{"id":932,"date":"2005-04-18T13:40:01","date_gmt":"2005-04-18T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/18\/afya-msumbiji-sea-zaidi-zinahitajika-kuwasaidia-wakulima-walioathiika-na-ukimwi\/"},"modified":"2005-04-18T13:40:01","modified_gmt":"2005-04-18T13:40:01","slug":"afya-msumbiji-sea-zaidi-zinahitajika-kuwasaidia-wakulima-walioathiika-na-ukimwi","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/18\/afya-msumbiji-sea-zaidi-zinahitajika-kuwasaidia-wakulima-walioathiika-na-ukimwi\/","title":{"rendered":"AFYA&ndash;MSUMBIJI: Se&#341;a Zaidi Zinahitajika Kuwasaidia Wakulima Walioathi&#341;ika na Ukimwi"},"content":{"rendered":"<p>MAPUTO, Ap&#341;ili 14 (IPS) &ndash; Akiwa amelala katika mkeka uliochakaa katika kibanda, Ma&#341;ia mwenye um&#341;i wa miaka 20 alikuwa akijitahidi na pumzi yake wakati alipokuwa akielezea kwa nini yeye na wajomba zake watano wa kike na wa kiume ambao ni yatima anaowatunza hawajapata chakula.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Ma&#341;ia, ambaye jina lake limebadilishwa ili kulinda si&#341;i za kifamilia, alikuwa akielekea kufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi, ikiwa ni pamoja na kukosa lishe. &#8221;Ilibidi niuze shamba langu ili kuweza kuishi,&#8221; alisema kwa kugugumia. Machozi yalimtoka na kuti&#341;i&#341;ika mashavuni mwake. &#8221;Sijanywa vidonge vyangu (kwa ajili ya kifua kikuu) kwa siku tano sasa, kwasababu nina njaa sana. Vidonge vitanifanya nijisikie mgonjwa, kama nitakunywa bila ya chakula.&#8221; <\/p>\n<p>Ma&#341;ia alielezea kwamba aliacha shule akiwa na miaka 15 ili kuwatunza wazazi wake, ambao walikuwa wagonjwa kwa muda m&#341;efu kabla hawajafa&#341;iki dunia. Mume wake alimfukuza alipoanza kuumwa, na watoto aliokuwa nao ni wa dada zake watatu, ambao wote hao walikwishafa&#341;iki na Ukimwi. Mpwa wake mkubwa mwenye um&#341;i wa miaka 14 taya&#341;i ana mtoto. <\/p>\n<p>Ma&#341;ia alifa&#341;iki dunia Mwezi mmoja baada ya mahojiano. Ilibidi watoto aliokuwa akiwatunza kuondoka katika nyumba walimokuwa wakiishi kutokana na mtu mmoja kuja na kudai nyumba hiyo ilikuwa ni ya kwao. Ji&#341;ani, ambaye alikuwa akimtembelea Ma&#341;ia, ambaye pia anaishi na Vi&#341;usi Vya Ukimwi, aliwapatia yatima maskini wa Ma&#341;ia makazi ya muda. <\/p>\n<p>Familia hiyo inaishi Nicoadala, katika mkoa wa kaskazini wa Zambezia, ambao mwanzoni ulijulikana kama eneo maa&#341;ufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula katika Msumbiji, kutokana na kwamba unaweza kulisha nchi nzima. Lakini sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na madha&#341;a ya vita vya wenywewe kwa wenyewe ambavyo vilimalizika mwaka 1992, umaskini ulioenea sana, na hali ya hewa isiyoaminika imefanya familia nyingi kulima mazao ya chakula tu na kuwa na uwezo mdogo wa kupambana na gonjwa la Ukimwi ambalo linaongezeka kwa kasi kubwa nchini humo, pamoja na kwamba atha&#341;i zake kamili bado hazijaonekana. <\/p>\n<p>Mwaka 2003 kasi ya maambukizo ya Ukimwi nchini Msumbiji ilikuwa ni asilimia 13.6 na mwaka jana iliongezeka hadi asilimia 14.9. Shi&#341;ika la Kilimo na Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) plinakadi&#341;ia kwamba kati ya mwaka 1985 na 2020 Msumbiji itapoteza zaidi ya asilimia 20 ya nguvukazi yake katika kilimo kutokana na Ukimwi. <\/p>\n<p>Watunga se&#341;a waliowengi wanatambua kwamba Ukimwi siyo tatizo la kiafya tu, lakini kuunda se&#341;a za kutosha kuondokana na atha&#341;i mbaya za gonjwa hilo, hasa kwa wakulima wadogo wadogo &ndash; ambao wanafikia asilimia 77 ya idadi ya watu wote nchini Msumbiji &ndash; inabakia kuwa changamoto kubwa. <\/p>\n<p>Kinachoonekana wazi ni kwamba hadithi zinazotolewa zinatisha. &#8221;Hadithi ya familia hiyo (ya Ma&#341;ia na yatima zake) na wengine inatupa wazo zima la hali halisi,&#8221; alisema Be&#341;tine Niesten, ofisa mi&#341;adi wa FAO na kiongozi kiungo kuhusu masula ya Ukimwi. <\/p>\n<p>&#8221;Ni lazima tukumbuke atha&#341;i mbaya za Ukimwi ambapo Ukimwi unaweza kuongeza hata&#341;i ya upatikanaji wa chakula na lishe, na kwa upande mwingine unaweza kuongeza atha&#341;i za Ukimwi kutokana na kwamba watoto wanalazimika kuacha shule na vijana, hasa wa kike, kujiingiza katika vitendo hata&#341;i ili kuwawezesha kuishi,&#8221; alisema. <\/p>\n<p>&#8221;Bado ni changamoto kuhakikisha kwamba mashi&#341;ika ya ndani yanahakikisha yanaunganisha Ukimwi katika mi&#341;adi yao katika sekta ya kilimo,&#8221; Niesten alisema. &#8221;Pia ni vigumu kutambua familia kwasababu ya unyanyapaa unaohusiana na Ukimwi.&#8221; <\/p>\n<p>Tangu mwaka 1999 se&#341;a za se&#341;ikali ikiwa ni pamoja na sekta ya kilimo, zilielekezwa zaidi katika kuzuia Ukimwi. Mwaka 2002, se&#341;a zilianza kushughulikia suala la kupambana na Ukimwi, hasa katika maeneo ya vijijini. <\/p>\n<p>Tangu mwanzo wa mwaka jana, pesa kidogo zilipatikana kwa ajili ya matibabu kwa kutumia madawa ya kuongeza muda wa kuishi (ARVs) katika mfumo wa afya wa se&#341;ikali na kwa ajili ya matunzo ya wagonjwa.<\/p>\n<p>Tafiti nyingi kuhusu madha&#341;a ya ukimwi kwa wakulima wadogo wadogo zinahusu nadha&#341;ia na maneno. Utafiti uliofanywa huko Chokwe, katika mkoa wa kusini wa Gaza kuhusu uelewa wa wakulima kuhusu mbegu, uliofadhiliwa na FAO, na kuchapishwa Janua&#341;i 2004 ulihitimisha kwamba athali za ukimwi za muda m&#341;efu hazishughulikiwi kikamilifu. Utafiti unasema kwamba ukimwi, pamoja na sababu nyingine, unaweza kuondoa uelewa wa wakulima kuhusu usimamizi wa mbegu &ndash; jambo ambalo ni changamoto kubwa kwa usalama wa chakula katika ngazi ya kaya. <\/p>\n<p>Hata hivyo , utafiti ambao utatolewa katika mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi, chakula na usalama katika hali ya lishe nchini Af&#341;ika Kusini mwezi huu unataka kufiki&#341;iwa upya kwa maoni ya sasa. Inapendekezwa kwamba baadhi ya mabadiliko katika Kilimo kwenye ukanda wa Kusini mwa Af&#341;ika hayajatokana na ukimwi lakini yanawezekana kusababishwa zaidi na mabadiliko katika se&#341;a za kilimo. <\/p>\n<p>Watunzi wa se&#341;a nchini Msumbiji wanakubali kwamba kuna haja ya kuweka kipaumbele zaidi katika kupambana na atha&#341;i za gonjwa hilo hasa kwenye usalama wa chakula. Kwa sasa se&#341;ikali inatekeleza mipango tofauti katika mikoa yote 11 ya nchi hiyo, lakini idadi ya wakulima wadogo wadogo wanaofikiwa na mipango hiyo ni ndogo ikilinganishwa na hali ya ugonjwa huo. Zaidi ya watu milioni 1.5 wanaishi na vu&#341;usi nchini humo. <\/p>\n<p>Albe&#341;tina Alage, mkuu wa ida&#341;a ya kilimo katika maeneo ya vijijini ambaye anashughulikia pia masuala ya Ukimwi katika wiza&#341;a ya kilimo alisema, &#8221;Tumeendelea sana, lakini bado tuna matatizo. Ma&#341;a nyingine fedha kwa ajili ya mipango yetu hazipatikani kabisa.&#8221; <\/p>\n<p>Alage alielezea kwamba tangu mwaka 1999 wafanyakazi wa kukuza kilimo wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kuhusu mbinu mpya za kilimo na jinsi ya kuzuia maambukizo ya Ukimwi. &#8221;Tuna matatizo katika suala hilo kutokana na kwamba tuna wanawake wachache ambao ni wafanyakazi wa kuendeleza kilimo. Hivyo badala yake tunateua mwanamke katika jamii ili pia kusaidia katika vikao vyetu. Pia hatuna nyenzo nyingi za kutumika katika mawasiliano katika lugha za wenyeji,&#8221; alisema. <\/p>\n<p>Katika mipango ya mwaka 2002 iliyokuwa ikija&#341;ibu katika kupunguza atha&#341;i, Alage alitoa mfano wa kuwa na mashine za mifumo ya maadnalizi ya mazao ya jamii, ambayo itasaidia familia zilizoathi&#341;ika na ugonjwa na kuwapa muda wa kufanya kazi zao za mashambani vizu&#341;i na kuwatunza wagonjwa. &#8221;Halafu wanaweza kuunda vyama na kuomba mikopo,&#8221; alisema. <\/p>\n<p>FAO inasaidia se&#341;ikali ya mkoa wa katikati mwa nchi wa Sofala kutekeleza m&#341;adi wa ku&#341;efusha maisha ya wafanyakazi wa kuendeleza kilimo vijijini. Kiwango cha maambukizi ya vi&#341;usi mkoani Sofala ni zaidi ya asilimia 30, na wafanyakazi wa kilimo wako katika hata&#341;i zaidi ya kuambukizwa vi&#341;usi, kutokana na kuwa wanasafi&#341;i sana. Wanapelekwa katika maeneo bila ya familia zao na kuishi huko kwa muda m&#341;efu. <\/p>\n<p>Kutokana na ombi la se&#341;ikali ya mkoa FAO inasaidia wafanyakazi wa kilimo vijijini ambao wanatumia ARVs kwa kuwapatia pesa za usafi&#341;i ili waweze kufanya safa&#341;i za ma&#341;a kwa ma&#341;a katika miji mikuu ya mikoa kuweza kupata matibabu na kujipatia vidonge vyao &#8221;Kitengo cha kilimo mikoani kimeundwa vizu&#341;i sana. Ilikuwa ni ombi lao kutokana na kuwa na wasiwasi na idadi kubwa ya wafanyakazi wa kilimo waliokuwa wakiwapoteza kutokana na Ukimwi,&#8221; Niesten alielezea. <\/p>\n<p>FAO pia inasaidia wanafunzi 840 yatima wenye um&#341;i kati ya miaka 12&ndash;17 katika mikoa ya kati ya Manica na Sofala kuhusu stadi za maisha na mbinu za kilimo ambazo zinatolewa katika mashamba ya maja&#341;ibio. Wanafunzi wanajifunza jinsi ya kuzuia magonjwa, kutumia mbolea za chumvi chumvi na wakati huo huo wanajifunza stadi za maisha. Dhana na mpango huo, anaelezea Valentina P&#341;ospe&#341;i, mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika shi&#341;ika la FAO, &#8221;ni kwamba wanafunzi waje kuwafunza wazazi wao na jumuiya.&#8221; <\/p>\n<p>Eneo jingine ambalo ni muhimu kuhusu usalama wa chakula wa muda m&#341;efu ni haki ya u&#341;ithi. Shi&#341;ika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) na FAO kwa pamoja yanasaidia se&#341;ikali kuweka she&#341;ia zaidi kuwalinda watoto kutokana na Ukimwi. <\/p>\n<p>Shi&#341;ika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) pia linaunga mkono idadi kubwa ya p&#341;og&#341;amu zinazoelekezwa katika kubo&#341;esha usalama wa chakula kwa wafanyakazi wa kilimo vijijini wanaoishi na Ukimwi. Kwa mfano, WFP inatoa unga wa soya, wenye vi&#341;utubisho kwa zaidi ya watu 4,000, ikiwa ni pamoja na wanawake wajawazito, ambao wanatumia madawa ya ku&#341;efusha muda wa kuishi. Watu wenye Ukimwi wanahitaji asilimia 10&ndash;30 zaidi ya vyakula vya kuongeza nguvu kuliko mtu mzima. <\/p>\n<p>WFP pia inatoa mgawo wa chakula kwa watu 20,000 walioathi&#341;ika na gonjwa hilo na watoto yatima 50,000. <\/p>\n<p>Naibu mku&#341;ugenzi wa WFP, Ka&#341;in Manente, alielezea kwamba, &#8221;uendelevu ni muhimu. Hii ndiyo sababu msaada wetu upo kwa muda mfupi. Kwa mfano tunatoa ARVs kwa wagonjwa kwa miezi sita ya kwanza, ili kuwasaidia kuweza ku&#341;ejesha hali zao za kawaida katika kipindi kigumu zaidi. Tunapenda kuwasaidia watu kuongeza muda wao wa kuishi, hii pia inasaidia watoto kuendelea kusoma.&#8221; <\/p>\n<p>Kama ilivyo kwa Msumbiji, nchi nyingi kati ya mataifa 13 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Af&#341;ika (SADC) zinakabiliwa na tatizo kama hilo. Katika ukanda wa Kusini mwa Af&#341;ika wenye asilimia mbili ya watu wote ulimwenguni; kuna asilimia 70 ya watu wote ulimwenguni wanaoishi na vi&#341;usi vya Ukimwi na kuugua Ukimwi, hii ni kulingana na shi&#341;ika la misaada la kimataifa la ActionAid, lenye makao yake makuu nchini Af&#341;ika Kusini. (END\/2005)<\/p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MAPUTO, Ap&#341;ili 14 (IPS) &ndash; Akiwa amelala katika mkeka uliochakaa katika kibanda, Ma&#341;ia mwenye um&#341;i wa miaka 20 alikuwa akijitahidi na pumzi yake wakati alipokuwa akielezea kwa nini yeye na wajomba zake watano wa kike na wa kiume ambao ni yatima anaowatunza hawajapata chakula. Ma&#341;ia, ambaye jina lake limebadilishwa ili kulinda si&#341;i za kifamilia, alikuwa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":197,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-932","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/932","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/197"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=932"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/932\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=932"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=932"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=932"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}