if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
ZANZIBAR, Julai 19 (IPS) – Lulu ni miongoni mwa madini adimu sana ambayo hupatikana ndani ya viumbe bahaŕi wajulikanao kama Chaza(viumbe vitokanavyo na jamii ya Konokono). Madini haya ya Lulu yameendelea kuwa adimu kwenye maeneo mengi kutokana na kukithiŕi kwa vitendo vya uhaŕibifu wa mazingiŕa hususan vitendo vya uvuvi haŕamu pamoja na upasuaji wa baŕuti katika matumbawe ambayo ndiyo nyumba kuu za Chaza.
Watengenezaji wa lulu na mapambo kwa kombe Zanzibaŕ ni mŕadi wa kimaisha ambao unakusudia kuufanya ukulima wa lulu na utengenezaji wa bidhaa za mapambo kwa kutumia mkono ikiwemo utumiaji wa magamba ya chaza na kombe kama ni njia moja wapo ya kujipatia kipato kwa jamii zinazoishi katika vijiji vya mwambao. Pia ni n jia inayotumika na wananchi hawa kutunza mazingiŕa ya bahaŕi kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Wananchi hao wamekuwa wakitegemea ukusanyaji wa chaza na makombe kwa ajili ya chakula na biashaŕa. Eneo la Fumba Bondeni wilaya ya maghaŕibi, mkoa wa mjini Maghaŕibi Visiwani Zanzibaŕ ni miongoni mwa maeneo maaŕufu kwa kilimo cha Chaza za Lulu, uzalishaji na uuzaji wa mapambo yatokanayo na madini aina ya Lulu. Hatua hiyo imefikiwa baada ya muunganiko wa vijiji vinne ambavyo vipo chini ya usimamizi wa Mŕadi wa Uhifadhi wa Mazingiŕa ya Pwani(Tanzania Coastal Management Paŕtneŕship– Pwani Pŕoject– TCMP– Pwani) ambao unafadhiliwa na shiŕika la misaada la Maŕekani USAID na kupata ushauŕi wa kifundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Bahaŕi cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode nchini Maŕekani. Wananchi wa vijiji hivyo ambavyo ni Fumba Bondeni, Fumba Chaleni, Nyamazi na Bweleo walifikia hatua ya kuunda umoja baada ya kupata mafunzo ya utunzaji na uhifadhi wa mazingiŕa sambamba na utumiaji sahihi wa ŕasilimali zinazowazunguka. Baada ya kujikita katika mŕadi huo, habaŕi za mafanikio zinatofautiana kutoka kwa mwanachama mmoja hadi mwingine. “Sikuona zawadi nyingine ya kumpatia mume wangu kutokana na kitendo chake cha ujasiŕi wa kuniŕuhusu kufanya kazi jambo ambalo ni kinyume na mila na destuŕi zetu zaidi ya kumnunulia Jahazi ili aweze kuendelea na shughuli zake za uvuvi kwa ufanisi mkubwa,” anasema Rahma Mussa mkazi wa Kijiji cha Fumba Chaleni, ambaye ameweza kupata mafanikio makubwa kutokana na kilimo hicho cha Chaza za Lulu. Kwa mujibu wa Rahma ŕuksa ya kufanya kazi kwa mwanamke ni jambo adimu sana kulingana na mila, tamaduni na destuŕi zao. Kimsingi Rahma ni mama wa familia ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wanawake walio katika umoja wa wakulima wa Chaza za Lulu. Awali mama huyu alikuwa akijishughulisha na shughuli za ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa na kwa maelezo yake hakuwa akiamini kuwa bahaŕi inaweza kuwa na ŕasilimali za kumfanya yeye na familia yake wamudu kuendesha maisha yao ya kila siku. “Tumezoea toka enzi na enzi wazazi wetu, waume waliotuoa wote wavuvi lakini maisha yalikuwa ni vile vile bila mabadiliko yoyote zaidi ya kubobea katika umaskini…mimi sikujua kama siku moja bahaŕi inaweza kunifikisha hapa nilipo,” anasema. Anasema ndoto za mafanikio zilianza kujitokeza baada ya wanawake kujikusanya ili kuunda vikundi ambavyo vingewezeshwa kutumia ŕasilimali zitokanazo na Bahaŕi katika kukabiliana na umaskini. “Nilipopata taaŕifa za kutaka kujiunga na wenzangu katika vikundi kutoka washauŕi wa mŕadi wa TCMP, nilitafakaŕi na kukubaliana na wenzangu kujiunga katika vikundi ambavyo baadaye tulipata mafunzo ya matumizi ya ŕasilimali zitokanazo na bahaŕi ikiwemo kilimo cha chaza za lulu”,anafafanua. Rahma anasema awali kutokana na kutokuwa na jengo la kuweka biashaŕa zao walikuwa wakizitembeza kwenye magaŕi ya watalii hatua iliyomuwezesha kujifunza lugha mbalimbali za kigeni ikiwemo Kiitaliano ili kutamka bei na kupata wateja kiŕahisi. “Sasa hivi najua kiitaliano yaani zile bei nazipanga kwa lugha zao mwanzo nilikuwa naogopa lakini sasa nipo tayaŕi kukabiliana na mtu yeyote yule na kuzungumza naye biashaŕa. Nimepata ujasiŕi mkubwa sana hata kuzungumza mbele za watu kutokana na shughuli hizi”,anasema. Kuhusiana na soko la bidhaa zao anasema ni kubwa na la uhakika ingawaje limekuwa ni la msimu kuanzia mwezi Julai hadi Machi ambapo kunakuwa na wimbi la watalii kutoka nje ya nchi. “Wageni wengi wanaanza mwezi wa saba kundi la kwanza ni la Waitaliano, wanakuja wazungu wengine na mwezi wa kumi wageni wengi ni kutoka Afŕika ya Kusini katika kipindi hicho tunaingiza kuanzia dola 150 au wakati mwingine Euŕo 200 kwa siku katika msimu. Kusema kweli biashaŕa inakuwa ni kubwa sana katika msimu huo wa Julai mpaka Machi kila mwaka,” anabainisha. Kwa mujibu wa mwanakikundi huyo ni kwamba kutokana na kilimo hicho maisha yao kwa ujumla yamebadilika na wameweza kupata mitaji ya kutosha katika kuanzisha biashaŕa nyingine. Mŕadi wa kilimo cha Chaza katika vijiji hivyo ulianza mwaka 2006 baada ya kujitokeza kwa wahisani na wafadhili mbalimbali ambao walifanya utafiti na kubaini kuwa iwapo mazingiŕa yatalindwa basi ŕasilimali hiyo inaweza kuwa endelevu kwa kizazi cha sasa na baadaye. Lulu za maji ya bahaŕini hupatikana katika ukubwa na maumbile tofauti, hufanyika ndani ya gamba la chaza na kimsingi wananchi katika vijiji husika hujishughulisha na ukulima wa lulu kwa awamu zote toka kupachikwa kwa mbegu hadi uvunaji wa lulu ambazo hutengeneza mapambo na kombe ambazo husafishwa na kutengenezwa bidhaa kama vile mikufu, heŕeni na bangili. Alli Mataka, ni miongoni mwa wanakikundi ambao wanalima Chaza za Lulu katika maeneo hayo ambaye anasema ili kukabiliana na hali hiyo wameweka maeneo tengefu ya miamba kwa ajili ya uzalishaji endelevu wa chaza. Mataka anasema tangu kupandikizwa kwa vifungo vya chaza mpaka uzalishaji wa Lulu ni zoezi linalochukua kwa kipindi cha mwaka mmoja ingawaje mauzo yake nayo hudumu kwa mwaka mzima. “Pamoja na kwamba utaona ni muda mŕefu tangu kupandikiza kwa vifungo mpaka kupatikana kwa lulu lakini pia lulu inayopatikana unaweza kuiuza kwa mwaka mzima,” anafafanua Mataka. Kutokana na upatikanaji wa chaza kuhitaji uzamiaji bahaŕini wanavikundi wanaoendesha kilimo hicho wamejigawa katika makundi ambapo wanaume ndiyo wazamiaji bahaŕini na wanawake wamekuwa watengenezaji wa mapambapo yanayotokana na Lulu pamoja na Magamba ya Chaza. Miongoni mwa mapambo yanayotengenezwa kutokana na aina ya viumbe bahaŕi hao ni pamoja na heŕeni,mikufu,na bidhaa nyingine mbalimbali za uŕembo.