{"id":3962,"date":"2012-11-27T13:40:01","date_gmt":"2012-11-27T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/11\/27\/wakulima-wabeba-matumaini-ya-amani-na-maendeleo-katika-kongo-ya-drc\/"},"modified":"2012-11-27T13:40:01","modified_gmt":"2012-11-27T13:40:01","slug":"wakulima-wabeba-matumaini-ya-amani-na-maendeleo-katika-kongo-ya-drc","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/11\/27\/wakulima-wabeba-matumaini-ya-amani-na-maendeleo-katika-kongo-ya-drc\/","title":{"rendered":"Wakulima Wabeba Matumaini ya Amani na Maendeleo katika Kongo ya DRC"},"content":{"rendered":"<p>GOMA, Kongo ya DRC, Novemba 27 (IPS) &ndash; Ng&#8217;omne wa maziwa wanachungwa tena katika vilima vya kijani katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, masha&#341;iki mwa Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asia ya Kongo. Miaka ishi&#341;ini iliyopita, kuibuka kwa vita vya kikabila kulisamba&#341;atisha kabisa mkoa huo, na ku&#341;ejeshwa kwa shamba la Lushebe&#341;e kunaweza kuonekana kama dalili na uthibitisho wa amani tete.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Likiwa limeanzishwa katika miaka ya 1960 na mtumishi wa dini Ca&#341;bonel, shamba la Lushebe&#341;e lililazimika kufungwa mwaka 1993 wakati mapigano makali ya kikabila yalipoanza mwezi Machi mwaka huo katika eneo la Ntoto, katika jimbo la Walikale, kabla ya kuenea katika maeneo mengine ya Kivu Kaskazini: Masisi na Rutshu&#341;u, ikiwa ni pamoja na Kalehe, katika jimbo la Kivu ya Kusini.<\/p>\n<p>Nyumba, mashamba na shule, vituo vya afya na masoko na makanisa vilichomwa moto, na mifugo ilichinjwa au kuchukuliwa na wanamgambo. Mameneja wa shamba walilazimishwa kuachana na shughuli zao wakati familia nyingi zilikimbia Masisi kwenda katika mji mkuu wa jimbo, Goma, au kuingia katika nchi ji&#341;ani za Rwanda na Bu&#341;undi.<\/p>\n<p>Wakati wa miaka kumi ya kufungwa kwa shamba hilo, miti aina ya mika&#341;atusi ilikatwa na kuuzwa ili kulipia mishaha&#341;a ya wafanyakazi ambao walibakia nyuma kulinda mali zao.<\/p>\n<p>Katika ukanda huo, ambako mkaa ni chanzo cha kipekee cha nishati, ukataji ha&#341;amu wa miti unazidi kuongezeka, hata katika mbuga za wanyama.<\/p>\n<p>&#8220;Kaya tisa kati ya kumi hutumia mkaa kwa ajili ya kuongeza joto katika nyumba zao na kupikia,&#8221; alisema Emmanuel de M&eacute;&#341;ode, mku&#341;ugenzi wa Taasisi ya Utunzaji wa Mazingi&#341;a wa Asili Kongo.<\/p>\n<p>&#8220;Tangu mwaka 2003, tumeshapanda miti 20,000 ya mika&#341;atusi ili kuchukua nafasi ya ile iliyokatwa na kuuzwa,&#8221; Pad&#341;e Diog&#038;eg&#341;ave;ne Ha&#341;e&#341;imana, mku&#341;ugenzi wa shamba hilo, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Shamba la hekta 558 lilianza kufanya kazi tena mwaka 2003 kutokana na mchango wa eu&#341;o 33,000 kutoka shi&#341;ika la Saint Ave&ndash;Goma Ent&#341;aide (SAGE), chama ambacho kiliundwa nchini Ufa&#341;ansa mwaka 2002 kusaidia kujenga amani miongoni mwa vikundi vya kikabila vya Masisi kupitia shughuli za pamoja za kiuchumi.<\/p>\n<p>Fedha ziliwafikia wakulima kwa njia ya vifaa ambavyo vilikuwa vimeshanunuliwa. SAGE pia imelipatia shamba chumba cha ba&#341;idi kwa ajili ya kuhifadhia mazao yake ya maziwa na ga&#341;i aina ya 4&times;4 kusafi&#341;isha mazao kwenda katika soko la Goma.<\/p>\n<p>Mwezi Julai, shamba lilipokea msaada mwingine wa eu&#341;o 61,000, wakati huu kutoka Rota&#341;y Club ya Vannes, mji wa magha&#341;ibi mwa Ufa&#341;ansa, na kutoka shi&#341;ika la Rota&#341;y Inte&#341;national. Fedha hizi zimesaidia kusambaza vifaa vipya vya kugandishia na kufungia maziwa.<\/p>\n<p>Fundi kutoka kampuni ya Ulaya ambayo iliuza mashine hiyo kwa Lushebe&#341;e alitembelea shamba kutoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya jinsi ya kuhifadhi vifaa hivyo. &#8220;Kwa sasa tunafanya kazi kwa kujitegemea,&#8221; alisema Ha&#341;e&#341;imana.<\/p>\n<p>Kwa kuwa na vifaa vipya, shamba kwa sasa linafunga maziwa katika paketi za lita moja ambayo huuzwa kwa dola moja kila paketi, pamoja na kuwa mazao ya kila siku bado hayawezi kuzidi lita 50.<\/p>\n<p>&#8220;Wakazi wa Goma na wafanyakazi wa mashi&#341;ika ya misaada katika eneo lenye ukubwa wa mzunguko wa kilomita 20 (la Lushebe&#341;e) wanazidi kuzoea aina hii ya maziwa,&#8221; alisema Ha&#341;e&#341;imana.<\/p>\n<p>Ng&#8217;ombe wa shamba la Lushebe&#341;e kwa sasa wanafikia 420, kidogo zaidi ikilinganishwa na jumla ya ng&#8217;ombe 2,000 waliokuwa nao mwaka 1990. Shamba pia lilikuwa na wafanyakazi 1,000 miaka 20 iliyopita. Leo hii linaaji&#341;i wafanyakazi 60, huku wakipatiwa mishaha&#341;a ya kila mwezi ya kati ya dola 25 na 130.<\/p>\n<p>Lakini tangu mwezi Julai, shamba limeweza kuongeza uzalishaji wa siagi kutoka kilo tano hadi kilo 35 kwa kila siku.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa sasa, maziwa yetu yanapimwa kwanza kuangalia kuwepo kwa bakte&#341;ia kabla hayajaingizwa katika matenki makubwa na kuandaliwa kwa siagi,&#8221; alisema Ha&#341;e&#341;imana.<\/p>\n<p>Vipande vya siagi huuzwa kwa dola tano kwa kilo, ikilinganishwa na dola tatu kwa kilo kwa siagi iliyozalishwa mahali pengine &ndash; lakini walaji wakuu wanavutiwa kulipia kiasi kikubwa kutokana na ubo&#341;a wa maziwa yetu ambayo yameondolewa mafuta.<\/p>\n<p>&#8220;Ma&#341;a nyingi kichache ni kinyemi, na kinyemi ni kichache,&#8221; alisema Jacques Bonana, mmoja wa wateja wa shamba hilo. Bonana anafanya kazi katika shi&#341;ika la kibinadamu katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Lushebe&#341;e.<\/p>\n<p>Watu wengi wanakubaliana kuwa maziwa yetu ni bo&#341;a katika kanda, alisema Cha&#341;les Balume, mmiliki wa mgahawa mjini Goma.<\/p>\n<p>Akiongea na IPS katika F&#341;ancophonie Village mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC, katikati mwa Oktba, Ca&#341;ly Kasivita Nzanzu, wazi&#341;i wa jimbo wa kilimo na maendeleo ya kijijini katika Kivu ya Kusini, alisema &#8220;Kiwanda hiki kipya kitaleta maendeleo ya kweli ya kiuchumi na kijamii katika mkoa wa Lushebe&#341;e na katika Kivu ya Kaskazini yote.&#8221;<\/p>\n<p>Katika mkoa huu, ambako watu hawaaminiani na wanajamii wamezoea kuzu&#341;ula ovyo, Monsigno&#341; Th&eacute;ophile Kaboy, askofu wa Goma, hafichi wasiwasi wake.<\/p>\n<p>Anahofia ku&#341;ejea kwa wanamgambo kutoka Ntoto: Ra&iuml;a Mutomboki (neno lenye maana ya &#8220;tunasafisha watu wasiokuwa wazawa) ambao ma&#341;a nyingi wanapigana na Nyatu&#341;a (neno lenye maana ya &#8220;futilia na kung&#8217;oa wanaojiona kuwa ni wazawa&#8221; kwa lugha ya Kinya&#341;wanda). Kila kikundi cha wanamgambo kinasaidiwa na wanasiasa fulani. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>GOMA, Kongo ya DRC, Novemba 27 (IPS) &ndash; Ng&#8217;omne wa maziwa wanachungwa tena katika vilima vya kijani katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, masha&#341;iki mwa Jamhu&#341;i ya Kidemok&#341;asia ya Kongo. Miaka ishi&#341;ini iliyopita, kuibuka kwa vita vya kikabila kulisamba&#341;atisha kabisa mkoa huo, na ku&#341;ejeshwa kwa shamba la Lushebe&#341;e kunaweza kuonekana kama dalili na uthibitisho wa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":956,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3962","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3962","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/956"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3962"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3962\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3962"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3962"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3962"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}