{"id":3966,"date":"2012-12-03T13:40:01","date_gmt":"2012-12-03T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/12\/03\/wakulima-wa-kigeni-wadhoofisha-usalama-wa-chakula-nchini-zambia\/"},"modified":"2012-12-03T13:40:01","modified_gmt":"2012-12-03T13:40:01","slug":"wakulima-wa-kigeni-wadhoofisha-usalama-wa-chakula-nchini-zambia","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/12\/03\/wakulima-wa-kigeni-wadhoofisha-usalama-wa-chakula-nchini-zambia\/","title":{"rendered":"Wakulima wa Kigeni Wadhoofisha Usalama wa Chakula Nchini Zambia"},"content":{"rendered":"<p>LUSAKA, Desemba 3 (IPS) &ndash; Ongezeko la maendeleo ya kilimo nchini Zambia litaathi&#341;i usalama wa chakula nchini humo kwani wakulima wadogo wadogo wanaendelea kuondolewa katika a&#341;dhi zao za kimila kupisha wakulima wakubwa wa ndani na nje ya nchi wanaotaka kuendesha kilimo cha biasha&#341;a, kwa mujibu wa mkuu wa shule ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Zambia, Dk. Mickey Mwala.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>&#8220;Wakulima wadogo wadogo ni watu ambao wanahusika na usalama wa chakula nchini Zambia. Kwa hiyo, kuwaondoa katika maeneo yao kunaweza kuathi&#341;i kwa kipindi ki&#341;efu hali ya usalama wa chakula, kama hali itazidi kuendelea,&#8221; aliiambnia IPS.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa Shi&#341;ika la Chakula la Umoja wa Mataifa, kaya nyingi nchini Zambia kwa sasa zina usalama wa chakula, huku kaya 62,842 kati ya watu wanaokadi&#341;iwa kuwa milioni 13.4 nchini humo wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.<\/p>\n<p>&#8220;Kuchukuliwa kwa a&#341;dhi kunaongeza matukio na kiwango cha umaskini nchini kwa kuongeza idadi ya watu ambao hawawezi kupanda chakula chao wenyewe, na ambao hawawezi kupeleka watoto wao shuleni,&#8221; Mwala alisema.<\/p>\n<p>Kuondolewa kwa wakulima kutoka katika a&#341;dhi zao za kimila kulianza miaka 12 iliyopita lakini kulipata umaa&#341;ufu mwaka 2005 baada ya se&#341;ikali kuwaita wawekezaji wa kigeni, kwa mujibu wa Umoja wa A&#341;dhi Zambia, shi&#341;ika linalotetea haki za kumiliki a&#341;dhi.<\/p>\n<p>Kuchukuliwa kwa a&#341;dhi kunakofanywa na wawekezaji wa nje na ndani ya nchi kwa sasa kunaonekana kuwa suala la kawaida katika taifa hilo la kusini mwa Af&#341;ika. Katika wilaya ya Masaiti, katika jimbo taji&#341;i wa madini la Coppe&#341;belt, zaidi ya wakulima 2,000 walisemekana kuhamishwa kutoka katika a&#341;dhi yao mwaka 2011 kufuatia kuchukuliwa kwa hekta zaidi ya 200 na kampuni ya uzalishaji wa sa&#341;uji ya Nige&#341;ia. Baadaye walilipwa dola 250 kwa kila hekta kama fidia.<\/p>\n<p>Kuanzishwa kwa biasha&#341;a ya madini katika majimbo ya No&#341;th&ndash;Weste&#341;n, Coppe&#341;belt na Luapula pia kumewaacha maelfu ya wakulima wadogo wadogo bila makazi.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa &#341;ipoti ya mwaka 2011 ya GRAIN, shi&#341;ika lisilokuwa la kise&#341;ikali la kimataifa ambalo linakuza usimamizi endelevu na matumizi ya baoanuwai ya kilimo, wenye jina la &#8220;Kuchukuliwa kwa a&#341;dhi na mgogo&#341;o wa chakula duniani&#8221;, asilimia tatu ya a&#341;dhi ya kilimo nchini Zambia inadhibitiwa na wageni wanaoendesha kilimo cha chakula cha biasha&#341;a.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa Taasisi ya Oakland , shi&#341;ika la utafiti hu&#341;u wa se&#341;a, uwekezaji wa kilimo hapa unazidi kuongezeka wakati se&#341;ikali &#8220;inazidi kuuza kimyakimya na kuandaa kuendeleza kwa uchache hekta milioni 1.5 za a&#341;dhi yake.&#8221;<\/p>\n<p>Pamoja na kwamba hakuna utafiti umefanyika kuangalia idadi halisi ya wakulima waliohamishwa kutokana na kuchukuliwa kwa a&#341;dhi yao, Chama cha Wakulima cha Taifa cha Zambia chenye kifupi chake kwa lugha ya Kiinge&#341;eza kama ZNFU kilisema wakulima walioathi&#341;ika wanaweza kufikia maelfu.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa makamu wa &#341;ais wa ZNFU G&#341;aham Rae, kuhamishwa kwa wakulima kutoka katika a&#341;dhi yao ya jadi ni suala la kuangaliwa. &#8220;Limekuwa likiendelea kwa muda sasa na wakulima wetu wengi, hasa katika maeneo ya kijijini wameathi&#341;ika.<\/p>\n<p>&#8220;Hali ya usalama wa chakula inaweza kuwaathi&#341;ika kwasababu pengine tunazungumzia wakulima kwa maelfu ambao hawazalishi. Katika nchi kama Af&#341;ika Kusini, usalama wa chakula umejikita katika wakulima wakubwa, wakati kwa upande wetu sekta ya wakulima wadogo wadgo ina jukumu kubwa la usalama wa chakula. Hivyo usalama wa chakula unaweza kuathi&#341;ika kwa kiasi kikubwa, siyo tu katika ngazi ya kaya lakini pia ngazi ya taifa,&#8221; Rae alisema.<\/p>\n<p>Wakulima wadogo wadogo ni asilimia 70 ya jamii ya wakulima ya Zambia, kwa mujibu wa ZNFU. Umoja una wanachama 600,000 ambao ni pamoja na wakulima wadogo wadogo, wakulima wa dha&#341;ula, na wakulima wa biasha&#341;a. Kati ya idadi hiyo, theluthi mbili au 400,000 ni wakulima wadogo wadogo. Lakini idadi ya wakulima wadogo wadogo nchini wanaweza kuwa ma&#341;a mbili ya idadi hiyo na hata ma&#341;a tatu kwani wengi wao hawajajiunga na chama.<\/p>\n<p>Hen&#341;y Machina, mku&#341;ugenzi mtendaji wa Umoja wa A&#341;dhi Zambia, kikundi cha utetezi, analaumu kuhamishwa kwa wakulima kuwa kunatokana na ta&#341;atibu mbovu na ngumu za kupata hati miliki na she&#341;ia za &#8220;kizamani&#8221; ambazo hazitambui haki za kimila kama aina ya umiliki wa a&#341;dhi. Chini ya she&#341;ia nchini Zambia, hati miliki ndiyo uthibitisho pekee kuwa unamiliki a&#341;dhi hiyo.<\/p>\n<p>&#8220;Ili kupata hati miliki, inaweza kukuchukua kati ya miezi miwili hadi miaka 10. Mfumo ni wa kizamani mno na umejikita katika se&#341;ikali kuu &ndash; kwani unaweza kupata hati miliki kutoka kwa Wiza&#341;a ya A&#341;dhi pekee mjini Lusaka,&#8221; Machina aliiambia IPS.<\/p>\n<p> &#8220;Kwa wakulima katika maeneo ya vijijini, kupata hati miliki ni gha&#341;ama kubwa. Inabidi kulipia usafi&#341;i ikiwa ni pamoja na chakula na malazi kila wakati wanaposafi&#341;i kufuatilia. Na inaweza kuwagha&#341;imu hadi kwacha milioni 10 (kama dola 2,000) katika mchakato huo. Matokeo yake, wengi wanaona afadhali waachane na mchakato na hivyo kuendelea na kilimo,&#8221; alisema Machina.<\/p>\n<p>Kwa sasa asilimia 59 ya Wazambia wanaishi chini ya msta&#341;i wa umaskini, huku asilimia 65 ya wakazi wakiishi katika maeneo ya kijijini.<\/p>\n<p>P&#341;eto&#341;ious Nkhata, kutoka wilaya ya Mpongwe kwenye jimbo la Coppe&#341;belt, ni mmoja wa wakulima hao. Akiwa na um&#341;i wa miaka 68&ndash;anadai kuwa alihamishwa kutoka hekta zake 21 za a&#341;dhi ya jadi, ambazo amekuwa akilima kwa miaka 10 na zaidi, na kampuni ya kilimo cha biasha&#341;a ya Af&#341;ika Kusini mwaka 2008.<\/p>\n<p>Nkhata ambaye pamoja na wakulima wengine walihamishwa kutoka hekta 46,876 za shamba la biasha&#341;a aliiambia IPS kuwa walipata a&#341;dhi yao kutoka kwa kiongozi wa jadi lakini hawakupata hati miliki kutoka se&#341;ikalini.<\/p>\n<p>&#8220;Walituambia kuwa sisi ni watumiaji wasiokuwa &#341;asmi na ni wavamizi wa a&#341;dhi. Nilikuwa na hekta 21 &#8230; nilizipoteza zote &#8230;<\/p>\n<p>&#8220;Wakulima wa kilimo cha biasha&#341;a kutoka Af&#341;ika Kusini walifika na bunduki na kutishia kumpiga yeyote ambaye angekaidi am&#341;i ya kuondoka. Walichoma moto mali zetu zote za kaya zetu bila kutuambia. Tulikuwa ka&#341;ibu kaya 200. Walichoma moto maghala yangu ya kuhifadhia chakula, nguo, mablanketi, vitanda, televisheni &ndash; walichoma hata mashamba yangu,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Hata hivyo kampuni hiyo imeshauza a&#341;dhi na kufunga biasha&#341;a zake nchini Zambia. Jitihada za IPS za kutafuta maoni ya kampuni hiyo hazikuafanikiwa.<\/p>\n<p>Mwanashe&#341;ia mashuhu&#341;i ambaye anawakilisha wakulima waliohamishwa na ambaye hakutaka kutajwa, aliiambia IPS kuwa watu wenye kumiliki a&#341;dhi kijadi nchini Zambia hawana ulinzi wa kishe&#341;ia, na hata fidia zao zinatolewa kwa misingi ya kibinadamu tu.<\/p>\n<p>&#8220;Vifungu vya 33 na 34 vya She&#341;ia ya A&#341;dhi na Utoaji wa Hati Miliki vinasema kuwa hati miliki ni ushahidi wa kishe&#341;ia kuwa namiliki a&#341;dhi. Kanuni ya msingi ni kwamba mtu mwenye hati miliki ya a&#341;dhi anamiliki kila kitu katika a&#341;dhi hiyo. Haijalishi ni maendeleo gani umefanya katika a&#341;dhi hiyo kama huna hati miliki siyo yako,&#8221; alisema mwanashe&#341;ia huyo.<\/p>\n<p>&#8220;Tunachopigania tunapowawakilisha wateja wetu ambao a&#341;dhi yao imechukuliwa ni kupewa fidia kutokana na kufanya maendeleo katika a&#341;dhi &ndash; lakini wamiliki wapya wa a&#341;dhi hawana kifungo chochote cha she&#341;ia kinachowataka kulipa fidia.&#8221;<\/p>\n<p>Katibu mkuu katika Wiza&#341;a ya A&#341;dhi Daizy Ng&#8217;ambi aliiambia IPS kuwa kwa sasa se&#341;ikali inaandaa wa&#341;aka wa kazi kuwapatia usalama wamiliki wa jadi.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa sasa, hakuna kifungu kinachowalinda wamiliki wa jadi ambao hawana hati miliki. Lakini inaonekana kuwa wa&#341;aka utakapokamilika juu ya usalama wa wamiliki wa jadi na kupata maoni kutoka kwa wadau wote, masuala ya umiliki wa jadi na ulipaji sahihi wa fidia yatazingatiwa,&#8221; Ng&#8217;ambi alisema.<\/p>\n<p>Pia alisema wiza&#341;a yake inafanya kazi kubo&#341;esha teknolojia katika kuandaa hati miliki, ambayo inata&#341;ajiwa kupunguza ta&#341;atibu zinazochosha na ambazo zinachukua muda m&#341;efu.<\/p>\n<p>Pamoja na mabadiliko haya, Nkhata hatapata a&#341;dhi ambayo aliwahi kuimiliki. Kwa sasa Nkhata anaishi katika kijiji kidogo kilichozungukwa na mashamba ya wakulima wa biasha&#341;a yaliyozungukwa na fensi ya nyaya, baadhi ya kilomita 40 kutoka katika shamba lake la zamani. &#8220;Kwa sasa nimekwama. Hawajanipatia fidia yoyote au a&#341;dhi mbadala,&#8221; alisema<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>LUSAKA, Desemba 3 (IPS) &ndash; Ongezeko la maendeleo ya kilimo nchini Zambia litaathi&#341;i usalama wa chakula nchini humo kwani wakulima wadogo wadogo wanaendelea kuondolewa katika a&#341;dhi zao za kimila kupisha wakulima wakubwa wa ndani na nje ya nchi wanaotaka kuendesha kilimo cha biasha&#341;a, kwa mujibu wa mkuu wa shule ya kilimo katika Chuo Kikuu cha&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":959,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3966","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3966","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/959"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3966"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3966\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3966"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3966"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3966"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}