{"id":935,"date":"2005-04-19T13:40:01","date_gmt":"2005-04-19T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/19\/rushwa-kenya-ni-nati-ngumu-kuvunja\/"},"modified":"2005-04-19T13:40:01","modified_gmt":"2005-04-19T13:40:01","slug":"rushwa-kenya-ni-nati-ngumu-kuvunja","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/19\/rushwa-kenya-ni-nati-ngumu-kuvunja\/","title":{"rendered":"RUSHWA&ndash;KENYA: Ni Nati Ngumu Kuvunja"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Ap&#341;ili 16 (IPS) &ndash; Wakati se&#341;ikali ya Kenya inasafisha jina lake kutokana na madai ya &#341;ushwa, jitihada zake zinadhoofishwa na madai mapya ya &#341;ushwa katika mahakama. Utawala wa Rais Mwai Kibaki umeyumbisha mahakama katika ja&#341;ibio la kusafisha mfumo huo.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Bado haijafanikiwa. <\/p>\n<p>Katika &#341;ipoti yake ya Ap&#341;ili 7, Tume ya Majaji ya Kimataifa (ICJ) yenye makao yake makuu mjini Geneva ilisema &#341;ushwa katika mahakama imeendelea kubakia kuwa kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa utawala wa she&#341;ia nchini Kenya. <\/p>\n<p>Ripoti hiyo imetokana na uchunguzi wa kutafuta ukweli wa mambo nchini Kenya mwezi Desemba 2004 uliofanywa na ICJ kuhusu uhu&#341;u na uwazi wa mahakama. <\/p>\n<p>&#8221;Tulikusanya maoni na ushahidi tuliopata ni kwamba &#341;ushwa bado ipo lakini inatendeka katika hali ya usi&#341;i mkubwa kwasababu maofisa wa mahakana wanahofia (kuchukuliwa hatua),&#8221; alisema kiongozi wa ujumbe huo, Geo&#341;ge Kanyeihamba. <\/p>\n<p>Hatua wanazozungumzia ni pamoja na kufukuzwa kazi kwa majaji watano kati ya tisa katika Mahakama ya Rufaa, majaji 18 kati ya 36 na mahakimu 82 kati ya 254 waliohusishwa na &#341;ushwa. Kufukuzwa kwao kulitokana na &#341;ipoti iliyotolewa na Tume iliyoteuliwa na se&#341;ikali ya Uadilifu na Kupambana na Rushwa katika Mahakama nchini Kenya mwaka 2003. Majina ya maofisa wa mahakama waliohusishwa na &#341;ushwa yalichapishwa katika vyombo vya haba&#341;i. <\/p>\n<p>Kulingana na &#341;ipoti, majaji wa mahakama kuu walikuwa wakitoa maamuzi ya upendeleo kwa kupokea &#341;ushwa inayofikia kati ya dola 641 na 20,000 ikitegemeana na ugumu wa kesi. Rushwa za ngono pia zilikuwa sehemu ya &#341;ipoti. Mahakimu walipokea &#341;ushwa inayofikia kati ya dola 51 hadi 1,920. <\/p>\n<p>Masha&#341;ti mawili yalitolewa kwa majaji na mahakimu hao aidha kujiuzulu au wasubi&#341;i kufukuzwa kazi. Wengi wao walijiuzulu wenyewe na tangu wakati huo baadhi yao wamekuwa wakitafuta haki ya kishe&#341;ia kupinga kufukuzwa kwao kazi. <\/p>\n<p>Ni kesi moja tu kati ya zile zilizowasilishwa kwa mahakama iliyoanzishwa kuchunguza madai hayo imeweza kuamuliwa, kwa kuachiwa hu&#341;u kwa jaji wa mahakama ya &#341;ufaa mwishoni mwa mwaka jana. <\/p>\n<p>Halafu Rais Kibaki aliteua kaimu majaji wa Mahakama Kuu 28 kuchukua nafasi za majaji 18 ambao aidha walijiuzulu au walistaafu, na kuzusha wasiwasi kuhusu vigezo vilivyotumika kuwaingiza katika ofisi. Umma pia umeonyesha wasiwasi wake kutokana na kukosekana kwa uwazi katika mpango mzima wa uteuzi. <\/p>\n<p>Hata Jaji Mkuu Evans Giche&#341;u ali&#341;ipotiwa na vyombo vya haba&#341;i wiki iliyopita akisema kwamba se&#341;ikali inaingilia kazi za mahakama. Alizungumza katika mkutano wa siku tatu, ambao uliwakusanya wawakilishi 19 kutoka nchi za jumuiya ya madola kote ba&#341;ani Af&#341;ika, katika mji mkuu wa Kenya wa Nai&#341;obi. Mkutano huo uliegemea katika uwajibikaji na uhusiano kati ya nguzo tatu za se&#341;ikali: dola, mahakama na bunge. <\/p>\n<p>Kanyeihamba, ambaye pia ni mwanachama wa Mahakama Kuu ya Uganda, alitoa mwito kwa Kenya kuhakikisha uhu&#341;u wa mahakama. <\/p>\n<p>Rasimu ya katiba ya Kenya inatamka kuhusu uteuzi wa majaji, suala ambalo limekuwa na utata tangu &#341;ais Kibaki alipoteua wa&#341;ithi wa majaji walioathi&#341;ika na mabadiliko. Upinzani zaidi ulitokana na uteuzi wa jaji mkuu uliofanywa na &#341;ais mwaka jana, ambao wakosoaji wanaelezea kama uteuzi wa kisiasa. <\/p>\n<p>Ripoti ya ICJ inapendekeza kwamba kwa ajili ya uwazi na kuzingatia taaluma, uteuzi wote na kuongezewa vyeo katika mahakama uzingatie elimu, uadilifu, uwezo pamoja na uzoefu. Nafasi hizo inabidi zitangazwe na mapendekezo ya majina yawe mikononi mwa umma. <\/p>\n<p>Inaonekana kwamba se&#341;ikali pia imekubali kwamba mfumo wa sasa unaongeza &#341;ushwa katika mahakama. <\/p>\n<p>&#8221;Mfumo uliopo katika kuaji&#341;i majaji hautoshelezi na utabadilishwa tu kama &#341;asimu na katiba itapitishwa. Hakuna uwezekano wa aidha kumwondoa au kumteua jaji. Ni muhimu kwamba ushau&#341;i ufanyike kuhusu upendekezaji wa majina. Pia ni muhimu kwamba ushau&#341;iano uhusishe umma,&#8221; alisema Gichi&#341;a Kiba&#341;a, mku&#341;ugenzi wa masuala ya kishe&#341;ia katika wiza&#341;a ya she&#341;ia na mambo ya katiba. <\/p>\n<p>Wataalam wanasema uwazi pekee katika kuaji&#341;i maofisa wa mahakama hauwezi kutosha kumaliza &#341;ushwa katika mfumo wa mahakama. Jambo hili, wanasema, ni lazima liambatane na ongezeko la bajeti inayotengwa kwa ajili ya mahakama. <\/p>\n<p>&#8221;Mgawo mdogo wa bajeti katika mahakama, ambao unamaanisha mshaha&#341;a mdogo maana yake ni kwamba mtu anaweza kuyumbishwa,&#8221; Philip Kichana, mku&#341;ugenzi mtendaji wa ICK&ndash;Kenya aliliambia shi&#341;ika la haba&#341;i la IPS. <\/p>\n<p>Kwa sasa, mahakama inatumia asilimia moja ya bajeti nchini humo, kulingana na ICJ. Hii haitoshelezi kukidhi mahitaji ya wafanyakazi na vifaa muhimu kwa ajili ya uendeshaji wa utawala wa mahakama. <\/p>\n<p>Bajeti ya Kenya inafikia dola bilioni 5.4, hii ni kulingana na takwimu za se&#341;ikali. (END\/2005)<\/p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Ap&#341;ili 16 (IPS) &ndash; Wakati se&#341;ikali ya Kenya inasafisha jina lake kutokana na madai ya &#341;ushwa, jitihada zake zinadhoofishwa na madai mapya ya &#341;ushwa katika mahakama. Utawala wa Rais Mwai Kibaki umeyumbisha mahakama katika ja&#341;ibio la kusafisha mfumo huo. Bado haijafanikiwa. Katika &#341;ipoti yake ya Ap&#341;ili 7, Tume ya Majaji ya Kimataifa (ICJ) yenye&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":73,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-935","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/935","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/73"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=935"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/935\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=935"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=935"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=935"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}