{"id":3987,"date":"2013-05-03T13:40:01","date_gmt":"2013-05-03T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/05\/03\/timbuktu-yaejesha-hazina-zake\/"},"modified":"2013-05-03T13:40:01","modified_gmt":"2013-05-03T13:40:01","slug":"timbuktu-yaejesha-hazina-zake","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/05\/03\/timbuktu-yaejesha-hazina-zake\/","title":{"rendered":"Timbuktu Ya&#341;ejesha Hazina Zake"},"content":{"rendered":"<p>PARIS,, May 2 (IPS) &ndash; Pamoja na hali tata na vita vinavyoendelea, Mali itafanya kazi ya kujenga na kulinda u&#341;ithi wake wa kitamaduni, anasema wazi&#341;i wa utamaduni wa taifa hilo la Af&#341;ika Magha&#341;ibi B&#341;uno Ma&iuml;ga. Ma&iuml;ga alikuwa mjini Pa&#341;is akihudhu&#341;ia &#8220;siku ya mshikamano na Mali&#8221; iliyoandaliwa na Shi&#341;ika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) katika makao yake makuu hapa. Tukio hilo lilikusanya pamoja wataalam wa masuala ya utamaduni, wakuu wa se&#341;ikali, wanasanaa na wasomi kutathmini uha&#341;ibifu uliofanyika katika maeneo ya u&#341;ithi wa kitamaduni ya Mali na maandiko ya kizamani, na kuandaa mpango wa kuchukua hatua.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Wapiganaji wa jihadi&#8230;kwa kuchoma moto maandiko ya zamani, kuzuia masuala ya jadi katika mikoa wanayoikalia, kuzuia watu wasisikilize muziki, kupandikiza hofu &#8230;walitaka kutuvunja moyo, kuvunja hisia zetu za kitamaduni,&#8221; Ma&iuml;ga alisema. &#8220;Lengo lao lilikuwa kuha&#341;ibu zamani yetu, utamaduni wetu, utambulisho wetu, na kwa ujumla wake, utu wetu.&#8221;<\/p>\n<p>Ma&iuml;ga aliiambia IPS kuwa alikuwa na matumaini kuwa siku hiyo itaanzisha mwanzo wa kujenga upya u&#341;ithi wa Mali. &#8220;Natumaini kutakuwa na hatua thabiti, na hiyo ndiyo sabababu nimekuja hapa, pamoja na matatizo yote yanayoikabili nchi yetu.&#8221;<\/p>\n<p>Makabu&#341;i ya zamani kumi na sita na misikiti mikubwa mitatu katika mji wa kihisto&#341;ia wa Timbuktu yaliwekwa katika u&#341;ithi wa dunia wa UNESCO mwaka 1988. Kabu&#341;i la Askia katika mji wa Gao, ambalo lilijengwa mwaka 1495, liliongezwa katika o&#341;odha hiyo mwaka 2004.<\/p>\n<p>Mwezi Julai mwaka jana kabu&#341;i hili na msikiti wa Sidi Yahi liliingizwa katika o&#341;odha ya vitu vilivyopo hata&#341;ini kufuatia kuvunjwa kwa makabu&#341;i 11, na milango ya Sidi Yahi.<\/p>\n<p>Uvunjaji huo uliohusishwa na waasi wa Kiislam &ndash; ulifanyika wakati wa mwaka wa vita ambayo ilianza kaskazini mwa Mali Janua&#341;i 2012. Wakati vikosi vya Kifa&#341;ansa na Mali vilipochukua mji wa Timbuktu mwishoni mwa Janua&#341;i mwaka huu, waasi walio&#341;udi nyuma walichoma moto Taasisi ya Ahmed Baba, na kuvunja baadhi ya maandiko ya thamani ya zamani ambayo yalikuwa yakihifadhiwa hapo.<\/p>\n<p>Ma&iuml;ga aliwaambia waandishi wa haba&#341;i kuwa maandiko ya zamani yapatayo 2,000 hadi 3,000 inawezekana yalipotea lakini nya&#341;aka nyingine zinazokadi&#341;iwa kuwa 300,000 zimehifadhiwa katika mahali salama. Alikataa kutoa mahali zilipohifadhiwa nya&#341;aka hizo kutokana na sababu za kiusalama. Maandiko hayo mengi yameandikwa katika ka&#341;ne za 13 hadi 16 na yaliandikwa na wanazuoni maa&#341;ufu kutoka jiji hilo na maeneo mengineyo.<\/p>\n<p>Maandiko hayo yalikuwa katika mchakato wa kuwekwa katika kompyuta, lakini waasi walivunja kompyuta na vifaa vingine vilivyofungwa kwa ajili ya kazi hiyo, Ma&iuml;ga alisema. &#8220;Walivunja kila kitu,&#8221; aliiambia IPS, akiongeza kuwa mchakato wa kuingiza kwenye kompyuta bado ni kipaumbele kwa wiza&#341;a ya utamaduni, ma&#341;a tu amani itakapo&#341;ejea.<\/p>\n<p>&#8220;Mali ina utamaduni mkubwa na histo&#341;ia ambayo inahifadhi mshikamano wa kijamii,&#8221; Ma&iuml;ga alisema. &#8220;Kwa mamia ya miaka, jamii mbalimbali zimeishi pamoja zikiwa na tamaduni tofauti. Ni kutokana na tamaduni hizi tofauti, kumekuwepo na moyo huu wa uvumilivu, na ubunifu huu &#8230;ambao waasi wa Kiislam wameja&#341;ibu kuuvunja. Lazima tupingane na jambo hili.&#8221;<\/p>\n<p>Kufuatia siku ya mazungumzo, Mali na washi&#341;ika wake walipitisha &#341;asimu ya mpango wa utekelezaji kwa ajili ya &#8220;ujenzi upya wa u&#341;ithi wa utamaduni na kulinda maandiko ya zamani.&#8221; Laza&#341;e Eloundou, mkuu wa Kituo cha U&#341;ithi wa Dunia ba&#341;ani Af&#341;ika katika UNESCO, alisema kuwa gha&#341;ama za kuingiza kwenye kompyuta maandiko na kujenga upya makabu&#341;i zilikadi&#341;iwa kufikia kati ya dola milioni 10 na dola milioni 11.<\/p>\n<p>Alisema kuwa shi&#341;ika hilo limefungua akaunti maalum ya benki kupokea fedha kwa ajili ya kazi iliyopo mbeleni, na siku ya mshikamano ilikuwa na maana ya kutangaza juu ya haja ya kuchangia mpango huo kutoka kwa wahisani binafsi na wa umma.<\/p>\n<p>Au&#341;&eacute;lie Filipetti, wazi&#341;i wa utamaduni na mawasiliano wa Ufa&#341;ansa, ambaye alihudhu&#341;ia she&#341;ehe za ufunguzi, alisema kuwa taasisi za Ufa&#341;ansa zitashi&#341;iki katika kutoa mafunzo kwa wataalam wa utamaduni wa Mali katika maeneo ya uhifadhi na u&#341;ejeshaji wa u&#341;ithi wake.<\/p>\n<p>&#8220;Mali ni sehemu muhimu ya vyanzo vya sanaa, utamaduni na masuala ya ki&#341;oho, na jukumu la Ufa&#341;ansa, la UNESCO na jumuiya nzima ya kimataifa ni kusaidia watu wa Mali kutambua utu wao na faha&#341;i ya utamaduni wao,&#8221; Filipetti aliwaambia waandishi wa haba&#341;i.<\/p>\n<p>&#8220;Wakati Ufa&#341;ansa ilipoingilia kati katika mgogo&#341;o huo, ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda heshima ya taifa la Mali na zaidi ya hapo kulinda watu wa Mali,&#8221; Filipetti aliongeza. &#8220;Na watu wa Mali wanahitaji u&#341;ithi na utamaduni wao.&#8221;<\/p>\n<p>Taasisi kama ile ya mjini Pa&#341;is ya Quai B&#341;anly Museum, ambayo inalenga katika sanaa na ustaa&#341;abu wa jadi, na Maktaba ya Taifa ya Ufa&#341;ansa watatoa maa&#341;ifa yao ku&#341;ejesha na kujenga upya maeneo hayo, Filipetti alisema.<\/p>\n<p>&#8220;Hakuna kanuni ya ki&#341;oho au ya kiha&#341;akati ambayo inaweza kuwa na sababu ya kunyima watu histo&#341;ia yao,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Wakati mapigano yakiendelea, huku kukiwepo na mashambulizi ya kila upande, wataalam wanahofia kuwa sanaa za kitamaduni za Mali zitakuwa sehemu ya biasha&#341;a ha&#341;amu ya kimataifa ambayo ina thamani ya dola bilioni 6 hadi 8 kwa mwaka.<\/p>\n<p>Wakuu wa UNESCO walisema baadhi ya vitu taya&#341;i vinaaminika kuwa katika soko, lakini shi&#341;ika hilo lina matumaini kuwa se&#341;ikali za nchi ji&#341;ani zitachukua hatua kuzuia vifaa hivyo kuingia nchini mwao.<\/p>\n<p>Mku&#341;ugenzi mkuu wa UNESCO I&#341;ina Bokova alisema kuwa shi&#341;ika lake lingefanya kazi na washi&#341;ika wengine na shi&#341;ika la polisi la kimataifa la Inte&#341;pol kuzuia uuzaji wa vifaa hivyo. Pia alisisitiza umuhimu wa utamaduni kwa mataifa.<\/p>\n<p>&#8220;Tunataka kupeleka ujumbe wenye nguvu kuhusu umuhimu wa utamaduni, umuhimu wa u&#341;ithi,&#8221; aliwaambia waandishi wa haba&#341;i. &#8220;Ujumbe ambao unapinga uha&#341;ibifu wa u&#341;ithi kwasababu unaangamiza utambulisho wa watu.&#8221;<\/p>\n<p>Bokova, ambaye alitembelea Mali mwanzoni mwa mwezi wa Feb&#341;ua&#341;i akiwa na &#341;ais wa Ufa&#341;ansa F&#341;an&ccedil;ois Hollande, alisema aliona kwa macho yake kuchomwa moto kwa maandiko ya kale.<\/p>\n<p>&#8220;Kwetu sisi, Timbuktu, Gao, u&#341;ithi wa Mali ni vitu vinavyokwenda mbali zaidi ya kuo&#341;odheshwa katika U&#341;ithi wa Dunia kwasababu vinaonyesha maendeleo ya ustawi wa Uislam, na mjadala miongoni mwa tamaduni. Maandiko ya kale yana &#341;ikodi za sayansi ya Uislam, madawa, utabi&#341;i wa nyota, masuala ya ki&#341;oho, masuala ya falsafa,&#8221; Bokova alisema. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>PARIS,, May 2 (IPS) &ndash; Pamoja na hali tata na vita vinavyoendelea, Mali itafanya kazi ya kujenga na kulinda u&#341;ithi wake wa kitamaduni, anasema wazi&#341;i wa utamaduni wa taifa hilo la Af&#341;ika Magha&#341;ibi B&#341;uno Ma&iuml;ga. Ma&iuml;ga alikuwa mjini Pa&#341;is akihudhu&#341;ia &#8220;siku ya mshikamano na Mali&#8221; iliyoandaliwa na Shi&#341;ika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":861,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3987","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3987","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/861"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3987"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3987\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3987"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3987"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3987"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}