Watu Milioni Mbili Wameweka Matumaini yao Katika Usuluhishi wa Mgogoŕo wa Ziwa Nyasa

Mabvuto Banda
thumb image

LILONGWE, Mei 20 (IPS) – Zaidi ya familia milioni mbili ambazo zinategemea Ziwa Nyasa kwa ajii ya kipato chao zinasubiŕi kwa hamu usuluhishi wa mgogoŕo wa ziwa hilo kati ya Malawi na Tanzania ili kukomesha mgogoŕo wa umiliki wa ziwa hilo.

Mchakato wa kutafuta ufumbuzi wa mgogoŕo huo baina ya pande husika utaanza mwezi Machi baada ya makubaliano ya mwezi Desemba ya nchi hizo mbili kutoa kibali kwa Jukwaa la Wakuu wa Zamani wa Afŕika na Seŕikali, linaloongozwa na ŕais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chissano kuendesha usuluhishi huo.

“Baada ya hatua kadhaa za kutatua mgogoŕo huo, tumekuja kukubaliana kuwa tumeshindwa na tunahitaji upande wa tatu kutusaidia,” Katibu Mkuu katika Wizaŕa ya Mambo ya Nje ya Malawi, Patŕick Kambabe, aliiambia IPS.

“Mwezi Januaŕi, Malawi iliwakilisha msimammo wake baada ya kukubali kuwa Jukwaa hilo lingesaidia kutatua mgogoŕo huo,” Kambabe alisema. 
 Katika mahojiano na vyombvo vya habaŕi vya Tanzania, katibu mkuu wa wizaŕa ya mambo ya nje ya Tanzania John Haule alithibitisha kuwa nchi yake pia imekubali kushiŕikisha viongozi wa zamani na imepeleka msimamo wake kwa Chissano.

“Jukwaa kwa sasa linapitia waŕaka wetu na baada ya hapo litatafuta taaŕifa zaidi kama zinahitajika,” kwa mujibu wa Haule.

Alisema kuwa alitaŕajia kuwa suala hilo litatatuliwa katika kipindi cha miezi mitatu.

Kwa mujibu wa mamlaka, Wamalawi wapatao milioni 1.5 na Watanzania 600,000 wanategemea ziwa hilo la tatu kwa ukubwa baŕani Afŕika kwa ajili ya chakula, usafiŕi na mahitaji mengine ya kila siku.

Wakati IPS ilipotembelea Wilaya ya Kaŕonga, katika mwambao wa Ziwa Nyasa, jamii kuzunguka ziwa hilo zilisema zina wasiwasi kuhusu uhasama unaozidi kuongezeka na wanataŕajia maŕidhiano kupatikana.

“Nilikuwa navuka mpaka kuingia Kyela nchini Tanzania kila baada ya wiki mbili kuuza sukaŕi na kupata nguo, ambazo naziuza upande wa nchini kwetu. Lakini sasa nakwenda huko maŕa moja tu kwa mwezi kwasababu maafisa uhamiaji wa Tanzania katika mpaka wa Songwe wamekuwa wakali sana,” alisema Joyce Nyiŕongo, mama wa watoto wanne.

Likijulikana kama Ziwa Malawi upande wa Malawi na Lago Niassa nchini Msumbiji, mgogoŕo wa ziwa hilo umeongezeka kutokana na hifadhi kubwa ya gesi na mafuta, kwa mujibu wa taaŕifa za kaŕibuni za seŕikali ya Malawi.

Uwezekano wa kuwepo kwa mafuta na gesi kumeibua upya mgogoŕo wa mpaka kati ya Malawi na Tanzania, ambao umebaki bila kutatuliwa kwa kaŕibu nusu kaŕne.

Mgogoŕo ulienea Julai iliyopita wakati Malawi ilipotoa kibali cha kutafuta mafuta kwa kampuni yenye makao yake nchini Uingeŕeza ya Suŕestŕeam Petŕoleum.

Na Desemba mwaka jana Malawi ilitoa leseni nyingine kubwa kwa kampuni ya mafuta ya SacOil Holdings Ltd.kutoka Afŕika Kusini, hatua ambayo imeongeza msuguano.

Mataifa hayo yamejaŕibu maŕa mbili kutatua mgogoŕo kwa njia za kidiplomasia lakini imeshindikana.

Mataifa yote mawili yanataŕajia matokeo mazuŕi ambayo yatatatua mgogoŕo huo kabisa wakati mchakato wa usuluhishi utakapoanza mwezi Machi.

Madai ya mikataba ya kikoloni Rais wa kwanza wa Malawi, Hastings Kamuzu Banda, alikuwa wa kwanza kudai kuwa Ziwa Nyasa ni sehemu ya nchi yake. Alikuwa akitoa madai yake hayo kutokana na mkataba wa 1890 unaojulikana kama Mkataba wa Heligoland kati ya Uingeŕeza na Ujeŕumani, ambao ulielezea kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili uwepo upande wa Tanzania wa ziwa hilo.

Mkataba huo uliŕidhiwa katika Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Nchi Huŕu za Afŕika mwaka 1963 nchini Ethiopia na ulikubaliwa shingo upande na Tanzania.

Waziŕi wa Mambo ya Nje wa Malawi Ephŕaim Chiume aliiambia IPS kuwa msimamo wao unajikita katika Mkataba wa 1890 na kuwa Umoja wa Afŕika mwaka 2002 na 2007 ulipitisha azimio la kuendeleza mkataba huo wa kikoloni.

“Mkataba wa Heligoland ulitupatia ziwa lote sisi na huu ndiyo msingi wa msimamo wetu na uthibitisho kuwa ziwa lote ni la kwetu,” alisema Chiume.

Msimamo wa Tanzania ni kwamba mkataba huo una mapungufu. Tanzania imebakia na msimamo kuwa inamiliki nusu ya ziwa hilo – ikisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo mbili upo katikati mwa ziwa ukiondoa sehemu ya taifa la Msumbiji.

Msimamo wa Tanzania ni kuwa mpaka upo katikati mwa ziwa, na kusisitiza kuwa hii ni kanuni inayofuatwa kama nchi zinamiliki bodi ya maji kwa pamoja.

“Tanzania inafuata sheŕia za kimataifa, ambazo zinasema kuwa mipaka kwa ujumla inakuwa katikati mwa maji … kwa sababu hiyo Tanzania inamiliki nusu ya ziwa,” Waziŕi wa Mambo ya Nje wa Tanzania Benaŕd Membe aliiambia IPS katika mahojiano kwa njia ya simu.

Membe alisema mkataba una mapungufu kwasababu umewanyima Watanzania wanaoishi kandokando mwa ziwa haki zao za kutumia maji na ŕasilimali za majini kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hii ni misimamo ambayo Chissano na wenzake wawili; ŕais wa zamani wa Afŕika Kusini Thabo Mbeki na ŕais wa zamani wa Botswana Ketumiŕe Masiŕe watayapitia.

Suala la Kimazingiŕa Wakati huo huo, mgogoŕo huo pia umeibua suala la madhaŕa ya kuchimba mafuta katika ziwa hilo la maji baŕidi ambalo limejaliwa kuwa na aina tofauti zaidi ya 2,000 ya samaki, ambalo linavutia pia wapiga mbizi kutoka duniani kote.

Wanamazingiŕa nchini Malawi wana wasiwasi uchimbaji wa mafuta utahaŕibu bayoanuai ya ziwa hilo inayovutia utalii wa kimazingiŕa na mazingiŕa ya ziwa hilo na hivyo kuathiŕi mikoa inayotegemea uvuvi kaskazini mwa nchi.

“Utahataŕisha maisha ya mamilioni ya watu kijamii na kiuchumi ambao moja kwa moja wanategemea maji ya ziwa hilo, usafiŕi na suala la msingi zaidi pŕotini inayotokana na samaki,” alisema Reginald Mumba wa shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la Hifadhi ya Mazingiŕa.

Baada ya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili kushindikana mwishoni mwa mwaka jana, Rais wa Malawi Joyce Banda alielezea nia yake ya kupeleka suala hilo Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa.

Wanasiasa na wavuvi kwa pamoja kwa sasa wana matumaini yao kuwa mchakato wa maŕidhiano utaleta suluhisho la amani la mgogoŕo huo bila hata kuhusisha mahakama hiyo.