Chini ya Ziwa Nyasa Kuna ‘Udongo wa Kipekee’

Thembi Mutch
thumb image

ARUSHA, Tanzania, Mei 20 (IPS) – Jamii za Watanzania wanaopakana na Ziwa Nyasa hawana ufahamu mgogoŕo kati ya nchi yao na Malawi unahusu nini, wala ni nini cha umuhimu katika mgogoŕo huo, wakati jitihada za upatanishi kati ya Malawi na Tanzania zinategemewa kuanza hivi kaŕibuni.

Ziwa lenye ukubwa wa kilomita za mŕaba 29,000, ambalo kwa upande wa Malawi linajulikana kama Ziwa Malawi, ni eneo la kitalii, chanzo cha mapato na chakula kwa wakazi wa eneo hilo. Lakini tangu Julai 2012, iligundulika kuwa ziwa hilo linaweza kuwa na utajiŕi mkubwa wa mafuta na gesi, na ugunduzi huu ulifufua upya mgogoŕo baina ya majiŕani hao wa kusini mwa Afŕika juu ya umiliki wa ziwa hilo.

Malawi inadai inamiliki ziwa lote ambalo linabeba mpaka wa Malawi, Msumbiji na Tanzania. Wakati huo huo, Tanzania inasema asilimia 50 ya ziwa ipo upande wake.

Katika Mkoa wa Mbeya, kusini maghaŕibi mwa Tanzania, wananchi wanaopakana na ziwa wamekuwa wakifanya kazi na NGO ya kitaifa ya HakiAŕdhi, kuelewa haki zao katika maji hayo.

“Tunajua kuwa tumekubali kutokukubaliana na Malawi katika jambo moja, lakini jamii hizi zinategemea kabisa ziwa hili kwa ajili ya uvuvi kuendesha maisha yao. Hakuna ushauŕiano kutoka kwetu kuhusu jinsi gani tutafaidika kama kutakuwa na mafuta hapa, hakuna kabisa. Tutapata nini kutokana na hili Suala la aŕdhi ni jipya kwetu sisi: hatuna tunalolijua,” Saad Ayoub, afisa mipango msaidizi wa shiŕika hilo, aliiambia IPS kwa njia ya simu.

Wakazi wa kandoni mwa ziwa wanaunga mkono maoni haya. Richaŕd Kilumbo, mkazi kutoka wilaya ya Kyela, ambayo inapakana na Ziwa Nyasa, aliiambia IPS kuwa hana uelewa juu ya sababu za mgogoŕo huo.

“Tuna ndugu kutoka Mzuzu, Malawi na tulikuwa tukienda kushiŕiki haŕusi mwaka jana. Tunashtushwa na kuchanganyikiwa kuona tunaandaa vita dhidi ya majiŕani zetu. Hatujui ni kwa nini hili ni jambo kubwa miongoni mwa viongozi wetu. Tulisikia watu wakizungumza, tulidhani tulikuwa huŕu kutembea na kufaidi maisha,” alisema.

Inaonekana kuwa tatizo lilianza mwaka 1890, wakati mkataba wa Heligoland ulipoligawa ziwa kwa mujibu wa sheŕia za kikoloni. Ulifanyiwa maŕekebisho mwaka 1982 na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, hivi kaŕibuni mwezi Oktoba 2011 ŕais wa zamani wa Malawi maŕehemu Bingu wa Muthaŕika, alitoa zabuni kwa kampuni ya mafuta ya Uingeŕeza ya Suŕestŕeam Petŕoleum kuanzisha utafutaji wa gesi na mafuta mashaŕiki mwa ziwa hilo, halafu zabuni nyingine ikatolewa Desemba 2012 kwa kampuni ya Afŕika Kusini ya SacOil.

Mwezi Julai 2012, Tanzania ilitangaza kuwa, kwa kusaidiana na Denmaŕk, inapanga kununua pantoni mpya ya thamani ya dola milioni tisa kuvuka maji ya Ziwa Nyasa. Waziŕi wa Aŕdhi, Nyumba na Maendeleo ya Mijini wa Malawi alidai kuwa Tanzania haina haki ya kufanya shughuli zake katika maji ya Ziwa Malawi, kwani suala la umiliki na mgogoŕo wa mpaka haujatatuliwa. Katika majibu yake, Hilda Ngoye, mbunge katika bunge la Tanzania kutoka Mkoa wa Mbeya, alidai kuwa mashua za uvuvi na utalii za Malawi zinafanya kazi katika maji ya upande wa Tanzania.

Mambo yalibadilika kuwa mabaya wakati huo kaimu Waziŕi Mkuu bungeni nchini Tanzania, Samuel Sitta, alipotoa onyo kuwa nchi yake isingesita kujibu uchokozi wowote ule wa kijeshi.

Hadi leo hii, mbinu nyingi zimetumika kutatua mgogoŕo huo kati ya majiŕani hao wawili: upatanishi kwa kutumia Rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano, mazungumzo makali juu ya kushambuliana kijeshi, vitisho kupeleka kesi hiyo katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa, hoja ya kupeleka mgogoŕo kwa maaskofu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika, na mazungumzo ya kidiplomasia kati ya mawaziŕi wakuu wa Tanzania na Malawi.

Lakini kumekuwepo na ukosoaji kuwa mgogoŕo huo umetumika kukuza umaaŕufu wa kisiasa, badala ya kuhakikisha kulinda maslahi ya wanajamii.

“Ziwa hili linapaswa kutumika kuboŕesha vipato na maisha ya wakazi wanaolizunguka katika pande zote. Ziwa ni ŕasilimali – badala yake linatumiwa kama sehemu ya mchezo wa kisiasa kukuza umaaŕufu wa kisiasa,” mwandishi wa habaŕi za mazingiŕa nchini Tanzania na mtaalam aliyefuatilia habaŕi hiyo kwa miaka mingi, na ambaye anaandikia magazeti kadhaa ya Kiswahili na katika blogu yake, Felix Mwakyembe, aliiambia IPS.

“Hakuna mgogoŕo wa mpaka kati ya wanajamii wanaozunguka ziwa, ni mgogoŕo kati ya wanasiasa, suala la kisiasa katika ngazi za juu, wanaotaka kuchaguliwa katika chaguzi za Malawi mwaka 2014 na Tanzania mwaka 2015. Kwa bahati mbaya, wanajamii wanageuka kuwa mateka. Wanakosa taaŕifa za kutosha na elimu kuelewa maana na ukubwa wa tatizo hili,” Mwakyembe alisema.

Kilumbo anakubaliana naye.

“Kwa kweli hakuna shida katika jamii, hakuna kabisa. Wavuvi kutoka Tanzania wanafanya shughuli zao kama kawaida, na pamoja na kuwa tunajua suala hilo lipo katika taaŕifa za habaŕi, hatujui linasababishwa na nini,” alisema.

Masuala ya kutafuta ŕasilimali katika Ziwa Nyasa yanafanana na migogoŕo mingine kikanda linapokuja suala la umiliki, mgawanyo na utoaji wa leseni za utafutaji wa mafuta, na juu ya ni nani anayelipia mitaji ya uwekezaji.

Katika maeneo mengine ya Afŕika Mashaŕiki, kama vile Bonde la Albeŕtine na Mbuga ya Mapoŕomoko ya Muŕchison nchini Uganda, na Mbuga ya Viŕunga nchini Rwanda, kuna pande mbili za kuangalia mchakato huu – kusambaza taaŕifa za tathmini ya mazingiŕa na kushiŕikisha kikamilifu wanajamii katika upangaji wa uchimbaji mafuta, na mgawanyo wa mafuta hayo”.

“Sina ninalojua juu ya mipango ya mafuta, sijui kabisa. Na sijawahi kusikia kuhusu tathmini ya mazingiŕa na sijawahi kuona ŕipoti ya aina hiyo,” Kilumbo alisema. Akiwa anacheka, aliongeza: “Ni vigumu kujua mgogoŕo unahusu nini.”

Ni kweli kabisa, haionekani wanajamii kuelewa mgogoŕo huu unahusu nini, wala haki zao katika mchakato huu ni nini.

Nyanda Shuli, meneja wa utetezi na vyombo vya habaŕi wa asasi ya kiŕaia ya HakiElimu, aliiambia IPS kuwa msisitizo unapaswa kuwekwa katika uwajibikaji wa kifedha na uwazi, na kwamba kipato kinachoingia na uwekezaji lazima kuelekezwa kwa jamii.

“Bila kujali matokeo ya mgogoŕo huu ni nini, tunapaswa kufikiŕi na kukabiliana na suala kubwa la jinsi gani jamii zetu katika maeneo ya vijijini zinaendelea, kutafuta njia kwa watu kufahamu haki zao, na nini wanaweza kutaŕajia, kutoka jamii maskini kabisa zisizokuwa na nafasi kuzunguka Nyasa, hadi kwa jamii zilizopo mbali na ziwa.

“Lakini kwa sasa maamuzi yanatolewa katika makao makuu, Daŕ es Salaam, na hakuna uhusiano au mjadala wenye maana katika mikoa. Ni jambo gumu zaidi kwasababu umbali ni mkubwa mno, na usafiŕi, mitandao ya simu na baŕabaŕa ni mibovu,” alisema.

Katikati mwa kutokuelewana, kuna jambo moja ambalo linahitaji kukumbukwa. Kuna “udongo wa kipekee” chini ya ziwa, na uwezekano wa kupatikana kwa mafuta mengi na gesi asilia.

Hadi leo hii, hakuna ushahidi wa wazi kuwa jamii zinazozunguka ziwa, iwe upande wa Malawi au Tanzania, watakuja kufaidika na utajiŕi huo.

Lakini kwa wakati huu, Kilumbo ana imani kuwa kuna samaki wa kutosha kuvua.

“Ndiyo, naweza kusema Wamalawi wanapata samaki wengi, lakini hii inatokana na kwamba sisi Watanzania tunapenda samaki wadogo na wachanga. Lakini kuna samaki wa kutosha. Sijui kama kuna mipango ya kuchimba mafuta, sijui kabisa.”