{"id":3953,"date":"2012-10-30T13:40:01","date_gmt":"2012-10-30T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/10\/30\/kuwapatia-wanawake-adhi-ni-kuwapatia-maisha-ya-baadaye\/"},"modified":"2012-10-30T13:40:01","modified_gmt":"2012-10-30T13:40:01","slug":"kuwapatia-wanawake-adhi-ni-kuwapatia-maisha-ya-baadaye","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/10\/30\/kuwapatia-wanawake-adhi-ni-kuwapatia-maisha-ya-baadaye\/","title":{"rendered":"Kuwapatia Wanawake A&#341;dhi ni Kuwapatia Maisha ya Baadaye"},"content":{"rendered":"<p>YAOUNDE, Oktoba 30 (IPS) &ndash; Kwa taabu Cla&#341;isse Kimbi anaweza kuendesha maisha kwa kutegemea kipande kidogo cha a&#341;dhi katika kijiji cha Kom katika Mkoa wa Kaskazini Magha&#341;ibi mwa Came&#341;oon. Leo hii, akiwa mama wa watoto sita anapata shida kulisha watoto wake na yeye mwenyewe. Lakini miaka mitano iliyopita, mume wake na watoto wake walikuwa wakionekana watu wenye uwezo.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Mwaka 2007, akiwa analima a&#341;dhi yenye ukubwa wa hekta tano, Kimbi aliweza kulisha familia yake bila shida, na bado angepata chakula cha ziada kwa ajili ya kukiuza. Katika nchi ambapo asilimia 40 ya wakazi wanaishi chini ya msta&#341;i wa umaskini, familia yake ilionekana kuwa miongoni mwa familia taji&#341;i.<\/p>\n<p>Lakini mambo yalibadilika wakati mume wake alipofa&#341;iki dunia miaka mitano iliyopita. Ka&#341;ibu kila kitu kilichukuliwa kutoka kwake na watoto wake.<\/p>\n<p>&#8220;Siku moja tu baada ya mazishi ya mume wangu, shemeji zangu walipo&#341;a hekta tano za a&#341;dhi ya mume wangu ambazo nimekuwa nikilima kwa miaka 27,&#8221; aliiambia IPS. Mila za eneo hilo zinawapatia wanaume haki ya ku&#341;ithi a&#341;dhi.<\/p>\n<p>&#8220;Mambo sasa yamekuwa mabaya mno kiasi kwamba ilibidi kuwaachisha baadhi ya watoto shule,&#8221; alisema. <\/p>\n<p>Wawili kati ya watoto wake hao hawaendi shule ya sekonda&#341;i, na wengine watatu wanakwenda kwa shida mno shule ya msingi. Pamoja na tangazo la Rais Paul Biya la kutoa elimu ya msingi bu&#341;e nchini Came&#341;oon mwaka 2004, lakini wazazi bado wanatakiwa kulipia ada kusaidia shule zenye miundombinu duni kufanya kazi.<\/p>\n<p>Tatizo la Kimbi siyo la pekee. Takwimu kutoka Taasisi ya Takwimu ya Taifa ya mwaka 2010 inaonyesha kuwa wanawake ni asilimia 52 ya wakazi wote wa Came&#341;oon milioni 20.<\/p>\n<p>Na pamoja na kuwa wanawake wanazalisha asilimia 80 ya mahitaji ya chakula nchini Came&#341;oon kwa mujibu wa Wiza&#341;a ya Kilimo na Maendeleo Vijijini, wanamiliki asilimia mbili tu ya a&#341;dhi, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 za Mtandao wa Usawa wa Jinsia Came&#341;oon.<\/p>\n<p>&#8220;Kama tunaongelea kuhusu jamii ya usawa na ya haki, tunapaswa wanawake kudhibiti kwa uchache asilimia 35 ya a&#341;dhi,&#8221; Judith Awondo, m&#341;atibu wa mtandao huo, asasi isiyokuwa ya kise&#341;ikali ambayo inafanya kazi kuwapatia uwezo wanawake, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Pamoja na kwamba She&#341;ia ya Umilikaji wa A&#341;dhi ya Mwaka 1974 nchini Came&#341;oon inahakikishia usawa wa kumiliki a&#341;dhi &#341;aia wote, she&#341;ia za kimila na destu&#341;i zinabagua wanawake dhidi ya haki zilizopo katika she&#341;ia. Hii imesababisha matatizo katika uchumi wa wanawake.<\/p>\n<p>&#8220;Kukosekana kwa uwezo kwa wanawake kumiliki a&#341;dhi na kudhibiti njia za kumiliki &#341;asilimali kunawaweka katika nafasi duni katika suala zima la uzalishaji wa kilimo na ukuaji wa kiuchumi, usalama wa chakula, kipato cha familia na ushi&#341;iki sawa katika utawala,&#8221; Fon Nsoh, m&#341;atibu wa NGO ya nchini humo ya Vuguvugu la Haki ya Chakula Came&#341;oon, aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa utafiti wa kaya wa mwaka 2007, asilimia 52 ya watu wanaoishi katika kaya maskini nchini Came&#341;oon ni wanawake.<\/p>\n<p>Matatizo ya umiliki wa a&#341;dhi kwa wanawake na wanajamii yamezidishwa zaidi na upokonyaji wa a&#341;dhi unaoongozwa na makampuni ya kimataifa na jamii taji&#341;i, kwa mujibu wa Nsoh. Alitoa mfano wa &#8220;He&#341;akles Fa&#341;ms&#8221; katika Mkoa wa Kusini Magha&#341;ibi mwa Came&#341;oon kama suala &#8220;gumu zaidi na linalopingwa zaidi.&#8221;<\/p>\n<p>Novemba 7, 2011,Kitengo cha Mahakama Kuu cha Kupe&ndash;Muanenguba katika Mkoa wa Kusini Magha&#341;ibi kilitoa am&#341;i kuwa m&#341;adi huo usimamishwe. Lakini Nsoh alielezea wasiwasi wake kuwa kampuni hiyo ilikuwa inaendelea kuandaa shamba la miwese la hekta 73,000 na kuwa na kibali cha umiliki cha miaka 99 kinachotokana na mazingi&#341;a ya kashfa.<\/p>\n<p>Mashi&#341;ika yenye makao yake nchini Ma&#341;ekani ya Taasisi ya Oakland na G&#341;eenpeace, shi&#341;ika la mazingi&#341;a la kimataifa, yalitoa &#341;ipoti inayopendekeza kuwa m&#341;adi huo uliopo katika eneo ambalo linatajwa kuwa na utaji&#341;i wa baoanuwai kati ya maeneo makuu ya hifadhi, unaweza kuathi&#341;i vibaya watu wapatao 45,000.<\/p>\n<p>Mashi&#341;ika ya mazingi&#341;a yanatuhumu kampuni ya kilimo ya He&#341;akles Fa&#341;ms yenye makao yake mjini New Yo&#341;k kutokana na kuendelea na mipango yake pamoja na pingamizi mbili za mahakama na kukosekana kwa kibali cha se&#341;ikali, na huku kukiwa na upinzani mkubwa kutoka kwa jamii.<\/p>\n<p>&#8220;Kuna mamia ya watu huko ambao wanaweza kupoteza mashamba yao, hasa wanawake ambao hawakuwa sehenu ya mazungumzo,&#8221; Nsoh aliiambia IPS.<\/p>\n<p>Kwa sasa anafanya kazi pamoja na NGOs nyingine na mashi&#341;ika ya ki&#341;aia kuwezesha mageuzi ya She&#341;ia ya Umilikaji wa A&#341;dhi ya mwaka 1974 ambayo inaongoza masuala ya a&#341;dhi nchini Came&#341;oon.<\/p>\n<p>&#8220;She&#341;ia ya A&#341;dhi ya Mwaka 1974 imepitwa na wakati. Imepitishwa kama miaka 38 iliyopita na haiendani tena na siku za sasa hivi na uhalisia wa siku hizi,&#8221; Nsoh alisema.<\/p>\n<p>Kifungu cha 12 cha She&#341;ia ya A&#341;dhi ya mwaka 1974 kinasema &#8220;se&#341;ikali itakuwa inadhibiti a&#341;dhi yote. Katika uwezo huu itaingilia kati kuhakikisha matumizi sahihi ya a&#341;dhi au katika maslahi muhimu, ulinzi au se&#341;a za uchumi wa taifa.&#8221;<\/p>\n<p>Nsoh anasema kuwa kifungu hicho kinawaondoa wanajamii katika mijadala inayohusu a&#341;dhi, huku akitoa mfano wa kesi kadhaa ambapo se&#341;ikali imechukua a&#341;dhi kwa ajili ya uwekezaji, bila hata kushau&#341;iana na wanajamii wanaoishi katika a&#341;dhi hiyo.<\/p>\n<p>Pamoja na NGOs nyingine na mashi&#341;ika ya ki&#341;aia, vuguvugu la Nsoh linashinikiza kuwepo kwa she&#341;ia shi&#341;ikishi zaidi, akisema kuwa she&#341;ia inapaswa kutokusema tu kuwa wanajamii washi&#341;ikishwe katika mazungu&#341;umzo ya a&#341;dhi, lakini pia sehemu kubwa iwahusu wanawake na makundi yaliyopo pembezoni linapokuja suala zima la a&#341;dhi, ili angalau waweze kuwa na udhibiti nayo.<\/p>\n<p>Tangu mwaka jana makundi haya yamekuwa yakifanya kazi ya kuja na muswada wa haki ya a&#341;dhi ili iweze kuwasaidia kuondokana na vikwazo vya upatikanaji wa a&#341;dhi. She&#341;ia inayopendekezwa inataka kuhakikisha kuwa kuna she&#341;ia juu ya mila za kibaguzi ambazo zinazuia wanawake wasipate a&#341;dhi.<\/p>\n<p>&#8220;Hatimiliki lazima zitambue umiliki wa mwanaume na mwanamke na majina mawili ya mume na mke yaandikwe kwenye hati hiyo ili kuondokana na mfumo dume wa u&#341;tihi wa a&#341;dhi ambao umeenea sana nchini Came&#341;oon,&#8221; Nsoh alisema. Aliongeza kuwa mahitaji kama hayo yangewezesha kuwa vigumu kwa wanawake kama Kimbi kunyimwa a&#341;dhi yao na wanafamilia wengine kama mmoja wa wanandoa wao akifa&#341;iki.<\/p>\n<p>Mbali na wito wa kutaka wanawake kuingizwa katika kamati zote zinazohusika na masuala ya a&#341;dhi, mashi&#341;ika ya ki&#341;aia katika taifa hili la Af&#341;ika ya Kati yanashinikiza pia ku&#341;ahisishwa kwa ta&#341;atibu ndefu na zinazochosha za kupata hatimiliki, na gha&#341;ama za kupata hati hizo kupunguzwa kufikia kiwango ambacho wanawake wanaweza kumudu, hasa wanawake maskini ambao wamekuwa maskini kutokana na se&#341;a zilizopo.<\/p>\n<p>&#8220;Tunahitaji kupitia upya she&#341;ia hii na kuipatia mwelekeo wa kijinsia,&#8221; Nsoh alisema.<\/p>\n<p>Alisema pamoja na kwamba se&#341;ikali bado haijajibu madai ya mashi&#341;ika ya ki&#341;aia, ana matumaini kuwa hatimaye itakuja kujibu. Wakati wa maonesho ya wakulima na wafugaji ya mwaka 2011 yaliyoandaliwa huko Ebolowa Mkoa wa Kusini mwa Came&#341;oon, Rais Biya alielezea haja ya kupitia upya she&#341;ia hiyo.<\/p>\n<p>Inaweza kuchukua muda m&#341;efu, lakini kutokana na kuwa natoka katika mamlaka ya juu kabisa ya kisiasa nchini, hakuna wasiwasi kuwa itafanyika,&#8221; Nsoh alisema. Hata hivyo, bado amechanganyikiwa juu ya kasi ndogo ambayo matukio hayo yanafanyiwa kazi, kwasababu hii ina maana kuwa wanawake wengi wa Came&#341;oon wanaendelea kuteseka na kunyimwa haki.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>YAOUNDE, Oktoba 30 (IPS) &ndash; Kwa taabu Cla&#341;isse Kimbi anaweza kuendesha maisha kwa kutegemea kipande kidogo cha a&#341;dhi katika kijiji cha Kom katika Mkoa wa Kaskazini Magha&#341;ibi mwa Came&#341;oon. Leo hii, akiwa mama wa watoto sita anapata shida kulisha watoto wake na yeye mwenyewe. Lakini miaka mitano iliyopita, mume wake na watoto wake walikuwa wakionekana&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":687,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3953","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3953","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/687"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3953"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3953\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3953"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3953"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3953"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}