{"id":3991,"date":"2013-05-20T13:40:01","date_gmt":"2013-05-20T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/05\/20\/chini-ya-ziwa-nyasa-kuna-udongo-wa-kipekee\/"},"modified":"2013-05-20T13:40:01","modified_gmt":"2013-05-20T13:40:01","slug":"chini-ya-ziwa-nyasa-kuna-udongo-wa-kipekee","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/05\/20\/chini-ya-ziwa-nyasa-kuna-udongo-wa-kipekee\/","title":{"rendered":"Chini ya Ziwa Nyasa Kuna &#8216;Udongo wa Kipekee&#8217;"},"content":{"rendered":"<p>ARUSHA, Tanzania, Mei 20 (IPS) &ndash; Jamii za Watanzania wanaopakana na Ziwa Nyasa hawana ufahamu mgogo&#341;o kati ya nchi yao na Malawi unahusu nini, wala ni nini cha umuhimu katika mgogo&#341;o huo, wakati jitihada za upatanishi kati ya Malawi na Tanzania zinategemewa kuanza hivi ka&#341;ibuni.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Ziwa lenye ukubwa wa kilomita za m&#341;aba 29,000, ambalo kwa upande wa Malawi linajulikana kama Ziwa Malawi, ni eneo la kitalii, chanzo cha mapato na chakula kwa wakazi wa eneo hilo. Lakini tangu Julai 2012, iligundulika kuwa ziwa hilo linaweza kuwa na utaji&#341;i mkubwa wa mafuta na gesi, na ugunduzi huu ulifufua upya mgogo&#341;o baina ya maji&#341;ani hao wa kusini mwa Af&#341;ika juu ya umiliki wa ziwa hilo.<\/p>\n<p>Malawi inadai inamiliki ziwa lote ambalo linabeba mpaka wa Malawi, Msumbiji na Tanzania. Wakati huo huo, Tanzania inasema asilimia 50 ya ziwa ipo upande wake.<\/p>\n<p>Katika Mkoa wa Mbeya, kusini magha&#341;ibi mwa Tanzania, wananchi wanaopakana na ziwa wamekuwa wakifanya kazi na NGO ya kitaifa ya HakiA&#341;dhi, kuelewa haki zao katika maji hayo.<\/p>\n<p>&#8220;Tunajua kuwa tumekubali kutokukubaliana na Malawi katika jambo moja, lakini jamii hizi zinategemea kabisa ziwa hili kwa ajili ya uvuvi kuendesha maisha yao. Hakuna ushau&#341;iano kutoka kwetu kuhusu jinsi gani tutafaidika kama kutakuwa na mafuta hapa, hakuna kabisa. Tutapata nini kutokana na hili  Suala la a&#341;dhi ni jipya kwetu sisi: hatuna tunalolijua,&#8221; Saad Ayoub, afisa mipango msaidizi wa shi&#341;ika hilo, aliiambia IPS kwa njia ya simu.<\/p>\n<p>Wakazi wa kandoni mwa ziwa wanaunga mkono maoni haya. Richa&#341;d Kilumbo, mkazi kutoka wilaya ya Kyela, ambayo inapakana na Ziwa Nyasa, aliiambia IPS kuwa hana uelewa juu ya sababu za mgogo&#341;o huo.<\/p>\n<p>&#8220;Tuna ndugu kutoka Mzuzu, Malawi na tulikuwa tukienda kushi&#341;iki ha&#341;usi mwaka jana. Tunashtushwa na kuchanganyikiwa kuona tunaandaa vita dhidi ya maji&#341;ani zetu. Hatujui ni kwa nini hili ni jambo kubwa miongoni mwa viongozi wetu. Tulisikia watu wakizungumza, tulidhani tulikuwa hu&#341;u kutembea na kufaidi maisha,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Inaonekana kuwa tatizo lilianza mwaka 1890, wakati mkataba wa Heligoland ulipoligawa ziwa kwa mujibu wa she&#341;ia za kikoloni. Ulifanyiwa ma&#341;ekebisho mwaka 1982 na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, hivi ka&#341;ibuni mwezi Oktoba 2011 &#341;ais wa zamani wa Malawi ma&#341;ehemu Bingu wa Mutha&#341;ika, alitoa zabuni kwa kampuni ya mafuta ya Uinge&#341;eza ya Su&#341;est&#341;eam Pet&#341;oleum kuanzisha utafutaji wa gesi na mafuta masha&#341;iki mwa ziwa hilo, halafu zabuni nyingine ikatolewa Desemba 2012 kwa kampuni ya Af&#341;ika Kusini ya SacOil.<\/p>\n<p>Mwezi Julai 2012, Tanzania ilitangaza kuwa, kwa kusaidiana na Denma&#341;k, inapanga kununua pantoni mpya ya thamani ya dola milioni tisa kuvuka maji ya Ziwa Nyasa. Wazi&#341;i wa A&#341;dhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijini wa Malawi alidai kuwa Tanzania haina haki ya kufanya shughuli zake katika maji ya Ziwa Malawi, kwani suala la umiliki na mgogo&#341;o wa mpaka haujatatuliwa. Katika majibu yake, Hilda Ngoye, mbunge katika bunge la Tanzania kutoka Mkoa wa Mbeya, alidai kuwa mashua za uvuvi na utalii za Malawi zinafanya kazi katika maji ya upande wa Tanzania.<\/p>\n<p>Mambo yalibadilika kuwa mabaya wakati huo kaimu Wazi&#341;i Mkuu bungeni nchini Tanzania, Samuel Sitta, alipotoa onyo kuwa nchi yake isingesita kujibu uchokozi wowote ule wa kijeshi.<\/p>\n<p>Hadi leo hii, mbinu nyingi zimetumika kutatua mgogo&#341;o huo kati ya maji&#341;ani hao wawili: upatanishi kwa kutumia Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano, mazungumzo makali juu ya kushambuliana kijeshi, vitisho kupeleka kesi hiyo katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa, hoja ya kupeleka mgogo&#341;o kwa maaskofu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Af&#341;ika, na mazungumzo ya kidiplomasia kati ya mawazi&#341;i wakuu wa Tanzania na Malawi.<\/p>\n<p>Lakini kumekuwepo na ukosoaji kuwa mgogo&#341;o huo umetumika kukuza umaa&#341;ufu wa kisiasa, badala ya kuhakikisha kulinda maslahi ya wanajamii.<\/p>\n<p>&#8220;Ziwa hili linapaswa kutumika kubo&#341;esha vipato na maisha ya wakazi wanaolizunguka katika pande zote. Ziwa ni &#341;asilimali &ndash; badala yake linatumiwa kama sehemu ya mchezo wa kisiasa kukuza umaa&#341;ufu wa kisiasa,&#8221; mwandishi wa haba&#341;i za mazingi&#341;a nchini Tanzania na mtaalam aliyefuatilia haba&#341;i hiyo kwa miaka mingi, na ambaye anaandikia magazeti kadhaa ya Kiswahili na katika blogu yake, Felix Mwakyembe, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>&#8220;Hakuna mgogo&#341;o wa mpaka kati ya wanajamii wanaozunguka ziwa, ni mgogo&#341;o kati ya wanasiasa, suala la kisiasa katika ngazi za juu, wanaotaka kuchaguliwa katika chaguzi za Malawi mwaka 2014 na Tanzania mwaka 2015. Kwa bahati mbaya, wanajamii wanageuka kuwa mateka. Wanakosa taa&#341;ifa za kutosha na elimu kuelewa maana na ukubwa wa tatizo hili,&#8221; Mwakyembe alisema.<\/p>\n<p>Kilumbo anakubaliana naye.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa kweli hakuna shida katika jamii, hakuna kabisa. Wavuvi kutoka Tanzania wanafanya shughuli zao kama kawaida, na pamoja na kuwa tunajua suala hilo lipo katika taa&#341;ifa za haba&#341;i, hatujui linasababishwa na nini,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Masuala ya kutafuta &#341;asilimali katika Ziwa Nyasa yanafanana na migogo&#341;o mingine kikanda linapokuja suala la umiliki, mgawanyo na utoaji wa leseni za utafutaji wa mafuta, na juu ya ni nani anayelipia mitaji ya uwekezaji.<\/p>\n<p>Katika maeneo mengine ya Af&#341;ika Masha&#341;iki, kama vile Bonde la Albe&#341;tine na Mbuga ya Mapo&#341;omoko ya Mu&#341;chison nchini Uganda, na Mbuga ya Vi&#341;unga nchini Rwanda, kuna pande mbili za kuangalia mchakato huu &ndash; kusambaza taa&#341;ifa za tathmini ya mazingi&#341;a na kushi&#341;ikisha kikamilifu wanajamii katika upangaji wa uchimbaji mafuta, na mgawanyo wa mafuta hayo&#8221;.<\/p>\n<p>&#8220;Sina ninalojua juu ya mipango ya mafuta, sijui kabisa. Na sijawahi kusikia kuhusu tathmini ya mazingi&#341;a na sijawahi kuona &#341;ipoti ya aina hiyo,&#8221; Kilumbo alisema. Akiwa anacheka, aliongeza: &#8220;Ni vigumu kujua mgogo&#341;o unahusu nini.&#8221;<\/p>\n<p>Ni kweli kabisa, haionekani wanajamii kuelewa mgogo&#341;o huu unahusu nini, wala haki zao katika mchakato huu ni nini.<\/p>\n<p>Nyanda Shuli, meneja wa utetezi na vyombo vya haba&#341;i wa asasi ya ki&#341;aia ya HakiElimu, aliiambia IPS kuwa msisitizo unapaswa kuwekwa katika uwajibikaji wa kifedha na uwazi, na kwamba kipato kinachoingia na uwekezaji lazima kuelekezwa kwa jamii.<\/p>\n<p>&#8220;Bila kujali matokeo ya mgogo&#341;o huu ni nini, tunapaswa kufiki&#341;i na kukabiliana na suala kubwa la jinsi gani jamii zetu katika maeneo ya vijijini zinaendelea, kutafuta njia kwa watu kufahamu haki zao, na nini wanaweza kuta&#341;ajia, kutoka jamii maskini kabisa zisizokuwa na nafasi kuzunguka Nyasa, hadi kwa jamii zilizopo mbali na ziwa.<\/p>\n<p>&#8220;Lakini kwa sasa maamuzi yanatolewa katika makao makuu, Da&#341; es Salaam, na hakuna uhusiano au mjadala wenye maana katika mikoa. Ni jambo gumu zaidi kwasababu umbali ni mkubwa mno, na usafi&#341;i, mitandao ya simu na ba&#341;aba&#341;a ni mibovu,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Katikati mwa kutokuelewana, kuna jambo moja ambalo linahitaji kukumbukwa. Kuna &#8220;udongo wa kipekee&#8221; chini ya ziwa, na uwezekano wa kupatikana kwa mafuta mengi na gesi asilia.<\/p>\n<p>Hadi leo hii, hakuna ushahidi wa wazi kuwa jamii zinazozunguka ziwa, iwe upande wa Malawi au Tanzania, watakuja kufaidika na utaji&#341;i huo.<\/p>\n<p>Lakini kwa wakati huu, Kilumbo ana imani kuwa kuna samaki wa kutosha kuvua.<\/p>\n<p>&#8220;Ndiyo, naweza kusema Wamalawi wanapata samaki wengi, lakini hii inatokana na kwamba sisi Watanzania tunapenda samaki wadogo na wachanga. Lakini kuna samaki wa kutosha. Sijui kama kuna mipango ya kuchimba mafuta, sijui kabisa.&#8221; <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>ARUSHA, Tanzania, Mei 20 (IPS) &ndash; Jamii za Watanzania wanaopakana na Ziwa Nyasa hawana ufahamu mgogo&#341;o kati ya nchi yao na Malawi unahusu nini, wala ni nini cha umuhimu katika mgogo&#341;o huo, wakati jitihada za upatanishi kati ya Malawi na Tanzania zinategemewa kuanza hivi ka&#341;ibuni. Ziwa lenye ukubwa wa kilomita za m&#341;aba 29,000, ambalo kwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":966,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3991","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3991","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/966"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3991"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3991\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3991"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3991"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3991"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}