{"id":3981,"date":"2013-03-04T13:40:01","date_gmt":"2013-03-04T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/03\/04\/tanzania-watoaji-huduma-za-uzazi-wa-mpango-wa-kujitolea-wawafikia-wananchi-wa-vijijini\/"},"modified":"2013-03-04T13:40:01","modified_gmt":"2013-03-04T13:40:01","slug":"tanzania-watoaji-huduma-za-uzazi-wa-mpango-wa-kujitolea-wawafikia-wananchi-wa-vijijini","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/03\/04\/tanzania-watoaji-huduma-za-uzazi-wa-mpango-wa-kujitolea-wawafikia-wananchi-wa-vijijini\/","title":{"rendered":"TANZANIA &ndash; Watoaji Huduma za Uzazi wa Mpango wa Kujitolea Wawafikia Wananchi wa Vijijini"},"content":{"rendered":"<p>PANGANI, FEB 4 (IPS) &ndash; Hashim Ali Said ni mtoaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii (CBD) ambaye ana dhami&#341;a ya kweli ya kusaidia jamii yake katika kijiji cha Mkalamo na vijiji vingine vya ji&#341;ani. &#8220;Kuna wakati wanajamii wanakuja kunigongea mlango hata saa sita za usiku kutaka niwapatie kondomu kwa ajili ya kupanga uzazi na kujilinda na magonjwa ya kujamiiana,&#8221; anasema Said mwenye um&#341;i wa mika 42.<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Said, baba wa mtoto mmoja wa kike anasema alianza kueneza elimu ya idadi ya watu, afya na mazingi&#341;a (PHE) katika jamii yake baada ya kupata elimu ya jinsi ya kuunganisha dhana ya uzazi wa mpango na hifadhi ya mazingi&#341;a mwaka 2009 kutoka m&#341;adi wa BALANCED ambao unatekeleza mi&#341;adi inayojikita katika suala zima la uzazi wa mpango ili kuchangia shughuli za hifadhi ya mazingi&#341;a zinazoendeshwa na Kituo cha Rasilimali za Pwani (CRC) na M&#341;adi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingi&#341;a ya Baha&#341;i na Pwani (TCMP&ndash;Pwani) ambao unafadhiliwa na USAID. <\/p>\n<p>Anasema kwa sasa emeelimisha familia nyingi katika jamii yake umuhimu wa uzazi wa mpango, kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOs) na kutumia majiko banifu.<\/p>\n<p>&#8220;Nina mifano mingi ya wanafamilia katika jamii yangu ambao hawakuwa wakijali suala la kuachanisha um&#341;i kati ya mtoto na mtoto, lakini kwa sasa wanajali kuzaa watoto wao kwa nafasi nzu&#341;i,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Said na CBDs wengine katika vijiji kadhaa vinavyozunguka Mbuga ya Wanyama ya Saadani katika mwambao wa Baha&#341;i ya Hindi wilayani Pangani wamepata heshima kubwa kutoka kwa jamii zao kutokana na kazi yao. Wamepewa majina kama ya watoaji wa huduma za afya, wakombozi, wafanyakazi wa afya na hata kuitwa madakta&#341;i.<\/p>\n<p>&#8220;Watu wanatuheshimu kwasababu wakati wote tupo kwa ajili ya kuwahudumia. Wanatambua kuwa hata kama wakija kwetu saa sita za usiku tutawapatia huduma,&#8221; Said alisema.<\/p>\n<p>Watoaji wa huduma za uzazi wa mpango katika vijiji vingine walizungumzia umuhimu wa kuwa na CBDs katika jamii zao. Wanasema watu wanapendelea huduma zao kutokana na kwamba wako ka&#341;ibu nao, huduma hizo zinapatikana wakati wowote wanapozihitaji na zimeweza kupunguza umbali na haja ya kusafi&#341;i ma&#341;a kwa ma&#341;a kwenda kwenye vituo vya afya vilivyo ka&#341;ibu kwa ajili ya kupata huduma hizo na pia huduma za CBDs zinatolewa bu&#341;e. <\/p>\n<p>Mmoja wa wamiliki wa maduka yanayouza kondomu katika kijiji cha Mkalamo anasema idadi ya watu wanaokwenda kununua kondomu dukani kwake imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na huduma za CBDs kuwa za bu&#341;e.<\/p>\n<p>Hata kama wanaweza wasijue mchango mkubwa wanaoutoa katika kusaidia kuokoa maisha ya akina mama na watoto wa kike na wa kiume kitaifa na hata kimataifa, jitihada za CBDs zinaonekana kutambuliwa na &#341;ipoti ya Shi&#341;ika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) inayojulikana kama &#8220;State of the Wo&#341;ld Population Repo&#341;t 2012 &#8220;By Choice, Not by Chance: Family Planning, Human Rights and Development&#8221; .<\/p>\n<p>&#8220;Kufanya huduma za uzazi wa mpango zipatikane kwa kila mtu katika nchi zinazoendelea kunapunguza gha&#341;ama za huduma za afya ya uzazi na watoto wachanga,&#8221; inasema &#341;ipoti hiyo. &#8220;Uzazi wa mpango una faida kubwa kwa wanawake, familia na jamii kwa ujumla. Kwa kumwezesha mtu kuchagua idadi ya watoto anaotaka na kutoa nafasi ya kutosha kati ya mtoto na mtoto, uzazi wa mpango umewawezesha wanawake na watoto wao kuishi maisha ma&#341;efu na yenye afya.&#8221; <\/p>\n<p>Said anasema elimu ya idadi ya watu, afya na mazingi&#341;a imemweza kumshawishi yeye mwenyewe kununua jiko banifu kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kuni katika familia yake ambayo ni chanzo cha kuangamiza misitu na kuha&#341;ibu mazingi&#341;a nchini. &#8220;Katika siku za zamani nilikuwa natumia jiko la mafiga matatu ambalo lilitumia kuni nyingi na kutoa moshi mwingi. Moshi ulinifanya kununua sufu&#341;ia kila siku kwani zilichakaa mapema kutokana na moshi mwingi,&#8221; anasema. &#8220;Moshi pia ulihata&#341;isha afya ya familia kwani uliongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya kupumua&#8221;. Jiko la mafiga matatu alilokuwa akitumia katika familia yake lilitumia tak&#341;ibani vipande 8 vya kuni kwa kupikia kwa wakati mmoja wakati jiko banifu analotumia sasa hutumia vipande 2 tu vya kuni.<\/p>\n<p>&#8220;Mke wangu alikuwa akilalamika kila siku kutokana na kwenda po&#341;ini kukusanya kuni ma&#341;a kwa ma&#341;a, lakini sasa amepunguziwa mzigo wa kwenda po&#341;ini ma&#341;a kwa ma&#341;a,&#8221; anasema. &#8220;Mke wangu anasema jiko hilo pia limempunguzia muda alioutumia kuchochea kuni jikoni.&#8221;<\/p>\n<p>Said anasema amepata ombi maalum kutoka kwa mke wake kutengeneza jiko jingine kwa ajili ya kutumiwa na wapangaji katika nyumba yao.<\/p>\n<p>Dhami&#341;a ya kweli ya kusaidia jamii yake imeivutia zahanati ya Mkalamo kumchagua kuwa de&#341;eva wa piki piki ya kubebea wagonjwa ya magu&#341;udumu matatu. <\/p>\n<p>&#8220;Moyo wangu wa kujitolea umefanya kituo cha afya kunichagua kujiunga kwenye kampeni ya kudhibiti ugonjwa wa mala&#341;ia na kupata zawadi ya baiskeli kutoka Wiza&#341;a ya Afya. Ma&#341;a tu baada ya kampeni, nilichaguliwa kuwa de&#341;eva wa pikipiki ya kubebea wagonjwa ya magu&#341;udumu matatu,&#8221; anasema. Kuwa de&#341;eva wa pikipiki ya kubebea wagonjwa ni kazi nyingine ya kujitolea anayoifanya Said kusaidia jamii yake. &#8220;Nimekuwa nikiendesha pikipiki hii tangu Septemba 2012 bila kupata motisha wowote. Naamka wakati wowote ninapopata taa&#341;ifa ya kuwepo kwa dha&#341;ula ya mgonjwa kijijini na kijiji cha ji&#341;ani cha Mbulizaga ili kumuwahisha katika zahanati yetu. Namshuku&#341;u Mungu kwa kunifanya kuwa na moyo wa kujitolea,&#8221; anasema. <\/p>\n<p>Mbali na majukumu ya kueneza huduma na elimu ya idadi ya watu, afya na mazingi&#341;a, Said ni mfano tosha wa wanaume wanaojali uzazi wa mpango katika jamii yake. &#8220;Nina mtoto mmoja tu ambaye ana miaka minne. Kama Mungu akipenda nikapata mtoto mwingine sasa, nafasi ya kutoka mtoto mmoja hadi mwingine itakuwa kubwa na iliyopangiliwa vizu&#341;i. Na, katika mipango yangu siwezi kuwa na watoto zaidi ya 4,&#8221; anasema. <\/p>\n<p>Said pia ni mfano wa kuigwa kwa wanaume wengi katika maeneo ya vijijini na mijini nchini Tanzania ambao bado wanadhani jukumu la kupanga uzazi ni la wanawake pekee. Wanawake na wanaume wana jukumu la kupanga uzazi, kulinda afya za familia na kutunza mazingi&#341;a na maliasili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>PANGANI, FEB 4 (IPS) &ndash; Hashim Ali Said ni mtoaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii (CBD) ambaye ana dhami&#341;a ya kweli ya kusaidia jamii yake katika kijiji cha Mkalamo na vijiji vingine vya ji&#341;ani. &#8220;Kuna wakati wanajamii wanakuja kunigongea mlango hata saa sita za usiku kutaka niwapatie kondomu kwa ajili ya kupanga&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":536,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3981","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3981","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/536"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3981"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3981\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3981"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3981"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3981"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}