{"id":931,"date":"2005-04-18T13:40:01","date_gmt":"2005-04-18T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/18\/rushwa-kenya-wafadhili-watishia-kusitisha-misaada\/"},"modified":"2005-04-18T13:40:01","modified_gmt":"2005-04-18T13:40:01","slug":"rushwa-kenya-wafadhili-watishia-kusitisha-misaada","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/18\/rushwa-kenya-wafadhili-watishia-kusitisha-misaada\/","title":{"rendered":"RUSHWA&ndash;KENYA: Wafadhili Watishia Kusitisha Misaada"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Ap&#341;ili 13 (IPS) &ndash; Se&#341;ikali ya Kenya kwa ma&#341;a nyingine tena ipo matatani kutokana na &#341;ushwa ambayo wafadhili wanasema inadhoofisha jitihada za kutekeleza mageuzi yaliyotajwa katika Mkakati wa Kufufua Uchumi nchini humo.\n <\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Wakionyesha dhami&#341;a yao, wafadhili wamedai kwamba se&#341;ikali ionyeshe ma&#341;a moja dhami&#341;a yake ya kupambana na ufisadi kwa kuziba mianya ambayo inasababisha &#341;ushwa. Kama &#341;ushwa inashughulikiwa, wanasema, wafadhili watakuwa hawana njia ila kuendelea kuipatia Kenya msaada wa kifedha. <\/p>\n<p>&#8221;Tunapenda kusisitiza kwamba kiwango cha msaada wetu kitategemeana na mafanikio ya se&#341;ikali katika kutekeleza (Mkakati wa Kufufua Uchumi) ERS, na hasa katika kupambana na &#341;ushwa,&#8221; Makhta&#341; Diop, mku&#341;ugenzi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake nchini Kenya, E&#341;it&#341;ea na Somalia, alisema. Alikuwa akizungumza katika mkutano wa pili wa Kikundi cha Ushau&#341;iano (CG) kwa ajili ya Kenya, uliofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Nai&#341;obi Ap&#341;ili 11&ndash;12. <\/p>\n<p>Mkutano huo ulifanya tathmini ya mafanikio katika kutekeleza mkakati wa kufufua uchumi kwa kuweka kipaumbele maalum katika vikwazo na changamoto zilizoikabili se&#341;ikali. Mkutano huo uliwaleta pamoja wahisani, viongozi wa juu se&#341;ikalini, wabunge, sekta binafsi na mashi&#341;ika ya ki&#341;aia. <\/p>\n<p>Mkutano wa ushau&#341;iano wa kwanza nchini Kenya ulifanyika mjini Nai&#341;obi mwezi Novemba 2003. Hapo awali, mikutano ya kila mwaka ya kikundi cha ushau&#341;iano, au wafadhili wasiokuwa maalum ilifanyikia mjini Pa&#341;is au London. <\/p>\n<p>Wakati se&#341;ikali ya Rais Mwai Kibaki ilipokuja mada&#341;akani mwezi Desemba 2002, iliweka Mkakati wa Kufufua Uchumi wa miaka mitano (2003&ndash;2007). <\/p>\n<p>Mkakati huo, ambao unafanya kazi kama mwongozo katika kufanikisha maendeleo kwa kuweka kipaumbele katika kujenga mazingi&#341;a ya utulivu wa njia kuu za kiuchumi kwa kukuza ukusanyaji wa kodi, kubo&#341;esha utawala, kuka&#341;abati na kupanua miundombinu, na kuwekeza katika mtaji wa nguvukazi kwa maskini. <\/p>\n<p>Balozi wa Uinge&#341;eza nchini Kenya, Edwa&#341;d Clay, anasema &#341;ushwa imeigha&#341;imu nchi hiyo ya Af&#341;ika Masha&#341;iki zaidi ya dola milioni 187 tangu Kibaki alipochukua mada&#341;aka. Wakikanusha dai hilo, viongozi wa se&#341;ikalini walikuwa wakielezea mafanikio ya kiuchumi ya Kenya, kama kigezo kwamba vita dhidi ya ufisadi ilikuwa ikizaa matunda. <\/p>\n<p>&#8221;Ni kitu cha kutia moyo kutambua kwamba usimamizi huu wa mafanikio wa se&#341;a za njia kuu za uchumi kumeanza kuzaa matunda mazu&#341;i. Hasa, GDP (Pato la Ndani) limeongezeka kutoka wastani wa chini ya asilimia moja katika muongo uliopita hadi 2.6 mwaka 2004, na inakadi&#341;iwa kuja kufikia asilimia 3.5 mwaka 2005,&#8221; David Mwi&#341;a&#341;ia, wazi&#341;i wa fedha wa Kenya, alisema. <\/p>\n<p>Lakini Diop alisema kwamba takwimu iliyotolewa na Mwi&#341;a&#341;ia inabakia kuwa ndogo mno kwa Kenya kuweza kufikia Malengo Makuu ya Maendeleo ya Milenia ( MDG) ya kupunguza nusu ya umaskini ifikapo mwaka 2015. <\/p>\n<p>Madai ya kuenea kwa &#341;ushwa katika se&#341;ikali ya &#341;ais wa zamani Daniel a&#341;ap Moi (1978&ndash;2002) kulisababisha Shi&#341;ila la Fedha Ulimwenguni (IMF) kusitisha kutoa misaada kwa nchi hiyo mwaka 2001. <\/p>\n<p>Lakini mkutano wa kikundi cha kutoa ushau&#341;i cha wafadhili mwaka 2003 na se&#341;ikali kilishuhudia IMF iki&#341;ejesha kuikopesha Kenya dola bilioni 252.75 kupiga vita umaskini. <\/p>\n<p>Mwezi Juni 2004, Benki ya Dunia, moja ya wafadhili wakuu wa Kenya, ilitoa dola milioni 263 kwa ajili ya mi&#341;adi ya maendeleo katika usafi&#341;i, kilimo na sekta ya maji. <\/p>\n<p>Sasa hivi wafadhili wameonyesha kwamba ili misaada ya kifedha iweze kuendelea kutolewa, ni lazima se&#341;ikali kutekeleza she&#341;ia za kupiga vita umaskini. &#8221;Kama she&#341;ia zitatekelezwa, Kenya itaweza kuwa na kiwango cha ubo&#341;a katika vita dhidi ya &#341;ushwa, ambayo ni ahadi iliyotolewa na se&#341;ikali ilipochaguliwa mada&#341;akani,&#8221; Diop alisema. <\/p>\n<p>Kibaki alikuwa hana mzaha na &#341;ushwa ma&#341;a tu alipoingia mad&#341;akani kama alivyoahidi wakati wa kampeni zake za uchaguzi kabla hajaingia mada&#341;akani. <\/p>\n<p>Umoja wa Ulaya (EU),mfadhili wa pili kwa kutoa misaada mingi katika nchi hiyo, pia umetoa msimamo wake wa wazi kuhusu &#341;ushwa. Katika mkutano wa Ap&#341;ili 11 mjini Nai&#341;obi, De&#341;ek Fee, kiongozi wa ujumbe wa EU, aliwaambia waandishi wa haba&#341;i kwamba Kenya ni lazima kuonyesha dhami&#341;a yake kufutilia mbali ufisadi kabla wafadhili hawajaamua kutoa misaada. Dhami&#341;a hiyo iwe ni pamoja na kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa ngazi za juu wa se&#341;ikali waliohusishwa na &#341;ushwa. <\/p>\n<p>Majina ya mawazi&#341;i wa juu wa se&#341;ikali walio ka&#341;ibu na Kibaki yamekuwepo katika kashfa ambazo zimekuwa msingi wa msuguano kati ya se&#341;ikali na wajumbe wa kigeni katika siku za hivi ka&#341;ibuni. <\/p>\n<p>Moja ya kashfa hizo, ambayo inajulikana kama kashfa ya Anglo&ndash;Leasing, ambayo iliwekwa juani Ap&#341;ili iliyopita, inahusu utoaji wa zabuni bila kufuatwa kwa ta&#341;atibu na malipo katika kutengeneza pasi za kusafi&#341;ia zisizoweza kughushiwa na magaidi na ujenzi wa maaba&#341;a ya ida&#341;a ya upelelezi wa makosa ya jinai. Aliyekuwa wazi&#341;i wa usalama wa taifa Ch&#341;is Mu&#341;unga&#341;u, pamoja na mwenzake wa fedha Mwi&#341;a&#341;ia, walidaiwa kupitisha malipo ya ka&#341;ibu dola milioni 93 kwa kampuni ya Anglo&ndash;Leasing, ambayo ni kampuni ya nje ya kughushi. <\/p>\n<p>Mawazi&#341;i hao wamekanusha madai hayo kwa kupitia taa&#341;ifa kwa vyombo vya haba&#341;i. Lakini makatibu wao wakuu walifukuzwa na kushitakiwa mahakamani mwezi wa Feb&#341;ua&#341;i. <\/p>\n<p>Katika hotuba yake Ap&#341;ili 11, Kibaki alisema kwamba hatua za kishe&#341;ia zinachukuliwa kushughulikia &#341;ushwa. Alitaja She&#341;ia ya Kupambana na Rushwa na Makosa ya Kiuchumi ya Mwaka 2003, ambayo iliunda Tume ya Kupambana na Rushwa ya Kenya (KACC) iliyopewa jukumu la kuchunguza viongozi waliohusishwa na &#341;ushwa. <\/p>\n<p>Chombo hicho, ambacho wakosoaji wamekielezea kuwa kinakosa meno, hakina uwezo wa kufungua mashitaka. Lakini se&#341;ikali inasema tume hiyo taya&#341;i imeshapeleka zaidi ya kesi 47 katika ofisi ya Mwanashe&#341;ia Mkuu ili kuchukuliwa hatua. <\/p>\n<p>Se&#341;ikali pia ilihusika katika jitihada za kuondoa vikwazo vinavyozuia ukuaji wa uchumi. &#8221;Inabidi tufanye kazi katika mazingi&#341;a mazu&#341;i kuweza kukuza uwekezaji katika sekta binafsi. Hii inaendelea lakini katika kasi ndogo sana,&#8221; Mukhisa Kituyi, wazi&#341;i wa biasha&#341;a, aliliambia shi&#341;ika la haba&#341;i la IPS. <\/p>\n<p>Vikwazo hivi ni pamoja na uhalifu, ambao ni tatizo kubwa nchini Kenya. Kulingana na takwimu za se&#341;ikali, kiwango cha uhalifu katika miezi ya Janua&#341;i na Feb&#341;ua&#341;i mwaka huu na kipindi kama hicho mwaka jana zinaonyesha ongezeko la asilimia 43.3 katika kesi za mauaji. <\/p>\n<p>Mwezi uliopita Mkuu wa polisi Meja Jene&#341;ali Mohammed Hussein Ali alisema jeshi lake lilikamata bunduki 443 na &#341;isasi 5,316 mwaka 2004. Hadi ilipofika mwishoni mwa Janua&#341;i mwaka huu, polisi walipokonya bunduki zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha she&#341;ia 27 na &#341;isasi 218, alisema. <\/p>\n<p>Mwishoni mwa mkutano wa wafadhili Ap&#341;ili 12, se&#341;ikali ilitoa mkakati wa utekelezaji kupunguza &#341;ushwa katika kipindi cha miaka miwili, kuanzia Ap&#341;ili 2005. <\/p>\n<p>&#8221;Ni wa&#341;aka wa se&#341;ikali, tumeandaa wenyewe. Rushwa ni tatizo letu na tutapambana nayo. Kinachofanya mkakati huu wa utekelezaji kuwa tofauti ni kwamba una muda maalum kwa maana ya kwamba kila kitu kina muda wake maalum. Kazi nyingi zitafanyika mwaka huu na mwaka kesho,&#8221; Mwi&#341;a&#341;ia aliwaambia waandishi wa haba&#341;i katika mkutano kwa waandishi wa haba&#341;i siku ya Jumanne. <\/p>\n<p>Wafadhili wanasema mpango huo usambazwe kwa Wakenya wote ili waweze kumiliki mpango mzima wa kupambana na ufisadi. &#8221;Ni mwanzo mzu&#341;i sana na msingi wa kuchunguza se&#341;ikali itafanya nini kupambana na &#341;ushwa. Se&#341;ikali ipeleke mpango mzima wa utekelezaji na kuufanya kufikiwa na Wakenya wote,&#8221; Diop aliuambia mkutano. <\/p>\n<p>Alisema wafadhili watatoa ahadi tu baada ya se&#341;ikali kutekeleza mabadiliko yaliyopo katika mpango huo, ambao utekelezaji wake utafuatiliwa. &#8221;Kutakuwa na mfumo wa ufuatiliaji wa mpango huo,&#8221;alisema. <\/p>\n<p>Umoja wa Ulaya pia umekubali mpango huo. &#8221;Nafiki&#341;i mpango huo umeweka msingi mzu&#341;i kwa ajili ya hatma ya baadaye kwa upande wa utawala. Tutakuja kuujadili zaidi na se&#341;ikali katika wiki chache zijazo,&#8221; Fee alisema. <\/p>\n<p>Mwaka jana EU ilisitisha msaada wa kusaidia bajeti ya nchi hiyo unaofikia Eu&#341;o milioni 50 kutokana na madai ya &#341;ushwa dhidi ya se&#341;ikali, baada ya balozi wa Uinge&#341;eza Clay kuwa wa kwanza kutoa taa&#341;ifa za &#341;ushwa. (END\/2005) <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Ap&#341;ili 13 (IPS) &ndash; Se&#341;ikali ya Kenya kwa ma&#341;a nyingine tena ipo matatani kutokana na &#341;ushwa ambayo wafadhili wanasema inadhoofisha jitihada za kutekeleza mageuzi yaliyotajwa katika Mkakati wa Kufufua Uchumi nchini humo. Wakionyesha dhami&#341;a yao, wafadhili wamedai kwamba se&#341;ikali ionyeshe ma&#341;a moja dhami&#341;a yake ya kupambana na ufisadi kwa kuziba mianya ambayo inasababisha &#341;ushwa&#8230;.<\/p>\n","protected":false},"author":73,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-931","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/931","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/73"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=931"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/931\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=931"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=931"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=931"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}