{"id":3980,"date":"2013-03-04T13:40:01","date_gmt":"2013-03-04T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/03\/04\/wakazi-wa-makazi-duni-wasema-hapana-kwa-fedha-za-damu-slum-dwelles-say-no-to-blood-money\/"},"modified":"2013-03-04T13:40:01","modified_gmt":"2013-03-04T13:40:01","slug":"wakazi-wa-makazi-duni-wasema-hapana-kwa-fedha-za-damu-slum-dwelles-say-no-to-blood-money","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2013\/03\/04\/wakazi-wa-makazi-duni-wasema-hapana-kwa-fedha-za-damu-slum-dwelles-say-no-to-blood-money\/","title":{"rendered":"Wakazi wa Makazi Duni Wasema &#8220;Hapana &#8221; kwa Fedha za Damu &ndash; Slum Dwelle&#341;s Say &#8220;No&#8221; to Blood Money"},"content":{"rendered":"<p>NAIROBI, Jan 10 (IPS) &ndash; Huku ikiwa imebakia miezi miwili kabla Wakenya hawajapiga ku&#341;a kwa kile kinachoonekana kama uchaguzi wenye ushindani mkubwa na uliogawanyika sana katika histo&#341;ia ya nchi, wengi wanahofia kuwa taifa hili la Af&#341;ika Masha&#341;iki lenye wakazi wanaozidi milioni 40 hawajaona kumalizika kwa ghasia za uchaguzi. Hii inajitokeza pamoja na kwamba wanasiasa wawili maa&#341;ufu &ndash; Uhu&#341;u Kenyatta na William Ruto &ndash; bado wanasubi&#341;i hatma yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) wakikabiliwa na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007&ndash;2008.<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Vu&#341;ugu za baada ya uchaguzi, ambazo zilisadikika kusababishwa na kuhamasishwa na vyama hivi viwili vya kisiasa, ziliacha maelfu ya watu kufa&#341;iki dunia, zaidi ya 3,000 kuje&#341;uhiwa na mamia kwa maelfu kuyahama makazi yao.<\/p>\n<p>&#8220;Hata hivyo, bado wanasiasa wasiokuwa wastaa&#341;abu wanaendelea kueneza ushawishi wao katika makazi duni nchini kote Kenya. Hapa (katika makazi duni), kwa kiasi cha dola moja au mbili, na hata chini ya hapo, watu wanaweza kutishiwa, kuje&#341;uhiwa au hata kuuawa kwa wale wanaoonekana kuwa wapinzani wa kisiasa,&#8221; Pete&#341; Muga, mchambuzi wa kisiasa aliyepo mjini Nai&#341;obi, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Uhaba wa aji&#341;a na umaskini umeacha mamilioni ya wapiga ku&#341;a katika makazi mbalimbali duni kushawishiwa na wanasiasa ambao hawana hofu kuhusu kuchukua hatua kali kunyamazisha wapinzani.<\/p>\n<p>&#8220;Lakini kutokana na wanasiasa hao kukosa nguvu za kukabiliana na wapinzani katika boksi la ku&#341;a, wanawapatia pesa vijana katika makazi duni kufanya mambo yao mabaya,&#8221; Muga aliongeza.<\/p>\n<p>Kampeni ya kusema &#8220;hapana&#8221;<\/p>\n<p>Katika jitihada za kuzuia madha&#341;a mabaya zaidi yanayohusiana na &#341;ushwa ya uchaguzi na ghasia zilizochochewa na uchaguzi wa mwaka 2007&ndash;2008, wakazi wa makazi duni ya Matha&#341;e &ndash; makazi makubwa zaidi mjini Nai&#341;obi ambayo yana wakazi 500,000 &ndash; wamenzisha ha&#341;akati zenye jina la &#8216;Tia Rwabe Zi&#8217; (Sema Hapana kwa shilingi za Kenya 200).<\/p>\n<p>&#8220;Wanasiasa wanatupatia ksh 200 (kama vile dola mbili) kupambana na wale ambao hawawaungi mkono,&#8221; Julia Njoki, mwanachama mwanzilishi wa Tia Rwabe Zi, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>&#8220;Ma&#341;a nyingi, wagombea wanaoisigishana wanatoka makabila tofauti. Uadui huu ma&#341;a nyingi unageuka kuwa ukabila. Wakati tukiongea, Matha&#341;e taya&#341;i imeshagawanyika, kuna baadhi ya makabila ambayo hayawezi kuishi au kugombea nafasi za kisiasa katika baadhi ya maeneo,&#8221; aliongeza.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa Njoki, ha&#341;akati hizi zilitokana na kifo na uha&#341;ibifu ulioshuhudiwa wakati wa mgogo&#341;o wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007&ndash;2008, ambao ulichochewa na wakazi wa makazi duni.<\/p>\n<p>&#8220;Katika ha&#341;akati hizi tunasema hapana kwa hongo za uchaguzi. Wengi wetu sisi ni vijana, ambao ni watoto wa kiume na watoto wa kike na wanawake. Pia tumewafikia wengine katika makazi mengine duni kama vile Kibe&#341;a,&#8221; alisema, akimaanisha makazi duni makubwa zaidi mjini Nai&#341;obi, moja ya makazi duni makubwa kabisa ba&#341;ani Af&#341;ika.<\/p>\n<p>Umaskini unaendesha vyama vya siasa. <\/p>\n<p>Lakini kampeni hiyo imechukua mwelekeo utakaokuwa na kazi kubwa na haitaweza kuwa na ushindi wa kiu&#341;ahisi.<\/p>\n<p>Hata kumbukumbu za umwagaji damu za mwaka 2007&ndash;2008 hazitazuia wananchi wa Kenya maskini kufanya kile ambacho wanaweza kufanya kupunguza mzigo wa mazingi&#341;a duni wanayoishi.<\/p>\n<p>Wakati wakazi wa makazi duni ya Kibe&#341;a walianzisha mfumo wa &#8216;vyoo vya ku&#341;usha&#8217;, Wakenya wengi wenye makazi yenye hadhi na vyoo bo&#341;a waliwacheka wenzao.<\/p>\n<p>Lakini kwa wakazi wa makazi duni wenyewe, kulazimishwa kujisaidia katika mifuko ya plastiki na kutupa uchafu hewani kutokana na kukosa vyoo na maeneo ya kutupia taka siyo jambo la kuchekelea. Wala jambo la kukojoa kwenye makontena ya plastiki halifai kuchekelea.<\/p>\n<p>Wakati wakazi mbalimbali wameweza kuchukua hatua kukabiliana na mustakabali wa wakazi wa makazi duni wasiokuwa na vyoo, siyo mambo mengi ambayo yamebadilika.<\/p>\n<p>Wakati wa usiku, vyoo vya jadi vinakuwa eneo ambalo halifai kufika kutokana na kukosekana kwa usalama. Matokeo yake, wakazi wengi wanaamka na kujisaidia kwenye mifuko ya plastiki katika umbali mdogo kutoka milangoni mwao, na kutokuonekana kwa maji&#341;ani zao tu kutokana na giza.<\/p>\n<p>&#8220;Bado watu wanatumia vyoo vya ku&#341;usha kwasababu kutumia vyoo vya umma siyo bu&#341;e. Fedha zinakwenda kwenye uka&#341;abati,&#8221; Ve&#341;onica Wamaitha, mkazi wa Kibe&#341;a, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Katika siku nzu&#341;i, watu wanaoishi katika makazi duni wanaingiza dola mbili hadi tatu, lakini ma&#341;a nyingi wanaweza kukaa wiki nzima bila kuingiza hata senti moja.<\/p>\n<p>&#8220;Lakini bado watu wanapaswa kula,&#8221; Rob Wangai, mkazi wa makazi duni ya Matha&#341;e, aliiambia IPS. &#8220;Hakuna kitu ambacho ni cha bu&#341;e. Hata tumeamua kutumia umeme ambao umeunganishwa kinyume cha she&#341;ia; matokeo yake, ni ma&#341;a chache sana tunamaliza wiki bila kuzuka kwa moto mahali fulani.&#8221;<\/p>\n<p>Kutokana na hali hii ya watu wanaoishi katika mazingi&#341;a machafu, wanasiasa wamepata majibu ya matatizo yao.<\/p>\n<p>&#8220;Wakazi wa Kenya wamegawanyika sana katika maeneo makuu mawili, wale wanaoishi katika msta&#341;i wa umaskini na tabaka la kati. Tabaka la kati kwa kiasi lina elimu na wanaelewa dhana ya kujitegemea &ndash; hali hiyo haipo kwa maskini,&#8221; Ken Ochiel, mchambuzi wa kisiasa mjini Nai&#341;obi, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Alisema wale wanaoishi katika umaskini bado wana imani kuwa viongozi wa kisiasa wanabeba ufunguo wa maisha mazu&#341;i ya baadaye.<\/p>\n<p>&#8220;Huu ni ugonjwa ambao unakula jamii yetu. Viongozi ambao wana pesa na wanaweza kutoa &#341;ushwa kwa wapiga ku&#341;a wanachaguliwa kiu&#341;ahisi. Lakini kwa uhakika, hawabo&#341;eshi hali ya maisha ya maskini ambao wanawapigia ku&#341;a,&#8221; alielezea Vesca Kangongo, ambaye anagombea ugavana katika Mkoa wa Bonde la Ufa.<\/p>\n<p>Maoni yake yanaungwa mkono na mwanamke pekee anayegombea u&#341;ais, Mheshimiwa Ma&#341;tha Ka&#341;ua, ambaye alisema, &#8220;Ni kwa nini kaka zangu ambao wanagombea uongozi wa juu nchini wana pesa nyingi, baadhi zimeibwa kutoka katika hazina za umma. Nawataka Wakenya kupigia ku&#341;a viongozi wanaoangalia masuala ambao wanaweza kubo&#341;esha hali ya maisha katika nchi hii.&#8221;<\/p>\n<p>Ka&#341;ua pia amedai kuwa wanasiasa wako nyuma ya mawimbi ya hivi ka&#341;ibuni ya ghasia na mauji katika makazi duni ya Matha&#341;e, ambayo yaliibua kumbukumbu za machafuko ya mwaka 2007&ndash;2008 ambapo Matha&#341;e, Kibe&#341;a na makazi mengi ya mjini yalibadilika kuwa maeneo ya mauaji na uha&#341;ibifu wakati makabila yalipoanza kupigana.<\/p>\n<p>&#8220;Katika kila uchaguzi mkuu, wanasiasa wanapeleka aska&#341;i wao wa miguu katika makazi duni, kutokana na kuwa tabaka la kati haliwezi kukubali dola mbili kutishia watu, na hata kuua,&#8221; kwa mujibu wa Muga, wakati maskini wanakuwa &#341;ahisi kuathi&#341;ika na &#341;ushwa.<\/p>\n<p>Ochiel anakubaliana. &#8220;Wanasiasa wanatambua kuwa tabaka la kati ni gumu kulishawishi kwa ahadi, ikilinganishwa na watu ambao unaweza kuwaendesha kwa mlo mmoja kwa siku. Makazi duni pia yanakaliwa na watu wanaofanana tabaka lao ambao ni &#341;ahisi kuwapata.&#8221;<\/p>\n<p>Hata hivyo, wanakampeni ya Tia Rwabe Zi wana nia ya kuleta mabadiliko mwaka huu.<\/p>\n<p>Kundi hilo linafanya mikutano ya ma&#341;a kwa ma&#341;a na kuzungumza kwa nguvu dhidi ya ghasia na kukaa bila kazi. &#8220;Tunahamasisha kila mmoja kupata aji&#341;a na hata kumtaa&#341;ifu mwingine kama kuna nafasi ya aji&#341;a. Lazima watu wawe na kazi za kufanya ili kuondokana na taabu,&#8221; Njoki alielezea.<\/p>\n<p>Wakati wakikubaliana kuwa kuta&#341;ajia watu kukataa hongo huku wakiwa katika umaskini mkubwa na njaa ni jambo ambalo ni gumu &ndash; na mabadiliko hayo hayatakuja ma&#341;a moja &ndash; alisisitiza kuwa wanachama wa kampeni hiyo wanashawishiwa kuwa jitihada zao ni hatua katika mwelekeo sahihi.<\/p><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>NAIROBI, Jan 10 (IPS) &ndash; Huku ikiwa imebakia miezi miwili kabla Wakenya hawajapiga ku&#341;a kwa kile kinachoonekana kama uchaguzi wenye ushindani mkubwa na uliogawanyika sana katika histo&#341;ia ya nchi, wengi wanahofia kuwa taifa hili la Af&#341;ika Masha&#341;iki lenye wakazi wanaozidi milioni 40 hawajaona kumalizika kwa ghasia za uchaguzi. Hii inajitokeza pamoja na kwamba wanasiasa wawili&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":720,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3980","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3980","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/720"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3980"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3980\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3980"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3980"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3980"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}