{"id":926,"date":"2005-04-11T13:40:01","date_gmt":"2005-04-11T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/11\/utamaduni-uganda-waislamu-wataka-mabadiliko-katika-muswada-wa-haki-za\/"},"modified":"2005-04-11T13:40:01","modified_gmt":"2005-04-11T13:40:01","slug":"utamaduni-uganda-waislamu-wataka-mabadiliko-katika-muswada-wa-haki-za","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/04\/11\/utamaduni-uganda-waislamu-wataka-mabadiliko-katika-muswada-wa-haki-za\/","title":{"rendered":"UTAMADUNI&ndash;UGANDA: Waislamu Wataka Mabadiliko Katika Muswada wa Haki za"},"content":{"rendered":"<p>KAMPALA, Ap&#341; 7 (IPS) &ndash; Wafuasi wa jumuiya ya Waislamu walio wachache nchini Uganda wamepinga muswada wa mahusiano ya nyumbani katika nchi yao, kwa kusema unakwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu. <\/p>\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Wakionyesha kuchukizwa kwao, maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za nchi (polisi inakadi&#341;ia idadi yao kuwa 7,000), wakiongozwa na Shehe Ramadhan Mubajje, walifanya maandamano katika mji mkuu wa Uganda wa Kampala kupinga muswada huo wiki iliyopita. Muswada huo sasa upo bungeni. <\/p>\n<p>Waandamanaji hao, ambao ni pamoja na wanawake, vijana na wazee walivalia hijabs, au vazi la Kiislamu, linalofunika vichwa vyao. Wakati wa tukio hilo, walibeba mabango na bende&#341;a yanayopinga vifungu vya muswada huo vinavyohusu ndoa za mita&#341;a, maha&#341;i, kuwekana kinyumba na um&#341;i wa kuolewa &ndash; vitu ambavyo vinafanywa na Waislamu. <\/p>\n<p>Wakiandamana kuelekea bungeni, walionyesha saini ya vidole vinne, wakimaanisha tabia ya kuoa hadi wake wanne, kama inavyoelezewa katika Uislamu. Waandamanaji walidai kwamba muswada huo ulipingana na mafundisho ya Ko&#341;an, na kwamba unaegemea katika she&#341;ia za Kik&#341;isto. <\/p>\n<p>Kwa kipindi cha miaka mingi, wanaha&#341;akati wanawake wameona muswada huo kama chombo chenye nguvu ambacho kingeweza kuwalinda kutokana na mila mbaya kama vile toha&#341;a kwa wanawake (FGM), maha&#341;i na u&#341;ithi wa mjane. Wanawake wamekuwa wakiituhumu se&#341;ikali kutokana na kuchelewa kupitisha muswada huo, ambao umekuwa makabatini kwa ka&#341;ibu miaka 40. <\/p>\n<p>Muswada huo unaojulikana kama Muswada wa Mahusiano ya Nyumbani (DRB), unawapa &#8221;wanaume na wanawake haki sawa za ndoa, wakati wa kuoana na wakati wa kuachana &#8221;. <\/p>\n<p>Wanaha&#341;akati wanasema muswada huo utatoa mchango mkubwa katika kupunguza kuenea kwa Ukimwi. Wanawake, hasa wale wanaobeba mzigo mkubwa wa kuwalea wanaoishi na Vi&#341;usi Vya Ukimwi, wana uwezekano mkubwa wa kupata vi&#341;usi kuliko wanaume. <\/p>\n<p>Kulingana na Shi&#341;ika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (UNAIDS), zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi mapya ya Vi&#341;usi Vya Ukimwi duniani kote yanawapata wanawake. Na katika nchi ambapo vijana wanafikia asilimia 60 ya maambukizi yote, wanawake wanaoambukizwa wanazidi idadi ya wanaume kwa uwiano wa 2 kwa 1. UNAIDS pia inakadi&#341;ia kwamba ka&#341;ibu watu milioni nane katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a (kati ya wanawake milioni 10 walioambukizwa duniani kote) wanaishi na vi&#341;usi. <\/p>\n<p>Wakisimamia msimamo wa dini yao, viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Uganda wamepinga madai kwamba hawajui mabadiliko yanayojitokeza sasa katika jamii. <\/p>\n<p>&#8221;Ko&#341;an inahusika na maeneo yote katika ndoa, watoto na mahusiano. Hakuna haja kuandaa she&#341;ia nyingine kwa ajili ya Waislamu. Mwanaume anaweza kuoa kutegemeana na uwezo wake wa kutunza na kuima&#341;isha mahusiano yake,&#8221; Shehe Mubajje alisema katika maandamano hayo. <\/p>\n<p>Katika taa&#341;ifa yao kwa Naibu Spika wa Bunge Rebecca Kadaga, Mubajje alisema Waislamu wanataka jina la muswada libadilishwe na um&#341;i wa kuoa au kuolewa uwe ni wakati mwanamke anapofikia &#8216;um&#341;i wa ba&#341;ehe&#8217; kuliko miaka 18 iliyopendekezwa. <\/p>\n<p>Wakati ambapo Tume ya Haki za Binadamu nchini Uganda mwezi Feb&#341;ua&#341;i iliomba bunge kuha&#341;amisha ndoa za mita&#341;a, kwa madai kwamba zinadhoofisha utu wa wanawake na maisha ya kifamilia, katika Uislamu, siyo tu mwanaume anatetea ndoa za mita&#341;a. Hata wanawake wanatetea. <\/p>\n<p>&#8221;Wanawake wengi sana wanatafuta wanaume wa kuwaoa. Kuna wajane wengi. Kama she&#341;ia itazuia wanaume wasioe zaidi ya mke mmoja, nani atawaoa wajane &#8221; anauliza Fatuma Kamulali, mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Wanawake wa Kiislamu nchini Uganda chenye makao yake makuu mjini Kampala. <\/p>\n<p>Fa&#341;idah Kakai&#341;e, ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho, alisema: &#8221;She&#341;ia isiwanyime wanaume zetu kuoa idadi ya wanawake wanaowataka. Mwanaume anaoa kumfu&#341;ahisha Allah (Mungu) na siyo kumfu&#341;ahisha mwanadamu.&#8221; <\/p>\n<p>Kulingana na utafiti uliofanywa na Chama cha Wanashe&#341;ia Wanawake (FIDA) mwaka 1999, ka&#341;ibu asilimia 85 ya wanawake waliohojiwa nchini Uganda walisema wasingeweza kuwa katika ndoa za mita&#341;a kama wangekuwa na uchaguzi. <\/p>\n<p>&#8221;Wanawake hao hawakuwa na fu&#341;sa ya kusoma. Hakuna ambaye aliwahi kuwafikia kuelewa vifungu vya muswada huo,&#8221; No&#341;ah Matovu Winyi, mwenyekiti wa FIDA, alisema katika mahojiano na gazeti la &#8220;Sunday Monito&#341;&#8221; linalochapishwa nchini humo. <\/p>\n<p>Baadhi ya wanaha&#341;akati wanaamini kwamba kuna vifungu maalum vya muswada ambavyo vimetafs&#341;iwa vibaya. &#8221;Nafiki&#341;i Waislamu wanatafsi&#341;i vibaya DRB, hasa kifungu kinachohusu ndoa za mita&#341;a,&#8221; Solome Nakawesi Kimbugwe, m&#341;atibu wa Mtandao wa Wanawake wa Uganda aliliambia shi&#341;ika la haba&#341;i la IPS katika mahojiano kwa njia ya simu. <\/p>\n<p>&#8221;Nafiki&#341;i kuingia kwao mitaani kuandamana kunaonyesha Tume ya Bunge inabidi i&#341;udi katika chombo cha uandishi,&#8221; alisema. <\/p>\n<p>Wiki iliyopita Tume ya She&#341;ia na Masuala ya Bunge ilikubaliana na baadhi ya madai ya jumuiya ya Waislamu, kwa &#8216;kuondoa&#8217; baadhi ya vifungu vya muswada, kutokana na kuonekana kwa mapungufu ya kitamaduni na kidini. <\/p>\n<p>Tume ilipendekeza kwamba jina la muswada libadilishwe na kuwa &#8216;She&#341;ia ya Ndoa na Familia&#8217; na kwamba she&#341;ia hiyo inatakiwa kutambua jumuiya zinazotumia &#8216;zawadi za ndoa&#8217;, ikimaanisha maha&#341;i. <\/p>\n<p>Pia ilipendekeza kwamba neno &#8221;u&#341;ithi wa mjane&#8221; liandikwe upya na nafasi yake ichukuliwe na neno &#8221;kuolewa upya kulingana na destu&#341;i za kimila &#8221;. <\/p>\n<p>Hata hivyo, wafuasi wa jumuiya ya Kiislamu, ambao wanafikia asilimia 16 ya idadi ya watu wote nchini Uganda, bado hawajachukua hatua zozote kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na tume. <\/p>\n<p>= 04071653 ORP015 NNNN (END\/2005) <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>KAMPALA, Ap&#341; 7 (IPS) &ndash; Wafuasi wa jumuiya ya Waislamu walio wachache nchini Uganda wamepinga muswada wa mahusiano ya nyumbani katika nchi yao, kwa kusema unakwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu. Wakionyesha kuchukizwa kwao, maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za nchi (polisi inakadi&#341;ia idadi yao kuwa 7,000), wakiongozwa na Shehe Ramadhan Mubajje, walifanya maandamano&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":15,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-926","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/926","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/15"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=926"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/926\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=926"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=926"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=926"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}