{"id":881,"date":"2005-02-28T13:40:01","date_gmt":"2005-02-28T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/02\/28\/afya-mauritania-maambukizi-madogo-ya-hiv-unyanyapaa-mkubwa-kuhusu\/"},"modified":"2005-02-28T13:40:01","modified_gmt":"2005-02-28T13:40:01","slug":"afya-mauritania-maambukizi-madogo-ya-hiv-unyanyapaa-mkubwa-kuhusu","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2005\/02\/28\/afya-mauritania-maambukizi-madogo-ya-hiv-unyanyapaa-mkubwa-kuhusu\/","title":{"rendered":"AFYA&ndash;MAURITANIA: Maambukizi Madogo ya HIV, Unyanyapaa Mkubwa Kuhusu"},"content":{"rendered":"<p>NOUAKCHOTT, Feb 26 (IPS) &ndash; Katika mji mdogo wa Elmina nje kidogo ya mji mkuu wa Mau&#341;itania, Nouakchott, waelimishaji kuhusu Ukimwi hawa&#341;uhusu uki&#341;itimba wa kidini wala kiutamaduni kujipenyeza.<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Kipande cha mti kilichofungwa kondomu kinatumika kuwaelimisha watu kuhusu hata&#341;i za kufanya ngono zembe &ndash; labda eneo ambalo halijata&#341;ajiwa kabisa katika nchi ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu, na ambapo mazungumzo ya wazi kuhusu kujamiiana yamekuwa ni mwiko. <\/p>\n<p>&#8220;Tulipokuwa tunafanya kazi hii ya kuhaba&#341;isha tunabeba picha ya kiungo cha mwanaume, na baada ya kuonyesha kwa njia ya mfano tunasambaza kondomu ambazo tunazipata,&#8221; anasema Aichetou Gueye, mwenyekiti wa Muungano wa Vyama Vya Ushi&#341;ika katika Maendeleo ya Uchumi, shi&#341;ika linalohamasisha watu kuhusu gonjwa hilo. <\/p>\n<p>Waelimisha &#341;ika wanatumiwa kuhakikisha kwamba wahusika wanajisikia vizu&#341;i na walimu wao, ambao bila ya wasiwasi wanahakikisha kwamba taa&#341;ifa zinasambzwa vizu&#341;i zaidi. <\/p>\n<p>&#8220;Kama tunakuta nyumba yenye mama mzee, tunamchukua mwanamke wa um&#341;i mkubwa kufanya naye mazungumzo. Kama anakuwa na wasichana wadogo tunatumia msichana kuendesha mafunzo,&#8221; Gueye aliiambia IPS. Kondomu zinazotolewa kwa wale wanaohudhu&#341;ia mada&#341;asa zinatolewa na mashi&#341;ika yasiyokuwa ya kise&#341;ikali (NGOs). <\/p>\n<p>Lakini, siyo wanawake tu ambao wanaelezewa kuhusu uume wa bandia. <\/p>\n<p>&#8220;Tunawalenga pia wanaume, kwasababu Ukimwi unaathi&#341;i wote wanawake kwa wanaume. Tunawafahamisha kwamba ni vema wakatumia kondomu ili kujilinda kutokana na kwamba tunatambua inafanya kazi vizu&#341;i,&#8221; anabainisha Gueye. Kwa kuongeza, waelimishaji wanatoa taa&#341;ifa jinsi ya kuwalea watu wanaougua magonjwa yanayotokana na Ukimwi. <\/p>\n<p>Maambukizi ya Vi&#341;usi Vya Ukiwmiw (HIV) nchini Mau&#341;itania ni ya chini &ndash; chini ya asilimia moja, hii ni kulingana na takwimu za se&#341;ikali. <\/p>\n<p>Hata hivyo, wanaha&#341;akati kama Gueye wanaamini kwamba jitihada za pamoja kuhamasisha watu kuhusu Ukimwi bado ni muhimu &ndash; kutokana na unyanyapaa kuhusu gonjwa hili katika nchi hii ya kaskazini&ndash;magha&#341;ibi mwa Af&#341;ika. Hii inaweza kuonekana kutokana na takwimu ndogo ya watu ambao wanajitokeza kutumia huduma za bu&#341;e katika vituo vya kupima HIV na kutoa ushau&#341;i nasaha. <\/p>\n<p>&#8220;Watu wanaogopa vituo hivi&#8230;Bado hawapo wazi kuhusu gonjwa hili kutokana na kuhofia kukimbiwa na jamii kama watakutwa wameambukizwa,&#8221; anasema Gueye, akiongeza kwamba suala hili limewalazimu wanawake kuzungumzia zaidi hata&#341;i ya Ukimwi. <\/p>\n<p>&#8220;Wanawake wamekuwa wakiongoza kwasababu tunatambua kwamba kila mahali, ni wao wanaoathi&#341;ika zaidi na ugonjwa,&#8221; anasema. Wanawake ni asilimia 51 ya jumla ya watu wote milioni 2.5 nchini Mau&#341;itania. <\/p>\n<p>Se&#341;ikali pia inakubali kuhusu unyanyapaa unaozunguka HIV, kwa kusema imehusisha pia viongozi wa dini katika vita vya kuwafanya watu kuzungumza wazi kuhusu gonjwa hilo. <\/p>\n<p>&#8220;Tumewasiliana na Maimamu (viongozi wa kidini) kusaidia katika kuwahamasisha watu katika masuala yote ya gonjwa hilo, ikiwa ni pamoja na atha&#341;i za unyanyapaa,&#8221; Koita Bama&#341;ian, mku&#341;ugenzi mkuu wa kitengo cha haki za binadamu aliiambia IPS. <\/p>\n<p>&#8220;Pia tumeunda kamati ambayo itakuwa na makao yake katika wiza&#341;a ya afya kushughulikia mapambanao dhidi ya Ukimwi. Timu yetu inafanya jambo hili kwa kushau&#341;iana na mashi&#341;ika yasiyokuwa ya kise&#341;ikali ya ndani na ya kimataifa.&#8221; <\/p>\n<p>Kwa wale wanaojikuta wameambukizwa HIV, kuna matumaini ya kupata madawa ya kuongeza muda wa kuishi (ARV). Se&#341;ikali inasema kwamba, kutokana na msaada wa NGOs, vituo vya afya ya jamii nchini kote vimesambaziwa madawa hayo ya ku&#341;efusha maisha. <\/p>\n<p>&#8220;Tunataka wagonjwa kutumia jambo hili, sambamba na mpango wa &#8216;3 kwa 5&#8217; ,&#8221; anasema Bama&#341;ian. Mpango huu uliozinduliwa mwaka 2003 na Shi&#341;ika la Afya Ulimwenguni, unataka kusambazia wagonjwa wa Ukimwi milioni tatu katika dunia inayoendelea madawa ya ARV bu&#341;e ifikapo mwaka 2005. <\/p>\n<p>Kiwango cha vitendo vya jadi vinavyosababisha kuenea zaidi kwa HIV pia vinapewa kipaumbele nchini Mau&#341;itania &ndash; hasa vitendo vya ukeketaji wa wanawake. <\/p>\n<p>Katika vitendo hivi, vifaa duni na visivyochemshwa ma&#341;a nyingine hutumiwa kutekeleza zoezi hilo kwa wasichana na wanawake mbalimbali &ndash; kitu kinachoweza kusababisha vi&#341;usi vya Ukimwi kuenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. <\/p>\n<p>Kulingana na Aissata Kane, ambaye aliwahi kuwa mwanamke wa kwanza kushika uwazi&#341;i nchini Mau&#341;itania na sasa hivi mwenyekiti wa chama cha wanawake katika nchi zinazoongea lugha ya Kifa&#341;ansa, nchi hiyo ina vitendo vingi zaidi vya ukeketaji ba&#341;ani Af&#341;ika. <\/p>\n<p>Katika kabila la Soninke, kwa mfano, hadi asilimia 98 ya wasichana na wanawake wana&#341;ipotiwa kulazimishwa kufanyiwa toha&#341;a &ndash; ambayo pia inajulikana kama kutahi&#341;i wanawake. Miongoni mwa kabila la Fulanis, kiwango kinabakia asilimia 72, ambapo ka&#341;ibu asilimia 30 ya wasichana na wanawake katika kabila la Wolof wanafanyiwa toha&#341;a. <\/p>\n<p>&#8220;Hatujawahi kuwa na she&#341;ia dhidi ya vitendo hivi, lakini sasa tunataka se&#341;ikali kuvitokomeza kabisa,&#8221; anasema Kane. &#8220;Hii inaweza kufanyika kwa kupitia se&#341;a kali na she&#341;ia zinazowahusu wote wanaojihusisha katika kufanya vitendo hivyo.&#8221; <\/p>\n<p>Wale wote ambao wanahusika katika kufanya vitendo vya toha&#341;a wanategemea kazi hiyo kuendeshea maisha yao. Matokeo yao, kuna jitihada za kutafuta shughuli mbadala za kuweza kuwaingizia kipato watu hao, kama vile utengezaji wa nguo na udadizi. <\/p>\n<p>Kwa kuongeza, wanaha&#341;akati wanaja&#341;ibu kuwaelimisha wazazi kuhusu ukweli kwamba kupinga vitendo vya jadi vya toha&#341;a kwa wanawake kunaweza kumgha&#341;imu binti maisha. <\/p>\n<p>Mila na destu&#341;i nyingine zinazohusu wanawake pia zinahitaji kutizamwa, anasema Ishmael Noko, katibu mkuu wa Shi&#341;ikisho la Makanisa ya Kiluthe&#341;i Ulimwenguni &ndash; kikundi kinachowakilisha ka&#341;ibu Wak&#341;isto milioni 66 ulimwenguni kote. <\/p>\n<p>Wakati wa matukio ya wiki hii ya kuadhimisha miaka kumi na tatu ya shughuli za shi&#341;ikisho hilo nchini Mau&#341;itania, Noko alionya dhidi ya tabia ya kuwakemea wanawake wanaoja&#341;ibu kutoa maoni yao wakati wa kufanya tendo la ndoa. <\/p>\n<p>Wanawake wanaohofia waume zao wanaweza kuwa na HIV wanajikuta wakilazimishwa kufanya ngono bila ya kutumia kondomu. Ma&#341;a nyingi wanaume wanadai kwama matumizi ya ka&#341;atasi za nailoni kunapunguza utamu wakati wa kufanya tendo la ndoa, au wanatumia madai ya wenzi wao kuwaona siyo waaminifu hivyo kuwataka watumie kondomu. <\/p>\n<p>&#8220;Kuwa&#341;uhusu wanawake kuwa na sauti katika masuala ya ngono kutazaa mazingi&#341;a tofauti ambapo ugonjwa uliolazimishwa kwa mtu hauwezi kujitokeza,&#8221; Noko aliiambia IPS huko Nouakchott. &#8220;Kama hatutafanya jambo hili, tutakuwa tunajidhoofisha wenyewe na tunaweza kusahau kuhusu kushinda vita dhidi ya gonjwa la Ukimwi.&#8221; <\/p>\n<p>Maneo haya yaliungwa mkono na Maye mint Haidy, mwenyekiti wa Chama cha Kuwasaidia wanawake na Kuwalinda Watoto cha Mau&#341;itania. <\/p>\n<p>&#8220;Ni wanaume ambao wanatoa maamuzi linapokuja suala la kujadili ngono. Kama mwanamke hawezi kuongea kuhusu ngono, atamwambia mume wake nini kuhusu matumizi ya kondomu &#8221; aliuliza.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NOUAKCHOTT, Feb 26 (IPS) &ndash; Katika mji mdogo wa Elmina nje kidogo ya mji mkuu wa Mau&#341;itania, Nouakchott, waelimishaji kuhusu Ukimwi hawa&#341;uhusu uki&#341;itimba wa kidini wala kiutamaduni kujipenyeza. Kipande cha mti kilichofungwa kondomu kinatumika kuwaelimisha watu kuhusu hata&#341;i za kufanya ngono zembe &ndash; labda eneo ambalo halijata&#341;ajiwa kabisa katika nchi ambayo wakazi wake wengi ni&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":73,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-881","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/881","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/73"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=881"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/881\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=881"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=881"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=881"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}