{"id":3912,"date":"2012-09-06T13:40:01","date_gmt":"2012-09-06T13:40:01","guid":{"rendered":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/06\/tanzania-kuhifadhi-kasa-kwa-kutumia-teknolojia-ya-satelaiti\/"},"modified":"2012-09-06T13:40:01","modified_gmt":"2012-09-06T13:40:01","slug":"tanzania-kuhifadhi-kasa-kwa-kutumia-teknolojia-ya-satelaiti","status":"publish","type":"post","link":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/2012\/09\/06\/tanzania-kuhifadhi-kasa-kwa-kutumia-teknolojia-ya-satelaiti\/","title":{"rendered":"TANZANIA: Kuhifadhi Kasa kwa Kutumia Teknolojia ya Satelaiti"},"content":{"rendered":"<p>DAR ES SALAAM, Septemba 6 (IPS) &ndash; Asasi isiyokuwa ya kise&#341;ikali inayojihusisha na hifadhi ya kasa katika pwani ya Baha&#341;i ya Hindi nchini Tanzania imeanza kutumia teknolojia ya Satelaiti kubo&#341;esha hifadhi ya wanyama hao wa baha&#341;ini waliopo katika hata&#341;i ya kutoweka.\n<\/p>\n<p><!&ndash;&ndash;mo&#341;e&ndash;&ndash;><\/p>\n<p>Akizungumza hivi ka&#341;ibuni wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa washi&#341;ika wa m&#341;adi wa Pwani unaopata ufadhili kutoka Shi&#341;ika la Misaada la Watu wa Ma&#341;ekani (USAID), Afisa wa shi&#341;ika la Sea Sense, Boniventu&#341;e Mchomvu alisema shi&#341;ika lake &#8220;linatumia teknolojia ya kisasa zaidi ya kufanya utafiti muhimu juu ya tabia za kasa kwa kutumia teknolojia ya satelaiti.&#8221; <\/p>\n<p>Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi minne iliyopita, vibandiko vyenye uwezo wa kuwasiliana na mitambo ya satelaiti na kutoa taa&#341;ifa za mwenendo wa kasa vimeshafungwa kwa kasa sita. Vibandiko hivyo, kwa mujibu wa Mchomvu, huwasilisha taa&#341;ifa kwenye mitambo ya satelaiti kila ma&#341;a baada ya kasa kujitokeza nje ya maji kwa ajili ya kupumua, na hivyo &#341;ahisi kutoa taa&#341;ifa mahali ambapo kasa yupo.<\/p>\n<p>&#8220;Katika kipindi cha wiki chache tu, kasa waliovikwa vibandiko hivyo wameshatoa taa&#341;ifa muhimu sana juu ya mwenendo wao. Mmoja wa kasa, mwenye jina la Mwisho ameshasafi&#341;i kuelekea eneo la malisho kaskazini mwa Mombasa wakati mwenzake Zianna kwa sasa anaogelea kupitia mwambao wa Kenya kuelekea nchini Somalia na haonyeshi dalili ya kuhitimisha safa&#341;i yake. Tulia ameamua kuelekea upande wa kusini na alikuwa akipita eneo la Kilwa&#8221;, alisema.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa Mchomvu, kuelewa mwenendo wa kasa ni jambo muhimu mno kujua maisha ya viumbe hao. &#8220;Mfano, tumeshagundua kuwa kuna eneo la Temeke ambalo kasa wote, wawe wanaelekea kaskazini au kusini, ni lazima wapitie hapo ndipo waanze safa&#341;i yao. Utafiti utatusaidia kujua eneo hilo lina nini hadi kuwa makutano ya kasa wote,&#8221; alisema. Kupata taa&#341;ifa kutasaidia Sea Sense kubaini maeneo muhimu ya malisho nchini Tanzania na katika ukanda mzima pia&#8221;. <\/p>\n<p>Alisema taa&#341;ifa hizo pia zitasaidia kujua ni maeneo gani hata&#341;i zaidi kwa kasa wanaosafi&#341;i kutoka eneo moja kwenda jingine na kuelekeza jitihada katika kupunguza hata&#341;i katika maeneo hayo, hasa katika maeneo yenye hata&#341;i ya kasa kunasa kwenye nyavu za wavuvi,&#8221; alisema.<\/p>\n<p>Pamoja na kasa, Sea Sense pia inashi&#341;ikiana na jamii za pwani ncini Tanzania kuhifadhi wanyama wengine waliopo katika hata&#341;i ya kutoweka kama vile nguva, nyangumi, pomboo na papa nyangumi.<\/p>\n<p>Kwa mujibu wa tovoti ya shi&#341;ika hilo, &#8220;viumbe hawa, pamoja na makazi yao wanakabiliwa na mustakabali wa maisha usiokuwa na uhakika, hasa kutokana na shughuli za mwanadamu katika ukanda wa pwani. Maisha yao yanawezekana tu kama kuna jitihada za kuhifadhi eneo zima la pwani ikiwa ni pamoja na baoanuai ya baha&#341;i na kubo&#341;esha maisha ya watu wanaoishi katika maeneo ya mwambao.&#8221;<\/p>\n<p>Kasa ni miongoni mwa viumbe wa baha&#341;i waliopo katika hata&#341;i ya kutoweka, kwani tafiti duniani kote zinaonyesha kuwa miaka hamsini iliyopita kulikuwa na kasa wengi katika baha&#341;i, lakini kutokana na sababu nyingi idadi ya kasa wamezidi kupungua. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na watu kupendelea kula nyama ya kasa, mayai na kujenga hoteli katika fukwe zinazotumiwa na kasa hao kwa ajili ya kutaga na kutotoa watoto.<\/p>\n<p>Wakati maendeleo ni muhimu katika maeneo ya mwambao wa pwani, ni muhimu kuhifadhi kasa kwani wanasaidia sana katika hifadhi ya mazingi&#341;a ya baha&#341;i. Baadhi ya aina ya kasa wanafanya kazi kubwa ya kusafisha matumbawe na hivyo kuleta usawa wa baoanuai. <\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>DAR ES SALAAM, Septemba 6 (IPS) &ndash; Asasi isiyokuwa ya kise&#341;ikali inayojihusisha na hifadhi ya kasa katika pwani ya Baha&#341;i ya Hindi nchini Tanzania imeanza kutumia teknolojia ya Satelaiti kubo&#341;esha hifadhi ya wanyama hao wa baha&#341;ini waliopo katika hata&#341;i ya kutoweka. Akizungumza hivi ka&#341;ibuni wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa washi&#341;ika wa m&#341;adi wa&#8230;<\/p>\n","protected":false},"author":536,"featured_media":0,"comment_status":"open","ping_status":"open","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"footnotes":""},"categories":[1],"tags":[],"class_list":["post-3912","post","type-post","status-publish","format-standard","hentry","category-headlines"],"_links":{"self":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3912","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/users\/536"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=3912"}],"version-history":[{"count":0,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/3912\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=3912"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=3912"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"http:\/\/ipsnews.net\/swahili\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=3912"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}