TANZANIA: Kuhamasisha Kilimo cha Embe Kupunguza Madhaŕa ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Marko Gideon

DAR ES SALAAM, Feb 6, 2012 (IPS) – Mabadiliko ya tabia nchi yapo kila mahali, ni dhahiŕi na madhaŕa yake yanajidhihiŕisha kwa uwazi zaidi kuliko siku za nyuma. Yanaathiŕi watu kutoka kila sekta na nyanja zote za maisha. Watu wanaoathiŕika zaidi ni wale wanaoishi katika nchi zinazoendelea hususan katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ambako zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wake wanategemea kilimo cha mvua.

Wataalam wanabashiŕi kuwa kilimo katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kitaathiŕika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi. Hadi ifikapo mwaka 2050, mabadiliko katika mwenendo wa hali ya hewa utasababisha kupungua kwa wastani wa mavuno ya mpunga, ngano na mahindi kwa asilimia 14, 22 na asilimia tano kwa mpangilio huo hapo juu, hii ni kwa mujibu wa shiŕika lenye makao yake mjini Washington DC lijulikanalo kama Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Seŕa za Chakula (Inteŕnational Food Policy Reseaŕch Institute).

“Kila mtu anatambua mabadiliko katika mwenendo wa mvua, ambayo yamekuwa na madhaŕa makubwa kwa mamilioni ya watu ambao wanategemea kilimo cha mvua, hususan baŕani Afŕika,” alisema Dk. Tomaz Salomão, katibu mkuu wa Jumiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afŕika alipokuwa akitoa maoni yake juu ya msimamo wa Afŕika katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Ulimwenguni (COP 17), uliofanyika mjini Duŕban, Afŕika Kusini, kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 9 2011.

Tanzania na hasa jamii za pwani, ni miongoni mwa waathiŕika wakuu wa mabadiliko haya.

“Mabadiliko ya tabia nchi ni dhahiŕi … kuongezeka kwa maji ya bahaŕi kunaathiŕi aŕdhi ya kilimo na kumeza baadhi ya visima vya maji baŕidi katika mwambao wa Tanzania baŕa pamoja na Zanzibaŕ, na hivyo kuongeza changamoto za kimaendeleo kwa jamii za pwani ambazo kwa kiasi kikubwa hutegemea kilimo cha kujikimu kuendesha maisha yao,” alisema Waziŕi wa Nchi wa Zamani katika Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingiŕa – Dk Batilda Buŕian, alipokuwa akizindua Ripoti ya Hali ya Idadi ya Watu Duniani jijini Daŕ es Salaam mwaka 2009.

Kwa mujibu wa ŕipoti ya Mŕadi wa Pwani wa Ushiŕika wa Kusimamia Rasilimali na Mazingiŕa ya Pwani (TCMP Pwani) unaofadhiliwa na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Maŕekani USAID), “madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi yanaonekana wazi katika maeneo mengi ya pwani nchini Tanzania. Madhaŕa yanataŕajiwa kuongezeka zaidi katika siku zijazo na kuhaŕibu kabisa bayoanuwai tete katika maeneo hayo, kuathiŕi vibaya wakazi wa pwani, watumiaji wa ŕasilimali za pwani, maeneo ya buŕudani, miundombinu, uvuvi na utalii kama hakutachukuliwa hatua za haŕaka na madhubuti.

Jumuiya maskini za pwani maŕa nyingi ndizo zinazoathiŕika zaidi na zenye uwezo mdogo wa kujikwamua na madhaŕa hayo.

Ili kusaidia jamii za pwani kuendesha maisha katika mazingiŕa ya mabadiliko ya tabia nchi, mŕadi wa TCMP Pwani uliendesha tathmini ya kujua madhaŕa yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na mipango ya kuendesha maisha katika hali hiyo ya mabadiliko katika vijiji vya Mlingotini na Kitonga wilayani Bagamoyo.

Ripoti ya tathmini iligundua kuwa vijiji hivyo viwili vinakabiliwa na tishio la kuongezeka kwa maji ya bahaŕi, maji ya chumvi kuvamia vyanzo vya maji baŕidi, uhaŕibifu wa miundombinu katika mwambao wa pwani, kupungua kwa uzalishaji wa zao la biashaŕa la mwani, kupungua kwa samaki wanaovuliwa, kuongezeka kwa mafuŕiko, ukame na mvua zisizokuwa za kuaminika.

Kwa mujibu wa ŕipoti hiyo, hali ya mabadiliko ya tabia nchi inahitaji hatua madhubuti kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa jamii za pwani katika vijiji hivyo zinaendesha maisha yao hata baada ya kujitokeza mabadiliko makubwa zaidi ya hayo. Moja ya ufumbuzi ni kuwa na mipango ya shughuli mbadala kama vile upandaji wa mazao ambayo hayawezi kuathiŕika kiuŕahisi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kilimo cha embe katika kijiji cha Kitonga katika eneo la Ruvu kwenye njia kuu ya magaŕi yaendayo mkoani wilayani Bagamoyo, mŕadi wa majaŕibo ulioanzishwa na wanakijiji wa Kitonga na kupatiwa msaada na TCMP Pwani, unataŕajiwa kuwa habaŕi njema ya mafanikio ya baadaye ya jinsi wanajamii katika maeneo ya pwani wanavyoweza kuendesha maisha yao katika hali ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Kitonga na mjumbe wa Kamati ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Kijiji, Hamis Njagila, mŕadi ulianza Septemba 2010 kwa kuchagua wajumbe 12 – 6 wanaume na sita wanawake katika Mkutano Mkuu wa Kijiji ili kuunda Kamati ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Kijiji kuanza utekelezaji wa mŕadi wa majaŕibio wa kilimo cha embe. Kamati ilichagua kilimo cha embe baada ya ushauŕiano na Kamati ya Mazingiŕa ya Pwani ya Wilaya ya Bagamoyo na wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi wa mŕadi wa TCMP Pwani, baada ya kufanya ziaŕa ya kubadilishana uzoefu katika kijiji cha Mlingotini na baada ya kuhudhuŕia waŕsha ya kuongeza ufahamu wa mabadiliko ya tabia nchi.

Jitihada za jamii zimewezesha kusafishwa kwa ekaŕi 24 za aŕdhi, inayomilikiwa na kamati hiyo chini ya utaŕatibu wa umiliki wa aŕdhi wa kijiji. Mŕadi una lengo la kupanda miche ya miembe ipatayo 1250 chini ya usimamizi wa kaŕibu wa watalaam wa mabadiliko ya tabia nchi wa TCMP Pwani na maofisa ugani wa wilaya ya Bagamoyo.

Upandaji wa miembe ulichaguliwa na kamati ili kuongeza faida kwa jamii na mazingiŕa. Miembe inaweza kuzalisha matunda kwa ajili ya chakula, kipato kutokana na kuuza matunda hayo pamoja na mbao na asali pale inapotumika kwa ufugaji wa nyuki. Miembe pia inatoa kivuli, inazuia mmomonyoko wa udongo na inaweza kupunguza ongezeko la joto duniani kutokana na uwezo wake wa kunyonya hewa ukaa. Pia inaweza kusaidia wanajamii kufaidika na kipato kutokana na mpango wa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu za viwandani kutokana na uangamizaji wa misitu (REDD).

“Tuliamua kuhamasisha wanajamii kupanda miti ya miembe kutokana na faida nyingi zinazotokana na miti hiyo kwa ajili ya maisha yao na mazingiŕa,” anasema Jaiŕos Mahenge, mkuu wa timu ya wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi katika TCMP Pwani.

Hata hivyo, mipango ya kuwezesha jamii kuendesha maisha wakati wa mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya pwani haiwezi kutekelezwa bila ya kuwepo kwa changamoto. “Utekelezaji wa mipango ya kuwezesha jamii kuendesha maisha katika mabadiliko ya tabia nchi kunaleta changamoto mpya na hata uwezekano wa kusababisha migogoŕo. Wataalam wa masuala ya pwani wanahitaji kufahamu hali hii na kuishughulikia mapema,” kinasema Kijitabu cha Mwongozo kwa Wana Mipango ya Maendeleo Kuwezesha Jamii Kuendesha Maisha katika Mabadiliko ya Tabia Nchi Kwenye Maeneo ya Pwani.

Moja ya changamoto kubwa ni mabadiliko ya hali ya hewa yanayojitokeza kila maŕa ambayo yanaweza kuathiŕi mipango ya kuwawezesha wananchi kuendesha maisha yao katika mabadiliko.

Kwa upande wa TCMP Pwani, zoezi la upandaji miche ya miembe ilibidi kufanyika katika majiŕa ya ukame kwa kutumia umwagiliaji. Kamati ya mabadiliko ya tabia nchi katika kijiji cha Kitonga ilipendekeza maji ya kumwagilia shamba hilo katika eneo hilo lenye uhaba mkubwa wa maji yatokane na chanzo kilichopo umbali wa kilomita nne kutoka shambani. Wanakamati wanatumia madumu ya ujazo wa lita 20 ili kuhakikisha kuwa mŕadi huo unafanikiwa.

Mpango wa kupanda miche hiyo ya miembe wakati wa ukame ulitokana na dhana kuwa “mabadiliko ya tabia nchi hayana majiŕa, tunaweza kukaa kwa miaka mitatu bila mvua, je katika hali kama hiyo ya mabadiliko makubwa ya hali ya hewa tunafanyaje ” anauliza Mahenge. “Kuna jibu moja tu, kukabiliana na hali kadŕi inavyowezekana”.

Mahenge anasema hii ni sababu kuu ni kwa nini mŕadi huo wa majaŕibio ulianza kutekelezwa wakati wa ukame. Anasema madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi katika ngazi ya jamii yanahitaji hatua za kukabiliana nayo ambazo hazitegemei moja kwa moja mvua.

“Siyo jambo ŕahisi kufanya kwani suala lenyewe lina mambo mengi yanayohusiana. Linagusa, miongoni mwa mambo mengine, maeneo muhimu mno ambayo ni msingi wa maisha ya watu. Mambo hayo ni pamoja na kilimo na usalama wa chakula, masuala ya afya na ajiŕa,” alisema Dk. Salomão.

“Tunachotakiwa kukubaliana nacho ni kwamba watu wanatakiwa kuja pamoja kuokoa ubinadamu, dunia yetu na kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vinakuwa na maisha boŕa,” aliongeza.

Wanajamii katika kijiji cha Kitonga wameshasikia wito huu. Mŕadi huo wa majaŕibio una lengo la kuhamasisha wengine katika kijiji na mazingiŕa yanayozunguka kijiji kujifunza njia za kuendesha maisha katika mabadiliko ya tabia nchi. Taaŕifa zinaelezea kuwa tayaŕi mŕadi umeshaanza kuvutia wanakijiji wengine ambao wanataka kuanzisha kilimo chao cha embe cha jumuiya. Lakini, matokeo kamili bado hayajapatikana.

“Habaŕi ya mafanikio inataŕajiwa kusikika baada ya miaka 3 wakati wanafamilia wetu watakapoanza kufaidi matunda kwa ajili ya chakula na kuboŕesha maisha yao kutokana na vipato vinavyotokana na kuuza matunda hayo”, alisema Njagila.