{"id":3954,"date":"2012-10-31T13:40:01","date_gmt":"2012-10-31T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/10\/31\/kukuza-kilimo-cha-migomba-kukabiliana-na-mabadiliko-ya-tabia-nchi\/"},"modified":"2012-10-31T13:40:01","modified_gmt":"2012-10-31T13:40:01","slug":"kukuza-kilimo-cha-migomba-kukabiliana-na-mabadiliko-ya-tabia-nchi","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/10\/31\/kukuza-kilimo-cha-migomba-kukabiliana-na-mabadiliko-ya-tabia-nchi\/","title":{"rendered":"Kukuza Kilimo cha Migomba Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi"},"content":{"rendered":"<p>PANGANI, Oktoba 31 (IPS) &ndash; Haki ya chakula ni moja ya haki za msingi kabisa kwa mwanadamu. Hata hivyo, njaa inaendelea kuwakumba watu wengi duniani huku Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a ikiongoza kwa kuwa na wakazi wengi wanaokabiliwa na njaa kila mwaka. Mabadiliko ya tabia nchi yamezidisha kuenea kwa janga hili kutokana na kusababisha uzalishaji wa chakula kutokuwa endelevu.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Pamoja na takwimu za hivi ka&#341;ibuni za Umoja wa Mataifa kuonyesha kuwepo kwa mafanikio ya kupunguza njaa kwa wakazi wa dunia, hata hivyo, bado mtu mmoja katika kila watu nane wanatajwa kukabiliwa na njaa.<\/p>\n<p>Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa imepungua kwa watu milioni 130 tangu mwaka 1990, kutoka watu bilioni moja hadi milioni 868. Idadi kubwa ya watu hawa, milioni 852, wanaishi katika nchi zinazoendelea, jambo ambalo lina maana kuwa asilimia 15 ya watu katika nchi zinazoendelea wanaishi katika njaa, wakati ni watu milioni 16 tu wanakabiliwa na njaa katika nchi zilizoendelea.<\/p>\n<p>Ripoti ya Hali ya Kukosekana Kwa Usalama wa Chakula Duniani Mwaka 2012 (SOFI), ambayo imetolewa kwa pamoja na Shi&#341;ika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shi&#341;ika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), inasema kuwa kama &#8220;hatua stahiki&#8221; hazijachukuliwa kulisha watu wenye njaa na kupunguza kasi ya kupungua kwa uzalishaji wa chakula, lengo la kupunguza nusu ya watu wenye njaa katika ulimwengu unaoendelea ifikapo mwaka 2015 halitafikiwa. <\/p>\n<p>&#8220;Haba&#341;i njema ni kuwa tuna baadhi ya mafanikio lakini bado inaonyesha kuwa mtu mmoja katika kila watu nane anaishi na njaa. Jambo hili halikubaliki,&#8221; Mku&#341;ugenzi Mkuu wa FAO Jos&eacute; G&#341;aziano da Silva aliwaambia waandishi wa haba&#341;i katika makao makuu ya FAO siku za ka&#341;ibuni. &#8220;Katika FAO namba inayokubalika ya watu wenye njaa ni sifu&#341;i tu.&#8221;<\/p>\n<p>&#8220;Hata kama tunapunguza nusu ya watu wenye njaa ifikapo mwaka 2015, ni muhimu kuangalia mbele na kufikia kutokomeza kabisa njaa, na hivyo kujibu wito wa mkutano wa kilele wa Rio+20 wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki&ndash;moon wa &#8216;Changamoto ya Namba Sifu&#341;i ya Njaa&#8217;,&#8221; alisema G&#341;aziano da Silva.<\/p>\n<p>Hali ni mbaya zaidi ba&#341;ani Af&#341;ika, ambapo idadi ya watu wenye njaa imeongezeka katika kipindi cha miaka ishi&#341;ini iliyopita kutoka watu milioni 175 hadi milioni 239. Katika Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a, njaa imekuwa ikiongezeka kwa asilimia mbili kwa mwaka tangu mwaka 2007, kwa mujibu wa &#341;ipoti hiyo.<\/p>\n<p>Takwimu za hivi ka&#341;ibuni nchini Tanzania zinaonyesha kuwa asilimia 42 ya watoto wa chini ya um&#341;i wa miaka 5 wanapata lishe duni na wamedumaa na zaidi ya asilimia 50 ya watoto hao wana upungufu wa damu.<\/p>\n<p>Kuna mambo mengi yanayochangia kuenea kwa njaa katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a ambao pia unaongoza kwa umaskini duniani. Moja ya sababu hizo ni kuzidi kuenea kwa mabadiliko ya tabia nchi. <\/p>\n<p>Ili kujua atha&#341;i za mabadiliko ya tabia nchi kwa jamii, M&#341;adi wa TCMP&ndash; Pwani unaofadhiliwa na Shi&#341;ika la Misaada la Ma&#341;ekani (USAID) ulifanya utafiti wake hivi ka&#341;ibuni katika baadhi ya vijiji wilayani Pangani. Matokeo ya utafiti katika kijiji cha Mwembeni kata ya Madanga yalionyesha kilimo kuathi&#341;ika na hivyo kuwakosesha wananci wa kijiji hicho vyanzo muhimu vya chakula na mapato. <\/p>\n<p>&#8220;Matokeo ya utafiti shi&#341;ikishi uliofanyika katika kijiji cha Mwembeni juu ya atha&#341;i za mabadiliko ya tabia nchi na namna jamii inavyoweza kukabiliana nayo ulionyesha kuwa kijiji kimekumbwa na atha&#341;i za mabadiliko hayo kutokana na histo&#341;ia ya matukio ya majanga ya ukame unaojitokeza ma&#341;a kwa ma&#341;a na kunyesha kwa mvua kubwa za el nino mwishoni mwa miaka ya 1990&#8221;, anasema Jai&#341;os Mahenge, m&#341;atibu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi katika TCMP&ndash;Pwani.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa Mboni Salehe, katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya kijiji cha Mwembeni, kutokana na hali ya ukame iliyojitokeza katika miaka ya hivi ka&#341;ibuni, mashamba ya mpunga hayakuweza kutoa mazao hata kidogo kutokana na ukame kuathi&#341;i kilimo cha mpunga ikiwa ni pamoja na mazao mengine ya chakula.<\/p>\n<p>Amesema zamani wakulima kijijini humo waliweza kupata mvua za kutosha na kuendesha kilimo ma&#341;a nne kwa mwaka na kuvuna katika misimu yote, lakini sasa hali ni mbaya na uzalishaji wa chakula umepungua kwa kiasi kikubwa.<\/p>\n<p>&#8220;Tulikuwa na uwezo wa kuvuna mpunga, mihogo na miwa ambayo pia iliweza kutusaidia kuingiza kipato kutokana na kuuza ziada na hata kusafi&#341;isha kwenda Zanziba&#341;,&#8221; alisema Bi. Salehe hivi ka&#341;ibuni. &#8220;Lakini sasa mvua ni chache, mto Mzia umekauka, hauna maji tena. Chumvi imeongezeka katika Mto Pangani, mabonde ya mpunga yamevamiwa na chumvi na badala ya kuendesha kilimo cha mpunga na miwa, sasa mabonde hayo yamejaa miti aina ya mikoko.&#8221; <\/p>\n<p>Ili kukabiliana na hali hiyo, m&#341;adi wa TCMP&ndash;Pwani ulishau&#341;iana na wananchi na wadau wengine juu ya njia za kukabiliana na ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.<\/p>\n<p>&#8220;Katika hali ya kuweza kuelimishana na wananchi juu ya mabadiliko ya tabia nchi, tuliwaambia kuwa ufumbuzi siyo kukimbia kijiji, lakini namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo,&#8221; anasema Mahenge, na kusema kuwa moja ya ufumbuzi wa kukabiliana na ukame ni kupanda mazao yanayohimili ukame huo.<\/p>\n<p>Kilimo cha migomba ufumbuzi wa kukabiliana na atha&#341;i za ukame<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa Mahenge, kutokana na kiijiji cha Mwembeni kuwa na histo&#341;ia ya watu kupenda kupanda migomba, ambayo walisema inawasaidia wakati wa ukame, &#8220;tulishau&#341;iana na wanakijiji hao kupanda zao hilo ambalo angalau wana asili na uzoefu nalo ili kukabiliana na ukame badala ya kuchagua mbinu ambayo ni mpya kabisa kwao&#8221;.<\/p>\n<p>&#8220;Kwa kushi&#341;ikiana na wataalam wa kilimo wa wilaya ya Pangani tuligundua kuna taasisi za kilimo ambazo zimefanya utafiti wa aina ya migomba inayoweza kuhimili ukame, magonjwa na kuzaa katika kipindi cha muda mfupi. Tukaona mazao hayo yatakuwa ni suluhisho kwa eneo la Mwembeni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa suala zima la ukame,&#8221; anasema.<\/p>\n<p>Migomba kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Tenge&#341;u mkoani A&#341;usha iligawiwa kwa wanakijiji 20, ambao kila mmoja alipata miche 10 ya kupanda katika kipande chake cha shamba kwa kutumia mbinu za kitaalam. Akifafanua zaidi, Mahenge anasema mbinu hizo ni pamoja na kuzingatia kuwa nafasi kutoka mche hadi mche ni lazima kuwa mita 5, na shimo lenye upana wa futi 3 na u&#341;efu futi 3 na kina futi 3. Shimo linatakiwa kuchanganywa na mbolea ya kutosha na kuacha nafasi ya futi moja kutoka juu kwa ajili ya kuacha nafasi ya maji kutuama kwa muda m&#341;efu.<\/p>\n<p>Aina 5 za mbegu za migomba ziligawiwa kwa wananchi. Aina hizo ni pamoja na mkono wa tembo, mzuzu, williams, g&#341;andenine na Chinese Cavendish. Kila mkulima alipewa kwa mchanganyiko kuhakikisha kila mmoja anakuwa na aina zote za mbegu. <\/p>\n<p>Hata hivyo, kwa mujibu wa Mahenge, mwitikio wa wananchi juu ya m&#341;adi huo ulikuwa ni mkubwa kwani &#8220;jamii iliona ile miche 200 iliyoenda pale kijijini ni sawa na tone la maji katikati mwa Baha&#341;i, kwani ka&#341;ibu wananchi wote kutoka kijijini hapo walikuwa na hamu ya kupanda migomba hiyo&#8221;. <\/p>\n<p>M&#341;adi endelevu<\/p>\n<p>Kutokana na atha&#341;i za mabadiliko ya tabia nchi kudumu kwa miaka mingi, TCMP&ndash;Pwani ilihakikisha kuwa inaandaa m&#341;adi utakaoendeshwa na wananchi wenyewe na utakaohakikisha unadumu kwa miaka mingi hata kama m&#341;adi huo wa Pwani utakua umeshamaliza wakati wake wa utekelezaji.<\/p>\n<p>&#8220;Tumehakikisha m&#341;adi unakuwa endelevu kwa kuweka makubaliano na se&#341;ikali ya kijiji kuwa watu 20 waliopatiwa mbegu za migomba watakuwa ni chachu ya kusambaa kwa migomba hiyo katika kijiji kizima na kwingineko na tukakubaliana na se&#341;ikali ya kijiji kuwa machipukizi yote yatakayotokana na migomba hiyo yatasambazwa kwa wananchi wengine,&#8221; anafafanua Mahenge.<\/p>\n<p>Pia m&#341;adi unahakikisha uendelevu kwa kufanya kazi ka&#341;ibu na halmashau&#341;i ya wilaya, ambapo bwanashamba wa ta&#341;afa ya Madanga hufuatilia kwa ka&#341;ibu kuwasaidia wananchi katika masuala ya kitaalam kutokana na kuwa mmoja wa waanzilishi na wabunifu wa m&#341;adi wakati wote tangu mwanzo. Pia kikundi cha watu ishi&#341;ini kilichopewa mbegu za Migomba kina uongozi wao ambao unafanya ufuatiliaji wa maendeleo ya m&#341;adi pamoja na kuwa kila mmoja ana shamba lake binafsi analolihudumia.<\/p>\n<p>Mku&#341;ugenzi wa Wilaya ya Pangani, Neneka Rashid, anaunga mkono suala la uendelevu wa m&#341;adi huo kwa kusema kuwa mbegu hizo za migomba zinata&#341;ajiwa kusambaa kwa wananchi wengine na baadaye kutapakaa kwa ha&#341;aka katika kijiji kizima na vijiji vingine.<\/p>\n<p>Mahenge anasema kwa sasa jukumu la TCMP&ndash;Pwani ni kuendelea kufanya ufuatiliaji wa ka&#341;ibu kuhakikisha kwamba hiyo migomba inatoa mata&#341;ajio yaliyota&#341;ajiwa. &#8220;Kwa mujibu wa sifa ya hiyo migomba endapo itapatiwa matunzo mazu&#341;i ina uwezekano wa kutoa zao la kwanza ndani ya miezi 10 tu. Ni mata&#341;ajio yetu kuwa muda siyo m&#341;efu tutaanza kuona matunda,&#8221; alisema. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>PANGANI, Oktoba 31 (IPS) &ndash; Haki ya chakula ni moja ya haki za msingi kabisa kwa mwanadamu. Hata hivyo, njaa inaendelea kuwakumba watu wengi duniani huku Af&#341;ika Kusini mwa Jangwa la Saha&#341;a ikiongoza kwa kuwa na wakazi wengi wanaokabiliwa na njaa kila mwaka. Mabadiliko ya tabia nchi yamezidisha kuenea kwa janga hili kutokana na kusababisha&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":536,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3954","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3954","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/536"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3954"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3954\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3954"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3954"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3954"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}