababu katika mijadala walipata fu&#341;sa kujua matatizo ya kilimo wanachoendesha sasa na faida ya kilimo watakachoendesha baada ya mkakati kuanza kufanya kazi,&#8221; alisema na kuongeza kuwa &#8220;Kilimo cha sasa hakina faida kubwa kwao wala tija. Mkakati unasisitiza kilimo cha kisasa na chenye tija.&#8221; <\/p>\n<p> &#8220;Ni mkakati mzu&#341;i kama utatekelezwa, utekelezaji ni msingi mkuu na pia lazima kuwepo kwa ufuatiliaji wa utekelezaji huo.&#8221; <\/p>\n<p>Mkakati wa &#8220;Kilimo Kwanza&#8221; ulikuwa kaulimbiu ya mwaka wa fedha 2009\/2010. Akifafanua maana ya kaulimbiu hiyo wakati wa hotuba yake bungeni Juni 11, 2009, Wazi&#341;i wa Fedha na Uchumi wa wakati huo, Mustafa Mkulo alisema &#8220;Hatua zitachukuliwa kuhakikisha kuwa kilimo kinapatiwa &#341;asilimali zaidi ikiwemo pembejeo na zana za kilimo&#8221;. <\/p>\n<p>Kulingana na Wazi&#341;i Mkuu wa Jamhu&#341;i ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pete&#341; Pinda, &#8220;Ili kuutoa Uchumi wetu kutoka kwenye uchumi ulio nyuma na tegemezi na kuuingiza kwenye uchumi ima&#341;a, wa kisasa na endelevu tunahitaji kufanya mapinduzi katika sekta ya kilimo na viwanda. Mapinduzi haya yataongeza uzalishaji na tija na hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi,&#8221; alisema katika hotuba yake ya Juni 22, ya mapitio na mwelekeo wa kazi za se&#341;ikali na makadi&#341;io ya matumizi ya fedha ya Ofisi ya Wazi&#341;i Mkuu na Ofisi ya Bunge mwaka 2009\/20010, na kuongeza kuwa &#8220;uzalishaji wa mazao ya kilimo ukiongezeka, mavuno yataongezeka na hivyo ongezeko hilo litawawezesha wakulima kunufaika kupata kipato kutokana na kuuza mazao mengi zaidi nje. Hii pia, inavutia wawekezaji kujenga viwanda vya usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za viwandani kutokana na mazao ya kilimo. <\/p>\n<p>&#8220;Tukifanya mapinduzi hayo, tutakuwa tumetekeleza ahadi yetu ya maisha bo&#341;a kwa kila Mtanzania&#8221;, alisema Wazi&#341;i Mkuu. <\/p>\n<p>Kauli ya Wazi&#341;i Mkuu iliungwa mkono na Rais Jakaya M&#341;isho Kikwete. &#8220;Tumeamua kuzindua &#8216;Kilimo Kwanza&#8217; kama azma maalum ya kitaifa ya kuongeza kasi ya kuleta mapinduzi ya kilimo nchini,&#8221; alisema katika Tamko la Rais kwenye kijitabu cha &#8216;Kilimo Kwanza, Mapinduzi ya Kijani&#8217;. <\/p>\n<p>Rais alifafanua zaidi kuwa kilimo kwanza kinajumuisha se&#341;a na mikakati inayolenga katika kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili kilimo na pia kutumia fu&#341;sa lukuki zilizopo nchini. &#8220;Kwa hiyo kilimo kwanza itakua mhimili muhimu katika utekelezaji wa Di&#341;a ya Taifa ya Maendeleo 2025 na itaweka msukumo zaidi katika kufanikisha malengo yetu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii&#8221;. <\/p>\n<p>Pamoja na maneno mazu&#341;i ya viongozi wetu je kuna &#341;asilimali za kutosha kutekeleza mkakati wa kilimo kwanza nchini Tanzania  Jibu la swali hili linajibiwa na Rais Kikwete. &#8220;Nchi yetu yenye wakazi wapatao milioni 40 imejaaliwa kuwa na hekta milioni 44 za a&#341;dhi inayofaa kwa kilimo lakini ni asilimia 23 tu ndiyo inayotumika.&#8221;<\/p>\n<p>Kwa kutambua fu&#341;sa iliyopo katika kilimo, baadhi ya wanachama wa SACCOS ya Mkange ya UWAMKE (Umoja wa Wanawake Mkange) wilayani Bagamoyo wamejiingiza kwenye shughuli za kilimo baada ya kupata mtaji kutoka katika SACCOS hiyo. <\/p>\n<p>&#8220;Najivunia uzu&#341;i wa shamba langu, hata nikipeleka mgeni atajua kweli nimefanya kazi yenye tija,&#8221; anasema Mwanahamisi Ramadhani Kitivo. &#8220;Nilikopa shilingi milioni 2 kutoka katika SACCOS, nikalima eka&#341;i 5 za mahindi kwa kutumia t&#341;ekta, na eka&#341;i nyingine 3 za ufuta,&#8221; anaongeza Kitivo, mmoja wa wanawake wanaofaidika na kuwepo kwa SACCOS ya UWAMKE.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa taa&#341;ifa zilizotolewa na uongozi wa SACCOS hiyo hivi ka&#341;ibuni, kikundi hicho kilianzishwa na wanawake wachache wa Mkange mwaka 2009 ambao walianza kama mchezo wa kibati wa kupeana pesa. Mchezo uliendelea hadi waliposikia juu ya M&#341;adi wa Pwani wa Mpango wa Kuhifadhi Mazingi&#341;a na Rasilimali za Pwani (TCMP) kuwa inasaidia kutoa misaada ya kiuchumi na elimu ya uhifadhi wa mazingi&#341;a, ujasi&#341;iamali na ongezeko la kipato.<\/p>\n<p>TCMP ni mpango unaofadhiliwa na Shi&#341;ika la Misaada ya Kimataifa la Ma&#341;ekani (USAID) na kupata msaada wa kiufundi kutoka Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode, ambacho pia kipo nchini Ma&#341;ekani.<\/p>\n<p>&#8220;TCMP kwa kushi&#341;ikiana na ida&#341;a ya ushi&#341;ika ya wilaya ya Bagamoyo ilianza kusaidia kwa kutoa elimu ya mazingi&#341;a, ujasi&#341;iamali na kujiingizia kipato kwa kikundi hicho cha wanawake,&#8221; anasema Pat&#341;ick Kajubili, m&#341;atibu wa kitengo cha kukuza uchumi na kujiingizia kipato katika TCMP.<\/p>\n<p>Mashavu Ali, mwenyekiti wa UWAMKE na Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi katika kata ya Mkange na mmoja wa waanzilishi wa SACCOS hiyo anasema walianza na mtaji wa shilingi 100,000 ambapo walikuwa wakikopeshana watu 5 kwa awamu hadi mzunguko wa wajumbe 20 unapokamilika. <\/p>\n<p>Anasema waliendelea na mpango huo ambao haukuwa &#341;asmi ambao ulivutia zaidi idadi ya wanachama hadi kufikia 50 na fedha walizokuwa wakiweka kufika shs milioni 3. <\/p>\n<p>&#8220;Tulipokutana na TCMP baada ya kutupatia elimu ya ujasi&#341;iamali na hifadhi ya mazingi&#341;a, walitupatia pia &#341;uzuku ya shs milioni 1 kwa masha&#341;ti kuwa tukifanya vizu&#341;i wangetuongezea kiasi kingine cha fedha. Waliweza kutuongezea tena &#341;uzuku ya shs milioni 1.5 baada ya ku&#341;idhishwa na maendeleo ya kikundi chetu,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Mwenyekiti huyo anasema kwa sasa SACCOS hiyo ina jumla ya wanachama 74 ambapo wanawake ni 65 na wanaume ni 9, fedha kiasi cha shs millioni 14, shamba la ufuta la eka&#341;i 4 na eneo jingine la eka&#341;i 50 ambalo wamepewa na se&#341;ikali ya kijiji kwa ajili ya kupanda miti na kuanzisha ufugaji wa nyuki katika msitu wa miti ya kupanda.<\/p>\n<p>&#8220;Tumepanda ufuta mwaka huu ambapo mavuno yatakayopatikana yatatuwezesha kuendeleza malengo ya SACCOS yetu,&#8221; anasema Ali. &#8220;Malengo hayo ni pamoja na kujenga ofisi ya kikundi chetu&#8221;.<\/p>\n<p>Mashavu Ali pia ni mmoja wa wanachama wanaofaidika na SACCOS. Anasema kiasi cha fedha alichokopa kwenye SACCOS ametumia kubo&#341;esha nyumba yake ya kuishi, kununua jiko la Oven kwa ajili ya kuoka mikate ya biasha&#341;a na kusomesha mtoto wake sekonda&#341;i huko Zanziba&#341;. Mama huyu ambaye ni mjane pia amepata fu&#341;sa ya kutumia mkopo kuanzisha shamba la ufuta la eka&#341;i 3 ambalo pia linaendelea vizu&#341;i.<\/p>\n<p>Shaban Ramadhan, mweka hazina wa SACCOS hiyo pia ameweza kulima shamba la ufuta la eka&#341;i 8 baada ya kupata mkopo kutoka SACCOS. &#8220;Pia kuwepo katika kikundi kumetupatia fu&#341;sa ya kupata mafunzo ya watu, afya na mazingi&#341;a. Kikundi hiki haki&#341;uhusu kuingiza watu wanaoendeshaa shughuli za kuha&#341;ibu mazingi&#341;a &ndash; hatuingizi watu wanaokata mkaa, mbao wala wakataji miti ovyo&#8221; anasema Ramadhan. &#8220;Mwanachama anayeacha shughuli za utunzaji wa mazingi&#341;a na kufanya zinazoha&#341;ibu mazingi&#341;a tunamfukuza katika chama&#8221;.<\/p>\n<p>Kwa upande wake, Kitivo anajivunia kuwa na mazao mazu&#341;i ya ufuta na mahindi ambayo ameweza kulima kwa kutumia t&#341;ekta kutokana na mkopo alioupata kutoka SACCOS. Anasema SACCOS imekuwa mkombozi wa kweli kwani sasa anaweza kuendesha kilimo cha kisasa na pia amewekeza katika biasha&#341;a ndogondogo za kuuza chakula katika kata ya Miono.<\/p>\n<p>&#8220;SACCOS imenipatia mtaji wa kuendesha kilimo cha kisasa,&#8221; anasema. &#8220;Rai yangu kwa se&#341;ikali ni kwamba kilimo cha kutumia jembe la mkono hakiwezi hata kidogo kumkomboa mkulima wa kijijini kujinasua kutoka katika dimbwi la umaskini. Se&#341;ikali itafute njia ya kuwezesha wakulima wadogo wadogo kupata huduma ya t&#341;ekta ili waweze kuendesha kilimo chenye tija.&#8221;<\/p>\n<p>Anasema pamoja na mpango wa Kilimo Kwanza kuwa na mikakati mizu&#341;i ya kubo&#341;esha kilimo na maisha ya Watanzania hasa wanaoishi vijijini, baadhi ya mikakati ya mpango huo haina mafanikio makubwa kwa wakulima wa vijijini. Mfano mzu&#341;i ni mat&#341;ekta aina ya powe&#341; tille&#341; ambayo yamesambazwa kupitia mpango wa Kilimo Kwanza. &#8220;Mashamba mengi yana visiki ambavyo siyo &#341;ahisi kuving&#8217;oa kwa kutumia powe&#341; tille&#341;. T&#341;ekta pekee ndilo lenye uwezo wa kutifua a&#341;dhi vizu&#341;i na kuchimba visiki,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa wakulima hao, eka&#341;i 3 za ufuta zina uwezo wa kuzalisha tak&#341;ibani kilo 2000 ambapo kilo inauzwa kwa shs 1500 katika soko linalopatikana kiu&#341;ahisi katika mazingi&#341;a ya kijijini. Kiasi hiki cha fedha ni kikubwa hasa kwa wananchi wa vijijini ambao wengi wao wanaishi katika umaskini mkubwa wa chini ya dola mbili kwa siku.<\/p>\n<p>&#8220;Najivunia kilimo cha ufuta kwani kitaniwezesha ku&#341;ejesha mkopo na kuongeza akiba yangu katika SACCOS kwa kiasi kikubwa,&#8221; anasema Kitivo. <\/p>\n<p>Picha za makala haya zinaweza kupatikana katika tovuti ya https:\/\/tcmppwani.blogspot.com\/  <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>BAGAMOYO, Mei 28 (IPS) &ndash; &#8220;Kilimo Kwanza&#8221; ni mkakati mzu&#341;i kama utatekelezwa kwa ufanisi&#8221;, alisema Salum Shamte, Mwenyekiti wa Bodi ya Ba&#341;aza la Kilimo Tanzania wakati wa mahojiano maalum kwa njia ya simu na mwandishi wa makala haya. Akifafanua kuhusu mkakati huo, alisema unalenga katika kuwafanya wananchi kuendesha kilimo chenye faida na tija. Alisema Kutokana&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":536,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3993","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3993","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/536"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3993"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3993\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3993"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3993"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3993"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}